MICHAKATO

Levis Rocky Ndekeno

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Pages

Thursday, January 7, 2016

Watu 14 wauawa shambulio la waasi DR Congo

Watu 14 wameuawa baada ya waasi wa kundi FDLR kushambulia kijiji kimoja mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Ripoti kutoka shirika la habari la AFP na jeshi zinasema shambulizi hilo lilifanyika eneo la Miriki, Kilomita 110 (maili 65) kaskazini mwa mji wa Goma.

Viongozi kadhaa wa waasi wa FDLR wamehusishwa na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 katika nchi jirani ya Rwanda.

Kundi hilo la waasi wa Kihutu limedaiwa kuchochea vita vilivyodumu miongo miwili mashariki mwa DR Congo

Mshukiwa wa ugaidi afungwa miaka 20 Kenya

Mshukiwa wa ugaidi aliyeshtakiwa kuwaingiza watoto katika kundi la al-Shabab amehukumiwa kufungwa jela miaka 20 na mahakama Mombasa.

Samuel Wanjala Wabwire almaarufu Salim Mohammed alishtakiwa kuwapa watoto mafundisho ya itikadi kali.

Alikuwa ameshtakiwa pia kuwa mwanachama wa kundi hilo kutoka Somalia.

Watoto waliotoa ushuhuda kwenye kesi yake wanasema aliwafunza kwamba Wakristo ni makafiri ambao wanafaa kuuawa.

Baadhi ya watoto hao walisilimu.

Bw Wabwire alikuwa mwalimu wa shule ya msingi na pia imam katika Masjid Jihad.

Alikabiliwa pia na shtaka la tatu la kueneza itikadi kali na vita vya kidini. Anadaiwa kutoa mafunzo ya karate msikitini.

Alikamatwa mwezi Juni mwaka 2015 eneo la Kaloleni, jimbo la Kilifi.

‘Watu wengi’ wauawa kituo cha mafunzo Libya

Watu wengi wameuawa baada ya lori lililokuwa limetegwa bomu kulipuka katika kituo cha kuwapa mafunzo maafisa wa polisi katika mji wa Zliten, magharibi mwa Libya.

Mkazi wa Zliten ameambia BBC kwamba kulikuwa na makurutu 400 waliokuwa wakipokea mafunzo katika kituo hicho mlipuko ulipotokea.

Lori hilo lilikuwa la kubeba maji.

Haijabainika iwapo lililipuka langoni ama lililipuka ndani ya kituo hicho.

Meya wa Zliten Miftah Lahmadi anasema watu 40 wamefariki.

Majeruhi kwa sasa wanapelekwa hospitali zilizoko mji mkuu Tripoli kwa sababu hospitali ya Zliten imelemewa na majeruhi.

Shirika la habari la AFP linasema shirika la habari linalotii serikali iliyoko Tripoli linasema idadi ya waliofariki ni zaidi ya 50 na kwamba watu 127 wamejeruhiwa.

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, Martin Kobler, amesema shambulio hilo lilikuwa la kujitoa mhanga

Tanzania kutimua wageni wasio na vibali

Tanzania imeanza rasmi operesheni ya kuwasaka na kuwafurusha raia wa kigeni wanaoishi na kufanya kazi nchini humo kinyume cha sheria.
Naibu waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania Hamad Masauni ameambia wanahabari kwamba operesheni hiyo imeanzishwa baada ya kubainika kwamba kuna raia wengi wa kigeni wanaofanya kazi Tanzania kinyume cha sheria.
Operesheni hiyo hiyo inafanyika siku chache baada ya wizara inayohusika na ajira kumuagiza kamishna wa kazi nchini humo kufuta vibali vya kazi vya muda kwa wageni.
"Serikali haiwezi kukaa kimya wakati vijana wanakosa ajira huku kazi zile walizotakiwa kufanya zikifanywa na raia wa kigeni,” Bw Masauni amenukuliwa na gazeti la Mwananchi.
Afisa wa uhamiaji wa mkoa wa Dar es Salaam John Msumile amesema wanatarajia kuwakamata wageni zaidi ya 350.
Kuhusu vibali va kazi vya muda, Bw Masauni amesema serikali itaandaa utaratibu mwingine wa kushughulikia watu wanaotaka kufanya kazi Tanzania kwa muda.
Hii ni baada ya serikali kupokea malalamiko mengi kuhusu suala hilo.
Mwishoni mwa mwaka waziri katika afisi ya waziri mkuu anayehusika na ajira Jenista Mhagama pamoja na naibu waziri Anthony Mavunde walifanya ziara za kushtukiza katika kampuni mbalimbali.
Waligundua raia kadha wa kigeni waliokuwa wakifanya kazi bila vibali halali.

Irain yasema Saudi Arabia imeshambulia ubalozi

Kituo cha utangazaji cha Iran cha Irinn kimesema makombora yalianguka katika majengo ya ubalozi huo na kusababisha uharibifu.
Wakazi wa Sanaa wanasema kulitokea mashambulio kadha kutoka angani asubuhi, yakitekelezwa na majeshi ya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya waasi wa Houthi.
Uhusiano kati ya nchi hizo mbili umedorora tangu kuuawa kwa mhubiri wa Kishia Sheikh Nimr al-Nimr aliyeshtakiwa makosa yanayohusiana na ugaidi nchini Saudi Arabia.

Iran imesema Saudi Arabia imeshambulia ubalozi wake nchini Yemen kwa makombora.
Kituo cha utangazaji cha Iran cha Irinn kimesema makombora yalianguka katika majengo ya ubalozi huo na kusababisha uharibifu.
Wakazi wa Sanaa wanasema kulitokea mashambulio kadha kutoka angani asubuhi, yakitekelezwa na majeshi ya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya waasi wa Houthi.
Uhusiano kati ya nchi hizo mbili umedorora tangu kuuawa kwa mhubiri wa Kishia Sheikh Nimr al-Nimr aliyeshtakiwa makosa yanayohusiana na ugaidi nchini Saudi Arabia.
Ubalozi wa Saudi Arabia mjini Tehran ulishambuliwa na kuchomwa moto na waandamanaji wakati wa maandamano yaliyotokea maeneo ya Washia kulalamikia mauaji hayo.
Saudi Arabia nayo ilijibu kwa kukatiza uhusiano wa kidiplomasia na Iran, hatua ambayo washirika wake kama vile Bahrain, UAE, Kuwati, Sudan, Somalia na Djibouti walifuata.
Iran na Saudi Arabia zimekuwa zikiunga mkono makundi pinzani katika mizozo inayoendelea nchini Syria na Yemen.

Tazama picha ya kwanza ya filamu mpya ya Lupita Nyong'o "The Queen of Katwe"


picha ya kwanza ya filamu mpya ya muigizaji wa Kenya,Lupita Nyong'o The Queen of Katwe imesambaa mtandaoni. Filamu hiyo imefanywa na kampuni ya Disney. Muigizaji huyo anacheza kama mama wa Madina Nalwanga. Atacheza uhusika mkuu kwenye filamu nyingine iitwayo Americanah

Wafungwa wawili wa Guantanamo wapelekwa Ghana


Wafungwa wawili waliokuwa wakizuiliwa katika gereza la Guantanamo Bay, Cuba, wamehamishiwa Ghana.
Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema idhini ilitolewa kwa Khalid al-Dhuby kuachiliwa huru 2006 na kwa Mahmoud Omar Bin Atef mwaka 2009.
Wawili hao, wanaotoka Yemen, wamezuiliwa kwa zaidi ya mwongo mmoja na hawajawahi kufunguliwa mashtaka.
Ghana imetoa idhini kwa wawili hao kukaa nchini huko kwa miaka miwili, waziri wa mashauri ya kigeni wa Ghana Hanna Tetteh amesema.
Kwa mujibu wa stakabadhi za jeshi la Marekani, Mahmoud Omar Bin Atef ni raia wa Yemen aliyezaliwa Saudi Arabia mwaka 1979 .
Alikamatwa nchini Afghanistan 2001.
Khalid al-Dhuby naye ni mzaliwa wa Saudi Arabia, aliyezaliwa in 1981 na kwenda Afghanistan kupigana.
Taifa hilo la Afrika Magharibi hawalijawahi kuwapokea wafungwa kutoka Guantanamo awali.

Nchi kadha zimewapokea wafungwa wa zamani wa Guantanamo, zikiwemo Uganda na Cape Verde.
Watu 780 walizuiliwa Guantano tangu 2002, lakini kwa sasa ni 105 pekee waliosalia gerezani. Hamsini kati ya hao wameidhinishwa kuachiliwa huru.
Jela hilo ilijengwa na Marekani baada ya amshambulio ya tarehe 11 Septemba mwaka 2001 na hutumiwa na Washington kuwazuilia „wapiganaji maadui”.
Rais Barack Obama amesema anataka kufunga gereza hilo kabla ya kuondoka madarakani mapema 2017.