Mtangazaji
wa BBC TV, Komla Dumor amefariki dunia ghafla jana akiwa nyumbani kwake mjini
London, Uingereza.Alikuwa na umri wa miaka 41.
Dumor
aliyezaliwa nchini Ghana alikuwa mtangazaji wa BBC World News na aliendesha
kipindi cha Focus on Africa.
Mtangazaji
huyo alijiunga na BBC kama mtangazaji wa radio mwaka 2007 baada ya kufanya kazi
ya uandishi wa habari kwa zaidi ya muongo mmoja nchini Ghana. Rais wa Ghana,
John Dramani Mahama aliandika kwenye mtandao wa Twitter kuwa nchi yake
imepoteza mmoja wa mabalozi wake muhimu.
Posted in:
0 comments:
Post a Comment