MKE wa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji mstaafu Damian
Lubuva amefariki akiwa nchini India alikokuwa akitibiwa ugonjwa wa kisukari.
Rais Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi, Lubuva kutokana na kifo
hicho cha Martha Lubuva kilichotokea Januari 17 katika Hospitali ya Apollo
iliyopo New Delhi, India.
“Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa
za kifo cha mke wako,” alisema Rais Kikwete kupitia taarifa iliyotolewa juzi
kwa vyombo vya habari. Alisema,
“Ninawahakikishia kuwa niko pamoja nanyi katika kuomboleza msiba huu
mkubwa.”Mwili wa marehemu unatarajiwa kuletwa leo, Dar es Salaam.
Wakati huo huo, Rais Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Katibu Mkuu
wa Chama Cha Mapinduzi, Abdulrahaman Kinana kutokana na kifo cha Kada wa chama,
Deusdedith Mtambalike.
Mtambalike aliyewahi kuwa Muu wa Wilaya katika Wilaya mbalimbali nchini,
alifariki dunia Januari 16 mwaka huu nchini Afrika Kusini, alikokuwa akipatiwa
matibabu.
Licha ya kuwa kada hodari wa CCM, Mtambalike aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya
za Ngara na Muleba Mkoani Kagera, Igunga Mkoa wa Tabora, Ludewa Mkoa wa Iringa
na Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma.
“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha
Mheshimiwa Deusdedith Makandila Mtambalike, Kada makini wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), na mmoja wa Viongozi makini katika Utumishi wa Umma aliyewahi kushika
wadhifa wa Mkuu wa Wilaya katika Wilaya mbalimbali hapa nchini”, alisema.
Rais Kikwete alisema alimfahamu Mtambalike, kama mmoja wa Wakuu wa
Wilaya aliyekuwa makini katika kazi zake, ambaye aliutumikia wadhifa huo kwa
umakini na uaminifu mkubwa. Alisema kifo chake ni pigo kwa CCM, ambako alitoa
mchango wa mawazo na ushauri.
0 comments:
Post a Comment