MICHAKATO

Levis Rocky Ndekeno

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Pages

Tuesday, January 12, 2016

Museveni: Siwezi kuaachia madaraka kirahisi

Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda amesema hawezi
kuachia madaraka kwa sababu mazao yake yote aliyoyapanda ndiyo
yanaanza kutoa matunda.
Akizungumza kwenye mkutano wake wa kampeni za kuelekea Uchaguzi
Mkuu nchini humo, Museveni alisema akiachia madaraka kwa sasa
atakuwa hajawatendea haki raia wa Uganda.
“Wale wanaosema, ‘muache aende, muache aende’ wanapaswa
kufahamu kwamba huu siyo wakati wa kufanya hivyo,” alisema
Museveni wakati akihutubia mkutano wa kampeni katika wilaya ya
Ntungamo
“Huyu mzee aliokoa nchi hii, mnaweza kumtaka aondoke? Ninawezaje
kuacha shamba la migomba ambayo nimeipanda mwenyewe na
limeshaanza kutoa matunda?” alihoji Museveni na kuongeza:
“Lazima tuzingatie maendeleo, wakati wangu utafika na nitaondoka.”
Wagombea saba watashiriki kwenye kinyang’anyiro cha urais nchini
humo Februari 18 mwaka huu ili kumuondoa Museveni madarakani.
Kiongozi huyo aliyekaa madarakani tangu mwaka 1986, anachuana
vikali na wapinzani wake, Dk Kizza Besigye na Amama Mbabazi,
aliyekuwa waziri mkuu.Mbabazi alisema akishinda urais atapitisha
kipengele cha muda wa rais kukaa madarakani wa vipindi viwili.
“Wakati yeye (Museveni) aliponiambia kwamba hangestaafu na
kuniomba nimuunge aendelee kuwania urais , nilisema hapana na sasa
niko hapa,” alisema Mbabazi kwenye mkutano wa kampeni nchini humo
“Katika siku100 za kwanza nikiwa rais, tutarejesha vipindi vya rais
kukaa madarakani katika katiba na tutafanya tuwezalo kuhakikisha
kuwa katika miaka mitano ya kwanza tutafanya juu chini kuandaa kizazi
chenye umri mdogo ili kitwae madaraka Uganda,” alisema Mbabazi.
Museveni: Siwezi kuaachia madaraka kirahisi -

Mahakama yalipinga Bunge:Venezuela

Mahakama kuu ya Venezuela imeamuru masuala yote ambayo yatatekelezwa na bunge la nchi hiyo ambalo linadhibitiwa na upinzani hayatatambuliwa rasmi hadi pale wabunge watatu wanaoshtumiwa kutochagua kihalali watakapoondolewa.
Uamuzi huo bila shaka utaongeza sintofahamu iliyopo baina chama tawala cha Nicolas Maduro,na kile cha muungano wa upinzani kilichoshinda viti vingi bungeni katika uchaguzi wa December.
Bunge jipya la nchi hiyo linadaiwa kupuuza amri ya mahakama kuu iliyotoa zuio kuapishwa wa upinzani,ambao walikuwa wakihofia kuikosatheluthi mbili ya kura zote za bunge.

Picha za Salah Abdeslam zaibuka


Picha za kwanza za mshukiwa wa shambulizi la mji wa Paris Salah Abdeslam zimeripotiwa kuibuka, kwa mujibu wa kituo cha runinga cha urafansa BFM.
Picha hizo zilinaswa asubuhi ya tarehe 14 mwezi Novemba na camera za CCTV katika kituo kimoja cha mafuta nchini Ufarasa siku moja baada ya mashambulizi yaliyosababisha vifo vya watu 130.
Katika picha hizo Salah Abdeslam anaonekana mtulivu akitembea huku akiwa ameweka mikono yake mfukoni.
Salah Abdeslam anaripotiwa kuwaita marafiki zake wawili Mohammed Amri na Salah Hamza Attou akiwa mjini Paris mapema tarehe 14 mwezi Novemda waje kumpeleka nchini Ubelgiji.
Wakiwa njiani kutoka Paris kwenda Brussels, wanaume hao watatu walisimama katika kituo cha mafuta karibu na mpaka wa Ubelgiji kwa takriban dakika 15 ambapo Camera ya CCTV iliwanasa.
Wakati huo wanaume hao tayari walikuwa wamepita katika vizuizi vitatu vya polisi, lakini hawakusimamishwa kwa sababu Salah Abdeslam hakuwa amehusishwa na mashambulizi ya Paris.
Mohammed Amri na Salah Hamza Attou baadaye waliamuacha Salah Abdeslam katika wilaya ya Laeken mjini Brussels, na wawili hao walikamatwa katika eneo la Molenbeek siku moja baadaye na sasa wanakabiliwa na mashtaka ya ugaidi huku Salah Abdeslam akiwa bado hajapatikana.

Afisa mkuu wa polisi afungwa jela Uchina

Naibu mkuu wa polisi wa zamani nchini Uchina amefungwa jela miaka 15 kwa makosa ya ufisadi, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.
Li Dongsheng alikuwa na uhusiano na Zhou Yongkang, aliyefungwa jela maisha mwezi Juni mwaka jana kwa makosa ya ufisadi.
Habari za kuhukumiwa kwake zimeripotiwa katika mitandao ya kijamii ya runinga ya taifa nchini humo CCTV.
Afisa huyo anadaiwa kupokea hongo ya takriban yuan 22m ($3.3m; £2.3m).

Karibu 400 wanahitaji matibabu Madaya


Mkuu wa huduma za kibinadamu katika umoja wa mataifa anasema kuwa karibu watu 400 waliozingirwa katika mji wa Madaya nchini Syria wanahitajika kuondolewa mjini humo kwa dharuara ili kupata matibabu .
Stephen O'Brien alitayasema hayo baada ya mkutano wa baraza kuu la umoja wa mataifa uliofanyika kujadili hali katika mji huo unaodhibitiwa na waasi karibu na mji wa Damascus.
Mapema msafara wa malori ya misaada ulipeleka tani 40,000 kwa wenyeji ambao wamezigirwa na serikali kwa miezi kadha.
Umoja wa mataifa unasema kuwa umapata ripoti kuwa watu wanakufa kutokana na njaa.
Msaada wa siku ya Jumapili ndio wa kwanza kuruhusiwa kuingia katika mji wa Madaya tangu mwezi Oktoba wakati shirika la mpango wa chakula la umoja wa mataifa lilipeleka msaada wa mwezi mzima kwa watu 20,000.
Pia magari yaliyobeba misaada yaliingia miji miwili inayozingirwa na waasi katika mkoa wa kaskazini wa Idlib chini ya makubaliano kati ya pande zinazopigana.

Watu 10 wauawa katika mlipuko Uturuki


Mlipuko mkubwa umetokea katika mji mkuu wa Uturuki, Istanbul.
Mlipuko huo umetokea katikati mwa mji wa kale wa Istanbul.
Eneo hilo huwa kivutio kikuu cha watalii.
Maafisa wa polisi kwa sasa wamedhiiti eneo hilo.
Afisi ya gavana wa Istanbul inasema kuwa watu kumi wameuwawa na 15 kujeruhiwa.
Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa zasema kuwa ni shambulizi la kujitoa muhanga.

Kesi ya naibu rais wa Kenya yaendelea

Kesi ya uhalifu inayomkabili naibu rais wa Kenya William Ruto katika mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ya The Hague hatimaye imeanza.

Ruto yuko katika mahakama hiyo na mwandishi Joshua Arap Sang ambaye pia anajaribu kutoa ushahidi utakaosababisha kufutiliwa mbali kwa kesi hiyo inayohusishwa na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 nchini Kenya.

Mnamo mwezi Disemba mwaka jana mahakama hiyo ilifutilia mbali mashtaka dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kwa ukosefu wa ushahidi,lakini mwendesha mashtaka anahoji kwamba bwana Ruto na mwandishi Joshua Sang wana kesi ya kujibu.

Washtakiwa wanasema kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kutoa ushahidi wa kutosha kwa kesi hiyo kuendelea huku wakikana mashtaka hayo.