1. Askari akikuweka
chini ya ulinzi muulize kitambulisho ni haki yako.
2. Askari akikukamata
akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama
kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.
3. Askari
akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki
yako.
4. Unaruhusiwa na
sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya
kukamatwa.
5. Askari
anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako
kujikinga naye.
6. Askari
haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kukri
amri halali.
7. Askari
haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.
8. Askari
haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.
9. Askari lazima
akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.
10. Kibali kieleze
jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au
uchanganuzi wa mtu au sehemu.
11. Hairuhusiwi
kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.
12. Ni haki yako
kumpekua askari kabla hajakupekua ili asipandikize kitu.
13. Usipekuliwa
nyumbani bila kuwapo kiongozi wa mtaa.
14. Kila
kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.
15. Mali iliyochukuliwa
katika upekuzi lazima ibaki salama.
16. Mwanaume
haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.
17. Unaruhusiwa
kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.
18. Askari
haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.
19. Unaruhusiwa
kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki
yako.
20. Usilazimishwe
kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.
21. Usitoe maelezo
bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.
22. Unaruhusiwa
kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo chini ya ulinzi.
HIZI
ZOTE NI HAKI ZAKO, ZILAZIMISHE USIBEMBELEZE WALA USIZIOMBE.