MICHAKATO

Levis Rocky Ndekeno

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Pages

Tuesday, March 25, 2014

Hewa chafu inaua mamilioni duniani


Watu milioni saba walifariki mwaka 2012 kutokana na hewa chafu. Hii ni kwa mujibu wa shirika la afya duniani .

Ripoti ya shirika hilo inasema kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya hewa chafu na maradhi ya moyo, tatizo la kupumua na ugonjwa wa Saratani.
Taarifa zinazohusiana
afya

Kifo kimoja kati ya vinane duniani kilitokana na hewa chafu , na kuifanya hali hiyo kuwa moja ya hatari ya mazingira chafu afya ya binadamu.

Tarkriban watu milioni sita waliofariki dunia walikuwa Asia ya Mashariki na katika eneo la Pacific.

Shirika hilo limesema kuwa takriban watu milioni 3.3 walifariki kutokana na hewa chafu katika nyumba zao kwa kutumia mkaa kukipikia na wengine milioni 2.6 walifariki kutokana na hewa chafu nje ya nyumba zao , hasa katika nchi zinazostawi.

Afisaa mmoja mkuu wa shirika hilo, Daktari Maria Neira, amesema kuwa, hewa chafu ina hatari kubwa kwa afya ya watu kuliko ilivyodhaniwa hasa kwa kusababisha maradhi ya Moyo na Kiharusi.

Ripoti hii inaonyesha umuhimu wa kushirikiana katika kuhakikisha kuwepo kwa hewa safi.

Shirika hilo limesema kuwa kupunguzwa kwa viwango vya hewa chafu kunaweza kuokoa maisha ya watu.

Kadhalika shirika hilo limesema: "usafi wa hewa tunayopumua unazuia maradhi ya kuambukizana na pia kuondoa hatari kwa watoto, wazee na wanawake.''
Taarifa zinazohusiana

Wanaowania Tuzo za KILI 2014 ndio hawa, zilizoachwa ziko hapa pia


 (BASATA) limetangaza rasmi matokeo ya mchakato wa kuwapata wateule rasmi yaani ‘nominees’ wa vipengele 34 vya tuzo za muziki Tanzania.
 Kabla ya kuanza kutajwa kwa wanaowania tuzo za KTMA 2014, BASATA ilitangaza nyimbo ambazo zimetolewa kwenye kuwania tuzo hizi kutokana na sababu za kimaudhui kama unavyoona hapa chini.











Nyingine ni
 WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI – Tubonge ya Jose Chameleone, Nakupenda pia ya Wyre na Alaine, Badilisha ya Jose Chameleone, Kipepeo ya Jaguar, Kiboko changu ya Amani, Weasal na Radio.
 WIMBO BORA WA TAARAB – Wasiwasi wako wa Mzee Yusufu, asie kujua hakuthamini Isha na Saida Ramadhani, Nipe stara Rahima Machupa, sitaki shari Leila Rashid, fahari ya mwanamke ya Khadija Kopa, mambo bado Khadija Yusufu, kila muomba Mungu ya Mwanahawa Ally.
 WIMBO BORA WA RAGGA/DANCEHALL – Nishai ya Chibwa ft Juru, Sexy Lady ya Dr. Jahson, My sweet ya Jettyman Dizano, feel alright ya Lucky Stone na wine ya Princess Delyla.
 WIMBO BORA WA KUSHIRIKISHWA/KUSHIRIKIANA – Muziki gani ya Ney wa Mitego ft Diamond, Joto hasira ya Lady Jaydee ft Prof J, kidela ya Ally Kiba na Abdu Kiba, bila kukunja goti ya MwanaFA, Ay ft J Martins na tupogo ya Ommy Dimpoz ft J Martins.
 RAPA BORA WA MWAKA WA BENDI – Kitokololo, Chokoraa, Ferguson, Canal Top na Totoo ze bingwa.
 MTUMBUIZAJI BORA WA KIKE WA MUZIKI – Khadija kopa, Vanessa Mdee, Isha Ramadhani, Luiza Mbutu, Catherine (Cindy)
 MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA TAARAB – Enrico, Ababuu mwana wa Zanzibar na Bakunde.
 MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA (BENDI) – Allan Mapigo, C9, Enrico, Amoroso na Ababuu mwana wa Zanzibar.
 WIMBO BORA WA REGGAE – Niwe nawe ya Dabo, hakuna matata ya Lonka, tell me ya Dj Aron ft Fidempha, bado nahitaji ya Chikaka ft Bless P & Lazzy B, Bongo reggae ya Warriors from the east.
 WIMBO BORA WENYE VIONJO VYA ASILI YA KITANZANIA – Kwejaga nyangisha ya Batarokota, Nalonji ya Kumpeneka, bora mchawi Dar bongo massive, tumbo lamsokota ya Ashimba, Aliponji ya Wanakijiji na Agwemwana ya Cocodo african music band.


Monday, March 24, 2014

TAFADHALI ACHA KILA UNACHOFANYA NA SOMA HII, NI MUHIMU SANA.

Mwanamke huyu masikini yupo Labour sasa yapata siku mbili, tatizo ni kwamba ana hofu kubwa ya kufanyiwa upasuaji. Madaktari wamejaribu kufanya kila linalowezekana kwa uwezo wao lakini bado mambo yanelekea mrama.

Sasa kwa pamoja tuungane kumwambia Mungu kuwa hajalishi madaktari wamesema nini lakini Mama huyu ajifungue salama kwa njia sahihi.

Comment "Amen" kama unatarajia Taarifa nzuri hivi karibuni .Plezz DON'T IGNORE PLEASE SHARE FOR MORE PRAYERS! HII YAWEZA KUKUTOKEA HATA MAMA YAKO, DADA YAKO, MDOGO WAKO, HATA RAFIKI NA NDUGU YAKO WA KARIBU.....narudia usidharau plzzzzz

MBUNGE WA CCM AFIKISHWA KWA SPIKA KWA KUTOKUMLIPA MSHAHARA HOUSEBOY WAKE LIVE!!

Mbunge wa jimbo la Bahi (CCM) Omar Baduel amefikishwa kwa Katibu wa Bunge Dr Kashilila kwa kosa la kuto mlipa mshahara msaidizi wake wa jimbo kwa kipindi chote cha miaka minne,Said Kayumbo amelalamikia ofisi ya bunge na kuomba iingilie kati ili apate mshahara wake kwa miaka yote minne. Said kayumbo alisema mbunge huyo amekua akimpa 20,0000 au 30,000 wakati mshahara wa msaidizi wa mbunge ni 450,000.

Aidha mbunge huyo amekua na kashifa nyingi kama ile ya rushwa ambayo kesi yake inaendelea kisutu,mwezi wa february 2014 alisomewa tuhuma ya kula pesa ya mfuko wa jimbo,mwaka 2009 alifukuzwa uenyekiti wa halmashauri ya bahi kwa tuhumu za kuiba mifuko ya cement ya shirika la world vision kwenye kata yake ya Chipanga pamoja na tuhuma ya kushirikiana na mkurugenzi wa bah

SHOPRITE IMEUZWA WAFANYA KAZI WAGOMA NA KUANDAMANA MLIMANI CITY

Leo mida ya Jioni pale mlimani City nimeshuhudia wafanya kazi wa Duka Kubwa la Shoprite wakiwa wamegoma wakizua watu wasiingie kwenye duka hilo kwa kile kilichodaiwa kuwa duka hilo limeuzwa bila wao kupewa mafao yao ...Habari zilizopo ni kuwa duka hilo limenunuliwa na Super Market Ingine kubwa Nchini Kenya Ambayo inakuja kupanua biashara zake hapa Dar .....

ETI UGONJWA MKUBWA UNAOTUSUMBUA WA TANZANIA SIO UKIMWI WALA MALARIA NI HUU HAPA..NINI , EMBU SOMA KUJUA

Kwenye nchi zinazoendelea Tanzania ikiwemo magonjwa ya kuambukizwa yameonekana kuwa ndio tishio sana kwa afya za wananchi. Magonjwa kama ukimwi, malaria, TB, kichocho, kipindupindu na homa za matumbo yamekuwa yakisumbua sehemu kubwa ya watu katika nchi hizi.

Ili kuokoa afya za wananchi serikali za nchi hizi zinazoendelea zimekuwa zikiweka mipango kabambe ya kupambana na magonjwa haya. Mipango mingi iliyowekwa imefanikiwa ila sio kwa kiwango kikubwa sana. Hii ni kwa sababu kuna ugonjwa mwingine mkubwa zaidi ya magonjwa haya ya kuambukizwa unaosumbua wananchi.

Kabla hatujaangalia ugonjwa huo hebu tuangalie tofauti kati ya mataifa yenye magonjwa ya kuambukizwa na yale ambayo hayana kwa kiwango kikubwa. Ukiangalia kwa makini utagundua kwamba mataifa yanayosumbuliwa sana na magonjwa ya kuambukizwa ni mataifa ambayo watu wake ni masikini sana. Na hata ndani ya taifa sehemu ambazo magonjwa haya yameshamiri ni sehemu ambazo watu ni masikini. Nina hakika unajua kipindupindu huwa kinatokea maeneo gani sana sana.

Kwa mantiki hii basi ugonjwa mkubwa unaoisumbua nchi yetu sio ugonjwa wa kuambukiza bali ni umasikini. Umasikini ndio ugonjwa mkuu ambao unapoteza maisha ya wananchi wengi. Umasikini ndio ugonjwa mkubwa unaofanya maisha ya wananchi wengi kuwa magumu. Na kwa kuwa kwenye mipango ya kupambana na magonjwa umasikini haujawekwa, basi hakuna anayefunguka macho kuuangalia.

Ni umasikini unaofanya wengi kufanya ngono zembe na wakati mwingine ukahaba na kujikuta wanaambukizwa magonjwa ya zinaa na ukimwi. Ni umasikini unaofanya watu wakose maji safi na salama na kuishia kutumia maji machafu yanayowasababishia magonjwa ya tumbo na minyoo. Na ni umasikini unaofanya watu kukosa elimu na hivyo kushindwa kujikinga na magonjwa yanayoweza kuzuilika.

Tunawezaje kutokomeza ugonjwa huu?

Kwa kuwa ugonjwa huu hauko wazi basi serikali haijaweka mikakati ya kupambana nao au kuutokomeza. Hata baadhi ya mipango mingi iliyowahi kuwekwa kupambana na ugonjwa huu haikuzaa matunda yaliyotarajiwa na mwishowe kufa.
Mipango mingi imeshindwa kwa sababu serikali imekuwa ikiangalia sehemu isiyohusika kwenye kupambana na ugonjwa huu. Huwezi kuondoa umasikini kwa kutegemea misaada. Misaada haiondoi bali inaongeza umasikini.

Njia pekee ya kuondoa umasikini ni kuwajengea watu uwezo wa kufanya kazi yenye manufaa kwa watu wengine. Kuzalisha bidhaa au huduma zinazohitajika na watu wengine hivyo kutengeneza biashara kwa ngazi ya kitaifa na baadae kitaifa.

Serikali ingepaswa kuwajengea watu uwezo wa kuajiriwa, kujiajiri na kufanya biashara. Na kwa kuwa kuajiriwa nafasi hazitoshi basi kujiajiri na biashara ni njia nzuri za kupambana na ugonjwa huu. Kwa kuwa serikali haifanyi hivi je wewe unalala?

Usilale, tulishakubaliana kwamba usimlaumu yeyote, AMKA na chukua hatua juu ya maisha yako. Jijengee uwezo wa kujiajiri na kufanya biashara ili uweze kuutokomeza ugonjwa huu mbaya kwako, kwa familia yako na kwa jamii inayokuzunguka. Kama watu wachache tutachukua hatua hii baadae itasambaa na kufanyika na watu wanaotuzunguka na hatimaye taifa zima.

Unawezaje kujijengea uwezo?

Katika mtandao huu wa AMKA MTANZANIA tumeshajadili njia nyingi sana za kujijengea uwezo kwa kujifunza na kuchukua hatua. Anza kuzitumia njia hizi kwenye kazi na biashara zako na utaona mabadiliko makubwa. Kama wewe ni mgeni kwenye mtandao huu endelea kusoma makala nyingi utakutana na mawazo mengi juu ya kuchukua hatua na kubadilika.

Ili uweze kujiondoa kwenye ugonjwa huu wa umasikini inabidi ujue ni nini kinakufanya mpaka sasa unateseka na ugonjwa huo. Kwa kujua sababu itakuwa rahisi kwako kupambana nazo na hatimaye kushinda. Unaweza kuzijua sababu hizo kwa kusoma kitabu KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIO TAJIRI. Kupata kitabu hiko bonyeza maandishi hayo.

Njia kubwa ya kupambana na ugonjwa huu wa umasikini ni kujijengea uwezo. Na njia bora ya kujijengea uwezo ni kujifunza na kuchukua hatua ya kutekeleza yale unayojifunza. Kama unataka kujifunza zaidi juu ya biashara na mambo mengine jiunge na kisima cha maarifa na uchote maarifa yatakayokusaidia. Kujiunga na kisima cha maarifa bonyeza maandishi haya.

Kuanzia sasa jua ugonjwa namba moja unaotakiwa kupambana nao ni umasikini na usifikiri msaada utakusaidia kuondokana na umasikini.