Wenyeji wa
michuano ya kombe la dunia, Brazil wameianza vyema baada ya kuichapa Croatia
mabao 3-1.
Croatia ndio walikuwa
wa kwanza kupata bao baada ya mchezaji wa Brazil Marcelo kujifunga katika
dakika 11. Brazil walijipatia goli lao la kuwasazisha kutoka kwa Neymar
aliyezitikisa nyavu za Croatia katika dakika ya 29 kwa shuti la umbali wa yards
25. Mpaka timu hizo zinaenda mapumziko magoli yalikuwa 1-1.
Katika dakika ya 70 referee wa mchezo huo Yuichi Nishimura
aliwapa penalty Brazil iliyotumiwa vyema na Neymar aliyeipa Brazil bao la pili.
Wakati zikiwa zimesalia dakika 2 kumalizika kwa mchezo huo,
Brazil waliongeza bao la tatu lililofungwa kirahisi na Oscar aliyemwacha mlinda
mlango wa Pletikosa akijitupab kujaribu kuuokoa bila mafanikio.
Ushindi wa Brazil umepokelewa kwa furaha kubwa na mashabiki
wengi waliokuwa wamefurika kwenye uwanja uliopo mjini Sao Paulo.
Michuano hiyo inaendelea tena Ijumaa hii kwa mechi ya Mexico
vs Cameron, Spain vs Netherlands na Chile vs Australia.
0 comments:
Post a Comment