MICHAKATO

Levis Rocky Ndekeno

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Pages

Monday, June 9, 2014

Ubakaji 'Silaha ya vita'



Viongozi wa kimataifa wanakutana jijini London kwa wiki nzima, kwa kongamano la kumaliza dhulma za kimapenzi katika mataifa yanayokabiliwa na mizozo.Mkutano huo, wa siku nne umeandaliwa na Waziri wa masuala ya nchi za kigeni wa Uingereza, William Hague na muigizaji maarufu na mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa, Angelina Jolie. Kongamano hilo linajiri huku mataifa kadhaa barani Afrika yakikabiliwa na changamoto ya kumaliza ubakaji unaotumiwa kama silaha ya kivita. Ni mwanzo wa kuidhinishwa kampeni ya miaka miwili kutoa uhamasisho kuhusu kutumiwa kwa ubakaji na unyanyasaji wa kimapenzi kama silaha wakati wa vita. Waandalizi wa kongamano hilo wanasema wanataka huu uwe wakati ambapo ulimwengu utazinduka na kutangaza kwamba unyanyasaji wa kimapenzi sio jambo lisiloweza kuepukika wakati wa vita. Ujumbe ni ubakaji sio jambo lisiloweza kuepukika wakati wa vita. Uwajibikaji wa kimataifa Tangu William Hague na Angelina Jolie wazinduwe kampeni hiyo, mataifa mia moja na arobaini na nane yameidhinisha azimio la uwajibikaji wa kumaliza unyanyasaji huo wa kimapenzi katika mizozo. Lakini lengo sasa ni kuchukua hatua madhubuti, kuendeleza uchunguzi na kuripotiwa kwa visa hivyo vya unyanyasaji wa kimapenzi. Pia katika kutoa usaidizi zaidi kwa waathiriwa na kuhakikisha kuwa usawa wa kijinsia unahimizwa katika operesheni za siku zijazo za kulinda amani.  Kiwango cha jukumu hilo ni kikubwa: katika miaka ya tisaini, vita vya Bosnia vilisababisha kuwepo takriban waathiriwa elfu hamsini wa unyanyasaji wa kimapenzi. Takriban miongo miwili tangu vita hivyo vimalizike, ni wahalifu wapatao 60 pekee walioshtakiwa.

Wanawake 20 wanaume 3 watekwa Nigeria


Wapiganaji wanaoshukiwa kuwa wanachama wa Boko Haram wamewateka nyara wanawake 20 kutoka jamii inayohamahama Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Wanawake hao walichukuliwa katika Makazi ya Gakini Fulani karibu na mji wa Chibok ambako zaidi ya wasichana wanafunzi 200 walitekwa nyara Aprili, mwaka huu.
Walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa wapiganaji hao waliokuwa wamejihami kwa bunduki waliwalazimisha wanawake hao kuingia katika magari yao kabla ya kutoroka nao katika Jimbo la Borno.

Mlinzi mmoja wa kijiji alisema kuwa washambulizi hao pia waliwateka nyara wanaume watatu waliojaribu kuwazuia wasiondoke na wanawake hao.

Hadi sasa jeshi halijasema lo lote kuhusiana na tukio hilo.

Shambulio hilo lilitokea katika mji wa Chibok ambako wapiganaji wengine wa silaha waliwteka nyara zaidi ya wasichana 200 wanafunzi Aprili, mwaka huu.

Wakati huo jeshi la Nigeria limesema kuwa limewaua wapiganaji 50 katika kampeni yake dhidi ya magaidi mwishoni mwa wiki katika majimbo la Borno na Aladawa.

Mfululizo wa mashambulizi Kaskazini Mashariki mwa taifa hilo umeimarisha ukosoaji wa vyombo vya usalama vya Serikali.

Licha ya kuwepo kwa hali ya hatari katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria wanajeshi hawajachukua hatua dhabiti na wakati mwingine hawapo wakati washambulizi wanaotekeleza uhalifu wao