kitengo cha
Afrika kimebaini kuna watu wanaonunua matokeo bandia ya vipimo vya virusi vya
HIV yakionyesha hawana virusi hivyo nchini Uganda.
Picha za
Filamu zilizonaswa kisiri zinaonyesha namna ilivyo rahisi kutoa hongo kwa
wahudumu wa afya ili kupata vyeti hivyo bandia.
Baadhi ya
watu wanaonunua vyeti hivyo visivyokubalika kisheria wanasema wamefanya hivyo
ili kupata kazi, kusafiri kwenda ng'ambo ama kwa ajili ya kupata wapenzi wa
ngono.
Mwandishi wa
BBC wa Kampala Catherine Byaruhanga alilitembelea kliniki 15 bila ya
kujitambulisha.
Kumi na
mbili kati ya kiliniki hizo zilikuwa tayari kumpa vyeti bandia vya kuthibitisha
kuwa hawana virusi vinavyosababisha ukimwi vya HIV.
Wanaosimamia
kliniki hizo walitaka hongo kati ya Dola 10 na 20 kwa kila cheti.
Picha za
video tulizopiga kisiri katika maduka ya kupiga chapa katika maeneo mengi ya
mji mkuu wa Uganda, Kampala zinathibitisha kuwa mtu anaweza kuigiza cheti pia
kwa urahisi sana.
BBC
ilipomkabdihi Waziri wa Afya, Ruhakana Rugunda, ushahidi huo, alikubali kuwa
hiyo ni changamoto kubwa lakini akasisitiza kuwa Serikali itafanya kila juhudi
kuwakamata na kuwashitaki wanaohusika katika ufisadi huo.
Serikali ya
Marekani hutoa kiwango kikubwa cha peza za miradi inayotumiwa kupambana na
ukimwi nchini Uganda.
Balozi wa
Marekani alitoa wito kwa viongozi wa taifa hilo kufanya bidii zaidi kupambana
na kashfa hiyo.
Hata hivyo
alisema kuwa hana uhakika kuwa Dola za Marekani hazijatumiwa katika kliniki
hizo zinazotoa vyeti bandia.