Rapper
Ibrahim Musa aka ‘Roma Mkatoliki’ amesema kile kinachoonekanan kama ukimya wake
kinatokana na desturi aliyojiwekea tangu aanze muziki wa kutoa wimbo mmoja kwa
mwaka.
Akizungumza leo, Roma amesema ukiona yupo kimya katika
muziki ujue anafanya shughuli za kiujasiriamali ambazo ni tofauti na muziki.
“Mwaka jana
hakukuwa na kimya chochote kwa mtu anayemjua Roma kwa miaka yote,” amesema
Roma. Roma kwa mwaka anatoaga wimbo moja. Kwahiyo mtu yoyote ambaye ana ‘judge’
kwanini Roma alikuwa kimya, ujue huyo kamjua Roma juzi.2007 ilitoka nyimbo ya
kwanza, 2008 nyimbo ya pili, na nyimbo sita, kwahiyo kila mwaka natoaga nyimbo
moja,sijawahi kutoa nyimbo mbili kwa mwaka. Kwa mwaka jana ni 2030. Nilikuwa
kimya kwasababu ndio nyimbo iliyokuwa inachezwa.Na mwaka huu nitatoa nyimbo
moja nanitakuwa kimya mpaka mwakani ndio kawaida ya Roma.”
“Nimeandaa
nyimbo kama sita ndani ya ‘Tongwe records’ sema ni kuchagua nitoe nyimbo gani
kwa mwaka huu. Sema nilikuwa kimya kidogo kutokana na majukumu ya maisha.Kama kawaida
ya Roma ni nyimbo moja kwa mwaka, hata wimbo wangu 2030 ulitoka 28/12/2012.
Lakini wimbo huu ni wa mwaka 2013 ndio maana ulipata air time nzuri 2013,”
aliongeza.
Katika hatua
nyingine, Roma amesema mwaka huu anatarajia kurudi shule baada ya kuhitimu na
kushindwa kuendelea kutokana na muziki.
“Mimi ni
mjasiriamali pia najarajia kurudi shule hivi karibuni,kwasababu nilihitimu
nikashindwa kuendelea,ila mwaka huu nadhani suala la kurudi shule ni miongoni
mwa mikakati yangu kwa mwaka huu.”
0 comments:
Post a Comment