MICHAKATO

Levis Rocky Ndekeno

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Pages

Tuesday, May 17, 2016

WhatsApp inajiandaa kuja na huduma ya ‘video call’

WhatsApp inatarajia kuanzisha huduma ya mawasiliano ya video.
Hivi karibuni iliweka version ya majaribio kwa watumiaji wachache lakini imeitoa kwaajili ya kuifanyia marekebisho zaidi.
Video calling kwa WhatsApp imekuwa ikifanyiwa kazi kwa takriban miezi sita sasa ambapo December mwaka jana screenshots za version ya iOS ya app hiyo ilivuja ikionesha huduma hiyo.
Na sasa huduma hiyo iko mbioni kutambulishwa kwa watumiaji wa app hiyo duniani kote. Wikiendi iliyomalizika baadhi ya watumiaji waliripoti kuwa option ya WhatsApp ilipatikana kwenye beta version 2.16.80.

list za juu za nchi zisizokuwa waaminifu Tanzania ikiwepo


Utafiti umefanywa na wanafunzi wa University of Nottingham Uingereza ukihusisha nchi 159, wanafunzi wa chuo kikuu cha Nottingham wamefanya utafiti wa kugundua ni nchi zipi zinaoongoza kwa uaminifu au ukweli duniani, utafiti umefanywa ukihusisha nchi 159 ikiwemo Tanzania.Wanafunzi hao wamefanya tafiti huku wakichanganya na data za 2003 za ukwepaji kodi, rushwa na udanganyifu katika siasa lakini wamegundua kuwa nchi za Lithuania, Uholanzi, Uingereza, Sweden, Ujerumani na Italia zimetajwa katika list ya nchi zinazoongoza kwa uaminifu.Wakati nchi za Tanzania, China, Uturuki, Poland na Morocco zimetajwa kuwa ni miongoni mwa nchi zinazoongoza watu wake kutokuwa waaminifu, utafiti huo unaeleza kuwa watu wanaoishi katika nchi zenye rushwa na siasa za udanganyifu wamekuwa sio waaminifu au wakweli, wakati watu wanaotokea katika nchi ambazo hazina rushwa na ukwepaji kodi ni waaminifu.Tafiti zimefanyika katika chuo kikuu cha Nottingham Uingereza, lakini kimetajwa kufanya majaribio kwa kuhusisha vijana 2,586 wenye wastani wa umri wa miaka 22 kutoka nchi 23 zikiwemo Vietnam, Morocco, China, UK, Hispania, Sweden, Italy na Czech Republic. Utafiti huu umetolewa na dailyamail.co.uk March 11 2016.
IMEANDIKWA : dailymail.co.uk

Thursday, May 12, 2016

Ukata wa Pesa: Walimu walipwa vifaranga badala ya mshahara

Wakati nchini Tanzania walimu wakiomba kuongezewa mishahara, Mji mmoja nchini Uzbekistan umekua ukiwapa waalimu wake kuku kama mshahara badala ya pesa.Mamlaka za mji wa Nukus katika jimbo linalojitawala la Karakalpakstan wamekua wakitia vifaranga wachanga kwa walimu kutokana na uhaba wa pesa nchini humo. Kituo cha radio kinachofadhiliwa na Marekani{Radio Ozodlik} kimemnukuu mwalimu mmoja akilaani hatua hiyo kama aibu kubwa kwa mamlaka. Mwalimu huyo aliyeghadhabishwa na hatua hiyo amesema hataki vifaranga kwa sababu anaweza kuwapata sokoni, lakini wanataka pesa zao. Vifaranga wanaotolewa kama mshahara wana gharama ya dola mbili kila mmoja, ikiwa ni maradufu bei inayouzwa vifaranga sokoni. Mamlaka za Uzbekistan hazikubalii uhuru wa vyombo vya habari na raia wa huko hutegemea vyombo vya habari vya kimataifa kutoa sauti yao, ila hawajitambulishi. Uzbekistan imekumbwa na uhaba wa fedha kwa miaka sasa hali inayosababisha serikali kuchelewesha mishahara ya wafanyikazi na malipo ya uzeeni. Mapema mwezi huu wafanyikazi wa serikali katika mji mkuu,Tashkent walilalamikia kwamba hawakuwa wamelipwa mshahara kwa miezi miwili kwa sababu benki hazikuwa na pesa.

Instagram kuanza kutumia nembo mpya

Instagram imezindua nembo mpya katika hatua ya kutaka kujiboresha na kutoonekana kuwa programu ya picha pekee.Nembo hiyo imetengezwa kuimarisha ujumbe unaotumwa. Nembo hiyo inaonyesha kamera ya kawaida na rangi za upinde wa mvua. Zaidi ya picha milioni 80 na video husambazwa kila siku katika mtandao wa Instagram, mtandao huo una takriban wateja milioni 400 na uliipiku Twitter mwaka 2014. Viongozi wa mtandao wa Instagram waliiambia Newbeat, “Wakati Instagram ilipokuwa inaanza ilikuwa na eneo la kukarabati na kusambaza picha. Miaka mitano baadaye likawa ni eneo linalopendwa na jamii kubwa ulimwenguni ambapo watu husambaza picha na video.” Watumiaji pia watagundua kwamba eneo la bluu katika nembo ya mtandao huo limeanza kubadilika na kuwa jeupe. Mtindo huo mpya una lengo la kuimarisha picha na video zinazotumwa bila kubadilisha unavyoingia katika mtandao huo. Ubunifu wa nembo hiyo mpya ulianza mwaka mmoja uliopita. Aidha walitaka kutengeza nembo ambayo ingewakilisha mahitaji ya awali ya sasa na ya siku za baadaye.

Monday, May 9, 2016

Lady Jaydee kuwasha moto kwenye ‘Naamka Tena Concert’ May 20

Kwenye tamasha hilo litakalofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City, Jaydee atatumbuiza pamoja na bendi yake.
Hiyo itakuwa ni show yake kubwa zaidi tangia atumbuize June 2013 kwenye show ya kihistoria ya miaka 13 kwenye muziki kipindi ametoa album yake ‘Nothing But The Truth.’
Hivi karibuni Jaydee aliachia kazi mpya inayotamba kwa sasa, Ndindindi ambayo itakapatikana kwenye album yake mpya, Woman.

Gadner G Habash kwa hili umeteleza kaka

Huwa nakuwa mzito sana kumshauri mtu anayenizidi umri, uwezo, status na tena ninayemchukulia kama moja wa role models wangu. Pale ambapo nitahitajika kufanya hivyo kutokana na uzito wa jambo lenyewe, huamua kutumia keyboard ya computer kuyasema yale ambayo naamini kwa uelewa wangu yanaweza kumjenga pia lakini nikiyasema kwa staha ya hali ya juu.
Gadner G Habash ni miongoni mwa watangazaji wa redio ninaowaheshimu katika muda wote. Si tu kwasababu ni mtangazaji mkongwe, bali pia ni mtangazaji mwenye sauti ya pekee hewani na mwenye busara inayoweza kuhamisha milima. Anapokuwa anaongea jambo, mamlaka anayoyaweka kwenye sauti, hukufanya kila neno limtokalo mdomoni likuingie vyema masikioni.

Na kwa hakika tangu aachane na mke wake, Lady Jaydee, amekuwa akijibu maswali yanayowahusu kwa werevu mkubwa. Miongoni mwa interview yake iliyonivutia sana ni ile aliyofanya na Zamaradi Mketema kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV.
“Siwezi kusema najuta kwamba [Jaydee] alitokea kwenye maisha yangu na siwezi kusema kwamba najuta tuliachana. Lakini ninachoweza kusema tu kwamba kwa suala la Jaydee ni suala ambalo nilichagua sana lisiwe ni jambo ambalo nalizungumzia au kulitolea comment kwasababu yule ni public figure unaposema kitu kuhusu yeye tafsiri zinakuwa ni tofauti na vile unavyotarajia,” alisema Gardiner.
“Kwahiyo sina majuto yoyote, na sina aina yoyote ya chuki au uadui na nategemea hata yeye atakuwa anafeel the same,” alisisitiza.
Pia nilipenda majibu yake ya maswali kuwa Ndindindi ni wimbo alioandikiwa na ex wake huyo.
Hadi hapo niliendelea kuamini kuwa mtangazaji huyo ameufunga ukurasa wake na Lady Jaydee kwa amani na kila mmoja ameangalia hamsini zake, maisha yanaendelea. Sishangai kabisa kama ukweli halisi ni kwamba wawili hao wanachukiana baada ya kuachana kwasababu ni kitu cha kawaida. Na mara nyingi chuki huwa kubwa pale pendo linapochanganyikana na chuki na hasira ya kutendwa au kwasababu yoyote ile inayomfanya mmoja wapo kukatisha uhusiano kwa kosa la mwingine.
Lakini nashangaa sana kwa mtu smart kama Gardiner kutamka maneno ya kumdhalilisha ex wake mbele ya kadamnasi. Kuna video imesambaa na naamini itakuwa viral sana wiki hii inayomuonesha mtangazaji huyo akiwa jukwaani kama mshereheshaji wa tukio moja jijini Dar es Salaam akiongea maneno makali kumhusu ex wake ambaye licha ya kutomtaja inajulikana wazi alikuwa anamuongelea nani.
“My name is Captain Gardiner G Habash all the way from Clouds FM, Jahazi hatari sana,” anasikika akisema kwenye kipande hicho cha video. “Na sina neno na yule mtoto wa kike. Nimeshamkojoza kwa miaka kama 15 hivi,” anasema Gardiner na kisha Dj anaucheza wimbo wa Lady Jaydee, Ndindindi. Mtangazaji huyo anaonekana kuucheza pia wimbo huo jukwaani huku watu wakimshangilia.
Nimependa ujasiri wa Gardiner katika kulisema jambo hilo na kudhihirisha kwa mara nyingine tena kuwa hana tatizo na ex wake lakini sijapendezwa na uchaguzi wake wa maneno. Kimsingi ni clip ambayo kwa namna nyingi inamdhalilisha ex wake lakini pia inamuondolea Captain ile busara ambayo najua anayo.
Sijachachagua kuiweka clip hiyo hapa kutokana na kilichosemwa lakini ningemshauri kaka yangu Gardiner kuendelea kusimamia busara yake aliyonayo siku zote na kujiepusha na kauli tata kama hizi ambazo mara nyingi huwa zina madhara kwenye brand. Video hiyo haijamdhilisha Jide tu bali wanawake wote ambao kwa hakika kwa kauli yake inawaelezea kama ni vyombo vya starehe tu.
Na utashangaa jinsi ambavyo video fupi kama ile ikaondoa heshima ya Gardiner aliyoitengeneza kwa muda mfupi. Matusi anayotukanwa sasa kwenye ukurasa wake wa Instaram yanatoa jibu la ni kwa kiasi gani watu hawajapendezwa na kauli zake. Pia ni kauli mbaya katika kipindi hiki ambacho amerejea kwa kasi Clouds FM kukalia kiti chake kilichoshindikana kukaliwa na watangazaji wengi.
Bahati nzuri binadamu husahau mapema, yataisha tu lakini ni vyema Captain akawa mwangalifu na kauli zake katika siku za usoni sababu ‘kile kinachotokea au kusemwa kwenye starehe hakibaki hapo tu.’

Nauli za Mabasi yaendayo haraka ziko hapa, siku mbili bure

Baada ya Kampuni ya UDA-RT kuwasilisha maombi ya nauli zitakazotumika kwa mabasi yaendayo haraka kwa Mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) May 09 206 SUMATRA imetangaza nauli hizo.
SUMATRA imesema kuwa njia ya pembezoni (Freeder Route) nauli ya mtu mzima ni 400 na mwanafunzi 200 na njia kuu (Trunk Route) ni 650 na mwanafunzi 200 na kwa abiria atakayetumia kusafiri njia kuu (Freeder Route) na kuendelea na safari kwa njia ya pembezoni nauli yake itakuwa ni 800 na mwanafunzi 200. 
Huduma hiyo itatolewa kuanzia kesho bure kwa wananchi kwa siku mbili na May 12 2016 zitaanza kutozwa nauli zilizotajwa.
Msimamizi wa mradi kutoka DART, Eng Ronald Lwakatare amesema>>>‘Wakati huo tunafanya majaribio tutakuwa tunaangalia mfumo unavyofanya kazi kwa hiyo tutawabeba abiria kwa siku kadhaa bila kulipa nauli’