MICHAKATO

Levis Rocky Ndekeno

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Pages

Wednesday, January 29, 2014

Msanii wa Nigeria KCEE, adaiwa kulipa tshs mil 675 kufanya collabo na Nicki Minaj

Kama ulishangaa kusikia kuwa Diamond Platnumz alilipa dola 5,000 ili kumshirikisha Davido kwenye remix ya My Number One, huenda ukaishiwa nguvu kusikia kiwango kinachodaiwa kutolewa na msanii wa Nigeria, KCEE ili kufanya collabo na first lady wa YMCMB, Nicki Minaj.


Kuna tetesi kuwa KCEE amelipa kitita cha N68m, ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 675 za Tanzania ili amshirikishe malkia huyo mpya wa hip hop nchini Marekani. Kufuatia tetesi hiyo, meneja wa KCEE, Soso Sobrekon, ameongea na mtandao wa NET kufafanua mambo yalivyo.
“Tupo nchini Marekani kujaribu kupata collaboration. Ni kweli tupo kwenye mchakato wa kufanya wimbo na Nicki Minaj. Tulitaka kuifanya iwe surprise kwa mashabiki lakini kwakuwa tayari imejulikana, tunataka kuifanya iwe kuwa zaidi,” alisema.
Hata hivyo meneja huyo alikataa kuthibitisha kama kweli kiwango hicho ndicho walicholipa. “Tunataka kumuongeza msanii mwingine wa YMCMB ambaye ni mkubwa kuliko Nicki Minaj. Nicki ameshathibitishwa kuwa kwenye wimbo huo, lakini kwakuwa sasa kila mtu anafahamu, bado tutawasurprise mashabiki kwa kumchukua msanii mwingine kutoka YMCMB.’

Monday, January 27, 2014

JK aagiza JWTZ kujenga kambi ya muda Kilosa

RAIS Jakaya Kikwete, ameagiza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kujenga kambi ya muda ya mahema na mabati katika kijiji cha Magole mkoani Morogoro, ili waathirika wote wa mafuriko wasio na nyumba, waishi kwenye kambi hiyo. Mbali na agizo hilo, pia ameitaka Serikali kuandaa utaratibu wa kupata magodoro kutoka katika kampuni zinazotengeneza magodoro hayo na kuwagawia waathirika hao.
Ametoa maagizo hayo jana katika viwanja vya Shule ya Sekondari Magole, ambako kumewekwa kambi ya muda kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokea Januari 22, mwaka huu.
Akiwa katika kambi hiyo, Rais Kikwete aliyewasili jana mchana kwa helkopta ya Polisi, alishuhudia idadi kubwa ya waathirika waliokumbwa na mafuriko wakiwemo watoto wadogo, wakilala chini na kuwa hatarini kupatwa na magonjwa ya vichomi na kuhara.
Kabla ya kutembelea waathirika na kuwahutubia, Rais Kikwete alitembelea daraja lililoathirika na mafuriko, maeneo yaliyoathirika vibaya na kupewa taarifa ya athari ya mafuriko kwa kata za Wilaya ya Kilosa, Gairo na Mvomero.
“Mafuriko haya ni makubwa na hayajawahi kutokea , watu wameathiriwa kwa nyumba zao kubomoka, kujaa maji na kuwafanya kukosa makazi na wengi wao wanalala chini.
“Serikali itatafuta magodoro kati ya siku mbili hizi na kuyaleta hapa kwa waathirika wa mafuriko ili kila mmoja alale kwenye godoro na si chini, lengo ni kuwaepusha kupatwa na magonjwa hasa ya vichomi na kwa watoto kuhara.
“Wenye viwanda hivi vya magodogo waendelee kuzalisha kwa wingi na waliyokuwa nayo stoo walete …hatuwezi kuwaacha watu waendelee kulala chini,” alisema Rais Kikwete.
Kwa upande wa chakula, alisema Serikali inacho cha kutosha kwenye maghala yake ambayo aliagiza yafunguliwe na chakula hususani maharage na mahindi, yasambazwe kwa waathirika.
Aliomba pia wadau wengine waendelee kujitokeza kusaidia kutoa chakula hasa mchele. Kuhusu huduma ya maji, alisema itaendelea kutolewa na magari ya JWTZ, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na magari ya kampuni za ujenzi za China hadi huduma ya maji kwenye kijiji hicho na vingine itakapotengemaa.
Pia alizungumzia umuhimu wa kuwatafutia waathirika na wakazi wengine, maeneo mengine ya miiinuko yenye usalama kwa kujenga makazi yao ya kudumu.
Katika hatua nyingine, Rais Kikwete amewataka wakuu wa wilaya za Mkoa wa Morogoro pamoja na wakurugenzi watendaji wa halmashauri, kuwahudumia wananchi nyakati za matatizo, kwani uongozi wao utapimwa na wananchi kutokana na ushiriki wao wa moja kwa moja kwao.
Ametoa kauli hiyo, baada ya kutoridhishwa na takwimu za waathirika wa mafuriko zilizotolewa na uongozi wa Mkoa, kuhusu idadi ya kaya na watu waliokumbwa na mafuriko katika tarafa ya Magole, Wilaya ya Kilosa; Dakawa Wilaya ya Mvomero na Gairo kutoonesha mchanganuo halisia.
Kutokana na kasoro hizo, Rais alitoa siku moja ya jana kwa wakuu wa wilaya hizo na uongozi wa mkoa, wampatie takwimu kamili zikiwa na majina ya watu waliobomolewa nyumba ambao wanaishi kwa majirani na kambini, ili misaada inayotolewa iwafikie walengwa na si wajanja wachache ambao si walengwa.
“Uongozi unapimwa katika kipindi cha matatizo ya watu, sijaridhika na takwimu hizi, hazioneshi walengwa halisia... jipangeni vizuri mnipe taarifa kamili kesho (leo), ili Waziri William Lukuvi (Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge) na wengine wazifanyie kazi kuwezesha upatikanaji wa huduma bila kuachwa mtu aliyeathiriwa na mafuriko,” alisisitiza.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, alisema watu 12,472 walikumbwa na mafuriko hayo na kaya 2,759 zimeathiriwa, wakati nyumba 1,141 zilibomolewa na nyingine 2,922 kuzungukwa na maji.

Alisema kuna mahitaji ya tani 635.5 za chakula kwa miezi sita kuanzia sasa na Sh milioni 57 kwa ajili ya kujenga makazi ya muda.

Wizara za Fedha, Elimu kuwekwa ‘kitimoto’

Zitahojiwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu matumizi ya marejesho ya fedha za radaDar es Salaam. Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, PAC, imepanga kuzikutanisha kwa pamoja, Wizara za Fedha na Elimu wakati ikipokea taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) inayohusu matumizi ya fedha za marejesho ya rada jinsi zilivyotumiwa.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Deo Filikunjombe alisema kuwa wanatarajia kupokea taarifa hiyo kesho na watatumia fursa hiyo kujihakikishia kama matumizi hayo yalikuwapo au kama kulikuwa na ulaghai wa aina yoyote.
“Kwa sasa ni mapema kuanza kufikiri kwamba fedha hazikutumika inavyotakiwa, lakini kama kuna ujanja wowote ulifanyika tutabaini tu alisema na kuongeza:
“Ndiyo sababu katika kikao hiki tunakutana wote; CAG, Wizara ya Fedha na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ili kama kuna maswali basi kuwe na majibu yake papo hapo,” alisema Filikunjombe.
Alisema leo watapokea taarifa ya ukaguzi maalumu kuhusu mbolea ya ruzuku, pia shughuli nyingine ambazo kamati inatarajia kuzifanya katika kipindi cha wiki mbili zijazo ni pamoja na kutembelea bandari na kukagua mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe wilayani Ludewa.
Awali mwaka jana aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene, aliliambia Bunge kwamba fedha za rada zilizorejeshwa Sh72.3 bilioni ziliingizwa katika bajeti ya serikali kwa mwaka 2012/13.
Mbene alisema kwamba fedha hizo ni marejesho kwa Serikali ya Muungano kutokana na udanganyifu uliofanywa na Kampuni ya BAE Systems ya Uingereza wakati wa kuiuzia Serikali ya Tanzania rada ya kuongozea vyombo vya usafiri angani.
Fedha zilizorudishwa na kampuni hiyo baada ya Taasisi ya Uchunguzi wa Makosa Makubwa ya Jinai (SFO) ya Uingereza kubaini kuwa, baadhi ya maofisa wa Serikali ya Tanzania na mawakala wa ununuzi kupandisha bei baada ya kushawishiwa na kampuni hiyo.
Novemba mwaka jana Serikali ilianza kusambaza vitabu milioni 19.4 kwa shule za msingi nchini, ambavyo ilielezwa kuwa vimenunuliwa kwa chenji ya rada na asilimia 75 ya fedha hizo zimetumika kununulia vitabu hivyo na asilimia 25 zitatumika kununulia madawati.

Vita ya umeme

WAKATI Watanzania wakilia ugumu wa maisha pamoja na mambo mengine, kupanda kwa gharama za nishati ya umeme, imethibitishwa kuwa kuna wafanyabiashara wanapambana bei hiyo isishuke. Wafanyabiashara hao; wenye mitambo ya kufua umeme wa mafuta na waagizaji wa mafuta, wananufaika kwa kunyonya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), ambalo linalazimika kuwapa karibu Sh bilioni nne kila siku, ili lipate umeme huo wa mafuta kutoka kwao.
Akizungumza juzi katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kutembelea ujenzi wa bomba la gesi na mitambo ya kuchakata gesi Mtwara na Lindi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alisema wafanyabiashara hao wanauzia Tanesco umeme uniti moja kwa kati ya senti 33 na 50 ya dola ya Marekani.
Bei hiyo ya umeme kwa Tanesco ni kubwa kuliko ambayo shirika hilo linauza kwa wateja wanaotumia umeme mdogo wa majumbani, wa kati kwa wafanyabiashara, wa kati viwandani na mkubwa kwa viwanda vikubwa, na kubwa kuliko bei ya umeme ya mashirika ya umeme ya nchi za Afrika Mashariki.
Tanzania kwa sasa inatumia megawati 1,850 ambazo asilimia 80 kwa mujibu wa Pinda, zinazalishwa kwa mafuta ya dizeli na mazito; wakati asilimia nyingine ndizo zinazotokana na vyanzo vingine vya maji na gesi ya Songosongo.
Bei ya umeme Kwa mujibu wa takwimu za Tanesco, wateja majumbani wananunua uniti moja kwa senti 19 ya dola, wateja wa biashara senti 13 na viwanda vya kati na vikubwa senti 10. Umeme wa taa za barabarani ni senti 19.
Kwa nchi za Afrika Mashariki, hasa Kenya, Uganda na Rwanda, wateja majumbani hununua uniti moja kwa senti 20, wa biashara ni kati ya senti 16 na 20.
Viwanda vya kati Uganda bei ni senti 17, Kenya 14 na Rwanda 19. Kwa umeme wa viwanda vikubwa, bei kwa Uganda ni senti 12, Kenya 15 na Rwanda 19. Tanzania inaongoza kwa kutoza bei kubwa kwa taa za barabarani ambayo ni senti 19 sawa na Rwanda huku Kenya na Uganda bei kwa umeme huo ni senti 18.
Hali hiyo inadhihirisha kuwa pamoja na kupandisha bei ya umeme mwezi huu, bado gharama za umeme kwa Tanesco ni kubwa kuliko bei ya kuuzia, na kusababisha shirika hilo muhimu katika uchumi wa nchi, kujiendesha kwa hasara.
Suluhisho Pinda alisema bomba la gesi kutoka Mtwara likimalizika kujengwa na uzalishaji kuanza, Tanesco itanunua umeme huo kwa senti 8 na kufanya nishati hiyo kushuka bei. Kauli hiyo ya kushusha bei ya umeme baada ya gesi kuanza kutumika Dar es Salaam, pia ilipata kutolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
“Hii bei ya umeme iliyopo sasa ni ya muda tu na itashuka sana bomba la gesi litakapokamilika, kwa sababu hata mitambo ya kufua umeme inayotumia mafuta nayo itatumia gesi na mitambo mipya ya gesi italetwa, nataka Watanzania wakubali hivyo.
“Serikali inataka umeme mwingi utokane na gesi, jua, upepo na joto ardhi, lakini wapo wanaokataa bomba kuja Dar es Salaam na hao hao wanalalamika umeme kuwa juu, mtu yeyote ambaye anajua dunia inakwendaje, hawezi kupinga kujengwa bomba la gesi.
"Miaka ijayo, chanzo kikubwa cha umeme nchini kitakuwa gesi asilia… nyie mtanitukana, mtanisema sana, lakini mimi nitabaki kwenye utaalamu na wala siwezi kuyumba, tatizo la umeme wa Tanzania litatatuliwa na gesi, kila kitu kikikamilika Tanesco na Ewura (Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji) hawawezi kuendelea kuweka bei juu," alisema Profesa Muhongo.
Mapambano “Sisi tunaona kuwa suluhu ya kuondokana na gharama hizi ni gesi, lakini kuna watu wanajua watanyang’anywa tonge midomoni, vita hii tunaijua; lakini hatuwezi kurudi nyuma katika hili ni lazima tusonge mbele,” alisema Pinda.
Alisema nyuma ya mapambano ya kuzuia gesi kufika Dar es Salaam, wapo wafanyabiashara ambao wanahofia kuwa mwisho wa biashara yao ya kuuzia Tanesco umeme kwa bei ya juu umefika.
Alisema watu kwa sasa wananufaika na Tanesco kununua mafuta ya kuendeshea mitambo ya umeme. Katika hali hiyo, Pinda alisema uamuzi wa Serikali kuchimba gesi hiyo na kuisafirisha hadi Dar es Salaam si jambo jepesi, kwani utekelezaji wake unakabiliwa na mapambano na upinzani mkubwa kutoka kwa wenye mitambo ya kuzalisha umeme ambao kwa sasa wananufaika kutoka Tanesco.
Alisisitiza, kuwa Serikali imedhamiria kuachana na umeme huo wa mafuta na kama wafanyabiashara hao wanataka kuendelea na biashara hiyo, ni vema wabadilishe mitambo yao iwe ya gesi na si ya mafuta kama ilivyo sasa.
Mataifa, ushauri Pia alisema vita nyingine wanayokabiliana nayo ni ya nchi ambako kampuni za utafiti wa mafuta na gesi zinatoka, ambazo zinataka kampuni zao zipewe zabuni ya kutandaza bomba la gesi na kujenga mitambo ya kuchakata gesi.
“Wanalalamika gesi wametafuta na kugundua wao, halafu kandarasi anapewa China, sisi tumewajibu kuwa tumekimbilia China kwa sababu masharti yao ni nafuu kuliko yao,” alisema Pinda.
Katika hatua nyingine, Pinda alitaka wakazi wa Lindi na Mtwara kutambua kuwa gesi hiyo ni rasilimali ya Taifa na itanufaisha nchi nzima. Aliwataka wajiandae kwa uchumi huo kwa kuhakikisha wanatumia fursa zilizopo kufaidika. Aliwataka wasikubali fursa ya gesi ilete balaa nchini badala ya neema.
“Kama tunataka iwe neema tushirikiane na wadau wakubwa zaidi ili nchi yetu ipige hatua kimaendeleo.”
Kwa upande wake, Profesa Muhongo aliwataka wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara kusomesha watoto wao hasa katika Sayansi, ili wafaidike na uwepo wa gesi na mafuta katika mikoa hiyo.
Alisema Serikali imejitahidi kusomesha vijana katika eneo la gesi na wamekuwa wanahamasisha vijana wa mikoa hiyo kuchukua masomo ya Sayansi kwa vile wizara inagharimia baadhi ya vijana kusoma masuala ya gesi vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi.

Pinda katika ziara hiyo alielezea kuridhika na kazi inayoendelea katika mradi huo na akasema upo uwezekano mradi huo ukakamilika kabla ya muda wake uliopangwa wa miezi 18.

Birdman aonyesha choo chake kilichotengenezwa na dhahabu, kichokadiriwa kuwa na thamani ya $1mil.

Birdman boss wa record label ya YMCMB ambaye mara nyingi huwa anajisifia kwa matumizi yake makubwa ya pesa kwenye vitu luxury, ameendeleza hivyo vitendo  vya kufanya matumizi makubwa ya pesa.
Hivi karibuni ame-share picha ya choo chake ambacho kime-kuwa covered na material ya dhahabu pande zote.
Mfuniko wake na sehemu ya juu ya choo hicho ni dhahabu tupu na sehemu nyingine yote hautaweza kukiona hicho choo kwasababu kimefunikwa na dhahabu.

Gharama yake inakadiriwa ni dola millioni moja.

Sunday, January 26, 2014

VP urges technology institutes to produce skilled graduates

With the advent of oil and gas exploration and investments in the country, the government has urged technological Institutes and Universities to produce skilled and competent graduates who will serve in the sector instead of depending on foreign experts. 

Vice President Dr Mohamed Gharib Bilal made the call in Dar es Salaam over the weekend during the 7th graduation ceremony of the Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) in his speech read by the Minister for Science and Technology, Prof Makame Mbarawa.

He said highly skilled experts will also be needed in management, monitoring, supervision and construction of railways, ports, airports and other infrastructures following government’s plans to invest in infrastructures to speed up the growth of national economy.

“Following huge investments in oil, gas, and minerals, these areas need expertise to succeed,” he said. 

He also urged the Institute to take the many researches they have conducted to the market for public consumption. 

He hailed the progress made by the Institute over the years including expansion of courses, enrollment, improving its infrastructures.

“I congratulate you for working on developing Information and Technology (IT) centre, creativity in traffic lights, and telemedicine - a technological intervention in health care provision in various hospitals such as Muhimbili national hospital in Dar es Salaam and in Coast region and Mbeya referral hospitals,” he said.

For his part, DIT Principal, Prof John Kondoro said apart from introducing five new courses which started in 2013/14 academic year, in 2014/15 the Institute expects to introduce other three courses already accredited by NECTA which are Diploma in Food Science and Technology, Diploma in Biotechnology, and Diploma in Highway Engineering. 

He thanked the government, development partners and other stakeholders for their valuable support, saying they have enabled the Institute to establish new courses and fulfill its responsibilities.

Citing an example, he said there were a number of projects and courses jointly conducted by foreign institutes and Universities such as Masters Degree in Renewable Energy Engineering, a course prepared in collaboration with Kenya University, Mombasa Technical University, Jima University of Ethiopia and Politecnico di Milano of Italy.

Earlier, the Institute’s council Chairman, Prof Fredrick Mwanuzi said DIT will continue offering highly skilled courses because experience shows that there is a huge shortage of human resource in technological skills. 

During the graduation ceremony attended by government officials, Ambassadors, DIT officials and parents among many others, out of 682 all graduates, 176 were conferred with degrees in different engineering fields, 504 Diploma certificate, and two were awarded certificates. 

Waziri wa Fedha akiri hali ngumu

 Waziri wa Fedha, Saada Mkuya amekiri Serikali kuwa katika hali ngumu, lakini akasema kuwa mkakati uliopo ni kudhibiti matumizi ili yaendane na fedha iliyopo.
Waziri Saada alisema hayo kwa njia ya simu, alipotakiwa na Mwananchi Jumapili kujibu madai ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) juu ya kauli yake ya hivi karibuni aliyoitoa katika mkutano mjini Dodoma.
“Ni kweli nimesikia alichosema CAG na nadhani alimaanisha kudhibiti matumizi ya rasilimali kulingana na mahitaji. Siyo kwa Tanzania tu, nchi zote huwa zinazingatia matumizi ya rasilimali kulingana na mahitaji yaliyopo” alisema Saada na kuongeza:
“Sisi kama wizara tumejipanga kukusanya na kutegemea fedha zetu za ndani kupitia Mamlaka ya Mapato (TRA). Tunategemea misaada, lakini huwa inachelewa. Hata wakaguzi nao wanapaswa kuangalia hilo.”
Hata hivyo, Saada alisema kuwa Serikali ina fedha za kutosha kuendesha shughuli zake.
Alhamisi wiki hii CAG,Ludovick Utoh akifungua Mkutano wa pili wa Baraza la Wafanyakazi wa Ukaguzi nchini mjini Dodoma alisema, Serikali ya Tanzania iko hoi kifedha hivyo Bunge na Serikali lazima wajitathimini na kuongeza wanayo matumaini kutokana na ushauri ambao umekuwa ukitolewa na ofisi yake kufanyiwa kazi.


Vitu 10 usivyovitegemea utakavyojivunza ukifika miaka ya 30

11. Unasahau kwamba haupo kwenye miaka ya 20 tena

Baada ya kumaliza chuo miaka inaanza kuchanganya na kujua umri wako kunakua hakuna umuhimu tena  sababu ya kazi nyingi na maisha kuwa the same so inafikia kipindi unaweza kuwa na miaka 22 kiakili hata kiuchumi lakini kiuhalisia unakua ushafika miaka ya 30.
10. Watu wanaanza kufikiria kuna kitu hakipo sawa kama bado upo SINGLE
Sababu una miaka 30 na zaidi haimaanishi inabidi uwe umeoa au kuolewa. Hiki ni kitu ambacho utapata wakati mgumu kukielezea kwa wazazi wako.

09. Jina lako la katikati linakuwa “Busy” sababu ndio hivyo utakua muda wote
Kama unafamilia basi ndio inakua zaidi na kama hauna kazi pekee inaweza kukufanya uwe busy balaa.
08. Account yako ya facebook itaanza kujaa picha za watoto
haijalishi ni watoto wako au ni wa rafiki zako wanaoamua kukutag picha za watoto wao.duh! noma sana :-)
07. kuinvest kwenye quality itakua muhimu
utatumia pesa zaidi katika kupata nguo nzuri zaidi hat gari nzuri zaidi pia.
06. Mgongo utaanza kukuuma bila sababu
04. Utakua na marafiki walioachika
03. Muziki utakaocheza ni katika harusi na sherehe za ofisi
02. Hautataka kurudi katika miaka ya 20 tena
labda kama ni kurudi na kutumia pesa  zako kwa makini kuwekeza katika miaka ya 30 lakini zaidi ya hapo hautatamani kurudi tena miaka ya 20.
01. Hautangoja kufika miaka ya 40
kwasababu katika miaka ya 40 utakua umeshafanikisha mipango yako yote.

Saturday, January 25, 2014

Tuzo za Grammy 2014 Yatangazwa, Ikiwa Jay Z Anaongoza kwa Kuchaguliwa katika Category 9 Tofauti

Ile list ya Majina ya wasanii wanaowania tuzo za muziki za Grammy zinzotarajiwa kutolewa January mwakani tayari yamefahamika, Jay Z anaongoza kwa kupata nomination 9, akifuatiwa na Justin Timberlake, Kendrick Lamar, Macklemore & Ryan Lewis na Pharrell Williams wote wakiwa na nomination 7.



Hizi ni Tuzo za 56 za Grammy na  zitatolewa January 26, 2014.

Hii ni orodha kamili ya majina ya wasanii wanaowania tuzo za ‘56th Grammy Awards-2014’:


Album of the Year
Sara Bareilles – The Blessed Unrest
Daft Punk – Random Access Memories
Kendrick Lamar – Good Kid, M.A.A.D. City
Macklemore & Ryan Lewis – The Heist
Taylor Swift – Red

Record of the Year
Daft Punk feat. Pharrell Williams – “Get Lucky”
Imagine Dragons – “Radioactive”
Lorde – “Royals”
Bruno Mars – “Locked Out of Heaven”
Robin Thicke feat. Pharrell Williams & T.I. – “Blurred Lines”

Song of the Year
Pink feat. Nate Reuss – “Just Give Me a Reason”
Bruno Mars – “Locked Out of Heaven”
Katy Perry – “Roar”
Lorde – “Royals”
Macklemore & Ryan Lewis feat. Mary Lambert – “Same Love”

Best New Artist
James Blake
Kendrick Lamar
Macklemore & Ryan Lewis
Kacey Musgraves
Ed Sheeran

Best Pop Solo Performance
Sara Bareilles – “Brave”
Lorde – “Royals”
Bruno Mars – “When I Was Your Man”
Katy Perry – “Roar”
Justin Timberlake “Mirrors”

Best Pop Duo/Group Performance
Daft Punk feat. Pharrell Williams – “Get Lucky”
Pink feat. Nate Reuss – “Just Give Me a Reason”
Rihanna feat. Mikky Eiko – “Stay”
Robin Thicke feat. Pharrell Williams & T.I. – “Blurred Lines”
Justin Timberlake feat. Jay Z – “Suit & Tie”

Best Pop Vocal Album
Lana Del Rey – Paradise
Lorde – Pure Heroine
Bruno Mars – Unorthodox Jukebox
Robin Thicke – Blurred Lines
Justin Timberlake – The 20/20 Experience – The Complete Experience

Best Traditional Pop Vocal Album
Tony Bennett & Various Artist – Viva Duets
Michael Buble – To Be Loved
Gloria Estefan – The Standards
Cee Lo Green – Cee Lo’s Magic Moment
Dionne Warwick – Now
PHOTOS: Grammys 2013 — most memorable moments

Best Country Solo Performance
Lee Price – “I Drive Your Truck”
Hunter Hayes – “I Want Crazy”
Miranda Lambert – “Mama’s Broken Heart”
Darius Rucker – “Wagon Wheel”
Blake Shelton – “Mine Would Be You”

Best Country Duo/Group Performance
The Civil Wars – From This Valley
Kelly Clarkson feat. Vince Gill – “Don’t Rush”
Little Big Town – “Your Side of the Bed”
Tim McGraw, Taylor Swift, and Keith Urban – “Highway Don’t Care”
Kenny Rogers with Dolly Parton – “You Can’t Make Old Friends”

Best Country Song
Taylor Swift – “Begin Again”
Lee Brice – “I Drive Your Truck”
Miranda Lambert – “Mama’s Broken Heart”
Kacey Musgraves – “Merry Go Round”
Blake Shelton – “Mine Would Be You”

Best Country Album
Jason Aldean – Night Train
Tim McGraw – Two Lanes of Freedom
Kacey Musgraves – Same Trailer, Different Park
Blake Shelton – Based on a True Story
Taylor Swift – Red

Best Dance Recording
Duke Dumont feat. AME & MNEK – “Need U”
Calvin Harris feat. Florence Welch – “Sweet Nothing”
Kaskade – “Atmosphere”
Armin Van Buuren feat. Trevor Guthrie – “This Is What It Feels Like”
Zedd feat. Foxes – “Clarity”

Best Dance Album
Daft Punk – Random Access Memories
Disclosure – Settle
Calvin Harris – 18 Months
Kaskade – Atmosphere
Pretty Lights – A Color Map of the Sun

Best Rock Performance
Alabama Shakes – “Always Alright”
David Bowie – “The Stars (Are Out Tonight)”
Imagine Dragons – “Radioactive”
Led Zeppelin – “Kashmir”
Queens of the Stone Age – “My God is the Sun”
Jack White – “I’m Shakin’”

Best Rock Song
Gary Clark Jr – “Ain’t Messin Round”
Paul McCartney – “Cut Me Some Slack”
The Rolling Stones – “Doom and Gloom”
Black Sabbath – “God Is Dead?”
Muse – “Panic Station”

Best Rock Album
Black Sabbath – 13
David Bowie – The Next Day
Kings of Leon – Mechanical Bull
Led Zeppelin – Celebration Day
Queens of the Stone Age – …Like Clockwork
Neil Young With Crazy Horse – Psychedelic Pill


2013 List

Best R&B Performance
Tamar Braxton – “Love and War”
Anthony Hamilton – “Best of Me”
Hiatus Kaiyote feat. Q-Tip – “Nakamarra”
Miguel feat. Kendrick Lamar – “How Many Drinks?”
Snark Puppy with Lalah Hathaway – “Something”

Best R&B Song
Anthony Hamilton – “Best of Me”
Tamar Braxton – “Love and War”
PJ Morton feat. Stevie Wonder – “Only One”
Justin Timberlake – “Pusher Love Girl”
Fantasia feat. Kelly Rowland and Missy Elliot – “Without Me”

Best Urban Contemporary Album
Tamar Braxton – Love and War
Fantasia – Side Effects of You
Salaam Remi – One: In the Chamber
Rihanna – Unapologetic
Mack Wilds – New York: A Love Story

Best R&B Album
Faith Evans – R&B Divas
Alicia Keys – Girl on Fire
John Legend – Love in the Future
Chrisette Michele – Better
TGT – Three Kings

Best Rap Performance
Drake – “Started From the Bottom”
Eminem – “Berzerk”
Jay Z – “Tom Ford”
Kendrick Lamar – “Swimming Pools (Drank)”
Macklemore & Ryan Lewis feat. Wanz – “Thrift Shop”

Best Rap/Sung Collaboration
J. Cole feat Miguel – “Power Trip”
Jay Z feat. Beyonce – “Part II (On the Run)”
Jay Z feat. Justin Timberlake – “Holy Grail”
Kendrick Lamar feat. Mary J. Blige – “Now or Never”
Wiz Khalifa feat. The Weeknd – “Remember You”



Best Rap Song
ASAP Rocky feat. Drake, 2 Chainz, and Kendrick Lamar – “F***in’ Problems”
Jay Z feat. Justin Timberlake – “Holy Grail”
Kanye West – “New Slaves”
Drake – “Started From the Bottom”
Macklemore & Ryan Lewis – “Thrift Shop”

Best Rap Album
Drake – Nothing Was the Same
Jay Z – Magna Carta… Holy Grail
Kendrick Lamar – Good Kid, M.A.A.D. City
Macklemore & Ryan Lewis – The Heist
Kanye West – Yeezus

Best Song Written For Visual Media
Coldplay – “Atlas” from The Hunger Games: Catching Fire
Jessie J – “Silver Lining” from Silver Linings Playbook
Adele – “Skyfall” from Skyfall
Colbie Caillat feat. Gavin DeGraw – “We Both Know” from Safe Haven
Lana Del Rey – “Young and Beautiful” from The Great Gatsby
Regina Spektor – “You’ve Got Time” from Orange Is the New Black

Friday, January 24, 2014

Polisi wakamatwa kwa mauaji A.Kusini


Polisi wanne wamekamatwa kuhusiana na kisa cha kuwapiga risasi waandamanaji nchini Afrika Kusini siku ya Alhamisi.

Tshepo Babuseng, mwenye umri wa miaka 28, alipigwa risasi na polisi katika maandamano kuhusu swala la makaazi viungani mwa mji wa Johannesburg.

Ripoti za awali, zilisema kuwa umati wa watu uliwavamia polisi waliokuwa wanaondoa vifusi barabarani. Hapo ndipo polisi mmoja alipowapiga risasi waandamanaji hao.

Mmoja wa maafisa hao anakabiliwa na tuhuma za mauaji wakati wengine wakikabiliwa na kosa la ukandamizaji.

Msemaji wa polisi katika mkoa wa Gauteng, amesema kuwa polisi hao walio na umri wa kati ya miaka 33-49 watafikishwa mahakamani hivi karibuni.

Kitengo cha kuchunguza polisi kinasema kuwa kitafanya uchunguzi huru wa ndani kuhusiana na tuhuma hizo.
Kwa sasa polisi hao wameachishwa kazi kwa muda hadi kesi itakapoamuliwa.

Polisi nchini Afrika Kusini hutuhumiwa mara kwa mara kuhusu kuwatesa watu na kutumia njia zisizofaa kupambana na makundi ya watu wanaokuwa wanaandamana.

Mapema wiki hii kufuatia hatua ya polisi kuwapiga risasi watu wanne katika maandamano tofauti, waziri wa polisi Nathi Mthethwa aliambia BBC kuwa polisi watakawaua raia wasio na hatia hawatalindwa.

"polisi wanapata mafunzo kuwalinda raia na kuwahudumua. Hawafunzwi kuwaua,'' alisema waziri huyo.

Mwaka 2012, polisi waliwapiga risasi wafanyakazi 34 wa migodi waliokuwa wanagoma katika mgodi wa Marikana , tukio la kushangaza zaidi kuwahi kutokea tangu kumalizika kwa enzi ya ubaguzi wa rangi 1994.


Mwaka jana maafisa walinaswa kwa kanda ya video wakimfunga mwanamume kwenye gari kabla ya kumburura barabarani. Mwanamume huyo alipatikana akiwa amefariki.

Je unataka kubadilisha taaluma yako? Epuka makosa haya By Awali Mwaisanila on January 24, 2014



Kama kocha wa mambo ya taaluma, ninaweza kukwambia suala la kubadilisha taaluma ni kitu kinachohusiana sana na maadili yako, mahitaji yako, ujuzi na vitu unavyovipenda hata katika kipindi hiki ambacho hali ya uchumi si nzuri. Ukitaka kubadilisha  taaluma yako ili iwe na matokeo mazuri na yenye mtizamo chanya unahitaji mambo manne ya msingi; Unahitaji maelezo yanayojitosheleza, Ujasiri, Uthubutu na uwezo. Bila vitu hivyo utahangaika na utashindwa.


Kwahiyo unapotaka kuchukua maamuzi ya kubadili kazi ama taaluma yako hakikisha kwamba hisia zako ziko imara, hali yako ya kiuchumi imetulia na kielimu. Utapitia ngazi tofauti hivyo unahitaji umakini na uelewa wa kitu unachokifanya, unahitaji kuondoa mambo ya kuiga na kufuata mkumbo. Unapaswa kujiuliza je mpaka hapa nilipofika kitu gani cha msingi ambacho nimeweka kukifanya katika taaluma yangu? Changamoto gani nimepitia na je ninawajibika vipi katika nafasi niliyonayo sasa?. Hivyo unapofanya uamuzi vitu hivi vitano uvifuate kwa makini kwa kuwa vitaathiri maisha yako, Mahusiano yako, afya, fedha na maisha yako ya baadaye.

Makosa hayo ni kama yafuatayo
Athari za kukimbia, kukimbia taaluma uliyonayo kwa sababu umevunjika moyo na kama umesubiri muda mrefu kufanya mabadiliko ya hali yako ya sasa, umetengeneza mazingira ya kuichukia kazi yako, watu unaofanya kazi nao, kazi unayofanya na ujuzi unaotumia na unataka kukimbia mbali kabisa na taaluma hiyo. Kuna watu huwa hawaelewi kwanini wanafanya hicho wanachokifanya, na wanafanya kwa kusudi gani na mara nyingi hujaribu kukimbiakimbia kwenye taaluma. Hivyo kuishi kulingana na cheo au weledi alionao na kujikuta katika giza wa uitumia semina na mafunzo mbalimbali ili kuweza kuishi kila siku na kama dawa ya kuimarisha weledi huo.

Hiyo imesababisha watu kuishia wasikokutaka. Hivyo huhitaji matengenezo mapya kitaaluma kwasababu wamekuwa wakishi kulingana na watu wanavyokwenda. Usisubiri mpaka umechoshwa na hali uliyonayo sasa ili kufanya mabadiliko. Fanya maamuzi ya kujua taaluma yako sasa. Kufanya mambo yako yaanze kwenda vizuri anza kurekebisha mahusiano yako yaliyovunjika, tengeneza heshima, tafuta sauti yako,kuza ujuzi ulionao na ongeza uwezo wako kiujuzi. Hivyo ukiondoka hapo unakuwa na uwezo wa kwenda ngazi nyingine na itakuwa wazi kwako na kusonga mbele bila matatizo. Kukimbia hapo ulipo hautarekbisha matatizo yako ila yatajirudia kwenye taaluma nyingine ambayo unaiendea.

Kutokuwa na mpango madhubuti kiuchumi ambao utakutegemeza wakati wa mabadiliko.

Kuna watu wengi wanahitaji mabadiliko ya taaluma lakini hakuna fedha za kufanya hivyo wala mahali watakapo pata msaada. Hivyo hawafanyi uchunguzi itamgharimu kiasi gani kufanya mabadiliko hayo na hawana fedha za kufanya mabadiliko hayo.  Huweza kupata mshahara mara mbili au tatu zaidi unapokwenda kwenye taaluma nyingine inahitaji muda wa kutosha na juhudi ya ziada. Tafuta ushauri na hakikisha unaweza pata fedha za kukuwezesha kufanya mabadiliko na punguza matumizi ya fedha kwenye mambo yasiyo ya msingi.

Kukimbilia kazi ambayo huna uhakika kama una uwezo nayo au ndio unayotaka

Swali unalohitaji kujiuliza nina ujuzi gani na kipaji gani nataka kukitumia? Je ni jambo gani ninahitaji kusaidia? Je ni watu gani na mazingira gani na tamaduni gani ninaweza kufanya kazi nao ? Nina utu wa namna gani, nina maadili gani ambayo yatanisaidia katika kazi au taaluma hii? Nitakutana na changamoto gani katika taaluma hii? Kuna faida gani ambazo hazihitaji mjadala katika taaluma hii? Je ninataka kufika wapi na taaluma hii? Je inaendana na maisha na taratibu zangu za kuishi?

Kutofanya utafiti wa kutosha, mfano umekuwa karani kwa miaka mingi sasa unaona muda wa kustaafu umefika unaamua kuingia kwenye ufugaji. Je umefanya utafiti wa kutosha kufanya ufugaji?Je una ujuzi kuhusu ufugaji? Na je taaluma yako inaendana na kitu unachotaka kufanya? Utahitaji kujifunza upya kuhusu ufugaji na namna mambo yanavyokwenda. Kwasababu umetumia muda mwingi kuishi maisha tofauti na unayotaka uanze kufanya sasa.

Kukata tamaa mapema, kushindwa kufanya mabadiliko kitaaluma kunahusisha kukata tamaa mapema, huwezi kufanya mabadiliko bila kuweka jitihada ya kutosha, muda, kujitoa na kutumia fedha. Watu wengi hutegemea mabadiliko kutokea haraka sana labda kupanda cheo kwa sababu amekuwa kazini muda mrefu na vitu kama hivyo. Hivyo hukata tamaa na kutafuta mtu wa kumlaumu bila kujitizama kwamba wao wamefanya juhudi gani katika taaluma?


Je wanajua wapi wanakwenda au wanakwenda kwa sababu watu wanakwenda? Tumekuwa na watu wengi ambao wanataka kubadili kazi au taaluma bila kufanya uchungui wa kutosha. Jaribu kuangalia maisha yako na mabadiliko ya kitaaluma unayotaka kufanya kwa kufanya uchunguzi wa kutosha kabla ya kufanya mabadiliko hayo.

Thursday, January 23, 2014

Huyu ndiye mwandishi kutoka kenya aliyejitangaza kuwa anashiriki Mapenzi ya Jinsia moja.



Mwandishi maarufu wa vitabu nchini Kenya, Binyavanga Wainaina, amejitokeza hadharani kuwa yeye hushiriki mapenzi ya jinsia moja.

 Hii inamfanya Binyavanga kuwa mmoja wa wafrika mashuhuri kujitokeza hadharani.

 Alifichua hali hii katika taarifa yake kupitia kwa mtandano wa kijamii wa Twitter iliyowiana na siku ya kuzaliwa kwake.Ana umri wa miaka 43. (R.M).
Hii inakujia wakati ambapo kuna mjadala mkali nchini Kenya na katika baadhi ya mataifa ya Afrika kuhusiana na suala la haki za wapenzi wa jinsia moja.

 Hivi karibuni, Nigeria ilipitisha sheria ambayo inatoa adhabu kali kwa makundi ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, ilhali Rais wa Uganda alikataa kuhalalisha mswada kama huo uliopitishwa bungeni.

 Uamuzi wa Binyavanga kujitokeza hadharani umepokelewa kwa hisia mbali mbali nchini Kenya. Kunao waliompongeza ingawa baadhi wanahisi kuwa huenda jamii ikamnyanyapaa.

 Binyavanga aliwahi kushinda tuzo la mwanadishi bora zaidi Afrika la Caine mwaka 2002.


 Watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja nchini Kenya wanaweza kuadhibiwa kifungo cha miaka kumi jela ikiwa watapatikana na hatia.

Samsung Galaxy S5 inaweza kuzinduliwa February 23

Wale wanaoisubiria kwa hamu simu mpya ya Samsung wanaweza wasingoje kwa muda mrefu tena. Kuna tetesi kuwa kampuni hiyo inaweza kuitambulisja Galaxy S5, Feb. 23 kabla ya Mobile World Congress, ingawa simu hiyo itaingia sokoni April.

Kwa mujibu wa Eldar Murtazin, mhariri wa mtandao wa Mobile-Review.com , simu hiyo itatangazwa mjini Barcelona Feb. 23. Hakuna taarifa za kuaminika za namna simu hiyo itakavyokuwa lakini itapewa teknolojia ya mawasiliano kati yake na macho ya mtumiaji.

Watafiti: Kutumia smartphones usiku kunaharibu usingizi na utendaji kazi siku inayofuata

Tunafahamu usiku unaweza kuwa muda mzuri wa kupitia status za washkaji Facebook, kutazama picha mbalimbali Instagram ama kufuatilia mijadala kwenye Twitter lakini hicho kinaweza kuwa kikwazo kikubwa cha nia yako ya kutaka kupata usingizi wa kutosha ama kuwa na utendaji mzuri kazini.

 Kuzima smartphone saa 3 usiku kunaweza kukufanya ufanye kazi vizuri siku inayofuata, watafiti wamesema






Timu katika chuo kikuu cha Washington imesema matumizi ya simu usiku sana yanaweza kuharibu kabisa usingizi wako na namna utakavyofanya kazi siku inayofuata. Wameshauri wafanyakazi wawe na tabia ya kuzima simu ama lasivyo watajikuta wakishindwa kufurahia kazi kesho yake.
Watafiti hao wanasema kujiondoa kabisa na matumizi ya simu usiku ni njia ya kupata usingizi mzuri usiku. Wamewaomba waajiri kusubiri kutuma email hadi asubuhi
“Sababu ya hii kama tutakavyoelezea, ni kwamba smartphones ni mbaya kwa usingizi, na usingizi ni muhimu kwa uchapakazi wa mwajiriwa,” alisema Christopher Barnes, Profesa Msaidizi katika chuo kikuu cha Washington (Foster School of Business) aliyeongoza utafiti huo utakaochapishwa kwenye jarida la , Organizational Behavior and Human Decision Processes baadaye mwaka huu.
“Bahati mbaya smartphones zimetengenezwa mahsusi kuharibu usingizi. Sababu zinatufanya kiakili kuendelea na kazi hadi usiku, zinafanya kuwepo ugumu wa kujiondoa kisaikolojia kutoka kwenye masuala muhimu ya siku ili tupumzike na kulala. Pengine suala gumu kuliepuka kutoka kwenye smartphones ni kwamba zinatuweka kwenye mwanga, ukiwemo mwanga wa blue. Hata kiwango kidogo cha mwanga wa blue hupunguza uzalishaji wa kemikali ya usingizi, melatonin, ikimaanisha kuwa muonekano (display) unaweza kutengeneza madhara haya.”