KAULI YA NAPE
Nape
alipoulizwa na NIPASHE jana iwapo rasimu ya pili ya katiba mpya itapendekeza
muundo wa Muungano wa serikali tatu CCM itachukua hatua gani, alijibu: “Kwanini
tubashiri? Si usubiri kesho (leo) itokee.” Tume ya Mabadiliko ya Katiba yenye
wajumbe 30; wakiwamo 15 kutoka Tanzania Bara na 15 kutoka Zanzibar, ilitangazwa
na Rais Kikwete, Aprili 6 na kuapishwa Aprili 13, mwaka jana. Ilianza rasmi
kazi ya kukusanya maoni ya wananchi Mei mosi, mwaka jana. Baada ya kukamilisha
kazi hiyo, iliyachambua na kuandika Rasimu ya Katiba. Kazi ya kukusanya maoni
hayo iliwahusisha wananchi mmoja mmoja kupitia mikutano ya hadhara na ilikamilishwa
na Tume Desemba, mwaka jana. Baadaye Tume ilikutana na makundi maalumu na watu
mashuhuri, wakiwamo viongozi wakuu wastaafu na waliopo madarakani Januari 7-28,
mwaka huu. Baadaye, mabaraza ya katiba yaliipitia Rasimu ya Katiba kuanzia
Julai 12 hadi Septemba 2, mwaka huu na kutoa mapendekezo yake, ambayo
yaliwasilishwa kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Tume iliendelea kuyachambua
kabla ya kukabidhi rasimu ya pili ya katiba kwa Rais Kikwete na Rais Dk. Shein
leo. Baada ya rasimu ya pili ya katiba mpya kukabidhiwa kwa marais hao,
itachapishwa katika Gazeti la Serikali na kwenye magazeti mengine ndani ya siku
31. Katika kipindi hicho, Rais ataitisha kikao cha Bunge Maalumu la Katiba kwa
ajili ya kupitisha rasimu ya pili ya katiba mpya iliyopendekezwa. Bunge Maalumu
la Katiba, ambalo litafanyika kwa siku zisizozidi 70, linatarajiwa kuanza rasmi
Februari, mwakani, kwa ajili ya kujadili na kuipitisha rasimu ya pili ya katiba
iliyopendekezwa. Baada ya rasimu ya pili kupitishwa na Bunge Maalumu la Katiba,
itaitishwa kura ya maoni, ambayo itatoa fursa kwa wananchi kuamua ama kuikubali
au kuikataa.
Jaji Joseph
Warioba.
Ni rasimu ya
pili mfumo wa Muungano.
Nape: Tusubiri
tuone kitakachotokea
. Tume ya
Mabadiliko ya Katiba leo itakabidhi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. Jakaya
Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, rasimu ya pili na ya
mwisho ya katiba mpya, huku Watanzania wengi wakisubiri kwa hamu kubwa kuona
inapendekeza muundo gani wa Muungano baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukataa
serikali tatu.
Kwa mujibu
wa Katibu wa Tume hiyo, Assaa Rashidi, hafla ya kukabidhi rasimu ya pili
itafanyika katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam. Hatua hiyo
inachukuliwa na Tume hiyo inayoongozwa na Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph
Warioba, baada ya kupitia na kuchambua maboresho yaliyofanywa na mabaraza ya
katiba ya wilaya ngazi ya kata kwenye rasimu ya kwanza ya katiba mpya miezi saba
iliyopita. Rasimu ya kwanza ya katiba mpya, ambayo ilijadiliwa na mabaraza ya
katiba, kuanzia Julai 12 mpaka Septemba 2, ilizinduliwa na Makamu wa Rais, Dk.
Mohammed Gharib Bilal, Juni 4, mwaka huu Mambo makubwa yaliyopendekezwa kwenye
rasimu ya kwanza ya katiba mpya ni pamoja na mfumo wa Muungano wa serikali
tatu. Mengine ni kuruhusiwa mgombea binafsi, rais kutangazwa kushinda akipata
zaidi ya asilimia 50 ya kura zote zilizopigwa la sivyo uchaguzi urudiwe kwa
wagombea wawili wa nafasi hiyo walioongoza kwa kura. Mependekezo mengine
yaliyopendekezwa ni tume huru ya uchaguzi, mawaziri kutokuwa wabunge, idadi ya
mawaziri kutozidi 15 na spika wa bunge kutokuwa mbunge. Pamoja na yote hayo,
jambo kubwa lililopendekezwa na rasimu ya kwanza lililoishughulisha CCM ni
mfumo wa Muungano wa serikali tatu. Hali hiyo ilikifanya chama hicho Juni 10,
mwaka huu, kutoa mwongozo kwa wanachama wake kuhusu rasimu ya kwanza ya katiba
mpya, kikipinga mambo mengi yaliyomo ndani yake. Kwa mujibu wa mwongozo huo ni
kama vile CCM ilitaka kuendelea na katiba iliyopo, kwa kuwa inaunga mkono mambo
mengi ya katiba hiyo na kupinga yaliyopendekezwa kwenye rasimu ya kwanza ya
katiba mpya. Mwongozo huo ulitolewa baraka za kikao cha Kamati Kuu (CC) ya
Halmashauri Kuu (Nec) ya CCM, kilichofanyika mjini Dodoma, ikiwa ni siku saba
tangu Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutoa rasimu ya kwanza ya katiba mpya. Katika
mwongozo huo CCM iliichambua Ibara ya 57-66 ya rasimu ya katiba ya kwanza
inayoeleza kuwapo kwa mfumo wa serikali tatu, ambao utakuwa wa shirikisho
linaloundwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Tanzania Bara. Sura hiyo pia inaeleza kuwa shughuli
za Serikali ya Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kusimamiwa na Serikali ya
Jamhuri ya Muungano, Bunge la Jamhuri ya Muungano na Mahakama ya Jamhuri ya
Muungano. Katika mwongozo huo, CCM ilieleza kuwa pendekezo hilo ni tofauti na
sera yake kuhusu muundo wa Muungano wenye serikali mbili, ambazo ni Serikali ya
Jamhuri ya Muungano na SMZ. Mbali na kutoa mwongozo huo, Juni 11, mwaka huu,
CCM ilitangaza uamuzi wake wa kuijadili rasimu ya kwanza ya katiba mpya,
kuanzia ngazi ya matawi, wilaya na Taifa ili kupata maoni ya wanachama na
kuweka msimamo wake. Hata hivyo, CCM kupitia Katibu wake wa Nec, Itikadi na
Uenezi Taifa, Nape Nnauye, ilisema maoni ambayo yangetolewa na wanachama wake
yangepaswa kuzingatia maoni ya chama hicho yaliyotolewa mwanzoni mwa mchakato
wa mabadiliko ya katiba. Hata hivyo, hadi rasimu ya pili inakabidhiwa leo kwa
marais hao, CCM haijawahi kuweka wazi msimamo wake kuhusu rasimu ya kwanza ya
katiba mpya. Lakini habari kutoka ndani ya kikao cha Nec, kilichofanyika mjini
Dodoma, Agosti 25, mwaka huu, zilizochapishwa na baadhi ya vyombo vya habari,
ambazo CCM haikuzikanusha, zilieleza kuwa michang iliyotolewa na wajumbe wa
kikao hicho, wengi waling’ang’ania mfumo wa serikali mbili kama ilivyo kwenye
ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya mwaka 2010. Kwa mujibu wa chanzo hicho, baadhi
ya waliopinga walisema kuna haja ya kuendelea na mfumo wa serikali mbili, kwa
kuwa ndio unaokubalika. Hata hivyo, katika kikao hicho, Mwenyekiti wa CCM, Rais
Kikwete alinukuliwa akiwataka wana CCM nchini, kujiandaa kisaikolojia juu ya
muundo wa serikali tatu pindi Watanzania watakapoamua hivyo. Chanzo hicho cha
habari kilisema Rais Kikwete alitoa kauli hiyo baada ya Katibu wa Nec, Siasa na
Uhusiano wa Kimataifa wa CCM, Dk. Asha Rose-Migiro, kuwasilisha hoja yake
katika kikao hicho kilichokaa kama Baraza la Katiba. Licha ya Rais Kikwete
kutoa wito huo kwa wana CCM, Oktoba 2, mwaka huu, Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Wazazi ya chama hicho, Abdallah Bulembo, aliendeleza kauli zinazoonyesha
kumuingilia na kumshambulia vikali Jaji Warioba kwa kumtaka aache kuwasemea
Watanzania juu ya aina ya katiba wanayoitaka. Bulembo alimshambulia Jaji
Warioba alipokuwa mkoani Tanga, wakati akihutubia moja ya mikutano ya hadhara
ya wanachama wa CCM. Bulembo alinukuliwa katika vyombo vya habari akisema kuwa
siyo sahihi kwa Jaji Warioba kuwa msemaji wa Watanzania kuhusiana na mambo
wanayoyataka yaingizwe ndani ya katiba. “Jaji Warioba ni mmoja kati ya
Watanzania mamilioni na kwa hali hiyo hawezi kubeba mawazo ya Watanzania
wengine, ni vizuri akasimamia rasimu, badala ya kuwa msemaji wa wananchi,”
alisema Bulembo ambaye pia ni Mjumbe wa CC ya CCM. Bulembo alitoa kauli hiyo
wakati kukiwa na msuguano kati ya CCM na serikali yake kwa upande mmoja, na
vyama vitatu vya upinzani vyenye wabunge ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania. Kabla ya hapo, mwishoni mwa Septemba, mwaka huu, Jaji Warioba
akizungumza na waandishi wa habari, aliwakemea baadhi ya viongozi wa kisiasa
kwa kuiingilia mchakato wa kupata katiba mpya unaoendelea. Alisema baadhi ya
changamoto zilizojitokeza wakati wa kuendesha mabaraza ya katiba, ni kwa baadhi
ya vyama vya siasa kuingilia uhuru wa wajumbe katika kutoa maoni kuhusu Rasimu
ya Katiba, wakiwafundisha nini cha kusema. Jaji Warioba aliwasihi viongozi wa
vyama vya siasa kuwaachia wananchi, cha kusema kwani, katiba inayotafutwa ni ya
wananchi, na si ya vyama au kundi fulani. Aidha, Oktoba 3, mwaka jana, Jaji
Warioba alitoa karipio kwa Bulembo kwa kumtaka aache kupiga kelele dhidi yake
kwa kuwa hakumtuma kazi ya kukusanya maoni ya katiba mpya, bali alitumwa na serikali
kwa niaba ya wananchi. Jaji Warioba alisema Bulembo amekuwa na ajenda ya siri
dhidi yake (Warioba) na baadhi ya wajumbe wa Tume kwa kuwa amekuwa
akiwazungumzia wao binafsi kila anaposisimama katika majukwaa ya kisiasa. Alimtaka
Bulembo kuthibitisha kuhusu kauli ambazo amekuwa akizitoa kwenye mikutano ya
CCM katika mikoa ya Arusha, Tanga na Mbeya kuwa yeye (Warioba) amegeuka kuwa
msemaji wa wananchi katika mchakato mzima wa kupata Katiba mpya. Jaji Warioba
alitamtahadharisha Bulembo na kumtaka kuacha kupiga kelele pamoja na
kumshambulia badala yake azungumzie masuala yanayohusu rasimu ya katiba na siyo
kuwajadili wajumbe. Aidha, Jaji Warioba alimtaka Bulembo kuthibitisha kama
kauli ambazo alizitoa kwa nyakati tofauti katika mikoa hiyo ametumwa na CCM ama
ni kauli zake binafsi. Jaji Warioba alisisitiza kuwa siku zote Tume yake
imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria na kuwataka wanasiasa
akiwamo Bulembo kujadili rasimu iliyotolewa badala ya Tume au wajumbe wake. Alisema
hakutumwa na CCM kufanya kazi anayoifanya na kwamba kazi hiyo alipewa na
serikali kwa mujibu wa sheria na kwamba ataendelea kuifanya bila kusikiliza
maneno yanayosemwa dhidi yake. Jaji Warioba alisema kauli zilizotolewa na
Bulembo kwa nyakati mbalimbali zilichangia mchakato wa katiba kuwa mgumu
hususani wakati wananchi walipokuwa wakitoa maoni kupitia mabaraza ya katiba
mkoani Mbeya. Alisema haogopi wala hatetereki kwa kuwa anafanya kazi aliyotumwa
na wananchi. Alisema CCM iliishawasilisha maoni yake walipopewa nafasi ya
kufanya hivyo, na kwamba masuala mengine yanayojitokeza zikiwamo kauli za
Bulembo baada ya hapo hajui zinatoka wapi. Mbali na Bulembo, makada mbalimbali
wa CCM nchini tangu kutolewa kwa rasimu ya kwanza ya katiba walikuwa
wanamshambulia Jaji Warioba binafsi kwamba ndiye anayeshinikiza mfumo wa
serikali tatu kwa manufaa yake binafsi. Wapo wanachama wa CCM na makada wa
chama hicho ambao wakati wa mikutano ya mabaraza walisikika wakitoa kauli za
matusi na kashfa dhidi ya Jaji Warioba kwa madai kuwa ana lengo la kuuvunja
Muungano. Ikiwa Tume leo itapendekeza mfumo wa serikali tatu, kuna uwezekano wa
baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM ambao wataibuka tena nakumshambulia Jaji
Warioba kutokana na maamuzi hayo. Kama mfumo wa serikali tatu utaridhiwa tena
na tume, suala hilo huenda likazua mjadala mkali na malumbano katika Bunge
Maalum la Katiba ambalo CCM kina wajumbe wengi. Kama tume itabadili msimamo
wake wa awali na kutangaza mfumo wa Muungano wa serikali mbili, itakuwa imeipa
CCM furaha na kicheko.
KAULI YA NAPE
Nape
alipoulizwa na NIPASHE jana iwapo rasimu ya pili ya katiba mpya itapendekeza
muundo wa Muungano wa serikali tatu CCM itachukua hatua gani, alijibu: “Kwanini
tubashiri? Si usubiri kesho (leo) itokee.” Tume ya Mabadiliko ya Katiba yenye
wajumbe 30; wakiwamo 15 kutoka Tanzania Bara na 15 kutoka Zanzibar, ilitangazwa
na Rais Kikwete, Aprili 6 na kuapishwa Aprili 13, mwaka jana. Ilianza rasmi
kazi ya kukusanya maoni ya wananchi Mei mosi, mwaka jana. Baada ya kukamilisha
kazi hiyo, iliyachambua na kuandika Rasimu ya Katiba. Kazi ya kukusanya maoni
hayo iliwahusisha wananchi mmoja mmoja kupitia mikutano ya hadhara na
ilikamilishwa na Tume Desemba, mwaka jana. Baadaye Tume ilikutana na makundi
maalumu na watu mashuhuri, wakiwamo viongozi wakuu wastaafu na waliopo madarakani
Januari 7-28, mwaka huu. Baadaye, mabaraza ya katiba yaliipitia Rasimu ya
Katiba kuanzia Julai 12 hadi Septemba 2, mwaka huu na kutoa mapendekezo yake,
ambayo yaliwasilishwa kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Tume iliendelea
kuyachambua kabla ya kukabidhi rasimu ya pili ya katiba kwa Rais Kikwete na
Rais Dk. Shein leo. Baada ya rasimu ya pili ya katiba mpya kukabidhiwa kwa
marais hao, itachapishwa katika Gazeti la Serikali na kwenye magazeti mengine
ndani ya siku 31. Katika kipindi hicho, Rais ataitisha kikao cha Bunge Maalumu
la Katiba kwa ajili ya kupitisha rasimu ya pili ya katiba mpya iliyopendekezwa.
Bunge Maalumu la Katiba, ambalo litafanyika kwa siku zisizozidi 70, linatarajiwa
kuanza rasmi Februari, mwakani, kwa ajili ya kujadili na kuipitisha rasimu ya pili
ya katiba iliyopendekezwa. Baada ya rasimu ya pili kupitishwa na Bunge Maalumu
la Katiba, itaitishwa kura ya maoni, ambayo itatoa fursa kwa wananchi kuamua
ama kuikubali au kuikataa.
0 comments:
Post a Comment