Mbunge mmoja wa chama tawala nchini
Zimbabwe anatarajiwa kufikishwa kortini kujibu mashtaka ya kumtusi mke
wa Rais Robert Mugabe, Grace Mugabe.
Mbunge huyo Bw Justice
Wadyajena anadaiwa kutumia “lugha ya matusi” dhidi ya mwanachama
mwenzake wa chama tawala cha Zanu-PF aliyekuwa ameweka picha ya Bi
Mugabe kwenye gari lake.Kisa hicho kinatazamwa na wengi kama sehemu ya vizozo ya ndani ya chama kuhusu nani atamrithi Rais Robert Mugabe ambaye atatimiza umri wa miaka wa miaka 92 Februari.
Bw Wadyajena amenukuliwa kwenye nyaraka za mahakama kwamba alimwambia Jimayi Muduvuri: "Wewe ni mjinga sana, sawa na mama huyu wenu.” Atafikishwa kortini Victoria Falls.
Mke wa rais nchini Zimbabwe huitwa "amai", maana yake mama, na wafuasi wa chama cha Zanu-PF.
Mbunge huyo amekanusha madai hayo.
0 comments:
Post a Comment