Popo hutumiwa kutengeza kitoweo maarufu sana katika baadhi
ya maeneo ya Guinea, lakini sasa inahofiwa kuwa popo wanachangia kusambaa kwa
ugonjwa wa Ebola kusini mwa nchi hiyo.
NI marufuku kula na kuuza popo Guinea
Maafisa nchini humo sasa wamepiga marufuku uuzaji na ulaji
wa nyama ya popo katika juhudi za kudhibiti ugonjwa hatari wa Ebola, ambao
kufikia sasa umesababisha vifo vya watu 62.
Habari zinazohusiana
Ebola ni kiini cha ugonjwa hatari Guinea
Wasi wasi kuhusu virusi vya Ebola
Uganda imethibitisha kuwepo kwa Ebola
Taarifa zinazohusiana
Afrika
Nchi za kanda hiyo zikiwemo Liberia na Sierra Leone,
zimechukua hatua kabambe kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo zikiwemo
kuwafanyia uchunguzi wa kiafya watu wanaongia mipakani.
Maafisa wa afya wanapata msaada kutoka shirika la afya
duniani na ujumbe wa kuhamasisha watu unapeperushwa kupitia televisheni.
Watu watano kati ya sita walioingia nchini Liberia kutoka
Guinea walikua na ishara za ugonjwa huo na wamethibitishwa kufa.
Hatahivyo maafisa wa utawala nchini Liberia bado
hawajathibitisha kikamilifu kama kweli walikufa kutokana na ugonjwa wa Ebola.
0 comments:
Post a Comment