Saturday, October 25, 2014
Sunday, October 5, 2014
PICHA: GRADUATION EVENTS
Tunashukuru Mungu kw Designer wa Ndekeno Production team kw kuhitimu masomo yake ya shule ya msingi katika shule ya ST.Ann's iliyopo Mbezi- Makabe
Thursday, September 18, 2014
Sunday, September 14, 2014
Monday, September 8, 2014
Sunday, August 24, 2014
Remnant Christian Centre: PICHA: 1Year of ANNIVERSARY Remnant Christian Cent...
Remnant Christian Centre: PICHA: 1Year of ANNIVERSARY Remnant Christian Cent...: TUNAMSHUKUR MUNGU TUMEFIKISHA MWAKA TANGIA HUDU...
REMNANT CHRISTIAN CENTRE
REMNANT CHRISTIAN CENTRE
Wednesday, July 2, 2014
MASANJA MKANDAMIZAJI AANDIKIWA BARUA ''NI VIZURI UKACHAGUA MOJA! MASANJA MKANDAMIZAJI AANDIKIWA BARUA ''NI VIZURI UKACHAGUA MOJA!
KWAKO, Emmanuel Mgaya ‘Masanja’. Naamini u mzima na unaendelea
vyema na majukumu yako ya kila siku. Kwa upande wangu nipo sawa, nakimbizana na
maisha.
Nina machache ya kukushauri kuhusiana na maisha yako kama staa ambaye kwa sasa umetangaza kuokoka. Kwa maneno mengine ni kwamba, umeondoka kwenye utaifa, upo mikononi mwa Muumba wako.Nimekufahamu kwa kitambo kidogo. Kwangu mimi, wewe ni mmoja wa mastaa wa ukweli katika uchekeshaji Bongo. Mwenye kipaji cha hali ya juu na unayejua unachokifanya.
Tatizo ni kwamba, nashangazwa na aina ya maisha yako baada ya kutangaza kuokoka. Ninavyojua mimi, kuokoka ni kuachana na maisha ya awali ambayo (pengine) yalikuwa hayampendezi Mola na kugeukia katika maisha safi.Niliposikia umeokoka nilifurahi kuona kuwa umeelekea sehemu sahihi zaidi kiimani. Lakini moyoni nilikuwa na shaka kidogo maana wapo wasanii wengi kwenye uigizaji ambao walitangaza kuokoka lakini baadaye wakaonekana kwenye njia zao za awali.
Ukiachana na waigizaji, pia kuna wasanii wa Bongo Fleva ambao nao waliingia kwenye ulokole na mara wakaamua kurudia maisha yao ya awali.Baadaye nikasikia kuwa unasomea Uchungaji (ingawa inaelezwa kuwa ni Uinjilisti), hapo sikuwa na shaka tena na wokovu wako. Niliamini kwa mtu ambaye ameamua kuingia kwenye kufundisha wengine njia iliyo sahihi hawezi kudanganya kuwa ameokoka.
Siyo kama naingilia maisha yako au nakukosoa kwenye suala la imani yako. Uzuri ni kwamba, nami ninaamini katika imani yako, hivyo sioni tatizo kukushauri.Tatizo lipo kwenye staili yako ya maisha. Ni kweli kwamba umeokoka, lakini itawezekana vipi usuke mabutu kichwani? Maandiko yanaeleza wazi kuwa, wanaoamini ni barua inayosomeka kwa watu wote.
Je, watu watasoma nini kupitia mabutu? Unaweza kusema kuwa, imani ya mtu iko moyoni, hapo sitakubaliana na wewe, maana kinachoonekana nje, kinawakilisha kilichomo ndani.Vipi kama kanisa zima, wanaume wataingia wamesuka? Nafikiri si jambo sahihi. Watu watapata shaka na wokovu wako, tena mchunga kondoo. Wengine wanaweza kuona wokovu si jambo ‘serious’. Kwamba mtu anaweza kuingia na akaendelea na mambo yake yaleyale, jambo ambalo si la kweli.
Wokovu ni pamoja na mwonekano wa nje. Mavazi, mitindo ya nywele n.k.Jambo jingine ambalo limenishangaza ni namna unavyoingiza komedi kwenye mambo yanayohusu dini.Usahihi wa kufanya utani kwenye vichekesho huku ukitaja jina la Mungu unatokea wapi? Masanja tumezuiwa kufanya mzaha au kulitaja bure Jina la Mungu wetu.
Nakushauri kama ni kweli umeamua kuokoka, badilika lakini kama unahisi bado unatamani maisha ya kawaida na kujichanganya, chagua moja ili jamii isikutafsiri tofauti.Ni uamuzi wako kufuata au kuacha hapahapa, lakini la muhimu ni kwamba, nitakuwa nimeshakushauri. Ubarikiwe sana mpendwa!
Yuleyule,
Mkweli daima,
.........................
Joseph Shaluwa.

Saturday, June 28, 2014
TUZO ZA WATU ILIYOFANYIKA IJUMAA HII
Tuzo za watu
za Tanzania au Tanzania People’s Choice Awards zimetolewa Ijumaa hii kwenye
ukumbi uliopo Serena Hotel jijini Dar es Salaam. Jumla ya vipengele 11 vilikuwa
vinashindaniwa. Mshindi katika kila kipengele ameibuka na zawadi ya shilingi
milioni moja pamoja na trophy. Host wa tuzo hizo alikuwa mtangazaji mkongwe wa
radio, Jimmy Kabwe.
1.
MTANGAZAJI WA REDIO ANAYEPENDWA
Millard Ayo – Clouds FM
2. KIPINDI
CHA REDIO KINACHOPENDWA
Amplifaya – Clouds FM
3.MTANGAZAJI
WA RUNINGA ANAYEPENDWA
Salim Kikeke – BBC Swahili
4. KIPINDI
CHA RUNINGA KINACHOPENDWA
Mkasi – EATV
5.
MWANAMICHEZO ANAYEPENDWA
Juma Kaseja – Yanga
6.
MUONGOZAJI WA VIDEO ZA MUZIKI ZINAZOPENDWA
Nisher
7. VIDEO YA
MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIUME
My Number – Diamond
8. VIDEO YA
MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIKE
Yahaya – Lady Jaydee
09.
MUIGIZAJI WA KIUME KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA
King Majuto
10.
MUIGIZAJI WA KIKE KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA
Elizabeth ‘Lulu’ Michael
11. FILAMU
INAYOPENDWA
Ndoa Yangu
Wednesday, June 25, 2014
June 25: Ni Miaka miaka mitano tangu kifo cha Michael Jackson
Michael
Jackson alifariki June 25, 2009, katika muda aliokuwa akiutafuta sana usingizi
huku akijiandaa kurejea kwa kufanya ziara yake ambayo aliamini ingemuondoa
kwenye madeni mengi na kurudisha heshima yake kama mfalme wa pop. Katika siku
zake za mwisho, Michael Jackson aliondoka nchini Marekani akiwa na wanae watatu
muda mfupi baada ya kumalizika kwa kesi yake ya kulawiti watoto.
Alirejea
Marekani kimyakimya mwaka 2006, baada ya kukaa huko Bahrain kwa mwaka mzima na
miezi kadhaa nchini Ireland. Bill Whitfield na Jevon Beard walitumia miaka
miwili kama walinzi wa MJ walisimulia mengi kwenye kitabu kipya kiitwacho s
“Remember the Time: Protecting Michael Jackson in His Final Days.” Kipindi
Jackson anashuka kutoka kwenye ndege binafsi jijini Las Vegas, watu aliokuwa
nao walikuwa wanae na mlezi wa watoto wake tu. “Alikuwa peke yake,” Whitfield
alisema kwenye mahojiano na CNN. Kikawa kitu kisicho cha kawaida. Kuna kitu
hakipo sawa. Huu ni utani.”
Walinzi hao
ambao wakati mwingine hawakuwa wakilipwa mshahara kwa miezi, walikuwa wakitumia
fedha zao kusaidia masuala nyumbani kwa Jackson pale credit cards zake
zilipokuwa zikiishiwa. Beard aliiambia CNN kuwa mameneja wake walikuwa
wakimzunguka. “Jamaa alikuwa amechoka kiakili.” Whitfield na Beard walidai kuwa
Jackson alikuwa na mambo yake ya siri yaliyokuwa yakijulikana labda kwa
mashabiki wake waliokuwa wakimganda. Jackson alikuwa na mademu.
Mfalme huyo
wa pop alikuwa akitumia muda wa faragha na mwanamke nyuma ya pazia kwenye siti
ya nyuma ya gari wakati walinzi wakiendesha. Wanadai kuwa Jackson alikuwa
akipenda wasichana na walimuona kwa macho yao akiwabusu. Wanawake hao, ambao
walinzi waliamini walikuwa wakitokea Ulaya, hawakuwahi kwenda nyumbani kwake na
hawakuwahi kukutana na wanae.
Alikuwa
akirudi nyumbani kutoka kwenye mishe zake kabla ya wanae Prince, Paris na
Blanket hawajaamika. Jackson aliwaagiza walinzi wake kuwazuia kaka zake, dada
zake na baba yake kuingi kwake japo mama yake alikuwa akiruhusiwa kuingia
nyumbani kwake.
Pamoja na
kuwa hayupo tena, muziki wa Michael Jackson bado unaendelea kutoka ambapo sasa
album yake Xscape ipo sokoni na iliuza kopi milioni 2.3 katika wiki tatu tangu
itoke mwezi May. Ukurasa wake wa Facebook una likes milioni 75 ziadi hata
Justin Bieber, Lady Gaga, Katy Perry, Taylor Swift na Bruno Mars.
Chanzo: CNN.
Soma zaidi makala hiyo hapa.
Saturday, June 21, 2014
Meet Africa's first female captain flying the Dreamliner
Rubani wa kike wa Kenya, Irene Koki Mutungi ndiye rubani wa kwanza mwanamke wa Afrika kupaisha ndege kubwa aina ya Boeing 787 Dreamliner. Tazama mahojiano haya aliyofanyiwa na KTN.
Friday, June 13, 2014
Leo ni mwaka mmoja tangu Langa Kileo afariki dunia
Wakati ambapo mashabiki wa muziki wa Hip Hop nchini walikuwa
wameanza kusahau majonzi ya kumpoteza Albert Mangweha aka Ngwair mwezi May
mwaka jana, June 13, 2013 walitoneshwa tena kwa kifo cha mwana hip hop
mwingine, Langa Kileo aka Lyrically And Naturally Gifted African.
Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano wa hospitali ya taifa ya
Muhimbili, Aminiel Aligaesha Langa alifariki une 13, saa 11 jioni baada ya
kufikishwa hospitalini hapo tangia juzi mida ya jioni. Taarifa za awali zilidai
kuwa Langa alikuwa anaumwa Malaria kali iliyopelekea kukimbizwa Muhimbili jana
jioni.
Langa alikuwa ni mmoja wa matunda ya shindano la muziki la
Coca-Cola Pop Stars mwaka 2004 ambalo washindi wake waliounda kundi la
Wakilisha akiwa pamoja na Sarah Kaisi `Shaa’ na Witness Mwijage `Witness’
ambapo walitamba na nyimbo kama Unaniacha Hoi na Kiswanglish. Langa alizaliwa
Desemba 22, 1985 jijini Dar es Salaam katika familia ya wanandoa Vanessa Kimei
na mumewe Mengisen Kileo.
Alisoma Shule ya Msingi Olympio na Sekondari ya Loyola, zote
za jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, akiwa kidato cha pili alihamishiwa
Kampala, Uganda katika Shule ya Vienna na baadaye shule ya Hillside
International Academy, huko huko Uganda. Baadaye alirejea nchini na kujiunga na
masomo ya Stashahada ya Masoko katika Chuo cha Biashara Dar es Salaam (CBE),
Kampasi ya Dodoma (Global Publishers).
Wasanii na watu mbalimbali walituma salamu zao za rambirambi
kwa familia ya Langa na kuomboleza kifo hicho.
Joh Makini
Wiki mbili nyuma tulipanga kufanya trak kwa Dunga tukaisogeza
mbele kupisha msiba wa Ngwea nakumbuka mpaka session alipanga alhamis aliamplz
tumalize msiba lkn kumbe yeye ndio alikua anafata daah! Mara ya mwisho kuongea
ni uliponiambia nichek beat kwenye email alaf tuchangie mawazo kutakufuta idea
daaah! Baadae tena ukanitext umepata idea mbili platinum ideas tukienda studio
tunaua! Sasa umeondoka ghafla mimi na dunga tumebaki na beat tu sasa #RIP
LANGA.
THE CITY of PHD
DAAAAAAAH MUNGU TUSAIDIE!!MI NIMESHAKOSA AMANI KABISA HAPA
NILIPO!!!HAYA NI MAJONZI MAKUBWA!!REST IN PEACE LANGA!!GONE TOO SOON!!DAAAAAH
Nick Mweusi
KAMA HIZI HABARI ZA LANGA NI KWELI SHOW YANGU NA GNAKO CLUB
KAKALA HAiTAfANyIKA. RIP LANGA
Afande Sele The’King
Tunavyotaka sisi, sivyo anavyotaka yeye (Mungu) mapenzi yake
ni zaidi.
Mungu akupumzishe
pema LANGA KILEO
K Wa MaujanjaSaplayaz
Kapumzike na amani zote hatuta acha kukukumbuka daima
Mad Ice
Oh lord shed light on these dark moments of the Tanzanian
Music Industry! Its not even a week since we buried Ngwea and another one is
down :(… R.I.P Langa!
Cpwaa
Another Brother, Another Soldier, Another buddy,another
talented Tanzanian Hip Hop Artist gone!……bado siamini.. #RIPLanga
#BongoFlavaStayCalmAndUnited
Fina Mango
RIP Langa. Pole sana Mama na Mzee Kileo Mungu awake nguvu
Kwa wakati huu mgumu
D knob
Rip Langa. Sijui cha kuongea kiukweli Dah.
Nikki Mbishi
Langa unaenda wapi kichaa wangu?Mwanao bado nalia na Ngwea
halafu unasepa badala ya kubaki tuanue matanga.
Thursday, June 12, 2014
Picha:Mabanda ya wafanyabiashara wa soko la Karume yateketea kwa moto
Moto mkubwa umetetekeza kabisa soko kubwa kabisa la mitumba
la karume jijini Dar es Salaam usiku wa Jumatano, na kusababisha hasara kubwa
kwa wafanyabiashara wote wa soko hilo.
Baadhi ya
mabanda yakiteketea kwa moto
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, wamedai
moto huo ulianza kuteketeza mabanda hayo majira ya saa 4 usiku, huku wakijaribu
kutafuta msaada kuuzima bila mafanikio yeyote.
Wazima moto
walifanikiwa kuudhibiti moto uloweza kufikia karibu na kiwanda cha Breweries,
lakini haujasababisha hasara yeyote katika nyumba za jirani wa soko hilo kwa
mujibu wa mwandishi habari wa Raia Mwema Mbaraka Islam alipozungumza na Sauti
ya Amerika.
Anasema
hakuna kibada cha biashara kilichosalimika na hakuna mtu aliyefanikiwa kuokowa
mali yake. Mfanya biashara Wilson magembe anasema amepoteza kila kitu na
ilikuwa vigumu kuweza kuchukua bidhaa zao kwa sababu moto uliwaka kwa haraka
sana.
Picha: Jennifer Lopez na Pitbull wapamba sherehe za ufunguzi wa kombe la dunia 2014, Brazil
Maelfu ya
mashabiki wamejitokeza jioni ya leo kwa saa za Brazil (June 12) katika sherehe
za ufunguzi wa fainali za kombe la dunia 2014 kwenye uwanja wa ‘Arena de Sao
Paulo’ nchini Brazil, ambapo Jennifer lopez, rapper Pitbull na mwimbaji wa
Brazill Claudia Leitte wametumbuiza mbele ya mashabiki waliofurika kwa wingi na
kuimba wimbo rasmi wa kombe la dunia kwa mwaka huu ‘We Are One (Ola Ola)’.Maandalizi
ya sherehe hizo za ufunguzi yalifanywa kuanzia March mwaka huu, na jumla ya
masaa 84 yalitumika kwaajili ya rehearsal za sherehe hizo.Mechi ya ufunguzi wa
michuano hiyo inafanyika usiku huu kati ya wenyeji Brazil na Croatia.