MICHAKATO

Levis Rocky Ndekeno

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Pages

Monday, January 11, 2016

Myanmar yatafuta muafaka

Serikali ya Myanmar inafanya majadiliano na makundi kadhaa ya kikabila nchi humo ili kupata mwafaka.

Kikao hicho cha siku 5 kinafuatia kutiwa saini hapo October kwa makubaliano ya kusitisha mapigano baina ya serikali na makundi 8 ya wapiganaji.

Waandamana kupinga wahamiaji

Maelfu ya waandamanaji wamefanya mkutano katika mji wa Leipzig Kupinga wahamiaji.

Waandamanaji hao wanaopinga waislamu wanalaumu kuingia kwa wingi kwa wahamiaji kunasababisha ongezeko la udhalilishaji wa kijinsia na ujambazi unaolenga wanawake.

Wamemtolea hasira zao Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ambaye wanamlaumu kwa kile walichoita kuiteketeza nchi yao kwa kuruhusu wahamiaji zaidi ya milioni mwaka uliopita.

Maafisa nchini humo wanasema wengi waliohusika na matukio ya unyanyasaji wa kijinsia wakati wa mkesha wa mwaka mpya asili yao ni wahamiaji

UN wakuta hali mbaya Madaya,Syria


Image caption Magari ya Umoja wa mataifa UN,yakipeleka misaada

Mratibu wa msafara wa kutoa misaada katika mji wa Madaya nchini Syria, Yacoub El Hillo amesema wameowaona watoto wakiwa katika hali mbaya kutokana na kukosa chakula.

El Hillo ameongeza kuwa picha zilizopigwa awali zikionyesha wakazi wa maeneo hayo wakiwa katika hali mbaya kwa kukosa chakula ni za kweli kabisa na ni sawa na kile walichokishuhudia baada ya kufika eneo hilo.

Misaada ya chakula na dawa imepelekwa pia kwenye vijiji viwili kaskazini mwa Syria ambavyo vinaunga mkono Serikali na ambavyo vimeathirika kutokana na mashambulizi dhidi ya waasi.

Naye balozi wa umoja wa mataifa wa Syria Bashar Al Jaafari, amekaririwa akidai kuwa shida katika mji wa madaya imesababishwa na upande wa waasi.

Taarifa kuhusiana na hali ya kibinadamu Madaya ni matokeo ya taarifa za uongo na upuuziaji wa vitendo vibaya vinavyotokea katika maeneo mengine ambayo yanashambuliwa na makundi ya waasi.

Ukweli wa mambo kwa kile kinachoitwa mapigano ni kwamba katika baadhi ya maeneo waasi wanawatumia raia kama kinga yao”

Hata hivyo baadhi ya wanadai pia kuwa waasi wamehifadhi chakula kwaajili ya familia zao na wamekuwa wakiuza ziada ya chakula hicho kwa kiwango kikubwa ambacho ni Zaidi ya dola 400 kwa kilo moja ya mchele.

Serikali ya Syria imekanusha madai ya kwamba inatumia uhaba wa chakula kama moja ya mbinu za kivita

Thursday, January 7, 2016

Watu 14 wauawa shambulio la waasi DR Congo

Watu 14 wameuawa baada ya waasi wa kundi FDLR kushambulia kijiji kimoja mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Ripoti kutoka shirika la habari la AFP na jeshi zinasema shambulizi hilo lilifanyika eneo la Miriki, Kilomita 110 (maili 65) kaskazini mwa mji wa Goma.

Viongozi kadhaa wa waasi wa FDLR wamehusishwa na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 katika nchi jirani ya Rwanda.

Kundi hilo la waasi wa Kihutu limedaiwa kuchochea vita vilivyodumu miongo miwili mashariki mwa DR Congo

Mshukiwa wa ugaidi afungwa miaka 20 Kenya

Mshukiwa wa ugaidi aliyeshtakiwa kuwaingiza watoto katika kundi la al-Shabab amehukumiwa kufungwa jela miaka 20 na mahakama Mombasa.

Samuel Wanjala Wabwire almaarufu Salim Mohammed alishtakiwa kuwapa watoto mafundisho ya itikadi kali.

Alikuwa ameshtakiwa pia kuwa mwanachama wa kundi hilo kutoka Somalia.

Watoto waliotoa ushuhuda kwenye kesi yake wanasema aliwafunza kwamba Wakristo ni makafiri ambao wanafaa kuuawa.

Baadhi ya watoto hao walisilimu.

Bw Wabwire alikuwa mwalimu wa shule ya msingi na pia imam katika Masjid Jihad.

Alikabiliwa pia na shtaka la tatu la kueneza itikadi kali na vita vya kidini. Anadaiwa kutoa mafunzo ya karate msikitini.

Alikamatwa mwezi Juni mwaka 2015 eneo la Kaloleni, jimbo la Kilifi.

‘Watu wengi’ wauawa kituo cha mafunzo Libya

Watu wengi wameuawa baada ya lori lililokuwa limetegwa bomu kulipuka katika kituo cha kuwapa mafunzo maafisa wa polisi katika mji wa Zliten, magharibi mwa Libya.

Mkazi wa Zliten ameambia BBC kwamba kulikuwa na makurutu 400 waliokuwa wakipokea mafunzo katika kituo hicho mlipuko ulipotokea.

Lori hilo lilikuwa la kubeba maji.

Haijabainika iwapo lililipuka langoni ama lililipuka ndani ya kituo hicho.

Meya wa Zliten Miftah Lahmadi anasema watu 40 wamefariki.

Majeruhi kwa sasa wanapelekwa hospitali zilizoko mji mkuu Tripoli kwa sababu hospitali ya Zliten imelemewa na majeruhi.

Shirika la habari la AFP linasema shirika la habari linalotii serikali iliyoko Tripoli linasema idadi ya waliofariki ni zaidi ya 50 na kwamba watu 127 wamejeruhiwa.

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, Martin Kobler, amesema shambulio hilo lilikuwa la kujitoa mhanga

Tanzania kutimua wageni wasio na vibali

Tanzania imeanza rasmi operesheni ya kuwasaka na kuwafurusha raia wa kigeni wanaoishi na kufanya kazi nchini humo kinyume cha sheria.
Naibu waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania Hamad Masauni ameambia wanahabari kwamba operesheni hiyo imeanzishwa baada ya kubainika kwamba kuna raia wengi wa kigeni wanaofanya kazi Tanzania kinyume cha sheria.
Operesheni hiyo hiyo inafanyika siku chache baada ya wizara inayohusika na ajira kumuagiza kamishna wa kazi nchini humo kufuta vibali vya kazi vya muda kwa wageni.
"Serikali haiwezi kukaa kimya wakati vijana wanakosa ajira huku kazi zile walizotakiwa kufanya zikifanywa na raia wa kigeni,” Bw Masauni amenukuliwa na gazeti la Mwananchi.
Afisa wa uhamiaji wa mkoa wa Dar es Salaam John Msumile amesema wanatarajia kuwakamata wageni zaidi ya 350.
Kuhusu vibali va kazi vya muda, Bw Masauni amesema serikali itaandaa utaratibu mwingine wa kushughulikia watu wanaotaka kufanya kazi Tanzania kwa muda.
Hii ni baada ya serikali kupokea malalamiko mengi kuhusu suala hilo.
Mwishoni mwa mwaka waziri katika afisi ya waziri mkuu anayehusika na ajira Jenista Mhagama pamoja na naibu waziri Anthony Mavunde walifanya ziara za kushtukiza katika kampuni mbalimbali.
Waligundua raia kadha wa kigeni waliokuwa wakifanya kazi bila vibali halali.