Mwanzilishi
wa kampuni ya Microsoft, Bill Gates amesema hadi kufikia mwaka 2035 hakutakuwa
na nchini maskini duniani.
Kwenye
ripoti ya kurasa 25 iliyoandikwa na Gates na mke wake Melinda, ambao ni
wenyekiti wa Bill & Melinda Gates Foundation, wamedai kuwa duniani imekuwa
na afueni kuliko ilivyokuwa awali. Gates ametabiri kuwa hadi kufikia 2035,
hakutakuwa na nchini itakayobaki kuwa maskini.
“Nchi
maskini hazitakaa maskini daima. Baadhi ya nchini zinazoendelea tayari
zimeshaendelea,” alisema Gates kwenye ripoti yake ya mwaka. “Nina imani kubwa
kuhusu hili kiasi ambacho nipo tayari kufanya utabiri wangu. Hadi kufikia mwaka
2035, hakutakuwa na nchini maskini duniani.”
Gates
amesema katika kipindi hicho karibu nchi zote zitakuwa na kipato cha kati ama
zitakuwa tajiri.
0 comments:
Post a Comment