MICHAKATO

Levis Rocky Ndekeno

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Pages

Friday, May 6, 2016

Spika Paul Ryan ampinga Donald Trump

Spika wa Republican katika Baraza la Wawakilishi la Marekani,Paul Ryan,amesema hayupo tayari kumuunga mkono Donald Trump kuwa mgombea wa Urais kupitia chama hicho.
Mfanyabiashara huyo bilionea anaonekana dhahiri kushinda katika mbio za uteuzi kukiwakilisha chama hicho lakini Ryan alisema kuwa kabla hakuweza kuidhinisha suala hilo,Na kuwa Trump alipaswa kuwaonyesha watu kuwa anaheshimu taratibu za Republican na angepata kura za Wamarekani wengi zaidi.
Katika kulijibu hilo Trump lisema hakuwa tiyari kuunga mkono ajenda ya RyanMapema Marais wa zamani wa Marekani George W Bush na babaye George Bush waliweka wazi kuwa hawatunga mkono kupita kwa Trump.

Mfanyabiashara Jacob Juma auawa Nairobi

Mfanyabiashara mashuhuri Jacob Juma, ambaye amekuwa akizua mjadala mitandaoni Kenya kutokana na ujumbe wake anaoandika hasa kwenye Twitter, ameuawa kwa kupigwa risasi jijini Nairobi. Taarifa zinasema Bw Juma alipigwa risasi na watu ambao walikuwa wakiendesha pikipiki alipokuwa akielekea nyumbani kwake mtaa wa Karen mwendo wa saa nne usiku. Gari lake lilipatikana na zaidi ya matundu 10 ya risasi.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation la Kenya, polisi wanasema hakuna kilichoibiwa kutoka kwenye gari lake. Simu zake mbili na pesa vilipatikana ndani ya gari. Bw Juma alikuwa mwanakandarasi ambaye pia alihusika katika sekta ya uchimbaji madini.

WhatsApp kuja na ‘version’ rasmi ya kwenye computer

Najua kuwa kwa sasa unaweza kutumia WhatsApp kwenye computer yako kwa kuscan code maalum na kuunganisha app ya simu na whatsapp web. Lakini siku zijazo, utaweza kutumia WhatsApp ya kwenye computer inayojitegemea yenyewe, imebainika.Kuna tetesi kuwa WhatsApp itakuja kwenye desktop kwa computer za Mac na Windows katika nia ya kujipanua zaidi. WhatsApp ya kwenye computer itakuwezesha kupiga simu za sauti na video na huduma zingine.Ikianza, hautakuwa na haja tena ya kuscan QR code kujiunganisha na browser yako. Hatua hii itakuwa huduma mbadala wa huduma kama Slack, Messenger au Skype kwa mawasialino yasiyo kuwa ya maandishi.