Kama
ulishangaa kusikia kuwa Diamond Platnumz alilipa dola 5,000 ili kumshirikisha
Davido kwenye remix ya My Number One, huenda ukaishiwa nguvu kusikia kiwango
kinachodaiwa kutolewa na msanii wa Nigeria, KCEE ili kufanya collabo na first
lady wa YMCMB, Nicki Minaj.
Kuna tetesi
kuwa KCEE amelipa kitita cha N68m, ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 675 za
Tanzania ili amshirikishe malkia huyo mpya wa hip hop nchini Marekani. Kufuatia
tetesi hiyo, meneja wa KCEE, Soso Sobrekon, ameongea na mtandao wa NET kufafanua
mambo yalivyo.
“Tupo nchini
Marekani kujaribu kupata collaboration. Ni kweli tupo kwenye mchakato wa
kufanya wimbo na Nicki Minaj. Tulitaka kuifanya iwe surprise kwa mashabiki
lakini kwakuwa tayari imejulikana, tunataka kuifanya iwe kuwa zaidi,” alisema.
Hata hivyo
meneja huyo alikataa kuthibitisha kama kweli kiwango hicho ndicho walicholipa.
“Tunataka kumuongeza msanii mwingine wa YMCMB ambaye ni mkubwa kuliko Nicki
Minaj. Nicki ameshathibitishwa kuwa kwenye wimbo huo, lakini kwakuwa sasa kila mtu
anafahamu, bado tutawasurprise mashabiki kwa kumchukua msanii mwingine kutoka
YMCMB.’