Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Sufue Jumapili hii amelitaja baraza jipya la mawaziri.
Katika mabadiliko hayo mawaziri kadhaa wameondolewa kabisa kwenye baraza hilo,
wengine wamehamishiwa wizara, wengine wakipandishwa cheo huku kukiwepo sura
zingine mpya.
Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Sufue
Hata hivyo
hakuna mabadiliko kwenye Wizara za Uchukuzi, Ujenzi, Ofisi ya Rais, Ofisi ya
waziri Mkuu, Mambo ya nje, Afrika Mashariki, Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
na Kazi na Ajira.
Waziri wa
Fedha sasa ni Saada Mkuya huku manaibu wake wakiwa ni Mwigulu Nchemba na Adam
Malima. Nafasi hiyo iliachwa wazi kutokana na kifo cha Dr. Willliam Mgimwa
nchini Afrika Kusini mwanzoni mwa mwezi huu.
Wizara ya
Sheria na Katiba itakuwa chini ya Dr. Asha -Rose Migiro na naibu wake akibaki
kuwa Angela Kairuki na Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi imeenda kwa Dr
Titus Kamani huku naibu wake akiwa Kaika Telele.
Wizara ya
Maendeleo ya jamii jinsia na watoto imekabidhiwa kwa Sophia Simba na naibu wake
akiwa ni Pindi Chana.
Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi itaendelewa kuwa chini ya Shukuru Kawambwa na Naibu
wake ni Jenister Mhagama. Aliyekuwa naibu waziri wa mwanzo Philip Mulugo
ameondolewa.
Wizara ya
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi itaendelewa kuwa chini ya Anna Tibaijuka na
naibu wake akiwa George Simbachawene. Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika
waziri anabaki kuwa Christopher Chiza na naibu wake akiwa ni Godfrey Zambi na
Adam Malima akihamishiwa kwenye wizara ya fedha (Uchumi na Mapato).
Wizara ya
Nishati na Madini anabaki kuwa Prof Sospeter Muhongo na manaibu wake wakiwa ni
Steven Maselle na Charles Kitwanga. Wizara ya Maliasili na Utalii imekamatwa na
aliyekuwa naibu wake, Lazaro Nyalandu huku unaibu ukienda kwa Mahmoud Mgimwa.
Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii imeenda kwa aliyekuwa naibu Dr Seif Rashid na naibu
wake akipewa mbunge wa Serengeti Kebwe Stephen Kebwe huku ni Dr Hussein Mwinyi
aliyekuwa Waziri wa Afya akipewa wizara ya Ulinzi na JKT.
Wizara ya
Mambo ya ndani sasa itakuwa chini ya Mathias Chikawe aliyekuwa wizara ya Sheria
na Katiba, na naibu wake anaendelea kuwa Pereira Sillima. Nayo Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Waziri anabaki kuwa yuleyule Dr Fenella
Mukangara na shavu la unaibu likimwendea aliyekuwa mtangazaji wa TBC na mbunge
wa Kondoa Kusini, Juma Nkamia.
0 comments:
Post a Comment