MICHAKATO

Levis Rocky Ndekeno

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Pages

Tuesday, February 2, 2016

Brazil: Virusi vya Zika havitaathiri Olimpiki


Brazil Serikali ya Brazil imesema Michezo ya Olimpiki, inayotarajiwa kufanyika Agosti mwaka huu, haitaahirishwa kwa sababu ya mlipuko wa virusi vya Zika.
Maafisa wa serikali wamesema hakuna hatari yoyote kwa wanariadha na mashabiki, ila tu kwa wanawake wajawazito.
Awali, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilikuwa limeonya kuwa virusi vya Zika ni hatari kubwa kwa afya ya umma duniani na kutangaza hali ya tahadhari.
Shirika hilo limeyataka mataifa kuungana kuukabili ugonjwa huo.
Virusi hivyo vimehusishwa na kuzaliwa kwa watoto wanaozaliwa wakiwa na vichwa vidogo na ubongo uliodumaa
Wataalamu wameonya kwamba virusi hivyo vinavyoenezwa na mbu vinasambaa sana Amerika Kusini na kusababisha madhara makubwa.
"Lazima tuwafafanulie wale wanaojiandaa kuja Brazil, wanariadha, kwamba hawakabiliwi na hatari yoyote kama wewe si mwanamke mjamzito,” shirika la habari la Reuters limemnukuu msemaji wa Rais Dilma Rousseff, Jaques Wagner.

Rais Rousseff awali alikuwa ameidhinishwa wakaguzi wa afya na usafi kutumia nguvu, ikibidi, kufikia nyumba za watu binafsi, kama sehemu ya juhudi za serikali za kuangamiza maeneo ambayo mbu wanatumia kuzaana, hasa maji yaliyotulia.
Wakaguzi sasa wako huru kuitisha usaidizi wa polisi ikihitajika.
Zaidi ya wanajeshi 200,000 wanatumiwa kusaidia katika ukaguzi huo.
Wizara ya afya nchi humo imesema 25% ya nyumba 49 milioni nchini humo kwa sasa zimekaguliwa.

Ted Cruz amshinda Trump mchujo wa Iowa

Seneta wa Texas Ted Cruz ameshinda mchujo wa uchaguzi wa mgombea wa uchaguzi wa Republican katika jimbo la Iowa, Marekani.
Huo ndio mchujo wa kwanza katika uchaguzi wa urais wa 2016 ambao utafanyika baadaye mwezi Novemba.
Cruz amepata asilimia 28 ya kura.
"Huu ni ushindi wa wahafidhina jasiri," mgombea huyo amesema baada ya kubainika kwa ushindi wake.
Mfanyabiashara Donald Trump alikuwa akiongoza kwenye kura za maoni kabla ya kura kupigwa lakini sasa amekuwa wa pili na asilimia 24.
Seneta wa Florida Marco Rubio amefanya vyema kuliko ilivyotarajiwa, na akamaliza nambari tatu na asilimia 23.
Kura za mchujo wa chama cha Democratic bado zinahesabiwa.
Asilimia 85 ya kura ambazo zimehesabiwa zinaonyesha pengo kati ya Hillary Clinton na mshoshialisti wa chama cha Democratic Bernie Sanders ni 1% pekee.
Akizungumza baada ya matokeo kujulikana, Marco Rubio amempongeza Bw Cruz na kusema ndiye mgombea ambaye anaweza kuunganisha chama cha Republican ambacho kimegawanyika.
Dakika chache baadaye, Bw Trump alipanda jukwaani katika ukumbi mwingine na kumpongeza seneta huyo wa Texas, na kusema anaridhika kumaliza katika nambari mbili.
Wagombea wawili wamejiondoa kinyang’anyironi

Monday, February 1, 2016

Mapacha watenganishwa salama Uswiss

Madaktari nchini Uswiss wanasema kuwa wameweza kuwatenganisha watoto mapacha wa kike wa siku nane waliozaliwa huku viungo vyao vikiwa vimeshikana , wanaoaminiwa kuwa wachanga zaidi kuwahi kutenganishwa.
Mapacha hao , waliozaliwa mwezi Disemba walikua wameungana kwenye maini na kifua.
 Vyombo vya habari vya Uswis vinasema kua mpango wa awali wa madaktari ulikua ni kuwatenganisha baada ya miezi kadhaa, lakini walisogeza mbele tarehe ya upasuaji wao baada ya kila mmoja wao kupata hali inayotishia uhai wao . Imeripotiwa kua mafanikio ya upasuaji huo yalikua ni ya 1% .
Mapacha hao wanaoitwa Lydia and Maya, walizaliwa wiki nane kabla ya muda kamili wa kuzaliwa katika hospitali ya Inselspital katika mji wa Bern, sambamba na mapacha wengine watatu waliozaliwa wakiwa wametengana na wenye afya .
ydia na Maya kwa pamoja walizaliwa wakiwa na uzito wa kilo 2.2 kwa pamoja . Mmoja wao alikua na damu nyingi zaidi , na shinikizo kubwa la damu, huku mwingine akiwa hana damu ya kutosha.
Ilichukua muda wa saa tano kwa Jopo la madaktari 13 waliobobea kukamilisha jitihada za kuwatenganisha mapacha hao mnamo tarehe 10 Disemba.

Wanasayansi waruhusiwa kubadili DNA

Wanasayansi nchini Uingereza wamepewa idhini na idara inayohusika na masuala ya uzazi ya kufanyia viinitete vya binadamu mabadiliko ya kijenetiki.
Wanasayansi hao watafanya utafiti huo katika taasisi ya Francis mjini London.
Utafiti huo una lengo la kutoa uelewa kamili kuhusu siku za kwanza kwanza katika maisha ya binadamu.
Utaanza siku saba za kwanza baada ya kukutana kwa chembe chembe za mme na mke na kuonyesha kile ambacho husababisha mimba kutoka.
Mwaka uliopita wanasayansi nchini China walitangaza kuwa walifanyia mabadiliko ya kijenetiki viini tete vya binadamu kurekebisha hali ambayo husababisha tatizo la damu.
Hatua hiyo imezua maoni tofauti huku baadhi wakisema kuwa kuifayika mabadiliko DNA ni hatua ambayo imeenda mbali zaidi na huenda ikasababisha kuzaliwa watoto waliotengezezwa.

Sunday, January 31, 2016

Marais wapinga kutuma jeshi la AU Burundi

Muungano wa Afrika AU hautatuma kikosi cha walinda amani hadi pale serikali ya rais Pierre Nkurunziza itakapotoa mwaliko.
Msemaji wa Muungano wa Afrika AU, amesema kuwa umoja huo hautatuma majeshi ya kulinda amani nchini humo hadi pale watakapopokea mwaliko kutoka kwa taifa hilo la kanda ya Afrika Mashariki.
Kauli hiyo ni kinyume na pendekezo la awali la umoja huo ambao uliibua taharuki kuhusu uhalali wake na wajibu wake wa kulinda maisha ya wananchi.
Mjumbe maalum wa umoja huo kanda ya maziwa makuu Ibrahima Fall, anasema kuwa haijawahi kuwa nia ya AU kutuma walinda amani, bila ya idhini ya taifa husika.

Mkutano wa viongozi na marais wa Afrika huko Ethiopia ulishindwa kupitisha mswada uliohitajika ilikuwatuma wanajeshi wapatao 5000 kulinda amani nchini Burundi kufuatia mauaji ya mamia ya wapinzani wa rais Nkurunziza.
Machafuko nchini humo yalitibuka baada ya Nkurunziza kutangaza nia ya kuwania uchaguzi katika muhula wake wa tatu.
Wapinzani wake walisema Nkurunziza alikuwa anakiuka katiba ya taifa na kisha maandamano yakaanza kukotokea hata jaribio la mapinduzi ambayo ilizimwa na kisha rais huyo akaibuka mshindi katika uchaguzi ambao ulisusiwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa wa upinzani.

Kulikuwa na pendekezo la kutuma kikosi cha wapiganaji 5,000 wa muungano wa Afrika ilikuokoa maisha ya wapinzani wa rais huyo.
Awali rais Nkurunziza alionya kuwa majeshi yake yangewakabili vikali jeshi hilo ''Vamizi'' akisema kuwa nchi hiyo iko salama na kuwa ni vitongoji vichache tu vya Bujumbura ambavyo ni ngome ya upinzanani.
Kauli ya mwaka jana wa Nkurunziza kuamua kuwania urais kwa muhula wa tatu ilisababisha vurugu nchini humo, ambapo mamia ya watu wameuwawa na wengine wengi wakitorokea mataifa jirani.

Magufuli alaani kuuawa kwa rubani porini

Rais wa Tanzania John Magufuli amesema amesikitishwa sana kitendo cha kuuawa kwa rubani Mwingereza aliyekuwa akisaidiana na maafisa wa Tanzania kupambana na ujangili.

Rubani wa helkopta Kapteni Roger Gower, alifariki baada ya majangili kuifyatulia risasi na kuidondosha helkopta aliyokuwa akiiendesha wakati alipoungana na askari wanyamapori waliokuwa wakikabiliana na majangili katika pori la akiba lililopo katika wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu.

Askari mmoja wa Tanzania alijeruhiwa wakati wa kisa hicho.

Tembo watatu pia walipatikana wakiwa wameuawa.

Dkt Magufuli ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha waliomuua rubani huyo wanakamatwa na wanafikishwa mikononi mwa vyombo vya sheria, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa kurugenzi ya mawasiliano ya ikulu.

Polisi tayari wamewakamata washukiwa watatu kuhusiana na mauaji hayo.

Kiongozi huyo amesema serikali yake itahakikisha inaendeleza mapambano dhidi ya ujangili kwa nguvu zake zote.

Amewataka wananchi na wadau mbalimbali wa hifadhi ya wanyamapori, kutokatishwa tamaa na tukio hilo na wasaidie kuwafichua watu wote wanaojihusisha na ujangili ama biashara ya bidhaa zitokanazo na ujangili.

Hivi karibuni, utawala nchini Tanzania umekuwa ukikosolewa kwa kushindwa kutoa maelezo ya kina kuhusiana na uwindaji haramu wa pembe za ndovu.

Uwindaji haramu umeenea sana katika pori ya Maswa na sio tukio la kwanza ambapo wanaharakati wanaolinda wanyama wa porini wanashambuliwa na wawindaji haramu.

Meli kubwa iliyoinama yazua wasiwasi Ufaransa

Meli ya kubwa iliyoegemea upande mmoja inakaribia kufika katika pwani ya Ufaransa, maafisa wa bahari wanasema, ingawa kuna matumaini ya kuiokoa kabla ya kuzama. Meli hiyo kwa jina Modern Express ambayo, imesajiliwa Panama, ilianza kulala upande mmoja Jumanne baada ya kutokea kwa hitilafu za kimitambo. Mabaharia wote 22 wameondolewa kutoka kwenye meli hiyo.

Juhudi za kuisimamisha zimefeli, lakini maafisa wanasema jaribio jingine litafanywa leo Jumatatu.
Juhudi za leo zikishindikana, basi meli hiyo itagonga pwani ya Ufaransa kati ya Jumatatu usiku na Jumanne asubuhi. Hali mbaya ya hewa ilitatiza juhudi za uokoaji Jumapili. Meli hiyo imebeba tani 3,600 za mbao na mashine kadha za uchimbaji, na imeinama kwa pembe ya kati ya nyuzi 40 na 50. Ina tani 33 za mafuta.