Monday, March 31, 2014
Friday, March 28, 2014
Lil Wayne asisitiza "The Carter V" ndio itakuwa album ya mwisho ya The Carter
Album ya Lil
Wayne inayotarajiwa kutoka mwaka huu "The Catter v" itakuwa ndio
album yake ya mwisho kama solo artist, labda mtu ampe ofa ya dola miliomi 25
mpaka 35 kumfanya atengeneze album nyingine.
Wayne ametumia Interview alioifanya na MTV.com
kutangaza kuwa baada ya album hiyo ya tano ndio itakuwa mwisho wa kutoa kwake
kwa solo album.
"Nina plan ya kuwa hii ndio iwe album
yangu ya mwisho kama solo artist, ndio na ni kweli hii ndio Carter album ya
mwisho, ni album ya mwisho ya Carter, inaishia ya 5." Dola milioni 25
mpaka 35 zitanifanya nifanye solo album nyingine baada ya hii." amesema
Lil Wayne.
The Carter V haijasemekana official itatoka
tarehe ngapi kwa sasa, ila katika moja ya shows iliyofanyika New Orleand mwezi
uliopita, Drake alimuita Lil Wayne na kutangaza kuwa album yake itatoka tarehe
5 May.
The Carter V ikitoka itakuwa ni karibu miaka 3
tangu alipoiachia "The Carter 1V"
TUHUMA NZITO DHIDI YA WAZIRI MKUU NDANI YA BUNGE LA KATIBA
Dar es
Salaam. Hali ya hewa jana ilichafuka kwenye Bunge la Katiba baada ya mjumbe
Ezekiel Wenje kuwatuhumu Waziri Mkuu Mizengo Pinda na baadhi ya mawaziri kuwa
waliwahonga baadhi ya wajumbe wa kundi la 201.
Katika tuhuma hizo, Wenje alimtaja Waziri
Profesa Jumanne Maghembe, Dk. Shukuru Kawambwa na Gaudensia Kabaka akisema kuwa
walitoa rushwa ya vyakula, maji na vinywaji kwa wajumbe hao ili waunge mkono
msimamo wa serikali mbili.
Kauli hiyo, iliyotolewa katika mjadala wa
mabadiliko ya kanuni, ilisababisha mawaziri hao kunyanyuka kujibu tuhuma hizo,
huku Wenje akisisitiza kuwa aliyoyasema ni kweli tupu.
Vilevile baadhi ya wajumbe wanaotoka katika
kundi hilo walicharuka na kujaribu kujitetea huku mmojawapo akitishia kuwa
iwapo Wenje asingeomba radhi, asingetoka ndani ya Bunge hilo.
Hoja ilipoanzia
Wenje, ambaye pia ni mbunge wa Nyamagana
(Chadema), alianza kwa kueleza kwamba wapinzani “walilia” sana kuwa Bunge la
Katiba lisingekuwa na usawa kutokana na Chama cha Mapinduzi kuwa na wajumbe
wengi, ndipo ikaonekana wapatikane wajumbe wengine 201, lakini jambo la ajabu
ni kwamba walioteuliwa katika kundi hilo asilimia 80 ni makada wa CCM akiwamo
mzee maarufu ambaye ameingizwa kama mganga wa jadi.
Ingawa hakumtaja jina, Wenje alikuwa
anamaanisha kada mkongwe wa CCM, Kingunge Ngombale-Mwiru aliyeteuliwa kupitia
kundi la waganga wa jadi.
Kuhusu rushwa, Wenje alisema:“…Sasa kuna
wajumbe wa kundi la 201 walipelekwa kwa Profesa Maghembe na Dk. Kawambwa
wamepeana rushwa, vikao vingi vilifanyika usiku. Hii haikubaliki.”
Baada ya kauli hiyo ya Wenje, Profesa Maghembe
alisimama ghafla huku akionekana kutaharuki, ambapo Makamu Mwenyekiti Samia
Suluhu Hassan alimpa nafasi ya kujieleza.
Profesa Maghembe alikiri kuwakaribisha baadhi
ya wajumbe wa kundi hilo, akieleza kwamba ilikuwa ni katika hali ya ukarimu
uliozoeleka miongoni mwa jamii ya Kitanzania.
“Kuna kundi lipo hapa ambalo linafanya kazi ya
kudhalilisha wenzao. Ni kweli niliwaalika kwa chakula wajumbe hao kwa taratibu
za kawaida, lakini hakuna mbunge hapa anayeshindwa kujinunulia chakula, hakuna
anayeweza kupewa rushwa.
“Kwa sababu hiyo ninaomba kiti chako kimtake
mjumbe aliyewasilisha hoja hiyo aniombe radhi. Wenje aniombe radhi,” alisema
Profesa Maghembe akiwa katika hali ya hasira, huku kukiwa na sauti za kuzomea
na kushangilia kutoka kwa wajumbe.
Makamu mwenyekiti pia alifanya jitihada za
kuwataka wajumbe kuwa wavumilivu, huku akitoa nafasi kwa Dk. Kawambwa kujieleza
akisisitiza kwamba ni tuhuma nzito.
Kawambwa alisema: “Ni kweli nilikutana nao; ni
wajumbe ambao wanatoka kwenye taasisi zinazojihusisha na masuala ya elimu,
lakini mbona wameshafanya mikutano yao mingine mingi ambayo mimi hawakuniita.
Kama mtu akiwa hana hoja bora akae chini.”
Makamu Mwenyekiti alimtaka Wenje aombe radhi
kutokana na kauli yake, lakini katika hali ya kushangaza mjumbe huyo
alisisitiza kwamba Profesa Maghembe na Dk. Kawambwa wamekiri.
“Maghembe amekiri aliwaita wafugaji na wavuvi
ndiyo waliokula chakula cha rushwa, pia wapo wengine walienda kwa Waziri
Gaudensia Kabaka, kuna ushahidi mama mmoja siwezi kumtaja jina hapa alikwenda
huko akafukuzwa, nitakupa jina lake mwenyekiti baadaye. Aliambiwa kwamba anatoa
siri… hoja iliyojadiliwa huko ilikuwa ni kwamba msimamo ni wa serikali mbili…
rushwa ya chakula, maji na bahasha walipewa,” alisema Wenje na kusababisha
kulipuka kwa kelele zaidi.
Wenje aliongeza kuwa kuna wajumbe wengine
walikwenda hadi kwa waziri mkuu ambako walikula, walikunywa hadi saa 7:00
usiku.
Alisema wengine walikwenda kwa Gaudensia
Kabaka (Waziri wa Kazi na Ajira) na walikula na kunywa na kupewa bahasha.
Baada ya Wenje kukaa, baadhi ya wajumbe wa
kundi la 201 walichachamaa wakitaka kutetea hadhi yao, akiwamo mjumbe kutoka
kundi la wafugaji, Esther Juma aliyesema hawatendewi haki kama kundi kusema
kwamba walihongwa.
Alisema yeye ana ng’ombe 3,000 na asingeweza
kwenda kupokea rushwa ya chakula na kumtaka mbunge huyo kuwaomba radhi la sivyo
asingetoka mlangoni.
Wakati mjadala huo ukiendelea, mwenyekiti wa Bunge,
Samuel Sitta aliyekuwa ametoka kwa udhuru, alirejea kimya kimya, na kumtaka
Wenje kueleza iwapo anadhani kauli yake haikuwaudhi baadhi ya wajumbe.
Wenje alikiri kuwa ni kweli baadhi ya wajumbe
wameudhika kutokana na ukweli aliosema dhidi yao na kuwaomba radhi kwa ukweli
huo.
Kauli hiyo ilimfanya Sitta kutangaza kuwa
anapeleka suala hilo kwenye Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge na uamuzi
utakaotolewa atautangaza bungeni.
KUNDI LA UKAWA LAWA TISHIO BUNGENI..LAPANGWA KUSAMBARATISHWA
KUNDI la
wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba linalowashirikisha wanasiasa wa vyama vya
upinzani, maarufu kama Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), limekuwa mwiba
mkali kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho kinapanga mikakati
kulisambaratisha.
Ukawa inayoongozwa na vinara wa vyama vikubwa
vya CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi pamoja na vingine vidogo visivyokuwa na wabunge,
inaonekana kuwa mwiba kwa Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta kwa kudhibiti
uvunjwaji wa kanuni ili kuibeba CCM.
Awali CCM ililipuuza kundi hilo na kulibeza,
lakini baada ya kuona nguvu yake wakati wa kumtetea Mwenyekiti wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba apewe muda wa kutosha, hofu ilitanda.
Tuesday, March 25, 2014
HABARI KWANZA: KAMATI YA UONGOZI YA BUNGE MAALUM YAFANYA KIKAO CH...
HABARI KWANZA: KAMATI YA UONGOZI YA BUNGE MAALUM YAFANYA KIKAO CH...: Mwenyekiti wa Bunge Maalum Mhe. Samuel Sitta akiongoza kikao cha kwanza cha kamati ya Uongozi baada ya kuundwa leo. Kamati ...
Popo waeneza Ebola Guinea
Popo hutumiwa kutengeza kitoweo maarufu sana katika baadhi
ya maeneo ya Guinea, lakini sasa inahofiwa kuwa popo wanachangia kusambaa kwa
ugonjwa wa Ebola kusini mwa nchi hiyo.
NI marufuku kula na kuuza popo Guinea
Maafisa nchini humo sasa wamepiga marufuku uuzaji na ulaji
wa nyama ya popo katika juhudi za kudhibiti ugonjwa hatari wa Ebola, ambao
kufikia sasa umesababisha vifo vya watu 62.
Habari zinazohusiana
Ebola ni kiini cha ugonjwa hatari Guinea
Wasi wasi kuhusu virusi vya Ebola
Uganda imethibitisha kuwepo kwa Ebola
Taarifa zinazohusiana
Afrika
Nchi za kanda hiyo zikiwemo Liberia na Sierra Leone,
zimechukua hatua kabambe kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo zikiwemo
kuwafanyia uchunguzi wa kiafya watu wanaongia mipakani.
Maafisa wa afya wanapata msaada kutoka shirika la afya
duniani na ujumbe wa kuhamasisha watu unapeperushwa kupitia televisheni.
Watu watano kati ya sita walioingia nchini Liberia kutoka
Guinea walikua na ishara za ugonjwa huo na wamethibitishwa kufa.
Hatahivyo maafisa wa utawala nchini Liberia bado
hawajathibitisha kikamilifu kama kweli walikufa kutokana na ugonjwa wa Ebola.
Uhuru ahimiza ushirikiano Afrika Mashariki
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amewataka wabunge wa bunge la
jumuia ya Afrika Mashariki kuhimiza utekelezaji wa sheria zilizopitishwa na
wabunge hao ili ziweze kuridhiwa na kutekelezwa na nchi washirika.
Miongoni mwa sheria zilizopitishwa na bunge hilo ni ushuru
wa forodha, soko la pamoja na sarafu ya pamoja, mkataba ambao bado haujaanza
kutekelezwa.
Taarifa zinazohusiana
Afrika Mashariki
Rais Uhuru Kenyatta ambaye ni mwenyekiti wa wakuu wa nchi za
jumuiya hiyo yuko mjini Arusha makao makuu ya jumuiya hiyo kuzungumza na
wafanyakazi na pia kuwafungulia kikao cha bunge kitakachodumu kwa wiki mbili
zijazo.
Rais Kenyatta amezidi kusisitiza kuwa ushirikiano wa nchi
hizo ndio ukombozi wao kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Rais Uhuru Kenyatta akiwa safarini kwenda Arusha
Rais Kenyatta kadhalika ameelezea nia ya mataifa yote ya
jumuiya ya Afrika Mashariki kupambana vikali na tatizo la ujangili na
kuutokomeza.
Rais Uhuru Kenyatta pia amesema jukumu la kukabiliana na
vitendo vya ujangili ni la wananchi wote kwa sababu lina athari kwa kila mtu
mkaazi wa Afrika Mashariki.
Ama kuhusu suala la uhuru wa uhamishaji wa mitaji na uhuru
wa wananchi wa Afrika Mashariki kutembea kutoka nchi moja kwenda nyingine,
amesema jambo hilo linaweza kumalizwa pindi kila nchi itapokamilisha taratibu
za matumizi ya vitambulisho kwa raia wake:
Rais Uhuru Kenyatta na ujumbe wake wamerejea nyumbani kwa
njia ya barabara kupitia mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Namanga. Ben
Mwang'onda Dira ya Dunia BBC, Arusha.
Hewa chafu inaua mamilioni duniani
Watu milioni saba walifariki mwaka 2012 kutokana na hewa
chafu. Hii ni kwa mujibu wa shirika la afya duniani .
Ripoti ya shirika hilo inasema kuwa kuna uhusiano mkubwa
kati ya hewa chafu na maradhi ya moyo, tatizo la kupumua na ugonjwa wa
Saratani.
Taarifa zinazohusiana
afya
Kifo kimoja kati ya vinane duniani kilitokana na hewa chafu
, na kuifanya hali hiyo kuwa moja ya hatari ya mazingira chafu afya ya
binadamu.
Tarkriban watu milioni sita waliofariki dunia walikuwa Asia
ya Mashariki na katika eneo la Pacific.
Shirika hilo limesema kuwa takriban watu milioni 3.3
walifariki kutokana na hewa chafu katika nyumba zao kwa kutumia mkaa kukipikia
na wengine milioni 2.6 walifariki kutokana na hewa chafu nje ya nyumba zao ,
hasa katika nchi zinazostawi.
Afisaa mmoja mkuu wa shirika hilo, Daktari Maria Neira,
amesema kuwa, hewa chafu ina hatari kubwa kwa afya ya watu kuliko ilivyodhaniwa
hasa kwa kusababisha maradhi ya Moyo na Kiharusi.
Ripoti hii inaonyesha umuhimu wa kushirikiana katika
kuhakikisha kuwepo kwa hewa safi.
Shirika hilo limesema kuwa kupunguzwa kwa viwango vya hewa
chafu kunaweza kuokoa maisha ya watu.
Kadhalika shirika hilo limesema: "usafi wa hewa
tunayopumua unazuia maradhi ya kuambukizana na pia kuondoa hatari kwa watoto,
wazee na wanawake.''
Taarifa zinazohusiana
Wanaowania Tuzo za KILI 2014 ndio hawa, zilizoachwa ziko hapa pia
(BASATA) limetangaza
rasmi matokeo ya mchakato wa kuwapata wateule rasmi yaani ‘nominees’ wa
vipengele 34 vya tuzo za muziki Tanzania.
Kabla ya kuanza
kutajwa kwa wanaowania tuzo za KTMA 2014, BASATA ilitangaza nyimbo ambazo
zimetolewa kwenye kuwania tuzo hizi kutokana na sababu za kimaudhui kama
unavyoona hapa chini.
Nyingine ni
WIMBO BORA WA AFRIKA
MASHARIKI – Tubonge ya Jose Chameleone, Nakupenda pia ya Wyre na Alaine,
Badilisha ya Jose Chameleone, Kipepeo ya Jaguar, Kiboko changu ya Amani, Weasal
na Radio.
WIMBO BORA WA TAARAB
– Wasiwasi wako wa Mzee Yusufu, asie kujua hakuthamini Isha na Saida Ramadhani,
Nipe stara Rahima Machupa, sitaki shari Leila Rashid, fahari ya mwanamke ya
Khadija Kopa, mambo bado Khadija Yusufu, kila muomba Mungu ya Mwanahawa Ally.
WIMBO BORA WA
RAGGA/DANCEHALL – Nishai ya Chibwa ft Juru, Sexy Lady ya Dr. Jahson, My sweet
ya Jettyman Dizano, feel alright ya Lucky Stone na wine ya Princess Delyla.
WIMBO BORA WA
KUSHIRIKISHWA/KUSHIRIKIANA – Muziki gani ya Ney wa Mitego ft Diamond, Joto
hasira ya Lady Jaydee ft Prof J, kidela ya Ally Kiba na Abdu Kiba, bila kukunja
goti ya MwanaFA, Ay ft J Martins na tupogo ya Ommy Dimpoz ft J Martins.
RAPA BORA WA MWAKA WA
BENDI – Kitokololo, Chokoraa, Ferguson, Canal Top na Totoo ze bingwa.
MTUMBUIZAJI BORA WA
KIKE WA MUZIKI – Khadija kopa, Vanessa Mdee, Isha Ramadhani, Luiza Mbutu,
Catherine (Cindy)
MTAYARISHAJI BORA WA
NYIMBO WA MWAKA TAARAB – Enrico, Ababuu mwana wa Zanzibar na Bakunde.
MTAYARISHAJI BORA WA
NYIMBO WA MWAKA (BENDI) – Allan Mapigo, C9, Enrico, Amoroso na Ababuu mwana wa
Zanzibar.
WIMBO BORA WA REGGAE
– Niwe nawe ya Dabo, hakuna matata ya Lonka, tell me ya Dj Aron ft Fidempha,
bado nahitaji ya Chikaka ft Bless P & Lazzy B, Bongo reggae ya Warriors
from the east.
WIMBO BORA WENYE
VIONJO VYA ASILI YA KITANZANIA – Kwejaga nyangisha ya Batarokota, Nalonji ya
Kumpeneka, bora mchawi Dar bongo massive, tumbo lamsokota ya Ashimba, Aliponji
ya Wanakijiji na Agwemwana ya Cocodo african music band.
Monday, March 24, 2014
TAFADHALI ACHA KILA UNACHOFANYA NA SOMA HII, NI MUHIMU SANA.
Mwanamke huyu masikini yupo Labour sasa yapata siku mbili, tatizo ni kwamba ana hofu kubwa ya kufanyiwa upasuaji. Madaktari wamejaribu kufanya kila linalowezekana kwa uwezo wao lakini bado mambo yanelekea mrama.
Sasa kwa pamoja tuungane kumwambia Mungu kuwa hajalishi madaktari wamesema nini lakini Mama huyu ajifungue salama kwa njia sahihi.
Comment "Amen" kama unatarajia Taarifa nzuri hivi karibuni .Plezz DON'T IGNORE PLEASE SHARE FOR MORE PRAYERS! HII YAWEZA KUKUTOKEA HATA MAMA YAKO, DADA YAKO, MDOGO WAKO, HATA RAFIKI NA NDUGU YAKO WA KARIBU.....narudia usidharau plzzzzz

MBUNGE WA CCM AFIKISHWA KWA SPIKA KWA KUTOKUMLIPA MSHAHARA HOUSEBOY WAKE LIVE!!
Mbunge wa jimbo la Bahi (CCM) Omar Baduel amefikishwa kwa Katibu wa Bunge Dr Kashilila kwa kosa la kuto mlipa mshahara msaidizi wake wa jimbo kwa kipindi chote cha miaka minne,Said Kayumbo amelalamikia ofisi ya bunge na kuomba iingilie kati ili apate mshahara wake kwa miaka yote minne. Said kayumbo alisema mbunge huyo amekua akimpa 20,0000 au 30,000 wakati mshahara wa msaidizi wa mbunge ni 450,000.
Aidha mbunge huyo amekua na kashifa nyingi kama ile ya rushwa ambayo kesi yake inaendelea kisutu,mwezi wa february 2014 alisomewa tuhuma ya kula pesa ya mfuko wa jimbo,mwaka 2009 alifukuzwa uenyekiti wa halmashauri ya bahi kwa tuhumu za kuiba mifuko ya cement ya shirika la world vision kwenye kata yake ya Chipanga pamoja na tuhuma ya kushirikiana na mkurugenzi wa bah

SHOPRITE IMEUZWA WAFANYA KAZI WAGOMA NA KUANDAMANA MLIMANI CITY
Leo mida ya Jioni pale mlimani City nimeshuhudia wafanya kazi wa Duka Kubwa la Shoprite wakiwa wamegoma wakizua watu wasiingie kwenye duka hilo kwa kile kilichodaiwa kuwa duka hilo limeuzwa bila wao kupewa mafao yao ...Habari zilizopo ni kuwa duka hilo limenunuliwa na Super Market Ingine kubwa Nchini Kenya Ambayo inakuja kupanua biashara zake hapa Dar .....
ETI UGONJWA MKUBWA UNAOTUSUMBUA WA TANZANIA SIO UKIMWI WALA MALARIA NI HUU HAPA..NINI , EMBU SOMA KUJUA
Kwenye nchi zinazoendelea Tanzania ikiwemo magonjwa ya kuambukizwa yameonekana kuwa ndio tishio sana kwa afya za wananchi. Magonjwa kama ukimwi, malaria, TB, kichocho, kipindupindu na homa za matumbo yamekuwa yakisumbua sehemu kubwa ya watu katika nchi hizi.
Ili kuokoa afya za wananchi serikali za nchi hizi zinazoendelea zimekuwa zikiweka mipango kabambe ya kupambana na magonjwa haya. Mipango mingi iliyowekwa imefanikiwa ila sio kwa kiwango kikubwa sana. Hii ni kwa sababu kuna ugonjwa mwingine mkubwa zaidi ya magonjwa haya ya kuambukizwa unaosumbua wananchi.
Kabla hatujaangalia ugonjwa huo hebu tuangalie tofauti kati ya mataifa yenye magonjwa ya kuambukizwa na yale ambayo hayana kwa kiwango kikubwa. Ukiangalia kwa makini utagundua kwamba mataifa yanayosumbuliwa sana na magonjwa ya kuambukizwa ni mataifa ambayo watu wake ni masikini sana. Na hata ndani ya taifa sehemu ambazo magonjwa haya yameshamiri ni sehemu ambazo watu ni masikini. Nina hakika unajua kipindupindu huwa kinatokea maeneo gani sana sana.
Kwa mantiki hii basi ugonjwa mkubwa unaoisumbua nchi yetu sio ugonjwa wa kuambukiza bali ni umasikini. Umasikini ndio ugonjwa mkuu ambao unapoteza maisha ya wananchi wengi. Umasikini ndio ugonjwa mkubwa unaofanya maisha ya wananchi wengi kuwa magumu. Na kwa kuwa kwenye mipango ya kupambana na magonjwa umasikini haujawekwa, basi hakuna anayefunguka macho kuuangalia.
Ni umasikini unaofanya wengi kufanya ngono zembe na wakati mwingine ukahaba na kujikuta wanaambukizwa magonjwa ya zinaa na ukimwi. Ni umasikini unaofanya watu wakose maji safi na salama na kuishia kutumia maji machafu yanayowasababishia magonjwa ya tumbo na minyoo. Na ni umasikini unaofanya watu kukosa elimu na hivyo kushindwa kujikinga na magonjwa yanayoweza kuzuilika.
Tunawezaje kutokomeza ugonjwa huu?
Kwa kuwa ugonjwa huu hauko wazi basi serikali haijaweka mikakati ya kupambana nao au kuutokomeza. Hata baadhi ya mipango mingi iliyowahi kuwekwa kupambana na ugonjwa huu haikuzaa matunda yaliyotarajiwa na mwishowe kufa.
Mipango mingi imeshindwa kwa sababu serikali imekuwa ikiangalia sehemu isiyohusika kwenye kupambana na ugonjwa huu. Huwezi kuondoa umasikini kwa kutegemea misaada. Misaada haiondoi bali inaongeza umasikini.
Njia pekee ya kuondoa umasikini ni kuwajengea watu uwezo wa kufanya kazi yenye manufaa kwa watu wengine. Kuzalisha bidhaa au huduma zinazohitajika na watu wengine hivyo kutengeneza biashara kwa ngazi ya kitaifa na baadae kitaifa.
Serikali ingepaswa kuwajengea watu uwezo wa kuajiriwa, kujiajiri na kufanya biashara. Na kwa kuwa kuajiriwa nafasi hazitoshi basi kujiajiri na biashara ni njia nzuri za kupambana na ugonjwa huu. Kwa kuwa serikali haifanyi hivi je wewe unalala?
Usilale, tulishakubaliana kwamba usimlaumu yeyote, AMKA na chukua hatua juu ya maisha yako. Jijengee uwezo wa kujiajiri na kufanya biashara ili uweze kuutokomeza ugonjwa huu mbaya kwako, kwa familia yako na kwa jamii inayokuzunguka. Kama watu wachache tutachukua hatua hii baadae itasambaa na kufanyika na watu wanaotuzunguka na hatimaye taifa zima.
Unawezaje kujijengea uwezo?
Katika mtandao huu wa AMKA MTANZANIA tumeshajadili njia nyingi sana za kujijengea uwezo kwa kujifunza na kuchukua hatua. Anza kuzitumia njia hizi kwenye kazi na biashara zako na utaona mabadiliko makubwa. Kama wewe ni mgeni kwenye mtandao huu endelea kusoma makala nyingi utakutana na mawazo mengi juu ya kuchukua hatua na kubadilika.
Ili uweze kujiondoa kwenye ugonjwa huu wa umasikini inabidi ujue ni nini kinakufanya mpaka sasa unateseka na ugonjwa huo. Kwa kujua sababu itakuwa rahisi kwako kupambana nazo na hatimaye kushinda. Unaweza kuzijua sababu hizo kwa kusoma kitabu KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIO TAJIRI. Kupata kitabu hiko bonyeza maandishi hayo.
Njia kubwa ya kupambana na ugonjwa huu wa umasikini ni kujijengea uwezo. Na njia bora ya kujijengea uwezo ni kujifunza na kuchukua hatua ya kutekeleza yale unayojifunza. Kama unataka kujifunza zaidi juu ya biashara na mambo mengine jiunge na kisima cha maarifa na uchote maarifa yatakayokusaidia. Kujiunga na kisima cha maarifa bonyeza maandishi haya.
Kuanzia sasa jua ugonjwa namba moja unaotakiwa kupambana nao ni umasikini na usifikiri msaada utakusaidia kuondokana na umasikini.

Thursday, March 20, 2014
Wednesday, March 19, 2014
Tuesday, March 18, 2014
Rick Ross – Mastermind Tracklist Lyrics 2014
1. Intro
2. Rich Is
Gangsta
3. Drug Dealer's Dream
4. Shots
Fired
5. Nobody
6. The Devil
Is A Lie (feat. JAY Z)
7. Mafia
Music III (feat. Sizzla & Mavado)
8. War Ready
(feat. Jeezy)
9. What A
Shame
10. Supreme
11. BLK
& WHT
12. Dope Bitch Skit
13. In Vein
(feat. The Weeknd)
14.
Sanctified (feat. Kanye West & Big Sean)
15. Walkin On Air (feat. Meek Mill)
16. Thug Cry
(feat. Lil Wayne)
Deluxe
1. Blessing
In Disguise (feat. Scarface & Z-Ro)
2. Paradise Lost
3. You Know I Got It (Reprise)