MICHAKATO

Levis Rocky Ndekeno

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Pages

Monday, January 4, 2016

Japan yataka mazungumzo ya amani na Urusi

Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe ameitisha mazungumzo ya amani kati yake na Rais wa Urusi Vladimir Putin kujadili mkataba wa Amani kati ya nchi hizo mbili.
Mataifa hayo mawili hayakutia saini mkataba wa amani baada ya kumalizika kwa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia kutokana na mzozo kuhusu umiliki wa visiwa vinne.
Bw Abe ameambia wanahabari kwamba viongozi wote wawili wanakubaliana kwamba ni jambo la kushangaza kuwa mkataba huo haujatiwa saini kwa miaka 70.
Tangu achukue uongozi 2012 Bw Abe amekuwa akijaribu kuimarisha uhusiano kati ya Tokyo na Moscow.
Muungano wa Usovieti uliteka visiwa kadha ambavyo Japan huviita Northern Territories mwaka 1945. Urusi huviita Southern Kurils.
Viongozi hao wawili walijadili suala hilo mara ya mwisho 2013.
Nchi hizo mbili zilirejesha uhusiano wa kidiplomasia mwaka 1956.
"Bila mkutano mkuu, tatizo la visiwa vya Northern Territories haliwezi likatatuliwa,'' alisema, alipokuwa akihutubia wanahabari kikao cha Mwaka Mpya.
Aliongeza kwamba ataendelea kuzungumza na Bw Putin “kila fursa inapotokea”

Marekani yafunga kituo cha ndege Ethiopia



Marekani imefungia kituo cha ndege zisizo na rubani nchini Ethiopia ambacho imekuwa ikitumia kushambulia wanamgambo wa al-Shabab katika taifa jirani la Somalia.
Maafisa wa Marekani wanasema kituo hicho cha siri kilikuwa cha muda tu na kwamba kwa sasa hakikihitajiki tena.
Kirasmi, Marekani ina kambi moja tu ya jeshi barani Afrika, ambayo imepewa jina Camp Lemonnier nchini Djibouti. Lakini huwa ina kambi nyingi za muda maeneo mengi barani.
Oktoba mwaka 2015, jarida la habari za ufichuzi The Intercept, lilichapisha nyaraka za siri za jeshi ambazo lilisema lilionyesha Marekani ilikuwa na kambi zaidi ya 14 za ndege zisizo na rubani barani Afrika.
Ndege hizo zimetumiwa kuua makamanda kadha wa al-Shabab, akiwemo kiongozi wa kundi hilo Ahmed Godane mwaka 2014.
Wakosoaji wanasema mashambulio hayo huwa hayapati shabaha wakati wote na mara nyingine huua watu wasio na hatia.
Vyombo vya habari Ethiopia vinasema Marekani ilianza kutumia kituo hicho kilichoko kusini mwa nchi hiyo 2011.
Ethiopia imekuwa mshirika wa karibu wa Marekani katika vita dhidi ya al-Shabab, na pia imekuwa na wanajeshi Somalia tangu 2006.

Bahrain yavunja uhusiano na Iran




Bahrain imetangaza kwamba imevunja uhusiao wa kibalozi na Iran, saa chache baada ya Saudi Arabia kuchukua hatua sawa.
Saudi Arabia iliwapa wanabalozi wa Iran siku mbili kuondoka nchini Saudi Arabia kufuatia mvutano uliotokana na kuuawa kwa mhubiri maarufu wa Kishia.
Bahrain hutawaliwa na Mfalme Msuni lakini raia wengi ni wa dhehebu la Shia.
Ufalme huo pia umewapa wanabalozi wa Iran saa 48 wawe wameondoka nchini humo.
Mhubiri huyo Sheikh Nimr al-Nimr aliuawa pamoja na watu wengine 46 baada ya kupatikana na makosa yanayohusiana na ugaidi.
Washia walishutumu hatua hiyo na maandamano yalishuhudia maeneo yenye Washia wengi.
Mjini Tehran, waandamanaji waliteketeza majengo ya ubalozi wa Saudi Arabia

 

CCM yamjia juu Lowassa

Juzi, Lowassa alikaririwa na vyombo vya habari kutoka Monduli
akisema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa maelekezo ya
Serikali imekuwa ikiwatoza kodi kubwa wafanyabiashara kwa
sababu waliifadhili Chadema kwenye kampeni za uchaguzi mkuu
mwaka jana.

Lowassa aliwahi kutoa kauli kama hiyo jijini Mwanza akiwa kwenye
msiba wa aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema wa mkoa wa Geita,
Alphonce Mawazo aliyeuawa kwa kushambuliwa kwa mapanga.
Pia wakati wa harambee ya Chadema iliyofanywa Septemba 22 mwaka
jana, mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alisema kulikuwa na
matajiri watano wenye uwezo kiuchumi ambao walikuwa tayari
kukisaidia kwenye shughuli zake za kampeni, lakini hawataki kutajwa
majina yao kwa hofu ya kufuatiliwa na vyombo vya dola.
Jana, akizungumza na waandishi wa habari jijini, Abdallah Bulembo,
ambaye ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, alisema kauli ya
Lowassa haina ukweli wowote na kwamba ina lengo la kuigombanisha
Serikali na walipakodi ambao wanahitajika sana kipindi hiki.
“Kama kweli Lowassa anawafahamu wafanyabiashara au kampuni
ambazo zinatozwa kodi kubwa kwa sababu walikuwa wamekifadhili
chama hicho, basi ni vizuri awataje ili wajulikane na waseme wao
wenyewe,” alisema Bulembo ambaye wakati wa kampeni alikuwa bega
kwa bega na mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli.
Akijibu suala hilo, Lowassa alisema kuna wafanyabiashara wengi
waliokuwa wakikifadhili chama ambao wanalalamika kutozwa kodi
kubwa. “Kuna watu wengi wanalia kutozwa kodi kubwa,” alisema Lowassa
ambaye aligombea urais kwa tiketi ya Chadema baada ya kuihama CCM
Julai mwaka jana. “Suala hapa si kuwataja majina, mkihitaji majina yao fanyeni research
(utafiti) mtawapata. Lakini mfahamu kwamba kuna tatizo hilo.” Alisema ana uhakika vyombo vya habari vitawapata watu hao na kwa kuwa ni wengi watatoa malalamiko yao.
Akifafanua zaidi, Bulembo alisema kauli ya Lowassa inadhoofisha nguvu
ya Rais Magufuli ambaye ameongeza makusanyo ya kodi kutoka Sh850
alipoingia madarakani hadi Sh1.3 trilioni kwa mwezi.
CCM yamjia juu Lowassa “Tunawahitaji walipakodi wengi wakati huu kwani tunahitaji kupata
fedha zaidi ili kutekeleza ahadi tulizowaahidi wananchi. Kauli ya
Lowassa inatugombanisha na walipakodi,” alisema.
Alisema anachofahamu ni kwamba kodi inatozwa bila kumpendelea
mfadhili wa CCM au kumwonea mfadhili wa Chadema.
“Masuala ya vyama ya siasa yameshapita, sasa hivi ni kujenga nchi na
kodi inatozwa bila kuangalia vyama vya siasa,” alisema Bulembo.
Alimwomba Lowassa kumsaidia Magufuli katika kazi ya kutafuta mapato
ili kuwaletea wananchi maisha mazuri
“Namwomba Lowassa tujenge nchi yetu, huu si wakati wa kufanya siasa,
asubiri mwaka 2020 kama atagombea tena urais tutakutana kwenye
majukwaa,” alisema.
Alisema kuendelea kupigana vijembe kipindi hiki ni kurudisha nyuma
maendeleo ambayo yanahitaji zaidi walipakodi.
“Kodi zina vipimo vyake kama kuna watu wameonewa ukweli
utajulikana,” alisema Bulembo ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya
CCM.
Alisema Serikali ya CCM itaendelea kutenda haki kwa wananchi wake ili
kukiwezesha chama hicho kushinda uchaguzi kwa kishindo mwaka
2020. Alipoulizwa kuhusu madai hayo, mkurugenzi wa idara ya elimu na
huduma kwa walipakodi wa TRA, Richard Kayombo alisema mamlaka
hiyo haijapata malalamiko yoyote.
Alisema mamlaka hiyo inafanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni
zilizowekwa na haifanyi kazi kwa kufuata maagizo ya vyama vya siasa.
“Sisi hatuko kwenye siasa tunafanya kazi zetu kwa kuongozwa na sheria
na kanuni. Hatumwonei mtu wala kupendelea,” alisema.
Kauli kama ya Lowassa ilitolewa pia na mkuu wa idara ya habari ya
Chadema, Tumaini Makene aliyesema hoja ni kueleza kuwapo kwa tatizo
ambalo halitaishia kwenye ubaguzi wa kiitikadi.
“Ukianza kubagua watu kivyama, huwezi kuishia hapo. Utaanza
kuwabagua kikabila, kikanda na hata kidini. Hii ni kinyume na ahadi ya
Rais Magufuli kuwa atakuwa Rais wa watu wote,” alisema Makene.
CCM yamjia juu Lowassa Makene alitoa mfano wa kukataliwa kwa misaada ya vifaatiba katika
zahanati za Serikali mkoani Kagera uliotolewa na mbunge wa Bukoba
Mjini, Wilfred Lwakatare. Mara baada ya kuingia Ikulu, Rais Magufuli alikutana na watumishi wa
Hazina na kuwaelekeza kukusanya kodi bila ya kuangalia sura, huku
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifanya ziara za mara kwa mara
bandarini ambako ameibua kashfa za ukwepaji kodi na upitishaji
makontena kifisadi.

Touadera achukua uongozi wa mapema CAR

Matokeo ya mapema ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati yanaonyesha Waziri Mkuu wa zamani Faustin Archange Touadera anaongoza.

Wagombea 30 walishiriki kwenye uchaguzi huo ambao huenda ukaingia kwa duru ya pili kati ya wagombea wawili watakaoongoza tarehe 31 Januari.

Bw Touadera hakupigiwa upatu kupata kura nyingi.

Alikuwa waziri mkuu kwenye serikali ya rais wa zamani Francois Bozize, aliyeondolewa madarakani 2013 na wapiganaji wa Kiislamu wa kundi la Seleka.

Upigaji kura ulifanyika tarehe 30 Desemba, walinda amani wa Umoja wa Mataifa wakilinda vituo vya kupigia kura.

CAR kwa sasa inaongozwa na kaimu rais Catherine Samba-Panza.

Bw Touadera, 58, alikuwa mhadhiri wa somo la hesabu chuo kikuu kabla ya kujiunga na siasa. Aliwania urais kama mgombea huru, bila kutumia chama chochote cha siasa.

Baada ya kura kuhesabiwa mji mkuu Bangui, yuko mbele sana ya mpinzani wake wa karibu Anicet Georges Dologuele, ambaye pia ni waziri mkuu wa zamani.

Kando na Bangui, kura nyingi hazijahesabiwa katika mikoa mingine ya CAR, sawa na za wakimbizi na raia wanaoishi nje ya nchi.

Bw Touadera ana zaidi ya kura 120,000 naye Bw Dologuele ana takriban kura 68,500.

Wa tatu ni Desire Kolingba, mwana wa rais wa zamani, tume ya uchaguzi imesema.

Wapiga kura 1.8 milioni walitarajiwa kushiriki kwenye uchaguzi huo.

Chuo kikuu cha Garissa chafunguliwa tena

Chuo kikuu cha Garissa kilichofungwa mwaka uliopita baada ya watu 148 kuuawa kwenye shambulio lililotekelezwa na wanamgambo wa al-Shabab, kimefunguliwa tena.

Wafanyakazi wamefika kazini leo huku usalama ukiwa umeimarishwa.

Kila aliyekuwa akiingia katika chuo kikuu hicho kilichoko eneo la kaskazini mashariki mwa Kenya amepekuliwa na maafisa wa usalama.

Kituo cha polisi, ambacho kitakuwa na maafisa zaidi ya 20 wa kutoa ulinzi, kimejengwa ndani ya chuo kikuu hicho.

Kitambulisha mada #GarissaUniversityReopens (Chuo Kikuu cha Garissa chafunguliwa tena) kimekuwa kikivuma katika mtandao wa Twitter nchini Kenya.

Wengi wanasema kufunguliwa kwa chuo hicho kunaonyesha Wakenya hawawezi kuvunjwa moyo na magaidi.

Msimamizi mkuu wa chuo kikuu hicho Prof Ahmed Warfa ameambia MICHAKATO Magazine kwamba wanafunzi wataanza kufika chuoni Jumatatu ijayo tarehe 11 Januari.

Hakukukuwa na sherehe yoyote maalum ya kuadhimisha kufunguliwa upya kwa chuo hicho.