Kiongozi
wa kanisa la Katoliki duniani, Papa Francis, ametoa wito kwa viongozi
wanaohudhuria mkutano wa kimataifa mjini Davos kuhakiksiha kuwa mali na utajiri
ulio hapa duniani unapaswa kuwahudumia raia badala ya kuwatawala.
Papa
huyo kutoka Brazil, amekuwa mkosoaji mkubwa wa mfumo ubepari ambao
unawakandamiza watu walio masikini na amekuwa katika mstari wa mbele kutetea
maslahi ya raia wa nchi hiyo ambao wengi wao ni masikini.
Katika
hotuba iliyosomwa kwa niaba ya papa na Kadinali Peter Turkson, kutoka Ghana,
ambaye ni mkuu wa tume ya haki na amani huko Vatican, Papa Francis, amewaomba
wafanyabiashara katika mkutano wa kimataifa wa kiuchumi kuusaidia umma, badala
ya kuruhusu umaskini usambae duniani.
Kuondoa umasikini duniani
Papa
Francis alitoa wito kwa viongozi hao kujitolea zaidi na kufanya mengi zaidi
kuliko kuzingatia maslahi ya kawaida na pia kutathmini jinsi kuhakikisha kuwa
utajiri wa taifa umesambazwa kwa raia wote.
Wakati
huo huo amewarai wafanyabiashara kuchukua jukumu hilo huku wakiwa na mtizamo na
mwelekeo wa kuimarisha hali ya maisha duniani.
Mapema
wiki hii shirika la Oxfam, liliripoti kuwa watu themanini na watano tajiri
zaidi duniani, wanamiliki utajiri ambao ni sawa na mali inayomilikiwa na zaidi
ya watu bilioni tatu na nusu wengi wao wakijumuisha nusu ya watu walio na
mapato ya chini zaidi duniani.
Amesema
ukuaji wa usawa ni zaidi ya ukuaji wa kiuchumi licha ya kuwa vyote
vinaambatana.
0 comments:
Post a Comment