MICHAKATO

Levis Rocky Ndekeno

Pages

Monday, January 4, 2016

Chuo kikuu cha Garissa chafunguliwa tena

Chuo kikuu cha Garissa kilichofungwa mwaka uliopita baada ya watu 148 kuuawa kwenye shambulio lililotekelezwa na wanamgambo wa al-Shabab, kimefunguliwa tena.

Wafanyakazi wamefika kazini leo huku usalama ukiwa umeimarishwa.

Kila aliyekuwa akiingia katika chuo kikuu hicho kilichoko eneo la kaskazini mashariki mwa Kenya amepekuliwa na maafisa wa usalama.

Kituo cha polisi, ambacho kitakuwa na maafisa zaidi ya 20 wa kutoa ulinzi, kimejengwa ndani ya chuo kikuu hicho.

Kitambulisha mada #GarissaUniversityReopens (Chuo Kikuu cha Garissa chafunguliwa tena) kimekuwa kikivuma katika mtandao wa Twitter nchini Kenya.

Wengi wanasema kufunguliwa kwa chuo hicho kunaonyesha Wakenya hawawezi kuvunjwa moyo na magaidi.

Msimamizi mkuu wa chuo kikuu hicho Prof Ahmed Warfa ameambia MICHAKATO Magazine kwamba wanafunzi wataanza kufika chuoni Jumatatu ijayo tarehe 11 Januari.

Hakukukuwa na sherehe yoyote maalum ya kuadhimisha kufunguliwa upya kwa chuo hicho.

0 comments:

Post a Comment