Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amewataka wabunge wa bunge la
jumuia ya Afrika Mashariki kuhimiza utekelezaji wa sheria zilizopitishwa na
wabunge hao ili ziweze kuridhiwa na kutekelezwa na nchi washirika.
Miongoni mwa sheria zilizopitishwa na bunge hilo ni ushuru
wa forodha, soko la pamoja na sarafu ya pamoja, mkataba ambao bado haujaanza
kutekelezwa.
Taarifa zinazohusiana
Afrika Mashariki
Rais Uhuru Kenyatta ambaye ni mwenyekiti wa wakuu wa nchi za
jumuiya hiyo yuko mjini Arusha makao makuu ya jumuiya hiyo kuzungumza na
wafanyakazi na pia kuwafungulia kikao cha bunge kitakachodumu kwa wiki mbili
zijazo.
Rais Kenyatta amezidi kusisitiza kuwa ushirikiano wa nchi
hizo ndio ukombozi wao kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Rais Uhuru Kenyatta akiwa safarini kwenda Arusha
Rais Kenyatta kadhalika ameelezea nia ya mataifa yote ya
jumuiya ya Afrika Mashariki kupambana vikali na tatizo la ujangili na
kuutokomeza.
Rais Uhuru Kenyatta pia amesema jukumu la kukabiliana na
vitendo vya ujangili ni la wananchi wote kwa sababu lina athari kwa kila mtu
mkaazi wa Afrika Mashariki.
Ama kuhusu suala la uhuru wa uhamishaji wa mitaji na uhuru
wa wananchi wa Afrika Mashariki kutembea kutoka nchi moja kwenda nyingine,
amesema jambo hilo linaweza kumalizwa pindi kila nchi itapokamilisha taratibu
za matumizi ya vitambulisho kwa raia wake:
Rais Uhuru Kenyatta na ujumbe wake wamerejea nyumbani kwa
njia ya barabara kupitia mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Namanga. Ben
Mwang'onda Dira ya Dunia BBC, Arusha.
0 comments:
Post a Comment