KUNDI la
wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba linalowashirikisha wanasiasa wa vyama vya
upinzani, maarufu kama Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), limekuwa mwiba
mkali kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho kinapanga mikakati
kulisambaratisha.
Ukawa inayoongozwa na vinara wa vyama vikubwa
vya CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi pamoja na vingine vidogo visivyokuwa na wabunge,
inaonekana kuwa mwiba kwa Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta kwa kudhibiti
uvunjwaji wa kanuni ili kuibeba CCM.
Awali CCM ililipuuza kundi hilo na kulibeza,
lakini baada ya kuona nguvu yake wakati wa kumtetea Mwenyekiti wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba apewe muda wa kutosha, hofu ilitanda.
0 comments:
Post a Comment