Zitahojiwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu
matumizi ya marejesho ya fedha za rada Dar es
Salaam. Kamati ya
Bunge ya Hesabu za Serikali, PAC, imepanga kuzikutanisha kwa pamoja, Wizara za
Fedha na Elimu wakati ikipokea taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG) inayohusu matumizi ya fedha za marejesho ya rada jinsi
zilivyotumiwa.
Akizungumza
Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Deo Filikunjombe alisema
kuwa wanatarajia kupokea taarifa hiyo kesho na watatumia fursa hiyo
kujihakikishia kama matumizi hayo yalikuwapo au kama kulikuwa na ulaghai wa
aina yoyote.
“Kwa
sasa ni mapema kuanza kufikiri kwamba fedha hazikutumika inavyotakiwa, lakini
kama kuna ujanja wowote ulifanyika tutabaini tu alisema na kuongeza:
“Ndiyo
sababu katika kikao hiki tunakutana wote; CAG, Wizara ya Fedha na Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi ili kama kuna maswali basi kuwe na majibu yake papo
hapo,” alisema Filikunjombe.
Alisema
leo watapokea taarifa ya ukaguzi maalumu kuhusu mbolea ya ruzuku, pia shughuli
nyingine ambazo kamati inatarajia kuzifanya katika kipindi cha wiki mbili
zijazo ni pamoja na kutembelea bandari na kukagua mradi wa kuzalisha umeme kwa
kutumia makaa ya mawe wilayani Ludewa.
Awali
mwaka jana aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene, aliliambia Bunge
kwamba fedha za rada zilizorejeshwa Sh72.3 bilioni ziliingizwa katika bajeti ya
serikali kwa mwaka 2012/13.
Mbene
alisema kwamba fedha hizo ni marejesho kwa Serikali ya Muungano kutokana na
udanganyifu uliofanywa na Kampuni ya BAE Systems ya Uingereza wakati wa kuiuzia
Serikali ya Tanzania rada ya kuongozea vyombo vya usafiri angani.
Fedha
zilizorudishwa na kampuni hiyo baada ya Taasisi ya Uchunguzi wa Makosa Makubwa
ya Jinai (SFO) ya Uingereza kubaini kuwa, baadhi ya maofisa wa Serikali ya
Tanzania na mawakala wa ununuzi kupandisha bei baada ya kushawishiwa na kampuni
hiyo.
Novemba
mwaka jana Serikali ilianza kusambaza vitabu milioni 19.4 kwa shule za msingi
nchini, ambavyo ilielezwa kuwa vimenunuliwa kwa chenji ya rada na asilimia 75
ya fedha hizo zimetumika kununulia vitabu hivyo na asilimia 25 zitatumika
kununulia madawati.
0 comments:
Post a Comment