MICHAKATO

Levis Rocky Ndekeno

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Pages

Sunday, February 16, 2014

Chadema yatishia kususia Bunge la Katiba

    Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akimtambulisha Grace Tendega Dar es Salaam jana kwa waandishi wa habari kuwa mgombea wa Uchaguzi Mdogo Jimbo la Kalenga. (Na Mpigapicha Wetu).

WAKATI keshokutwa Bunge Maalum la Katiba linaanza kukutana mjini Dodoma, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema huenda kikasusia Bunge Maalum la Katiba iwapo litaendeshwa kwa kufuata matakwa ya chama cha siasa na siyo ya wananchi.

Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alisema hayo jana wakati akielezea maamuzi ya Kikao cha Kamati Kuu (CC) kilichofanyika jana na kueleza kuwa chama hicho kinaenda katika Bunge hilo kikiwa na hadhari ya hilo.

Alisema wanaenda kwenye kikao hicho wakiwa na masikitiko kutokana na uteuzi wa wajumbe 201 wa bunge hilo waliotangazwa hivi karibuni kuwa karibu asilimia 75 hadi 80 ni wanaCCM.

Akijibu hilo, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema “Tumewazoea, sio mara ya kwanza kususa waache wasuse najua nia yao tangu mwanzo ni Katiba isipatikane. Katiba mpya itapatikana hata wakisusa”.

Naye Mbowe alifafanua “Hatuendi katika bunge hilo kugoma lakini mambo yakienda visivyo kwa kufuata matakwa ya chama cha siasa na siyo mapendekezo ya rasimu ya pili ya Katiba hiyo ambayo ni ya wananchi tutalizira Bunge hilo,” alisema.

Alibainisha kuwa chama hicho hawatasita kurejea kwa wananchi wakati Bunge likiendelea au likiwa limeisha iwapo wingi wa wabunge wa chama tawala utaathiri Bunge hilo.

“Sasa wananchi watatuelewa dhamira yetu ya kutaka wajumbe hao wasiteuliwe na Rais kwani tulibishana sana lakini baadaye tulikubaliana jambo ambalo limeonesha kwa kuteuliwa makada wengi kwa manufaa ya chama tawala,” alisema Mbowe.

Alisema ingefaa makundi yenyewe yangeteua wawakilishi wao na siyo kupeleka kwa Rais hivyo Bunge hilo linaloanza keshokutwa wanaenda kwa tahadhari.

Vikao vya Bunge Maalum la Katiba linatarajia kuanza keshokutwa likihusisha wajumbe ambao ni wabunge wote wa Baraza la Wawakilishi ,Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na wajumbe 201 walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete akishirikiana na Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein.

Wajumbe hao 201 wameteuliwa kutoka makundi tofauti yakiwemo ya Taasisi zisizo za kiserikali, vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, Taasisi za dini, Taasisi za elimu, watu wenye ulemavu, vyama vya wafanyakazi, vyama vinavyowakilisha wakulima, wafugaji, wavuvi na kundi la watu wenye malengo yanayofanana.

Bunge hilo litahusisha wajumbe takriban 650 wanaokwenda kuijadili rasimu ya pili ya Katiba na watatumia siku 70 na iwapo hazitatosha wataongezewa siku 20 ili kukamilisha mjadala huo. Kitakachofuata baada ya Bunge Maalum la Katiba ni wananchi kupiga kura ya maoni kupitisha Katiba hiyo mpya.

Katiba hiyo mpya itafuta Katiba ya sasa iliyodumu tangu Tanganyika ilipopata uhuru mwaka 1961 na mabadiliko kadhaa yaliyofuatia baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Alipoulizwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema “tumewazoea, sio mara ya kwanza kususa waache wasuse najua nia yao tangu mwanzo ni Katiba isipatikane. Katiba mpya itapatikana hata wakisusa”

JK achoshwa na Siasa chafu



MWENYEKITI wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete amewataka wanachama wake kuacha unyonge na kujibu mapigo ya wapinzani hasa wale ambao wanaendesha siasa za vurugu katika kampeni za chaguzi mbalimbali nchini.

Rais Kikwete amesema kuwa uvumilivu una ukomo, na kwamba sasa wanachama wa CCM hawana budi kuacha unyonge, kutokana na siasa hizo za vurugu zinazoendeshwa na vyama vya upinzani.

Aliyasema hayo jana mjini hapa wakati akifungua kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kitakachokutana kwa siku mbili chini ya uenyekiti wake, ambacho ajenda kuu ni kuzungumzia Bunge Maalumu la Katiba.

“Tumelizungumzia hili katika Kamati Kuu, tumekubaliana kuacha unyonge (makofi). Ndio watu wamelisema hili katika Kamati Kuu, tumesema jamani tumekubaliana kuacha unyonge,” alisema Rais Kikwete ambaye wakati anafungua kikao hicho waandishi wa habari walikuwamo, na akaongeza: “Wacha wakaseme (waandishi wa habari), ndio tumekubaliana kuacha unyonge. Kabisa. Hata kama leo katika taarifa za habari, zisiwekwe habari nyingine, msikike ninyi tu. Uvumilivu una ukomo wake.”

Mwenyekiti huyo wa CCM alisema wamefikia hatua hiyo kwa sababu yanayotokea yanasikitisha sana na akatoa mfano wa matukio kadhaa ya uvunjifu wa amani katika kampeni katika maeneo ya Igunga mkoani Tabora na Kahama mkoani Shinyanga.

“Maana tunashindana na wenzetu wagomvi maana wao ugomvi ndio sehemu ya mwongozo wa kufanya kazi ya siasa. Maana pale Kahama kijana wamemtoa macho kwa bisibisi. Acheni unyonge (makofi). “Nasema kwa kweli kwa sababu yanayotokea yanasikitisha. Pale Igunga kijana yule wamemmwagia tindikali, pale Kahama kijana wamemtoa macho kwa bisibisi. Tuache unyonge,” alisisitiza Rais Kikwete huku akishinikizwa kwa shangwe za CCM Oyee, Mapinduzi Daima.

Ingawa Rais Kikwete hakutaja chama, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimekuwa kikihusishwa na vurugu za uchaguzi katika maeneo mbalimbali yakiwamo ya Igunga na Kahama katika uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika hivi karibuni na pia katika chaguzi ndogo za ubunge.

Pongezi za ushindi

Akizungumzia uchaguzi mdogo wa kata 27 zilizofanyika hivi karibuni na CCM kuzoa kata 23, Rais Kikwete aliwapongeza wanaCCM kwa ushindi huo, lakini akawapa changamoto ya kuhakikisha wanarejesha kata hizo nne zilizokwenda kwa vyama vya upinzani.

“Huu ni ushindi mkubwa sana, ushindi mnono. Ni vizuri kutumia nafasi hii kujipongeza na kuwapongeza wenzetu kwa kazi nzuri, kazi nzuri waliyoifanya ya kujenga chama,” alisema Rais Kikwete na kuongeza: “Lakini tukumbushane kwamba kata nne hatukuzipata, hivyo tuna kazi ya kuzikomboa, sisi wakati wote nia yetu ni kushinda, kushindwa haiwezekani.”

Aidha, alizungumzia uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga mkoani Iringa, akisema hadi sasa hali ni shwari, hakuna migawanyiko wala misukosuko kama ilivyokuwa kwa Jimbo la Arumeru Mashariki ambalo alisema tangu mwanzo hadi mwisho, hali haikuwa shwari.

Alisema hadi sasa wana uhakika wa ushindi katika jimbo hilo, lakini akawataka wanaCCM kujiandaa vyema kwa kila hali na kuhakikisha ushindi unapatikana katika jimbo lililoachwa wazi kutokana na kifo cha aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa.

Mwanawe Geoffrey ndiye mgombea wa CCM. Pia aliwataka wanachama na viongozi wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani, nao kujiandaa kwa uchaguzi mdogo kwa sababu tayari Spika wa Bunge, ametoa taarifa serikalini kuhusu kuwa wazi kwa jimbo hilo kutokana na kifo cha mbunge wake, Said Bwanamdogo.

“Msikae tu kusubiri na kuendelea kuomboleza, kwa sababu Serikali haiombolezi, wao wanachotaka ni uchaguzi ujazwe, shughuli ziendelee. Maana watu wanaweza kusema hata orobaini bado. Kule Arumeru tuliambiwa tumbo bado halijapasuka. Kwani kwa Mgimwa orobaini tayari, mbona mchakato umeanza. “Ninyi fanyeni mchakato, orobaini yetu mnaweza kufanya wakati mambo mengine yakiendelea. Tujiandae mapema ili kuhakikisha tunashinda,” alisema Mwenyekiti huyo wa CCM na kuwapongeza viongozi wa mkoa na wilaya waliofanikisha ushindi katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki ambako mgombea wao, Mahmoud Thabit Kombo alishinda.

Alisema CCM ilibidi kumtosa aliyekuwa mbunge wao, Mansour Yussuf Himid, kwa sababu alikuwa akivaa magwanda ya chama hicho, lakini alikuwa akipinga sera na taratibu za chama hicho tawala.

“Kila akifungua mdomo wake anaitukana CCM, kila akifungua mdomo anapingana na sera za CCM. Tukasema inatosha, bora kuwa na mpinzani huko nje kuliko huyu, ndio maana niliwahi kusema katika NEC moja hapa kuwa sijui mtu anasema nitahama CCM, nikasema nendeni sasa hivi,” alisema Kikwete.




Birdman atangaza kuandaa birthday party ya kufuru, itakagharimu tshs mil 800, itakuwa na models 30 watupu na wengine 700 waliovaa nguo...soma zaid hapa




Katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ya miaka 45, Birdman ataangusha party ya nguvu itakayogharibu dola laki 5 (sawa na shilingi milioni 800) itakayokuwa na walimbwende watakaokuwa watupu, crew yote ya Young Money na gari zake zote zinazofikia thamani ya dola milioni 7.

 Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, sherehe hiyo itafanyika Jumamosi usiku katikati ya NBA All-Star Weekend. Rapper huyo amekodi uwanja alioupa jina “Birdman’s New Era Voodoo Lounge.”
 Pamoja na wanawake 30 walio watupu, kutakuwa na models wengine 700 watakaovaa nguo. Zaidi ya hapo atasafirisha gari zake kutoka Miami ambazo kwa pamoja zina thamani ya dola milioni 7 zikiwemo Bugatti 2, Maybachs, 2 na basi 3 za tour.
 Wageni waalikwa ni pamoja na James Harden, Paul George, Blake Griffin, Shaq, Kenny Smith na rappers wa Young Money, Lil Wayne, Drake, Nicki Minaj, na wengine. Pia wasanii wa zamani wa Cash Money, Mystikal, Turk, Juvenile, na Mannie Fresh watakuwepo.