Tunafahamu
usiku unaweza kuwa muda mzuri wa kupitia status za washkaji Facebook, kutazama
picha mbalimbali Instagram ama kufuatilia mijadala kwenye Twitter lakini hicho
kinaweza kuwa kikwazo kikubwa cha nia yako ya kutaka kupata usingizi wa kutosha
ama kuwa na utendaji mzuri kazini.
Timu katika
chuo kikuu cha Washington imesema matumizi ya simu usiku sana yanaweza kuharibu
kabisa usingizi wako na namna utakavyofanya kazi siku inayofuata. Wameshauri
wafanyakazi wawe na tabia ya kuzima simu ama lasivyo watajikuta wakishindwa
kufurahia kazi kesho yake.
Watafiti hao
wanasema kujiondoa kabisa na matumizi ya simu usiku ni njia ya kupata usingizi
mzuri usiku. Wamewaomba waajiri kusubiri kutuma email hadi asubuhi
“Sababu ya
hii kama tutakavyoelezea, ni kwamba smartphones ni mbaya kwa usingizi, na
usingizi ni muhimu kwa uchapakazi wa mwajiriwa,” alisema Christopher Barnes,
Profesa Msaidizi katika chuo kikuu cha Washington (Foster School of Business)
aliyeongoza utafiti huo utakaochapishwa kwenye jarida la , Organizational
Behavior and Human Decision Processes baadaye mwaka huu.
“Bahati
mbaya smartphones zimetengenezwa mahsusi kuharibu usingizi. Sababu zinatufanya
kiakili kuendelea na kazi hadi usiku, zinafanya kuwepo ugumu wa kujiondoa
kisaikolojia kutoka kwenye masuala muhimu ya siku ili tupumzike na kulala.
Pengine suala gumu kuliepuka kutoka kwenye smartphones ni kwamba zinatuweka
kwenye mwanga, ukiwemo mwanga wa blue. Hata kiwango kidogo cha mwanga wa blue
hupunguza uzalishaji wa kemikali ya usingizi, melatonin, ikimaanisha kuwa
muonekano (display) unaweza kutengeneza madhara haya.”
0 comments:
Post a Comment