Mkuu wa huduma za kibinadamu katika
umoja wa mataifa anasema kuwa karibu watu 400 waliozingirwa katika mji
wa Madaya nchini Syria wanahitajika kuondolewa mjini humo kwa dharuara
ili kupata matibabu .
Stephen O'Brien alitayasema hayo baada ya
mkutano wa baraza kuu la umoja wa mataifa uliofanyika kujadili hali
katika mji huo unaodhibitiwa na waasi karibu na mji wa Damascus.Mapema msafara wa malori ya misaada ulipeleka tani 40,000 kwa wenyeji ambao wamezigirwa na serikali kwa miezi kadha.
Msaada wa siku ya Jumapili ndio wa kwanza kuruhusiwa kuingia katika mji wa Madaya tangu mwezi Oktoba wakati shirika la mpango wa chakula la umoja wa mataifa lilipeleka msaada wa mwezi mzima kwa watu 20,000.
Pia magari yaliyobeba misaada yaliingia miji miwili inayozingirwa na waasi katika mkoa wa kaskazini wa Idlib chini ya makubaliano kati ya pande zinazopigana.
0 comments:
Post a Comment