MICHAKATO

Levis Rocky Ndekeno

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Pages

Friday, June 13, 2014

Leo ni mwaka mmoja tangu Langa Kileo afariki dunia


Wakati ambapo mashabiki wa muziki wa Hip Hop nchini walikuwa wameanza kusahau majonzi ya kumpoteza Albert Mangweha aka Ngwair mwezi May mwaka jana, June 13, 2013 walitoneshwa tena kwa kifo cha mwana hip hop mwingine, Langa Kileo aka Lyrically And Naturally Gifted African.
Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano wa hospitali ya taifa ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha Langa alifariki une 13, saa 11 jioni baada ya kufikishwa hospitalini hapo tangia juzi mida ya jioni. Taarifa za awali zilidai kuwa Langa alikuwa anaumwa Malaria kali iliyopelekea kukimbizwa Muhimbili jana jioni.
Langa alikuwa ni mmoja wa matunda ya shindano la muziki la Coca-Cola Pop Stars mwaka 2004 ambalo washindi wake waliounda kundi la Wakilisha akiwa pamoja na Sarah Kaisi `Shaa’ na Witness Mwijage `Witness’ ambapo walitamba na nyimbo kama Unaniacha Hoi na Kiswanglish. Langa alizaliwa Desemba 22, 1985 jijini Dar es Salaam katika familia ya wanandoa Vanessa Kimei na mumewe Mengisen Kileo.
Alisoma Shule ya Msingi Olympio na Sekondari ya Loyola, zote za jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, akiwa kidato cha pili alihamishiwa Kampala, Uganda katika Shule ya Vienna na baadaye shule ya Hillside International Academy, huko huko Uganda. Baadaye alirejea nchini na kujiunga na masomo ya Stashahada ya Masoko katika Chuo cha Biashara Dar es Salaam (CBE), Kampasi ya Dodoma (Global Publishers).
Wasanii na watu mbalimbali walituma salamu zao za rambirambi kwa familia ya Langa na kuomboleza kifo hicho.

Joh Makini

Wiki mbili nyuma tulipanga kufanya trak kwa Dunga tukaisogeza mbele kupisha msiba wa Ngwea nakumbuka mpaka session alipanga alhamis aliamplz tumalize msiba lkn kumbe yeye ndio alikua anafata daah! Mara ya mwisho kuongea ni uliponiambia nichek beat kwenye email alaf tuchangie mawazo kutakufuta idea daaah! Baadae tena ukanitext umepata idea mbili platinum ideas tukienda studio tunaua! Sasa umeondoka ghafla mimi na dunga tumebaki na beat tu sasa #RIP LANGA.

THE CITY of PHD ‏

DAAAAAAAH MUNGU TUSAIDIE!!MI NIMESHAKOSA AMANI KABISA HAPA NILIPO!!!HAYA NI MAJONZI MAKUBWA!!REST IN PEACE LANGA!!GONE TOO SOON!!DAAAAAH

Nick Mweusi

KAMA HIZI HABARI ZA LANGA NI KWELI SHOW YANGU NA GNAKO CLUB KAKALA HAiTAfANyIKA. RIP LANGA

Afande Sele The’King

Tunavyotaka sisi, sivyo anavyotaka yeye (Mungu) mapenzi yake ni zaidi.
 Mungu akupumzishe pema LANGA KILEO

K Wa MaujanjaSaplayaz

Kapumzike na amani zote hatuta acha kukukumbuka daima
 Mad Ice

Oh lord shed light on these dark moments of the Tanzanian Music Industry! Its not even a week since we buried Ngwea and another one is down :(… R.I.P Langa!

Cpwaa

Another Brother, Another Soldier, Another buddy,another talented Tanzanian Hip Hop Artist gone!……bado siamini.. #RIPLanga #BongoFlavaStayCalmAndUnited

Fina Mango ‏

RIP Langa. Pole sana Mama na Mzee Kileo Mungu awake nguvu Kwa wakati huu mgumu

D knob ‏

Rip Langa. Sijui cha kuongea kiukweli Dah.

Nikki Mbishi

Langa unaenda wapi kichaa wangu?Mwanao bado nalia na Ngwea halafu unasepa badala ya kubaki tuanue matanga.

LANGA NDANI YA THE JUMP OFF WITH JABIR SALEH

Thursday, June 12, 2014

Picha:Mabanda ya wafanyabiashara wa soko la Karume yateketea kwa moto


Moto mkubwa umetetekeza kabisa soko kubwa kabisa la mitumba la karume jijini Dar es Salaam usiku wa Jumatano, na kusababisha hasara kubwa kwa wafanyabiashara wote wa soko hilo.
Baadhi ya mabanda yakiteketea kwa moto

 Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, wamedai moto huo ulianza kuteketeza mabanda hayo majira ya saa 4 usiku, huku wakijaribu kutafuta msaada kuuzima bila mafanikio yeyote.

Wazima moto walifanikiwa kuudhibiti moto uloweza kufikia karibu na kiwanda cha Breweries, lakini haujasababisha hasara yeyote katika nyumba za jirani wa soko hilo kwa mujibu wa mwandishi habari wa Raia Mwema Mbaraka Islam alipozungumza na Sauti ya Amerika.

Anasema hakuna kibada cha biashara kilichosalimika na hakuna mtu aliyefanikiwa kuokowa mali yake. Mfanya biashara Wilson magembe anasema amepoteza kila kitu na ilikuwa vigumu kuweza kuchukua bidhaa zao kwa sababu moto uliwaka kwa haraka sana.







Picha: Jennifer Lopez na Pitbull wapamba sherehe za ufunguzi wa kombe la dunia 2014, Brazil





Maelfu ya mashabiki wamejitokeza jioni ya leo kwa saa za Brazil (June 12) katika sherehe za ufunguzi wa fainali za kombe la dunia 2014 kwenye uwanja wa ‘Arena de Sao Paulo’ nchini Brazil, ambapo Jennifer lopez, rapper Pitbull na mwimbaji wa Brazill Claudia Leitte wametumbuiza mbele ya mashabiki waliofurika kwa wingi na kuimba wimbo rasmi wa kombe la dunia kwa mwaka huu ‘We Are One (Ola Ola)’.Maandalizi ya sherehe hizo za ufunguzi yalifanywa kuanzia March mwaka huu, na jumla ya masaa 84 yalitumika kwaajili ya rehearsal za sherehe hizo.Mechi ya ufunguzi wa michuano hiyo inafanyika usiku huu kati ya wenyeji Brazil na Croatia.



Brazil waanza vyema kombe la dunia kwa kuichapa Croatia 3-1


Wenyeji wa michuano ya kombe la dunia, Brazil wameianza vyema baada ya kuichapa Croatia mabao 3-1.


 Croatia ndio walikuwa wa kwanza kupata bao baada ya mchezaji wa Brazil Marcelo kujifunga katika dakika 11. Brazil walijipatia goli lao la kuwasazisha kutoka kwa Neymar aliyezitikisa nyavu za Croatia katika dakika ya 29 kwa shuti la umbali wa yards 25. Mpaka timu hizo zinaenda mapumziko magoli yalikuwa 1-1.



Katika dakika ya 70 referee wa mchezo huo Yuichi Nishimura aliwapa penalty Brazil iliyotumiwa vyema na Neymar aliyeipa Brazil bao la pili.

Wakati zikiwa zimesalia dakika 2 kumalizika kwa mchezo huo, Brazil waliongeza bao la tatu lililofungwa kirahisi na Oscar aliyemwacha mlinda mlango wa Pletikosa akijitupab kujaribu kuuokoa bila mafanikio.

Ushindi wa Brazil umepokelewa kwa furaha kubwa na mashabiki wengi waliokuwa wamefurika kwenye uwanja uliopo mjini Sao Paulo.

Michuano hiyo inaendelea tena Ijumaa hii kwa mechi ya Mexico vs Cameron, Spain vs Netherlands na Chile vs Australia.

Agnes Masogange afunguka maisha yake ya jela yalivyokuwa

Wednesday, June 11, 2014