MICHAKATO

Levis Rocky Ndekeno

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Pages

Monday, May 9, 2016

NE-YO kutumbuiza Mwanza May 21


Mwanamuziki nguli kutoka nchini Marekani NE-YO anayetamba kwa muziki wa kizazi kipya anatarajia kufanya ziara nchini mwezi huu kwa mwaliko wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Jembe Media Limited.Akitangaza ujio wa mwanamuzi huyo, Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu alisema NE-YO atawasili nchini Mei 19 na Mei 21 atatoa burudani ya aina yake katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kwenye tamasha la Jembeka na Vodacom 2016 liloandaliwa na kampuni ya Jembe chini ya udhamini mkuu wa Vodacom Tanzania.Nkurlu alisema kuwa Vodacom imedhamini ujio wa mwanamuziki huyu kwa ajili ya kuwapatia burudani ya kimataifa wateja wake na watanzania wote kwa ujumla kupitia tamasha lake la Jembeka na Vodacom 2016.“Vodacom tunaamini kuwa wateja wetu wanahitaji kupata burudani baada ya majukumu ya kazi ya kila siku ndio maana tumekuwa tukidhamini michezo na matamasha mbalimbali ya muziki kwa ajili ya kuwapatia burudani kama ambavyo tumefanikisha kumleta NE-YO nchini,” alisema Nkurlu.Aliongeza kuwa mbali na kukonga nyoyo za wapenzi wa muziki NE-YO anayetamba kwa vibao maarufu baadhi yake vikiwa ni Let Me Love You, Beautiful Monster, Coming With You na She Knows featuring Juicy J atashiriki katika shughuli za kusaidia jamii kupitia taasisi ya Vodacom Foundation pia atashiriki katika hafla ya uzinduzi wa duka la Vodacom lililopo kwenye Mall kubwa jijini Mwanza.Aliwataka wasanii wa hapa nchini na wananchi kwa jumla kujitokeza kwa tamasha hilo ili wapate burudani ambapo pia wasanii watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali na kubadilishana uzoefu na mwanamuziki huyu wa kimataifa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi wa Tamasha la Jembeka festival 2016, Costantine Magavilla,alisema kuwa wanayo furaha kumleta mwanamuziki NE-YO kwenye tamasha hili na wana imani kuwa wapenzi wa muziki nchini watapata burudani iliyokuwa na hadhi ya kimataifa kutoka kwa msanii huyo.Alisema tamasha la Jembeka na Vodacom litaendelea kufanyika kila mwaka na litakuwa linasambaza burudani za kila aina kwa wapenzi wa muziki na burudani katika kona zote za Tanzania “Wapenzi wa muziki tunawataka wakae mkao wa kula kwa kuwa tutazidi kuuwapatia burudani za muziki wa hapa nchini na wa kimataifa.

Friday, May 6, 2016

Spika Paul Ryan ampinga Donald Trump

Spika wa Republican katika Baraza la Wawakilishi la Marekani,Paul Ryan,amesema hayupo tayari kumuunga mkono Donald Trump kuwa mgombea wa Urais kupitia chama hicho.
Mfanyabiashara huyo bilionea anaonekana dhahiri kushinda katika mbio za uteuzi kukiwakilisha chama hicho lakini Ryan alisema kuwa kabla hakuweza kuidhinisha suala hilo,Na kuwa Trump alipaswa kuwaonyesha watu kuwa anaheshimu taratibu za Republican na angepata kura za Wamarekani wengi zaidi.
Katika kulijibu hilo Trump lisema hakuwa tiyari kuunga mkono ajenda ya RyanMapema Marais wa zamani wa Marekani George W Bush na babaye George Bush waliweka wazi kuwa hawatunga mkono kupita kwa Trump.

Mfanyabiashara Jacob Juma auawa Nairobi

Mfanyabiashara mashuhuri Jacob Juma, ambaye amekuwa akizua mjadala mitandaoni Kenya kutokana na ujumbe wake anaoandika hasa kwenye Twitter, ameuawa kwa kupigwa risasi jijini Nairobi. Taarifa zinasema Bw Juma alipigwa risasi na watu ambao walikuwa wakiendesha pikipiki alipokuwa akielekea nyumbani kwake mtaa wa Karen mwendo wa saa nne usiku. Gari lake lilipatikana na zaidi ya matundu 10 ya risasi.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation la Kenya, polisi wanasema hakuna kilichoibiwa kutoka kwenye gari lake. Simu zake mbili na pesa vilipatikana ndani ya gari. Bw Juma alikuwa mwanakandarasi ambaye pia alihusika katika sekta ya uchimbaji madini.

WhatsApp kuja na ‘version’ rasmi ya kwenye computer

Najua kuwa kwa sasa unaweza kutumia WhatsApp kwenye computer yako kwa kuscan code maalum na kuunganisha app ya simu na whatsapp web. Lakini siku zijazo, utaweza kutumia WhatsApp ya kwenye computer inayojitegemea yenyewe, imebainika.Kuna tetesi kuwa WhatsApp itakuja kwenye desktop kwa computer za Mac na Windows katika nia ya kujipanua zaidi. WhatsApp ya kwenye computer itakuwezesha kupiga simu za sauti na video na huduma zingine.Ikianza, hautakuwa na haja tena ya kuscan QR code kujiunganisha na browser yako. Hatua hii itakuwa huduma mbadala wa huduma kama Slack, Messenger au Skype kwa mawasialino yasiyo kuwa ya maandishi.

Tuesday, April 26, 2016

Lucy Kibaki afariki

Aliyekuwa mke wa rais wa zamani nchini Kenya Lucy Kibaki amefariki. Lucy alifariki katika hospitali ya Bupa Cromwell mjini London. Alisafrishwa hadi mjini Landon wiki moja iliopita kwa matibabu

Sunday, April 24, 2016

Lady Jaydee - NdiNdiNdi (Official Music Video)

Icheck video ya wimbo wa Lady Jaydee ‘Ndindindi’ iliyoongozwa na Justin Campos.

Hii ndiyo maana ya wimbo wa Lady Jaydee ‘Ndindindi’

Lady Jaydee ametoa maana ya wimbo wake ‘Ndindindi’ ambalo lilikuwa ni fumbo lililokuwa linawapa majibu mengi yasiyokuwa na uhakika mashabiki wake.

Wimbo wa ‘Ndindindi’ unazidi kufanya kwenye medi mbalimbali na kumrudisha vizuri Jide aka Binti Komando kwenye muziki wa Bongo Fleva baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila ya kuachia wimbo wowote.

Akiongea kwenye kipindi cha FNL, kinachoruka kupitia EATV, Lady Jaydee alisema, “The Ndi mimi ni kitu tori wewe si kitu” lakini pia aliongezea “ili kuleta fleva ya muziki ndiyo nikaiita Ndindindi. Mimi ni kitu na wewe si chochote.”