MICHAKATO

Levis Rocky Ndekeno

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Pages

Tuesday, April 12, 2016

Watoto wengi hutumiwa na Boko Haram

Umoja wa mataifa unasema kuwa kutumiwa kwa watoto kama washambuliaji wa kujitoa mhanga na kundi la wanamgambo wa Boko Haram nchini Nigeria, imeongezeka tangu mwaka uliopita.
Shirika la kuhudumia watoto la umoja wa mataifa UNICEF linasema kuwa watoto 44 walitumiwa kufanya mashambulizi kama hayo nchini Cameroon, Chad na Nigeria mwaka uliopita, ikilinganishwa na watoto wanne waliotumiwa mwaka 2014.
Inaripotiwa kuwa washambuliaji watano wa kujitoa mhanga sasa ni watoto huku robo tatu wakiwa na wasichana.
UNICEF inasema kuwa wasichana hao wakati mwingine huleweshwa, kisha hufungwa milipuko kwenye miili yao na kulazimishwa kufanya mashambulizi.

Wanafunzi 62 wafukuzwa chuoni Nairobi

Jumla ya wanafunzi 62 wa chuo kikuu cha Nairobi nchini Kenya wamefukuzwa kutoka chuo hicho, baada ya kushuhudiwa ghasia zilizosababisa kufungwa kwa chuo kwa muda usio julikana wiki moja iliyopita.
Wanafunzi waliteketeza kwa moto afisi za chuo hicho kutokana na kile kinachotajwa kuwa matokeo ya uchaguzi wa kumchagua kiongozi wa wanafunzi chuoni.
Chuo kikuu cha Nairobi kiliseme kuwa kilichukua hatua hizo za kinidhamu dhidi ya wanafunzi walioshiriki katika kuharibu mali ya umma.

Rousseff kupigiwa kura ya kumtoa ofisini

Kamati ya bunge nchini Brazil imeidhinisha hatua ya kumuondoa madarakani Rais Dilma Rousseff, na kutoa fursa ya kupigwa kura baadaye wiki hii kuamua ikiwa ataondolewa ofisini.
Baada ya mjadala mkali, kamati hiyo ilipiga kura kwa asilimia 38 kwa 27 na kupitisha kuondolewa kwake madarakani.
Rais Rossef anakana madai ya kuvuruga akaunti za serikali ili kuficha kudorora kwa uchumi.
Amelaani hatua hiyo na kuitaja kuwa mapinduzi ya kisiaia. Shughuli za Rais zimehujumiwa na uchumi unaozidi kuzorota pamoja na sakata kubwa ya ufisadi inayoikumba kampuni ya mafuta ya serikali Petrobras.

Maji ni machafu mno nchini China

Serikali ya China inasema kuwa zaidi ya asilimia 80 ya maji ya maji ya kina kifupi yaliyo chini ya ardhi ni machafu mno na hata hayaweza kutumiwa kwa kunywa wala kuoga.
Wizara inayoshughulikia maji nchini China ilifanyika uchunguzi wa zaidi ya visima 2000 eneo la mashariki, na kugundua kuwa takriban asilimia 30 ya visima hivyo ndivyo vinaweza kutumiwa kwa kilimo na viwandani.
Karibu asilimia 50 ya sampuli za maji haitatumiwa na binadamu. Maafisa nchini China wameuhakikishia umma kuwa kiwango kikubwa cha maji kinachotumiwa mijini hutokana na kirefu chini ya radhi.

Thursday, February 4, 2016

Upimaji wa ubikira wakosolewa Afrika Kusini

Waziri mmoja wa Afrika Kusini ameshtumu kuwa kinyume cha sheria ufadhili wa elimu ya wasichana wanaopita kipimo cha ubikira.
Mwezi Uliopita,Manispaa ya uthukela katika jimbo la Kwazulu Natal nchini Afrika Kusini ilisema itawapa zawadi wanafunzi 16 wa kike kwa masharti kwamba wasalie mabikira.
''Mpango huo ulilenga kupunguza maambukizi ya virusi vya HIV na mimba za mapema miongoni mwa wasichana'',alisema Meya Dudu Mazibuko.
Katika taarifa ya gazeti la Daily Maverick,waziri wa maendeleo ya kijamii Bathabile Dlamini alielezea upimaji wa ubikira kama usiowezekana,mchafu na ukiukaji mkubwa na haki za kibiniaadamu.
''Kujamiana kwa mara ya kwanza hakutakikani,licha ya hilo kuna unyanyapaa miongoni mwa wasichana ambao hufeli kipimo hicho'',alisema,akiutaja mpango huo kama ''kosa la kingono''.
Bi. Dlamini ,ambaye ni kiongozi wa chama tawala cha ANC upande wa wanawake ndio kiongozi mwenye hadhi ya juu kupinga kipimo hicho.

Wanaotuhumiwa kumvua nguo Mtanzania mbaroni India

Wanaume wanne wanaotuhumiwa kuhusika katika kumshambulia na kumvua nguo mwanafunzi wa kike kutoka Tanzania wamekamatwa, shirika la habari la AP limeripoti.
Waziri wa mashauri ya kigeni wa India Sushma Swaraj, aliandika kwenye Twitter kwamba amezikitishwa sana na “kisa hicho cha aibu” kilichotokea Jumapili eneo la Bangalore.
Bi Swaraj amesema polisi wamewakamata washukiwa wanne ambao watafunguliwa mashtaka.
Wanafunzi Waafrika mjini Bangalore wamesema wanaishi na hofu ya kushambuliwa.
Bw Bosco Kaweesi, mshauri wa kisheria wa Chama cha Wanafunzi kutoka Afrika, anasema wanafunzi wengine watatu wa kike kutoka Tanzania waliokuwa pamoja na mwanafunzi huyo garini pia walipigwa.
Gari lao liliteketezwa.
Kaweesi amesema huenda kisa hicho kilitendeka kimakosa, akisema gari la wanafunzi hao lilikuwa limefuata gari la mwanafunzi kutoka Sudan ambalo lilimgonga na kumuua mwanamke aliyekuwa amelala pembezoni mwa barabara.
Wanafunzi hao hawakumfahamu mwanafunzi huyo wa kiume aliyetoka Sudan, ambaye pia alipigwa na gari lake kuteketezwa.

Trump ataka mchujo wa Iowa urudiwe


Donald Trump anataka uchaguzi wa mchujo wa kuteua atakayegombea urais kupitia chama cha Republican katika jimbo la Iowa urudiwe, akisema mshindi Ted Cruz alitumia ulaghai.
Bw Trump anasema wakati wa kikao cha Iowa, maafisa wa kampeni wa Cruz waliwaambia wapiga kura kwamba mgombea mwingine Ben Carson alikuwa amejitoa kwenye kinyang’anyiro hicho, habari ambazo hazikuwa za kweli.
Maafisa wa kampeni wa Cruz baadaye walimuomba radhi Carson, wakisema lilikuwa kosa lisilokusudiwa.
Bw Trump alimaliza wa pili katika mchujo huo wa kwanza kufanyika nchini humo kwa ajili ya uchaguzi mkuu baadaye mwaka huu.
Mchujo utakaofuata utafanyika New Hampshire Jumanne ijayo.
"Ted Cruz hakushinda Iowa, aliiba. Hii ndiyo maana kura zote za maoni zilionekana kukosea na ndiyo sababi alipata kura nyingi kuliko ilivyotarajiwa. Ni vibaya!,” Bw Trump amesema.
Awali, alikuwa ameandika kwenye Twitter kwamba Bw Cruz alishinda mchujo wa Iowa kwa njia haramu, lakini baadaye akafuta ujumbe huo.
Matamshi ya Bw Trump ni kinyume na hotuba yake ya kukubali kushindwa ambayo aliitoa Jumatatu usiku baada ya matokeo kujulikana, jambo ambalo lilishangaza wengi ikizingatiwa ukali wake.
Kambi ya Cruz haijafurahishwa na madai ya sasa ya Bw Trump.
“Ukweli umemfika nyota huyu wa runingani – alishindwa Iowa na sasa hakuna anayezungumza kuhusu ubabe wake, kwa hivyo anachomoza kwenye Twitter,” afisa wa mawasiliano wa Bw Cruz Rick Tyler aliandikia Politico kupitia barua pepe.
“Kuna makundi yanayosaidia watu kudhibiti uraibu wa kutumia Twitter, labda anafaa kuwasiliana na tawi moja.”
Katika historia, haijatokea uchaguzi wa mchujo ukarudiwa.
Bw Carson alikubali ombi la msamaha kutoka kwa Bw Cruz lakini maafisa wake wa kampeni wamesema kambi ya Cruz ilitumia “mbinu chafu”.
Jumatano, seneta wa Kentucky Rand Paul na seneta wa zamani wa Pennsylvania Rick Santorum walijitoa kwenye kinyang’anyiro cha kutafuta tiketi ya chama cha Republican baada ya kutofanya vyema Iowa.