MICHAKATO

Levis Rocky Ndekeno

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Pages

Monday, May 23, 2016

Siku 200 kwa Rais Magufuli kuiongoza Tanzania

Leo rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli ametimiza siku 200 tangu ameapishwa kuwa rais wa awamu ya tano kuiongoza Tanzania.

Tangu alipoapishwa Novemba 5 kwenye uwanja wa Uhuru na kuanza kazi siku hiyo hiyo aliyoapishwa, rais Magufuli amekutana na changamoto kadhaa zilizofanya uchumi wa nchi usikuwe kwa kasi inayotakiwa.
‘Hapa Kazi Tu’ ndiyo ulikuwa msemo wa rais Magufuli kwenye kampeni zake za kuwania urais lakini baadhi ya watu walidhani hayo yalikuwa ni maneno lakini kwenye utekelezaji wake wa vitendo usingeweza kufanya kazi kutokana na mizizi iliyopandikizwa tangu hapo awali.
Disemba 4 mwaka jana, Magufuli alifanya mkutano na wafanyabiashara na kuwapa siku saba wale wote waliopitisha makontena yao bandarini bila ya kuyalipia kodi ikiwa ni zaidi ya makontena 1300 yalipitishwa bila ya kulipiwa kodi.
Rais Magufuli ameweza kujitahidi kupunguza baadhi ya matumizi yasiyokuwa ya lazima kwa watu wachache na fedha zake kuzipeleka kwenye vitu vya msingi vyenye manufaa kwa wengi.
Hakika serikali ya Magufuli ina safari ndefu ya kupambana mpaka kumaliza awamu ya kwanza ya uongozi wake. “Kuanzisha mahakama ya mafisadi” ndiyo ilikuwa moja ya ahadi ya rais Magufuli aliyoitoa wakati wa kuomba kura kwa wananchi za Urais.
Rais Magufuli akiwa kwenye mapumziko nyumbani kwao, Chato alisema, “kama kule Dar es Salaam kuna mfanyakazi mmoja wa TRA analipwa mishahara hewa ya wafanya kazi 17.” Mpaka sasa agizo la rais kwa Wakuu wa Mikoa limetekelezeka kwa asilimia kubwa na kubaini zaidi ya watumishi hewa 2500 huku bado zoezi la uhakiki likiendelea zaidi.
Watumishi kadhaa mpaka sasa wamekutana na rungu la rais Magufuli na amefanikiwa kuwatumbua kutokana na oparesheni yake ya ‘Tumbua Majipu’ akiwemo aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Shinyanga [Anne Kilango], Waziri wa Mambo ya Ndani [ Charles Kitwanga], Mkurugenzi wa TIC [Juliet Kairuki], na wengine kibao.
Tatizo la sukari kwa sasa ndiyo changamoto kubwa inayokabiliana nayo serikali ya awamu ya tano huku baadhi ya maeneo sukari ikionekana kuuzwa kati ya shilingi 2500 mpaka 4000 kwa kilo moja.
Lakini wiki iliyopita Waziri Mkuu alizungumzia suala hilo bungeni na aliahidi serikali bado inalifanyia kazi tatizo hilo huku tukiendelea kusubiri tani elfu hamsini ambazo serikali imeziagiza nje ili zije kuziba tatizo la sukari lililopo nchini.
Hakuna binadamu aliye mkamilifu, kuna baadhi ya mambo rais Magufuli ameweza kuteleza kama binadamu lakini kwa kiasi kikubwa ameweza kuiongoza safari ya jahazi la Tanzania ipasavyo na kuwaacha midomo wazi wale walioamini kuwa hawezi.

Wednesday, May 18, 2016

Picha: Meli kubwa zaidi duniani yakamilika

Meli kubwa zaidi duniani imekamilika ikiwa na ukubwa wa viwanja vinne vya mpira wa miguu.
Meli hiyo iliyopewa jina la ‘Harmony Of The Seas’ imechukua miezi 32 mpaka kumaliza kutengenezwa. Ina vyumba 2747, mabwawa 23 ya kuogelea, hoteli na bar, sehemu za michezo, viwanja vya helkopta lakini pia ina uwezo wa kuchukua abiria 6780.








 Aidha gharama za kusafiri na meli hiyo ni £900 lakini kuingia mpaka sehemu za starehe inagharimu £2,760 kwa mtu mmoja. Watengenezaji wa meli hiyo wamesema ‘Harmony Of The Seas’ ni meli yao ya 25 kwenye kampuni Royal Caribbean International fleet.

Twitter yafanya mabadiliko makubwa

Mtandao wa kijamii Twitter yafanya mabadiliko makubwa  katika namna inavyohesababu herufi za tweets na hivyo kuwapa watumiaji uhuru wa kuandika ujumbe mrefu zaidi. Hivi karibuni itaacha kuhesabu picha na link kama sehemu ya herufu 140 za kikomo cha ujumbe unaoandikwa. Mabadiliko hayo yanaweza kuanza kuonekana katika wiki mbili zijazo.


Tuesday, May 17, 2016

WhatsApp inajiandaa kuja na huduma ya ‘video call’

WhatsApp inatarajia kuanzisha huduma ya mawasiliano ya video.
Hivi karibuni iliweka version ya majaribio kwa watumiaji wachache lakini imeitoa kwaajili ya kuifanyia marekebisho zaidi.
Video calling kwa WhatsApp imekuwa ikifanyiwa kazi kwa takriban miezi sita sasa ambapo December mwaka jana screenshots za version ya iOS ya app hiyo ilivuja ikionesha huduma hiyo.
Na sasa huduma hiyo iko mbioni kutambulishwa kwa watumiaji wa app hiyo duniani kote. Wikiendi iliyomalizika baadhi ya watumiaji waliripoti kuwa option ya WhatsApp ilipatikana kwenye beta version 2.16.80.

list za juu za nchi zisizokuwa waaminifu Tanzania ikiwepo


Utafiti umefanywa na wanafunzi wa University of Nottingham Uingereza ukihusisha nchi 159, wanafunzi wa chuo kikuu cha Nottingham wamefanya utafiti wa kugundua ni nchi zipi zinaoongoza kwa uaminifu au ukweli duniani, utafiti umefanywa ukihusisha nchi 159 ikiwemo Tanzania.Wanafunzi hao wamefanya tafiti huku wakichanganya na data za 2003 za ukwepaji kodi, rushwa na udanganyifu katika siasa lakini wamegundua kuwa nchi za Lithuania, Uholanzi, Uingereza, Sweden, Ujerumani na Italia zimetajwa katika list ya nchi zinazoongoza kwa uaminifu.Wakati nchi za Tanzania, China, Uturuki, Poland na Morocco zimetajwa kuwa ni miongoni mwa nchi zinazoongoza watu wake kutokuwa waaminifu, utafiti huo unaeleza kuwa watu wanaoishi katika nchi zenye rushwa na siasa za udanganyifu wamekuwa sio waaminifu au wakweli, wakati watu wanaotokea katika nchi ambazo hazina rushwa na ukwepaji kodi ni waaminifu.Tafiti zimefanyika katika chuo kikuu cha Nottingham Uingereza, lakini kimetajwa kufanya majaribio kwa kuhusisha vijana 2,586 wenye wastani wa umri wa miaka 22 kutoka nchi 23 zikiwemo Vietnam, Morocco, China, UK, Hispania, Sweden, Italy na Czech Republic. Utafiti huu umetolewa na dailyamail.co.uk March 11 2016.
IMEANDIKWA : dailymail.co.uk

Thursday, May 12, 2016

Ukata wa Pesa: Walimu walipwa vifaranga badala ya mshahara

Wakati nchini Tanzania walimu wakiomba kuongezewa mishahara, Mji mmoja nchini Uzbekistan umekua ukiwapa waalimu wake kuku kama mshahara badala ya pesa.Mamlaka za mji wa Nukus katika jimbo linalojitawala la Karakalpakstan wamekua wakitia vifaranga wachanga kwa walimu kutokana na uhaba wa pesa nchini humo. Kituo cha radio kinachofadhiliwa na Marekani{Radio Ozodlik} kimemnukuu mwalimu mmoja akilaani hatua hiyo kama aibu kubwa kwa mamlaka. Mwalimu huyo aliyeghadhabishwa na hatua hiyo amesema hataki vifaranga kwa sababu anaweza kuwapata sokoni, lakini wanataka pesa zao. Vifaranga wanaotolewa kama mshahara wana gharama ya dola mbili kila mmoja, ikiwa ni maradufu bei inayouzwa vifaranga sokoni. Mamlaka za Uzbekistan hazikubalii uhuru wa vyombo vya habari na raia wa huko hutegemea vyombo vya habari vya kimataifa kutoa sauti yao, ila hawajitambulishi. Uzbekistan imekumbwa na uhaba wa fedha kwa miaka sasa hali inayosababisha serikali kuchelewesha mishahara ya wafanyikazi na malipo ya uzeeni. Mapema mwezi huu wafanyikazi wa serikali katika mji mkuu,Tashkent walilalamikia kwamba hawakuwa wamelipwa mshahara kwa miezi miwili kwa sababu benki hazikuwa na pesa.

Instagram kuanza kutumia nembo mpya

Instagram imezindua nembo mpya katika hatua ya kutaka kujiboresha na kutoonekana kuwa programu ya picha pekee.Nembo hiyo imetengezwa kuimarisha ujumbe unaotumwa. Nembo hiyo inaonyesha kamera ya kawaida na rangi za upinde wa mvua. Zaidi ya picha milioni 80 na video husambazwa kila siku katika mtandao wa Instagram, mtandao huo una takriban wateja milioni 400 na uliipiku Twitter mwaka 2014. Viongozi wa mtandao wa Instagram waliiambia Newbeat, “Wakati Instagram ilipokuwa inaanza ilikuwa na eneo la kukarabati na kusambaza picha. Miaka mitano baadaye likawa ni eneo linalopendwa na jamii kubwa ulimwenguni ambapo watu husambaza picha na video.” Watumiaji pia watagundua kwamba eneo la bluu katika nembo ya mtandao huo limeanza kubadilika na kuwa jeupe. Mtindo huo mpya una lengo la kuimarisha picha na video zinazotumwa bila kubadilisha unavyoingia katika mtandao huo. Ubunifu wa nembo hiyo mpya ulianza mwaka mmoja uliopita. Aidha walitaka kutengeza nembo ambayo ingewakilisha mahitaji ya awali ya sasa na ya siku za baadaye.