MICHAKATO

Levis Rocky Ndekeno

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Pages

Tuesday, December 31, 2013

ANGALIA MATUKIO YALIYOTIKISA MWAKA 2013



Zimebaki siku chache kabla ya kuuaga mwaka 2013, mwaka ambao umekuwa na matukio mengi yaliyoitikisa nchi ya Tanzania, huku mengine yakiipa sifa kubwa.
Historia ya Tanzania kuwa na Katiba Mpya itakayopatikana kutokana na maoni ya wananchi ilianza Desemba 31, 2011 wakati Rais Jakaya Kikwete akilihutubia taifa, alikiri wazi kuwa sasa inahitajika Katiba Mpya ili kuendana na wakati wa sasa.
Baadaye Rais Kikwete aliwateua wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba na ilianza kazi yake ya miezi 18, kuanzia Mei 3, mwaka 2012.
Tume hiyo ilikusanya maoni ya wananchi nchi nzima na kuandaa rasimu ya kwanza ya Katiba ambayo iliitoa Juni 4, mwaka huu.
Baada ya kutolewa kwa rasimu hiyo wananchi walipewa muda wa kuipitia na kuitolea maoni katika Mabaraza ya Katiba ya wilaya, yaliyokaa kuanzia Julai 12 mpaka Septemba 2, mwaka huu.
Maoni hayo yalikusanywa na tume hiyo kwa ajili ya kuyachambua na kutoa rasimu ya pili ya Katiba ambayo inatarajiwa kutolewa Desemba 30, mwaka huu.
Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilitakiwa kumaliza kazi ya kuandaa rasimu ya pili Desemba 15, mwaka huu, lakini Rais Kikwete aliiongezea siku 14 zaidi na hivyo kuifanya iweze kuendelea na kazi hadi Desemba 30.
Hatua hiyo ya Rais Kikwete kuiongezea muda tume hiyo ilikuwa ya pili, kwani mara ya kwanza tume hiyo iliomba kuongezewa muda wa siku 45, kuanzia Novemba Mosi hadi Desemba 15, mwaka huu.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Kabla ya kuomba kuongezewa muda mara ya kwanza, tume ilitakiwa kukamilisha kazi yake Novemba 30.
Kwa uamuzi wake, wa kuiongezea Tume hiyo siku nyingine 14, Rais Kikwete ameiongezea tume hiyo jumla ya siku 59 kati ya 60 ambazo anaruhusiwa kisheria.
Kifo cha Dk Sengondo Mvungi
Hatua  ya Rais kuiongezea muda Tume ya Mabadiliko ya Katiba  ilitafsiriwa kama kutoa fursa kwa wajumbe wa tume hiyo kujipanga upya baada ya kifo cha mmoja wa wajumbe wa tume hiyo, Dk Sengondo Mvungi aliyefariki dunia Novemba 12, mwaka huu nchini Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa baada ya kujeruhiwa kwa mapanga na watu wanaotuhumiwa kuwa majambazi, nyumbani kwake mkoani Dar es Salaam.
Ujio wa Rais wa Marekani Barack Obama
Ni siku mbili za kihistoria ambazo zimeweka rekodi ya aina yake katika historia ya nchi hii, kuanzia maandalizi  ya ujio wake mpaka alivyowasili nchini Julai 1 na kuondoa Julai 3, mwaka huu.
Shughuli nyingi na barabara kadhaa zilifungwa ili kutoa nafasi kwa ugeni huo mkubwa uliojumuisha familia yake, wafanyakazi wa ikulu, walinzi na makachero wa usalama kutoka nchini Marekani.
Katika ziara yake hiyo, Rais aliwekea mkazo umuhimu ambao Marekani inauweka katika ushirikiano wetu wa kina na unaoendelea kuimarika na nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara kupitia mipango mbalimbali ikiwemo ile ya kuimarisha ukuaji wa uchumi, uwekezaji na biashara, uimarishaji wa taasisi za kidemokrasia na uwekezaji katika kizazi kipya cha viongozi wa Kiafrika.
Ziara ya Rais wa China, Xi Jinping
Ziara hii ilitokea ikiwa ni wiki mbili tangu achaguliwe Xi Jinping kuwa Rais wa China,  ambapo aliichagua Tanzania kuwa nchi ya kwanza kuitembelea barani Afrika.
Katika ziara hiyo Rais Jinping  alikutana na viongozi mbalimbali nchini, kusaini mikataba ya kidiplomasia 19, ukiwemo wa ujenzi wa Bandari wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Akiwa nchini Rais Jinping alitoa hotuba yake ya kwanza tangu achaguliwe kushika wadhifa huo, ambayo iligusia masuala ya kiuchumi, kisiasa sambamba na kueleza msimamo wa nchi yake kwa Tanzania na Afrika.
Rais huyo alikutana pia na jumuiya ya watu wa China na kutembelea makaburi ya wataalamu wa Kichina ambayo yapo Majohe, Ukonga ambako alitoa heshima zake kwa Wachina waliofariki dunia wakati wakijenga reli ya Tazara.
Bomu la Arusha
Mei 5, mwaka 2013 ni siku ambayo haitafutika katika historia ya Tanzania kutokana na tukio la kusikitisha la kutupwa kwa bomu kanisani, ambapo watu watatu walifariki dunia na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa.
Tukio hilo lilitokea mbele ya Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa nchini Tanzania, Askofu Mkuu Francisco Montecillo, Askofu Mkuu Josephat Lebulu wa Jimbo Kuu la Arusha, walipokuwa wakizindua jengo la Kanisa Katoliki, Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Olasiti, Arusha.
Mgogoro wa gesi Mtwara
Maelfu ya wakazi wa Mkoa wa Mtwara waliandamana wakipinga uamuzi wa Serikali kusafirisha gesi kwa njia ya bomba, kutoka mkoani hapo kwenda Dar es Salaam.
Maandamano hayo yaliyoratibiwa na vyama vya Chadema,CUF, NCCR-Mageuzi, Sau, Tanzania Labour Party (TLP), APPT- Maendeleo, ADC, UDP na DP yakishirikisha wananchi wa wilaya za mkoa huo, zikiwamo Tandahimba na Newala, yalianzia katika Kijiji cha Mtawanya hadi Mtwara mjini kupitia barabara ya kwenda Msimbati eneo ambako gesi asilia inapatikana.
Kufuatia fujo na vurugu zilizotokea katika maandamano hayo risasi na mabomu yalirindima, hali iliyozua hofu na tafrani mkoani hapo.
Sakata la Sheikh Ponda
Tukio la kujeruhiwa kwa Katibu wa Jumuiya ya Kiislamu nchini, Shekhe Ponda Issa Ponda ilikuwa miongoni mwa habari zilizoibua mjadala mzito huku kukiwepo na hali ya sintofahamu kama kiongozi alijeruhiwa kwa risasi au kitu chenye ncha kali.
Mkasa huo wa aina yake ulitokea Agosti 10, mwaka huu majira ya saa 12: 15 za jioni eneo la Barabara ya Tumbaku karibu na Fire, mkoani Morogoro mara baada ya kumalizika kwa Kongamano la Kiislamu lililofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja Cha Ndege, Kata ya Saba Saba.
Baada ya tukio hilo, uvumi ulisambaa maeneo mbalimbali nchini ukidai kuwa Shekhe Ponda amepigwa risasi na polisi na kufariki dunia.
Kuporomoka kwa ghorofa
Ilikuwa ni asubuhi ya Machi 29 ambapo jengo la ghorofa 16 lililokuwa linajengwa katika Mtaa wa Indira Gandhi  jijini  Dar es Salaam, liliporomoka na kusababisha vifo vya watu 36 na wengine kadhaa kufunikwa na kifusi.
Kuporomoka kwa ghorofa hilo kulizua huzuni, taharuki na simanzi kwa ndugu na jamaa waliofika kwenye eneo la tukio kutaka kufahamu nini kimetokea hali iliyosababisha kusimama kwa shughuli mbalimbali katikati ya jiji.
Matukio ya tindikali Mwaka 2013 kumekuwa na matukio mengi wa watu kumwagiwa tindikali hususan upande wa Zanzibar, ambapo matukio kadhaa yaliripotiwa.
Julai 19 mwaka huu Said Mohamed Saad ambaye ni Mkurugenzi wa Home Shopping Center alimwagiwa tindikali na mtu asiyefahamika kisha kutokomea na kumuacha bilionea huyo katika maumivu makali.
Saad alipelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu lakini ilishindikana kutokana na madhara makubwa aliyoyapata kutokana na tindikali hiyo hali iliyosababishwa kupelekwa Ujerumani kwa matibabu zaidi.
Matukio mengine yalitokea Zanzibar kuhusisha  raia wawili wa Uingereza, Kate Gee na Kirstie Trup waliomwagiwa tindikali, eneo la Mji Mkongwe na Padri wa Parokia ya Machui, Anselmo Mwang’amba .
Siku chache baada ya tukio hilo lilitia doa nchi ya Tanzania katika ramani ya kimataifa, jeshi la Polisi upande wa Zanzibar lilitangaza kukamata lita 29 za tindikali.
Mauaji ya kutumia silaha
Mwaka huu pia kulikithiri kwa mauaji ya  kinyama kwa kutumia silaha ambapo watu kadhaa walijikuta wakipoteza maisha na wengine kujeruhiwa, kutokana na vitendo hivyo vilivyoonekana kushika kasi nchini.
Miongoni mwa matukio hayo ni mauaji ya Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Minara Miwili, Evarist Mushi ambaye alipigwa risasi na watu wasiofahamika asubuhi ya Februari 17 mwaka huu.
Mauaji mengine yalitokea Agosti 7 kwa mfanyabiashara maarufu wa madini Erasto Msuya kuuawa kwa kupigwa risasi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro. Msuya alikuwa anamiliki vitegauchumi kadhaa na kuaminika kama mfanyabiashara aliyekuwa akiongoza kwa utajiri Mirerani aliuawa kwa kupigwa risasi zaidi ya 20.
Tukio lingine la mauaji lillilotokea Oktoba 13  eneo la Kibamba ambalo kwa kiasi kikubwa lilihusishwa na  ugomvi wa  kimapenzi ambapo Mtangazaji wa Kituo cha ITV, Ufoo Saro alijeruhiwa kwa  risasi huku mama yake mzazi akipoteza maisha kutokana na shambulio lililofanywa na mzazi mwenzie aliyejulikana kama Anthery Mushi.
Operesheni Tokomeza
Operesheni  hii iliyolenga kupambana na vitendo vya ujangili dhidi ya wanyamapori ilianza rasmi Oktoba 5, mwaka huu katika hifadhi za taifa, mapori ya akiba na mbuga za wanyama huku ikishirikisha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi, Usalama wa Taifa, Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Idara ya Wanyamapori. Mawaziri wanne waliopoteza  nafasi zao kufuatia operesheni hiyo, nao ni Balozi Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), Dk David Mathayo (Mifugo na Uvuvi), Dk Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani ya Nchi) na Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na JKT).

Ni rasimu ya pili mfumo wa Muungano.

                                                                                                                                             
      Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo itakabidhi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, rasimu ya pili na ya mwisho ya katiba mpya, huku Watanzania wengi wakisubiri kwa hamu kubwa kuona inapendekeza muundo gani wa Muungano baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukataa serikali tatu. Kwa mujibu wa Katibu wa Tume hiyo, Assaa Rashidi, hafla ya kukabidhi rasimu ya pili itafanyika katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam. Hatua hiyo inachukuliwa na Tume hiyo inayoongozwa na Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, baada ya kupitia na kuchambua maboresho yaliyofanywa na mabaraza ya katiba ya wilaya ngazi ya kata kwenye rasimu ya kwanza ya katiba mpya miezi saba iliyopita. Rasimu ya kwanza ya katiba mpya, ambayo ilijadiliwa na mabaraza ya katiba, kuanzia Julai 12 mpaka Septemba 2, ilizinduliwa na Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Juni 4, mwaka huu. Mambo makubwa yaliyopendekezwa kwenye rasimu ya kwanza ya katiba mpya ni pamoja na mfumo wa Muungano wa serikali tatu. Mengine ni kuruhusiwa mgombea binafsi, rais kutangazwa kushinda akipata zaidi ya asilimia 50 ya kura zote zilizopigwa la sivyo uchaguzi urudiwe kwa wagombea wawili wa nafasi hiyo walioongoza kwa kura. Mependekezo mengine yaliyopendekezwa ni tume huru ya uchaguzi, mawaziri kutokuwa wabunge, idadi ya mawaziri kutozidi 15 na spika wa bunge kutokuwa mbunge. Pamoja na yote hayo, jambo kubwa lililopendekezwa na rasimu ya kwanza lililoishughulisha CCM ni mfumo wa Muungano wa serikali tatu. Hali hiyo ilikifanya chama hicho Juni 10, mwaka huu, kutoa mwongozo kwa wanachama wake kuhusu rasimu ya kwanza ya katiba mpya, kikipinga mambo mengi yaliyomo ndani yake. Kwa mujibu wa mwongozo huo ni kama vile CCM ilitaka kuendelea na katiba iliyopo, kwa kuwa inaunga mkono mambo mengi ya katiba hiyo na kupinga yaliyopendekezwa kwenye rasimu ya kwanza ya katiba mpya. Mwongozo huo ulitolewa baraka za kikao cha Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu (Nec) ya CCM, kilichofanyika mjini Dodoma, ikiwa ni siku saba tangu Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutoa rasimu ya kwanza ya katiba mpya. Katika mwongozo huo CCM iliichambua Ibara ya 57-66 ya rasimu ya katiba ya kwanza inayoeleza kuwapo kwa mfumo wa serikali tatu, ambao utakuwa wa shirikisho linaloundwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Tanzania Bara. Sura hiyo pia inaeleza kuwa shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kusimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Bunge la Jamhuri ya Muungano na Mahakama ya Jamhuri ya Muungano. Katika mwongozo huo, CCM ilieleza kuwa pendekezo hilo ni tofauti na sera yake kuhusu muundo wa Muungano wenye serikali mbili, ambazo ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano na SMZ. Mbali na kutoa mwongozo huo, Juni 11, mwaka huu, CCM ilitangaza uamuzi wake wa kuijadili rasimu ya kwanza ya katiba mpya, kuanzia ngazi ya matawi, wilaya na Taifa ili kupata maoni ya wanachama na kuweka msimamo wake. Hata hivyo, CCM kupitia Katibu wake wa Nec, Itikadi na Uenezi Taifa, Nape Nnauye, ilisema maoni ambayo yangetolewa na wanachama wake yangepaswa kuzingatia maoni ya chama hicho yaliyotolewa mwanzoni mwa mchakato wa mabadiliko ya katiba. Hata hivyo, hadi rasimu ya pili inakabidhiwa leo kwa marais hao, CCM haijawahi kuweka wazi msimamo wake kuhusu rasimu ya kwanza ya katiba mpya. Lakini habari kutoka ndani ya kikao cha Nec, kilichofanyika mjini Dodoma, Agosti 25, mwaka huu, zilizochapishwa na baadhi ya vyombo vya habari, ambazo CCM haikuzikanusha, zilieleza kuwa michango iliyotolewa na wajumbe wa kikao hicho, wengi waling’ang’ania mfumo wa serikali mbili kama ilivyo kwenye ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya mwaka 2010. Kwa mujibu wa chanzo hicho, baadhi ya waliopinga walisema kuna haja ya kuendelea na mfumo wa serikali mbili, kwa kuwa ndio unaokubalika. Hata hivyo, katika kikao hicho, Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete alinukuliwa akiwataka wana CCM nchini, kujiandaa kisaikolojia juu ya muundo wa serikali tatu pindi Watanzania watakapoamua hivyo. Chanzo hicho cha habari kilisema Rais Kikwete alitoa kauli hiyo baada ya Katibu wa Nec, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa CCM, Dk. Asha Rose-Migiro, kuwasilisha hoja yake katika kikao hicho kilichokaa kama Baraza la Katiba. Licha ya Rais Kikwete kutoa wito huo kwa wana CCM, Oktoba 2, mwaka huu, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya chama hicho, Abdallah Bulembo, aliendeleza kauli zinazoonyesha kumuingilia na kumshambulia vikali Jaji Warioba kwa kumtaka aache kuwasemea Watanzania juu ya aina ya katiba wanayoitaka. Bulembo alimshambulia Jaji Warioba alipokuwa mkoani Tanga, wakati akihutubia moja ya mikutano ya hadhara ya wanachama wa CCM. Bulembo alinukuliwa katika vyombo vya habari akisema kuwa siyo sahihi kwa Jaji Warioba kuwa msemaji wa Watanzania kuhusiana na mambo wanayoyataka yaingizwe ndani ya katiba. “Jaji Warioba ni mmoja kati ya Watanzania mamilioni na kwa hali hiyo hawezi kubeba mawazo ya Watanzania wengine, ni vizuri akasimamia rasimu, badala ya kuwa msemaji wa wananchi,” alisema Bulembo ambaye pia ni Mjumbe wa CC ya CCM. Bulembo alitoa kauli hiyo wakati kukiwa na msuguano kati ya CCM na serikali yake kwa upande mmoja, na vyama vitatu vya upinzani vyenye wabunge ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kabla ya hapo, mwishoni mwa Septemba, mwaka huu, Jaji Warioba akizungumza na waandishi wa habari, aliwakemea baadhi ya viongozi wa kisiasa kwa kuiingilia mchakato wa kupata katiba mpya unaoendelea. Alisema baadhi ya changamoto zilizojitokeza wakati wa kuendesha mabaraza ya katiba, ni kwa baadhi ya vyama vya siasa kuingilia uhuru wa wajumbe katika kutoa maoni kuhusu Rasimu ya Katiba, wakiwafundisha nini cha kusema. Jaji Warioba aliwasihi viongozi wa vyama vya siasa kuwaachia wananchi, cha kusema kwani, katiba inayotafutwa ni ya wananchi, na si ya vyama au kundi fulani. Aidha, Oktoba 3, mwaka jana, Jaji Warioba alitoa karipio kwa Bulembo kwa kumtaka aache kupiga kelele dhidi yake kwa kuwa hakumtuma kazi ya kukusanya maoni ya katiba mpya, bali alitumwa na serikali kwa niaba ya wananchi. Jaji Warioba alisema Bulembo amekuwa na ajenda ya siri dhidi yake (Warioba) na baadhi ya wajumbe wa Tume kwa kuwa amekuwa akiwazungumzia wao binafsi kila anaposisimama katika majukwaa ya kisiasa. Alimtaka Bulembo kuthibitisha kuhusu kauli ambazo amekuwa akizitoa kwenye mikutano ya CCM katika mikoa ya Arusha, Tanga na Mbeya kuwa yeye (Warioba) amegeuka kuwa msemaji wa wananchi katika mchakato mzima wa kupata Katiba mpya. Jaji Warioba alitamtahadharisha Bulembo na kumtaka kuacha kupiga kelele pamoja na kumshambulia badala yake azungumzie masuala yanayohusu rasimu ya katiba na siyo kuwajadili wajumbe. Aidha, Jaji Warioba alimtaka Bulembo kuthibitisha kama kauli ambazo alizitoa kwa nyakati tofauti katika mikoa hiyo ametumwa na CCM ama ni kauli zake binafsi. Jaji Warioba alisisitiza kuwa siku zote Tume yake imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria na kuwataka wanasiasa akiwamo Bulembo kujadili rasimu iliyotolewa badala ya Tume au wajumbe wake. Alisema hakutumwa na CCM kufanya kazi anayoifanya na kwamba kazi hiyo alipewa na serikali kwa mujibu wa sheria na kwamba ataendelea kuifanya bila kusikiliza maneno yanayosemwa dhidi yake. Jaji Warioba alisema kauli zilizotolewa na Bulembo kwa nyakati mbalimbali zilichangia mchakato wa katiba kuwa mgumu hususani wakati wananchi walipokuwa wakitoa maoni kupitia mabaraza ya katiba mkoani Mbeya. Alisema haogopi wala hatetereki kwa kuwa anafanya kazi aliyotumwa na wananchi. Alisema CCM iliishawasilisha maoni yake walipopewa nafasi ya kufanya hivyo, na kwamba masuala mengine yanayojitokeza zikiwamo kauli za Bulembo baada ya hapo hajui zinatoka wapi. Mbali na Bulembo, makada mbalimbali wa CCM nchini tangu kutolewa kwa rasimu ya kwanza ya katiba walikuwa wanamshambulia Jaji Warioba binafsi kwamba ndiye anayeshinikiza mfumo wa serikali tatu kwa manufaa yake binafsi. Wapo wanachama wa CCM na makada wa chama hicho ambao wakati wa mikutano ya mabaraza walisikika wakitoa kauli za matusi na kashfa dhidi ya Jaji Warioba kwa madai kuwa ana lengo la kuuvunja Muungano. Ikiwa Tume leo itapendekeza mfumo wa serikali tatu, kuna uwezekano wa baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM ambao wataibuka tena nakumshambulia Jaji Warioba kutokana na maamuzi hayo. Kama mfumo wa serikali tatu utaridhiwa tena na tume, suala hilo huenda likazua mjadala mkali na malumbano katika Bunge Maalum la Katiba ambalo CCM kina wajumbe wengi. Kama tume itabadili msimamo wake wa awali na kutangaza mfumo wa Muungano wa serikali mbili, itakuwa imeipa CCM furaha na kicheko.
KAULI YA NAPE
Nape alipoulizwa na NIPASHE jana iwapo rasimu ya pili ya katiba mpya itapendekeza muundo wa Muungano wa serikali tatu CCM itachukua hatua gani, alijibu: “Kwanini tubashiri? Si usubiri kesho (leo) itokee.” Tume ya Mabadiliko ya Katiba yenye wajumbe 30; wakiwamo 15 kutoka Tanzania Bara na 15 kutoka Zanzibar, ilitangazwa na Rais Kikwete, Aprili 6 na kuapishwa Aprili 13, mwaka jana. Ilianza rasmi kazi ya kukusanya maoni ya wananchi Mei mosi, mwaka jana. Baada ya kukamilisha kazi hiyo, iliyachambua na kuandika Rasimu ya Katiba. Kazi ya kukusanya maoni hayo iliwahusisha wananchi mmoja mmoja kupitia mikutano ya hadhara na ilikamilishwa na Tume Desemba, mwaka jana. Baadaye Tume ilikutana na makundi maalumu na watu mashuhuri, wakiwamo viongozi wakuu wastaafu na waliopo madarakani Januari 7-28, mwaka huu. Baadaye, mabaraza ya katiba yaliipitia Rasimu ya Katiba kuanzia Julai 12 hadi Septemba 2, mwaka huu na kutoa mapendekezo yake, ambayo yaliwasilishwa kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Tume iliendelea kuyachambua kabla ya kukabidhi rasimu ya pili ya katiba kwa Rais Kikwete na Rais Dk. Shein leo. Baada ya rasimu ya pili ya katiba mpya kukabidhiwa kwa marais hao, itachapishwa katika Gazeti la Serikali na kwenye magazeti mengine ndani ya siku 31. Katika kipindi hicho, Rais ataitisha kikao cha Bunge Maalumu la Katiba kwa ajili ya kupitisha rasimu ya pili ya katiba mpya iliyopendekezwa. Bunge Maalumu la Katiba, ambalo litafanyika kwa siku zisizozidi 70, linatarajiwa kuanza rasmi Februari, mwakani, kwa ajili ya kujadili na kuipitisha rasimu ya pili ya katiba iliyopendekezwa. Baada ya rasimu ya pili kupitishwa na Bunge Maalumu la Katiba, itaitishwa kura ya maoni, ambayo itatoa fursa kwa wananchi kuamua ama kuikubali au kuikataa.

Jaji Joseph Warioba.
Ni rasimu ya pili mfumo wa Muungano.
Nape: Tusubiri tuone kitakachotokea
. Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo itakabidhi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, rasimu ya pili na ya mwisho ya katiba mpya, huku Watanzania wengi wakisubiri kwa hamu kubwa kuona inapendekeza muundo gani wa Muungano baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukataa serikali tatu.
Kwa mujibu wa Katibu wa Tume hiyo, Assaa Rashidi, hafla ya kukabidhi rasimu ya pili itafanyika katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam. Hatua hiyo inachukuliwa na Tume hiyo inayoongozwa na Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, baada ya kupitia na kuchambua maboresho yaliyofanywa na mabaraza ya katiba ya wilaya ngazi ya kata kwenye rasimu ya kwanza ya katiba mpya miezi saba iliyopita. Rasimu ya kwanza ya katiba mpya, ambayo ilijadiliwa na mabaraza ya katiba, kuanzia Julai 12 mpaka Septemba 2, ilizinduliwa na Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Juni 4, mwaka huu Mambo makubwa yaliyopendekezwa kwenye rasimu ya kwanza ya katiba mpya ni pamoja na mfumo wa Muungano wa serikali tatu. Mengine ni kuruhusiwa mgombea binafsi, rais kutangazwa kushinda akipata zaidi ya asilimia 50 ya kura zote zilizopigwa la sivyo uchaguzi urudiwe kwa wagombea wawili wa nafasi hiyo walioongoza kwa kura. Mependekezo mengine yaliyopendekezwa ni tume huru ya uchaguzi, mawaziri kutokuwa wabunge, idadi ya mawaziri kutozidi 15 na spika wa bunge kutokuwa mbunge. Pamoja na yote hayo, jambo kubwa lililopendekezwa na rasimu ya kwanza lililoishughulisha CCM ni mfumo wa Muungano wa serikali tatu. Hali hiyo ilikifanya chama hicho Juni 10, mwaka huu, kutoa mwongozo kwa wanachama wake kuhusu rasimu ya kwanza ya katiba mpya, kikipinga mambo mengi yaliyomo ndani yake. Kwa mujibu wa mwongozo huo ni kama vile CCM ilitaka kuendelea na katiba iliyopo, kwa kuwa inaunga mkono mambo mengi ya katiba hiyo na kupinga yaliyopendekezwa kwenye rasimu ya kwanza ya katiba mpya. Mwongozo huo ulitolewa baraka za kikao cha Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu (Nec) ya CCM, kilichofanyika mjini Dodoma, ikiwa ni siku saba tangu Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutoa rasimu ya kwanza ya katiba mpya. Katika mwongozo huo CCM iliichambua Ibara ya 57-66 ya rasimu ya katiba ya kwanza inayoeleza kuwapo kwa mfumo wa serikali tatu, ambao utakuwa wa shirikisho linaloundwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Tanzania Bara. Sura hiyo pia inaeleza kuwa shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kusimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Bunge la Jamhuri ya Muungano na Mahakama ya Jamhuri ya Muungano. Katika mwongozo huo, CCM ilieleza kuwa pendekezo hilo ni tofauti na sera yake kuhusu muundo wa Muungano wenye serikali mbili, ambazo ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano na SMZ. Mbali na kutoa mwongozo huo, Juni 11, mwaka huu, CCM ilitangaza uamuzi wake wa kuijadili rasimu ya kwanza ya katiba mpya, kuanzia ngazi ya matawi, wilaya na Taifa ili kupata maoni ya wanachama na kuweka msimamo wake. Hata hivyo, CCM kupitia Katibu wake wa Nec, Itikadi na Uenezi Taifa, Nape Nnauye, ilisema maoni ambayo yangetolewa na wanachama wake yangepaswa kuzingatia maoni ya chama hicho yaliyotolewa mwanzoni mwa mchakato wa mabadiliko ya katiba. Hata hivyo, hadi rasimu ya pili inakabidhiwa leo kwa marais hao, CCM haijawahi kuweka wazi msimamo wake kuhusu rasimu ya kwanza ya katiba mpya. Lakini habari kutoka ndani ya kikao cha Nec, kilichofanyika mjini Dodoma, Agosti 25, mwaka huu, zilizochapishwa na baadhi ya vyombo vya habari, ambazo CCM haikuzikanusha, zilieleza kuwa michang iliyotolewa na wajumbe wa kikao hicho, wengi waling’ang’ania mfumo wa serikali mbili kama ilivyo kwenye ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya mwaka 2010. Kwa mujibu wa chanzo hicho, baadhi ya waliopinga walisema kuna haja ya kuendelea na mfumo wa serikali mbili, kwa kuwa ndio unaokubalika. Hata hivyo, katika kikao hicho, Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete alinukuliwa akiwataka wana CCM nchini, kujiandaa kisaikolojia juu ya muundo wa serikali tatu pindi Watanzania watakapoamua hivyo. Chanzo hicho cha habari kilisema Rais Kikwete alitoa kauli hiyo baada ya Katibu wa Nec, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa CCM, Dk. Asha Rose-Migiro, kuwasilisha hoja yake katika kikao hicho kilichokaa kama Baraza la Katiba. Licha ya Rais Kikwete kutoa wito huo kwa wana CCM, Oktoba 2, mwaka huu, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya chama hicho, Abdallah Bulembo, aliendeleza kauli zinazoonyesha kumuingilia na kumshambulia vikali Jaji Warioba kwa kumtaka aache kuwasemea Watanzania juu ya aina ya katiba wanayoitaka. Bulembo alimshambulia Jaji Warioba alipokuwa mkoani Tanga, wakati akihutubia moja ya mikutano ya hadhara ya wanachama wa CCM. Bulembo alinukuliwa katika vyombo vya habari akisema kuwa siyo sahihi kwa Jaji Warioba kuwa msemaji wa Watanzania kuhusiana na mambo wanayoyataka yaingizwe ndani ya katiba. “Jaji Warioba ni mmoja kati ya Watanzania mamilioni na kwa hali hiyo hawezi kubeba mawazo ya Watanzania wengine, ni vizuri akasimamia rasimu, badala ya kuwa msemaji wa wananchi,” alisema Bulembo ambaye pia ni Mjumbe wa CC ya CCM. Bulembo alitoa kauli hiyo wakati kukiwa na msuguano kati ya CCM na serikali yake kwa upande mmoja, na vyama vitatu vya upinzani vyenye wabunge ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kabla ya hapo, mwishoni mwa Septemba, mwaka huu, Jaji Warioba akizungumza na waandishi wa habari, aliwakemea baadhi ya viongozi wa kisiasa kwa kuiingilia mchakato wa kupata katiba mpya unaoendelea. Alisema baadhi ya changamoto zilizojitokeza wakati wa kuendesha mabaraza ya katiba, ni kwa baadhi ya vyama vya siasa kuingilia uhuru wa wajumbe katika kutoa maoni kuhusu Rasimu ya Katiba, wakiwafundisha nini cha kusema. Jaji Warioba aliwasihi viongozi wa vyama vya siasa kuwaachia wananchi, cha kusema kwani, katiba inayotafutwa ni ya wananchi, na si ya vyama au kundi fulani. Aidha, Oktoba 3, mwaka jana, Jaji Warioba alitoa karipio kwa Bulembo kwa kumtaka aache kupiga kelele dhidi yake kwa kuwa hakumtuma kazi ya kukusanya maoni ya katiba mpya, bali alitumwa na serikali kwa niaba ya wananchi. Jaji Warioba alisema Bulembo amekuwa na ajenda ya siri dhidi yake (Warioba) na baadhi ya wajumbe wa Tume kwa kuwa amekuwa akiwazungumzia wao binafsi kila anaposisimama katika majukwaa ya kisiasa. Alimtaka Bulembo kuthibitisha kuhusu kauli ambazo amekuwa akizitoa kwenye mikutano ya CCM katika mikoa ya Arusha, Tanga na Mbeya kuwa yeye (Warioba) amegeuka kuwa msemaji wa wananchi katika mchakato mzima wa kupata Katiba mpya. Jaji Warioba alitamtahadharisha Bulembo na kumtaka kuacha kupiga kelele pamoja na kumshambulia badala yake azungumzie masuala yanayohusu rasimu ya katiba na siyo kuwajadili wajumbe. Aidha, Jaji Warioba alimtaka Bulembo kuthibitisha kama kauli ambazo alizitoa kwa nyakati tofauti katika mikoa hiyo ametumwa na CCM ama ni kauli zake binafsi. Jaji Warioba alisisitiza kuwa siku zote Tume yake imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria na kuwataka wanasiasa akiwamo Bulembo kujadili rasimu iliyotolewa badala ya Tume au wajumbe wake. Alisema hakutumwa na CCM kufanya kazi anayoifanya na kwamba kazi hiyo alipewa na serikali kwa mujibu wa sheria na kwamba ataendelea kuifanya bila kusikiliza maneno yanayosemwa dhidi yake. Jaji Warioba alisema kauli zilizotolewa na Bulembo kwa nyakati mbalimbali zilichangia mchakato wa katiba kuwa mgumu hususani wakati wananchi walipokuwa wakitoa maoni kupitia mabaraza ya katiba mkoani Mbeya. Alisema haogopi wala hatetereki kwa kuwa anafanya kazi aliyotumwa na wananchi. Alisema CCM iliishawasilisha maoni yake walipopewa nafasi ya kufanya hivyo, na kwamba masuala mengine yanayojitokeza zikiwamo kauli za Bulembo baada ya hapo hajui zinatoka wapi. Mbali na Bulembo, makada mbalimbali wa CCM nchini tangu kutolewa kwa rasimu ya kwanza ya katiba walikuwa wanamshambulia Jaji Warioba binafsi kwamba ndiye anayeshinikiza mfumo wa serikali tatu kwa manufaa yake binafsi. Wapo wanachama wa CCM na makada wa chama hicho ambao wakati wa mikutano ya mabaraza walisikika wakitoa kauli za matusi na kashfa dhidi ya Jaji Warioba kwa madai kuwa ana lengo la kuuvunja Muungano. Ikiwa Tume leo itapendekeza mfumo wa serikali tatu, kuna uwezekano wa baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM ambao wataibuka tena nakumshambulia Jaji Warioba kutokana na maamuzi hayo. Kama mfumo wa serikali tatu utaridhiwa tena na tume, suala hilo huenda likazua mjadala mkali na malumbano katika Bunge Maalum la Katiba ambalo CCM kina wajumbe wengi. Kama tume itabadili msimamo wake wa awali na kutangaza mfumo wa Muungano wa serikali mbili, itakuwa imeipa CCM furaha na kicheko.

KAULI YA NAPE
Nape alipoulizwa na NIPASHE jana iwapo rasimu ya pili ya katiba mpya itapendekeza muundo wa Muungano wa serikali tatu CCM itachukua hatua gani, alijibu: “Kwanini tubashiri? Si usubiri kesho (leo) itokee.” Tume ya Mabadiliko ya Katiba yenye wajumbe 30; wakiwamo 15 kutoka Tanzania Bara na 15 kutoka Zanzibar, ilitangazwa na Rais Kikwete, Aprili 6 na kuapishwa Aprili 13, mwaka jana. Ilianza rasmi kazi ya kukusanya maoni ya wananchi Mei mosi, mwaka jana. Baada ya kukamilisha kazi hiyo, iliyachambua na kuandika Rasimu ya Katiba. Kazi ya kukusanya maoni hayo iliwahusisha wananchi mmoja mmoja kupitia mikutano ya hadhara na ilikamilishwa na Tume Desemba, mwaka jana. Baadaye Tume ilikutana na makundi maalumu na watu mashuhuri, wakiwamo viongozi wakuu wastaafu na waliopo madarakani Januari 7-28, mwaka huu. Baadaye, mabaraza ya katiba yaliipitia Rasimu ya Katiba kuanzia Julai 12 hadi Septemba 2, mwaka huu na kutoa mapendekezo yake, ambayo yaliwasilishwa kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Tume iliendelea kuyachambua kabla ya kukabidhi rasimu ya pili ya katiba kwa Rais Kikwete na Rais Dk. Shein leo. Baada ya rasimu ya pili ya katiba mpya kukabidhiwa kwa marais hao, itachapishwa katika Gazeti la Serikali na kwenye magazeti mengine ndani ya siku 31. Katika kipindi hicho, Rais ataitisha kikao cha Bunge Maalumu la Katiba kwa ajili ya kupitisha rasimu ya pili ya katiba mpya iliyopendekezwa. Bunge Maalumu la Katiba, ambalo litafanyika kwa siku zisizozidi 70, linatarajiwa kuanza rasmi Februari, mwakani, kwa ajili ya kujadili na kuipitisha rasimu ya pili ya katiba iliyopendekezwa. Baada ya rasimu ya pili kupitishwa na Bunge Maalumu la Katiba, itaitishwa kura ya maoni, ambayo itatoa fursa kwa wananchi kuamua ama kuikubali au kuikataa.


Sunday, December 29, 2013

THE REAL RICK ROSS

Wakati wakuaga Mwili wa Langa

Mazishi ya Langa

The Life Story of lil Wayne Pt 2

The Life Story of lil Wayne Pt 1

Young Money - Girl I Got You



REMNANT CHRISTIAN CENTRE

Saturday, December 28, 2013

Enoch Mankayi Sontonga

Enoch Mankayi Sontonga 1873 - 18 April 1905 was the composer of Nkosi Sikelel' iAfrika (God Bless Africa), which has been part of the South African national anthem since 1994. It was also the official African National Congress (ANC) anthem since 1925 and is still the national anthem of Tanzania and Zambia. It was also sung in Zimbabwe and Namibia for many years. Sontonga, a Xhosa, was born in the city of Uitenhage in the Eastern Cape. He trained as a teacher at the Lovedale Institution and subsequently worked as a teacher and choirmaster at the Methodist Mission school in Nancefield, near Johannesburg for eight years. Sontonga married and had a son. His wife, Diana Mgqibisa, died in 1929. The first verse and chorus of Nkosi Sikelel' iAfrika was composed in 1897 and it was originally intended to be a school anthem . He wrote the tune the same year. It was first sung in public in 1899 at the ordination of Reverend Mboweni who was the first Tsonga Methodist minister.Later the Xhosa poet Samuel Mqhayi wrote a further seven verses. Sontonga died in 1905.The song started to be more well known after John Langalibalele Dube's Ohlange Institute's choir used it. They played it at the South African Native National Congress meeting in 1912. It was sung after the closing prayer and the ANC adopted it as its official closing anthem in 1925. It was recorded in London as "Nkosi sikelel’ iAfrika" in 1923 and it was published by the Lovedale Press in 1927.For many years the site of the grave of Sontonga was unknown, but it was finally located in the "Native Christian" section of the Braamfontein cemetery in the early 1990s; one of the reasons why his grave could not be found is that it was listed under "Enoch" and not "Sontonga".On 24 September 1996, the grave of Sontonga was declared a national monument and a memorial on the site was unveiled by President Nelson Mandela. At the same ceremony the South African Order of Meritorious Service (Gold) was bestowed on Enoch Sontonga posthumously.

Tuesday, December 24, 2013

Lil Wayne's Musical Career




 
Lil Wayne had begun to develop his interest in hip hop and rap music.The newest addition to the many "Lil's" in the hip hop music industry  by Cash Money Recording artists like Pimp Daddy and U.N.L.V., he began rapping at block parties. His performance at one of the parties caught the attention of Lil Slim, a Cash Money rapper. Through the recording artist, Lil Wayne met the Cash Money Records moguls, Brian "Baby" Williams and Ronald "Slim" Williams. Though his free styling talent left strong impressions on the two tycoons, Lil Wayne did not get a contract with Cash Money until he repeatedly left freestyles recording on Baby's answering machine.  At the tender age of 11 years old, Lil Wayne at last got his shot to sign up with Cash Money, being the Records' youngest rapper. A year after signing the contract, Lil Wayne caught in an incident that almost took his life. He accidentally shot himself in chest with his stepfather gun, putting him on life support for two weeks.  Recovering from his incident, Lil Wayne marched on to welcome his first gig, in which he was hooked up with another newcomer, Lil' Doggie, later more well-known as B.G., to form a rap group The B.G.'z. With this group, the young rapper only recorded and released one album, "True Story" (1995), which did not sell.It was during this time that he was forced to drop out of 10th grade. He has a daughter, Reginae Carter, with high school sweetheart, Antonia, but was not allowed to meet his child. However, things quickly changed for the better after his stepfather passed away in early 1997. Getting permission to work with Baby once more, he left his unsuccessful stories behind and then embarked to form a new group, called "The Hot Boys", with Juvenile, Turk, and B.G in 1997. Quickly, he and his group went on recording their notable debut album "Get It How You Live" (1997) ,"400 Degreez" (1998). It was supposed to be the album that beat the sales record of Juvenile's, who left Cash Money earlier. However, the sales of the album proved to be disappointing, selling only 536,000 copies in U.S. and 900,000 copies worldwide followed by "Guerilla Warfare" (1999), "Tha Block is Hot" (1999),that he really got his big break, being known all over the States. His solo album peaked at number three on Billboard's album chart and at number one on Billboard Top R'n'B/Hip-Hop Albums, went double platinum upon its release and even his lowest selling album is still certified as gold upon the album release by Recording Industry Association of America (RIAA). Despite his success in the music industry, Lil Wayne's childhood experiences, like many other rap and hip hop singers, were far from perfect.both albums earned them mild fame throughout the South and Midwest., while at the same time scoring him a nomination for 2000 Source Award for New Artist of the Year, Solo.  In the years to follow, the rapper who was originated from the 17th Ward of New Orleans released "Lights Out" (2000). The album was certified gold but did not achieve the same level of success as his debut album. Two singles were released from the album, 'Get Off The Corner' and 'Shine.' Despite the fact that the group was considerably successful, Lil Wayne and his friends officially went on their separate ways in 2001."500 Degreez" (2002), both failing to match the success of his seminal debut, receiving only gold certification from the Recording Industry Association of America (RIAA). His "500 Degreez" album got its name from Juvenile's multi-platinum album. In June 2004, this young American artist released his most recognized album yet, "Tha Carter" that peaked at number five on Billboard 200, and at number two on Billboard Top R'n'B/Hip-Hop Albums. Around this time, he collaborated with Destiny's Child and T.I. for the noteworthy Destiny's Child's song "Soldier", earning him prominent nominations, naming some were 2005 BET Award-Best Collaboration and 2006 Grammy Award-Best Rap/Sung Collaboration.Following the accomplishment of album "Tha Carter" and collaboration single "Soldier", he released "Tha Carter II" (2005) was a huge success, selling over 238,000 copies in its first week on sale. The lead single, 'Fireman' went into the US singles chart at number 32 and was followed with the release of 'Grown Man', 'Hustler Muzik' and 'Shooter'. That same year, Lil Wayne was made president of the Cash Money enterprise, as well as founding Young Money Entertainment.In the period of 2006 to 2007, he gained more fans. In 2007, however, Lil Wayne stepped down from these roles.Lil Wayne has appeared on a number of mixtapes and tracks by other artists, including Birdman, DJ Drama, Chris Brown and DJ Khaled.The release of Lil Wayne's next album, Tha Carter III was delayed when some of the tracks were leaked. As a response, he released the four leaked tracks as well as a few new tracks, as an interim album named The Leak. Tha Carter III was eventually released in June 2008 and sold over 1 million copies in its first week. The album's lead single, 'Lollipop', featuring Static, became Lil Wayne's most successful single to date. In 2007, however, Lil Wayne stepped down from these roles.Lil Wayne has appeared on a number of mixtapes and tracks by other artists, including Birdman, DJ Drama, Chris Brown and DJ Khaled.The release of Lil Wayne's next album, Tha Carter III was delayed when some of the tracks were leaked. As a response, he released the four leaked tracks as well as a few new tracks, as an interim album named The Leak. Tha Carter III was eventually released in June 2008 and sold over 1 million copies in its first week. The album's lead single, 'Lollipop', featuring Static, became Lil Wayne's most successful single to date. His star continued to shine as every albums he made in the following years sold quite well and climbed to notable spots on the charts. "Rebirth" in 2010 was certified gold despite getting panned by critics. "I Am Not a human Being" in the same year fared better as not only did it make it into the top 10 of Hot 200 like many of his other creations but he also gained back respect from the music reviewers.  He came back to his fullest in 2011 when releasing the fourth installment of "Tha Carter", selling 964,000 copies in its first week. Through "Tha Charter IV", he posted the biggest sales week for a male solo artist of all time after Usher's "Confessions" (1.10 million) and Garth Brooks' "Double Live" (1.09 million). He occupied the third and fourth places at the same time with his first best sales week contributed by "Tha Charter III", before Justin Timberlake barged in with "The 20/20 Experience" which pulled "Tha Carter IV" to the fifth slot on the list.After taking a rest from releasing an album, Weezy returned in 2013 with the second installment of "I Am Not a Human Being". With "I Am Not a Human Being II", he could easily bow at No. 1 on Hot 200 by selling between 190,000 to 210,000 copies in its first week based on one-day estimates.  Ahead of the album release, he caused a buzz on the web when he was hospitalized for seizures. Rumors suggested he was on drugs but he explained later that he was epileptic who had suffered multiple seizures before without public knowing about it.
 

Monday, December 23, 2013

Lil Wayne's Life


   
Lil Wayne( Dwayne Michael CarterJr) is an American rapper and member of the group Hot Boysin the game but is also one of its more colorful characters too. Nicknames: Best Rapper Alive, Birdman Jr., Dr. Carter, Gangsta D, Mr. Carter, Nino Brown, President Carter, Rapper Eater, Shrimp Daddy, Tune, Tunechi Lionchess, Weezy F Baby, Wizzle
. Weezy is rarely short of a few words or two and we have come up with a handful of utterly unforgettable Lil Wayne quotes..Born on September 27, 1982 in Hollygrove, New Orleans, Louisiana to Dwayne Michael Turner and Jacinda Carter, He was enrolled in Lafayette Elementary School, on the gifted program and later attended Eleanor McMain secondary School, where he was a member of the drama club ,When he was 11, he met the owner of Cash Money Records, Bryan Williams .Carter left freestyle raps on Williams answer machine and the label boss eventually became his mentor and included him on Cash Money-distributed tracks.When he was 12 years old, Carter accidentally shot himself in the chest with a .44 caliber. Two years later, he dropped out of school, though he did later earn his GED.who was then 19 years old, Lil Wayne was forced to bid goodbye to his father who abandoned him and his mother right after he was born. During that time, he and his mother were forced to survive by themselves in the criminal-infested community at Hollygrove division of New Orleans. Fortunate enough, soon afterwards, his mother met Reginald "Rabbit" McDonald, who eventually became his stepfather. Years later, his stepfather moved the family out from the poverty-stricken Hollygrove to East New Orleans by that time.Lil Wayne married Toya Johnson on Valentines Day 2004 but divorced in 2006. The pair have a daughter, Reginae Carter. Lil Wayne also has a son, Dwayne Carter III, though the identity of the mother is not known. In 2007, Lil Wayne was arrested for possession of marijuana and possession of a weapon (he had a pistol). In 2008, his tour bus was stopped in Arizona and he was again arrested with narcotic and weapon possession.