MICHAKATO

Levis Rocky Ndekeno

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Pages

Thursday, April 6, 2017

Jifunze haya toka kwa Bilionea aliyekataliwa mara nyingi zaidi

Tujifunze kutoka kwa ‘Ma Yun’ maarufu kwenye ulimwengu wa biashara ya mtandao kama Jack Ma. Bilionea kutoka China mwanzilishi na mwenyekiti mtendaji wa Alibaba Group, moja ya familia ya biashara ya mtandao iliyofanikiwa zaidi duniani
Jack Ma ni mtu wa kwanza kutoka China (Mainland China) kuonekana kwenye kurasa ya mbele ya jarida maarufu la Forbes. Mwaka 2014 dunia ilishuhudia IPO (Initial Public Offering- kuuzwa kwa mara ya kwanza kwa hisa za kampuni kwenye soko la hisa) kubwa zaidi kuwahi kutokea duniani kwenye soko la hisa la Newyork, na kuifanya Alibaba group kuweka rekodi kama world’s biggest public stock offering.
Pamoja na kupingwa mara kwa mara kuwa Alibaba hawaweki nguvu ya kutosha katika kuzuia udanganyifu wa mauzo kwenye mtandao wa Alibaba, Ma bado anaipeleka Alibaba kwenye mauzo ya hali ya juu na mafanikio makubwa. Rekodi ya shughuli za kibiashara zipatazo $463 bilioni zilifanyika kupitia mtandao wa Alibaba mpaka mwezi machi 2016.
Kampuni ya Alibaba imeweka malengo ya kutengeneza biashara zenye faida milioni 10 na si chini ya ajira milioni 100 kwa miaka 20 ijayo.
Mafanikio sio ajali. Haikumchukua Jack Ma usiku mmoja kufikia hatua hii kubwa na inayoshangiliwa kila kona ya dunia. Ilimgharimu mapambano na kukataliwa mara kadhaa lakini alisonga mbele.
Ma alianza kujifunza Kiingereza katika umri mdogo na kwa bidii ya hali ya juu, na hapo ndipo alipopata jina la “Jack” baada ya rafiki wa kigeni kushindwa kutamka jina lake la kichina. Akiwa kijana mdogo, Ma alihangaika kuingia chuo kikuu. Mitihani ya kujiunga na chuo kikuu hufanyika mara moja kila mwaka nchini China na ilimchukua Jack Ma miaka minne kufanikiwa, akajiunga kusoma digrii ya kiingereza-B.A in English (Jinsi gani Ma alipenda kiingereza).
Baada ya kumaliza chuo Jack ma aliomba kazi 30 tofauti bila mafanikio, zote alikataliwa. “Niliomba kazi ya upolisi; wakasema ‘wewe sio mzuri kwa kazi hii” Ma alimwambia mwanahabari Charlie Rose. KFC walivyoenda kwa mara ya kwanza kuanzisha biashara kwenye mji anaotoka Ma, Watu 24 waliomba kazi, 23 walifanikiwa kupata kazi. Alikuwa ni Jack Ma peke yake ambaye alikosa kazi hiyo. Lakini pia Ma aliomba kujiunga na chuo kikuu cha Harvard mara kumi na mara zote alikataliwa.
Maisha ya Jack ma ni ushahidi mwingine mkubwa wa bilionea aliyekutana na vikwazo na kukataliwa mara nyingi zaidi, lakini hakukata tamaa. Moja ya misimamo mikuu katika maisha yake ni kuzoea kukataliwa (Get used to rejection) na kuendelea kuifanya ndoto yako iishi (Keep your dream alive). May 2015 kwenye kituo cha televisheni cha KBS cha nchini Korea ya kusini, Ma alizungumza na vijana na wajasiriamali wadogo na kuwapa maneno yenye nguvu kubwa mno kwenye maisha yao , alisema ; Usiogope kila kosa unalofanya ni kipato kwako, kabla ya miaka 20 kuwa mwanafunzi mzuri, jifunze kwa nguvu. Kabla ya miaka 30 kuwa mfuasi wa mtu mwenye mafanikio, mwenye uzoefu na anayefanya vizuri kwenye maisha yake, nenda kwenye kampuni ndogo ndogo, mara nyingi kwenye kampuni kubwa ni kama unakuwa part of the big machines. Lakini ukienda kwenye kampuni ndogo ndogo unajifunza kuwa na shauku, unajifunza kuhusu ndoto zako. Unajifunza kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja. Kitu muhimu kabla ya miaka 30 sio kampuni gani uliyofanyia kazi, lakini ni bosi wa aina gani umekuwa chini yake. Hii ni muhimu sana, kwasababu kila bosi anakufundisha tofauti.
Ukiwa chini ya miaka 40 unahitaji kuchukua muda wako na kujiuliza kwa makini sana, kama unataka kufanya kazi kwaajili yako na kama kweli unataka kuwa mjasiriamali. Miaka 40 mpaka 50 hakikisha unafanya vitu ambavyo una uwezo navyo na unavijua zaidi, sio muda wa kujaribu tena. Weka malengo na maisha yako, kama Mungu atakupa uhai ukafika miaka 60 wekeza kwa vijana, fanya kazi na vijana kwasababu wao wana nguvu kuliko wewe, wanafikiri vizuri kuliko wewe. Ukiwa ndani ya miaka ya ishirini fanya makosa mengi, fanya makosa kadri ya uwezo wako kwa lengo la kujifunza zaidi.
Haijalishi ni mara ngapi umejaribu ukashindwa na kukataliwa, usiache kusonga mbele, unahitaji kufanikiwa mara moja tu kwenye maisha yako. Unahitaji kutengeneza uvumilivu mkubwa na hali ya kutokukatisha mambo yako (Procrastination). Jifunze zaidi katika umri mdogo kuliko kufikiria kulipwa pesa nyingi tu, work to learn and money will follow you. Tembea na ndoto zako popote uendako na uzifanyie kazi kila siku bila kuchoka wala kukata tama mpaka pale ushindi wako utakapotengeneza historia kama Jack Ma na Alibaba.

Monday, April 3, 2017

nchi 12 duniani zenye wafanyakazi wengi wa kike wenye elimu kubwa

Wanaharakati mbalimbali wa Haki za Wanawake duniani wanapambana kuhakikishaWanawake wanakuwa katika nafasi nzuri kazini, shuleni na popote inapowezekana ili kuwainua kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutamaduni.
April 2, 2017 nimekutana na stori hii  ambayo inahusu nchi zenye wafanyakazi wengi wa kike wenye kiwango cha juu zaidi cha elimu duniani ambapo Canada ikitajwa kuwa kinara kwa kuwa na wafanyakazi wa kike wenye elimu kubwa zaidi duniani.
Hizi hapa nchi 12 ambazo zina wafanyakazi wa kike wenye elimu kubwa zaidi duniani.
NafasiNchi% ya wafanyakazi wa kike wenye elimu kubwa
1Canada58%
2Cyprus50%
3Estonia50%
4Ireland49%
5Ubelgiji48%
6Luxembourg48%
7Lithuania47%
8Finland47%
9Norway47%
10Sweden44%
11Uingereza43%
12Uhispania42%

Thursday, March 23, 2017

Ijue haki yako unapokamatwa na polisi

1. Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho ni haki yako.
2. Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.
3. Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.
4. Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya kukamatwa.
5. Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.
6. Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kukri amri halali.
7. Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.
8. Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.
9. Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.
10. Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.
11. Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.
12. Ni haki yako kumpekua askari kabla hajakupekua ili asipandikize kitu.
13. Usipekuliwa nyumbani bila kuwapo kiongozi wa mtaa.
14. Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.
15. Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki salama.
16. Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.
17. Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.
18. Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.
19. Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.
20. Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.
21. Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.
22. Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo chini ya ulinzi.
                                       HIZI ZOTE NI HAKI ZAKO, ZILAZIMISHE USIBEMBELEZE WALA USIZIOMBE.

Monday, May 23, 2016

Siku 200 kwa Rais Magufuli kuiongoza Tanzania

Leo rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli ametimiza siku 200 tangu ameapishwa kuwa rais wa awamu ya tano kuiongoza Tanzania.

Tangu alipoapishwa Novemba 5 kwenye uwanja wa Uhuru na kuanza kazi siku hiyo hiyo aliyoapishwa, rais Magufuli amekutana na changamoto kadhaa zilizofanya uchumi wa nchi usikuwe kwa kasi inayotakiwa.
‘Hapa Kazi Tu’ ndiyo ulikuwa msemo wa rais Magufuli kwenye kampeni zake za kuwania urais lakini baadhi ya watu walidhani hayo yalikuwa ni maneno lakini kwenye utekelezaji wake wa vitendo usingeweza kufanya kazi kutokana na mizizi iliyopandikizwa tangu hapo awali.
Disemba 4 mwaka jana, Magufuli alifanya mkutano na wafanyabiashara na kuwapa siku saba wale wote waliopitisha makontena yao bandarini bila ya kuyalipia kodi ikiwa ni zaidi ya makontena 1300 yalipitishwa bila ya kulipiwa kodi.
Rais Magufuli ameweza kujitahidi kupunguza baadhi ya matumizi yasiyokuwa ya lazima kwa watu wachache na fedha zake kuzipeleka kwenye vitu vya msingi vyenye manufaa kwa wengi.
Hakika serikali ya Magufuli ina safari ndefu ya kupambana mpaka kumaliza awamu ya kwanza ya uongozi wake. “Kuanzisha mahakama ya mafisadi” ndiyo ilikuwa moja ya ahadi ya rais Magufuli aliyoitoa wakati wa kuomba kura kwa wananchi za Urais.
Rais Magufuli akiwa kwenye mapumziko nyumbani kwao, Chato alisema, “kama kule Dar es Salaam kuna mfanyakazi mmoja wa TRA analipwa mishahara hewa ya wafanya kazi 17.” Mpaka sasa agizo la rais kwa Wakuu wa Mikoa limetekelezeka kwa asilimia kubwa na kubaini zaidi ya watumishi hewa 2500 huku bado zoezi la uhakiki likiendelea zaidi.
Watumishi kadhaa mpaka sasa wamekutana na rungu la rais Magufuli na amefanikiwa kuwatumbua kutokana na oparesheni yake ya ‘Tumbua Majipu’ akiwemo aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Shinyanga [Anne Kilango], Waziri wa Mambo ya Ndani [ Charles Kitwanga], Mkurugenzi wa TIC [Juliet Kairuki], na wengine kibao.
Tatizo la sukari kwa sasa ndiyo changamoto kubwa inayokabiliana nayo serikali ya awamu ya tano huku baadhi ya maeneo sukari ikionekana kuuzwa kati ya shilingi 2500 mpaka 4000 kwa kilo moja.
Lakini wiki iliyopita Waziri Mkuu alizungumzia suala hilo bungeni na aliahidi serikali bado inalifanyia kazi tatizo hilo huku tukiendelea kusubiri tani elfu hamsini ambazo serikali imeziagiza nje ili zije kuziba tatizo la sukari lililopo nchini.
Hakuna binadamu aliye mkamilifu, kuna baadhi ya mambo rais Magufuli ameweza kuteleza kama binadamu lakini kwa kiasi kikubwa ameweza kuiongoza safari ya jahazi la Tanzania ipasavyo na kuwaacha midomo wazi wale walioamini kuwa hawezi.

Wednesday, May 18, 2016

Picha: Meli kubwa zaidi duniani yakamilika

Meli kubwa zaidi duniani imekamilika ikiwa na ukubwa wa viwanja vinne vya mpira wa miguu.
Meli hiyo iliyopewa jina la ‘Harmony Of The Seas’ imechukua miezi 32 mpaka kumaliza kutengenezwa. Ina vyumba 2747, mabwawa 23 ya kuogelea, hoteli na bar, sehemu za michezo, viwanja vya helkopta lakini pia ina uwezo wa kuchukua abiria 6780.








 Aidha gharama za kusafiri na meli hiyo ni £900 lakini kuingia mpaka sehemu za starehe inagharimu £2,760 kwa mtu mmoja. Watengenezaji wa meli hiyo wamesema ‘Harmony Of The Seas’ ni meli yao ya 25 kwenye kampuni Royal Caribbean International fleet.

Twitter yafanya mabadiliko makubwa

Mtandao wa kijamii Twitter yafanya mabadiliko makubwa  katika namna inavyohesababu herufi za tweets na hivyo kuwapa watumiaji uhuru wa kuandika ujumbe mrefu zaidi. Hivi karibuni itaacha kuhesabu picha na link kama sehemu ya herufu 140 za kikomo cha ujumbe unaoandikwa. Mabadiliko hayo yanaweza kuanza kuonekana katika wiki mbili zijazo.


Tuesday, May 17, 2016

WhatsApp inajiandaa kuja na huduma ya ‘video call’

WhatsApp inatarajia kuanzisha huduma ya mawasiliano ya video.
Hivi karibuni iliweka version ya majaribio kwa watumiaji wachache lakini imeitoa kwaajili ya kuifanyia marekebisho zaidi.
Video calling kwa WhatsApp imekuwa ikifanyiwa kazi kwa takriban miezi sita sasa ambapo December mwaka jana screenshots za version ya iOS ya app hiyo ilivuja ikionesha huduma hiyo.
Na sasa huduma hiyo iko mbioni kutambulishwa kwa watumiaji wa app hiyo duniani kote. Wikiendi iliyomalizika baadhi ya watumiaji waliripoti kuwa option ya WhatsApp ilipatikana kwenye beta version 2.16.80.