MICHAKATO

Levis Rocky Ndekeno

Pages

Sunday, January 19, 2014

Wasifu Wa Raisi Jakaya Mrisho Kikwete




Dr. Jakaya M Kikwete
 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania tangu 2011-12-30
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alizaliwa tarehe 7 Oktoba mwaka 1950 Msoga, mkoa wa Pwani, mtoto wa sita katika familia ya watoto tisa. Amemuoa mama Salma Kikwete na wamebarikiwa watoto nane.
Kazi
Mwaka 1976 alijiunga na Chuo Kikuu cha Maofisa wa Jeshi Monduli na kutunukiwa Cheo cha Luteni Kanali na baadaye kuwa Mkufunzi Mkuu na Kamisaa wa Siasa katika chuo hicho. Mheshimiwa Kikwete amefanya kazi katika Chama cha Mapinduzi kwa nyadhifa mbalimbali kwenye mikoa ya Singida na Tabora na  wilaya za Nachingwea na Masasi.

Mwaka 1988 aliteuliwa kuwa Mbunge na Naibu Waziri wa Nishati na Madini. Mwaka 1990 alichaguliwa kuwa mbunge wa  Jimbo la Bagamoyo na akateuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini. Nyadhifa nyingine alizoshika ni Waziri wa Fedha mwaka 1994 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuanzia mwaka 1995 hadi 2005.
Alishika rasmi wadhifa wa urais mwaka  2005 na kuchaguliwa tena 2010 kwa muhula mwingine wa  miaka mitano.
Elimu
Alipata elimu ya msingi na ya kati katika shule za Msoga na St. John Bosco Lugoba kati ya mwaka 1958 na 1965. Aidha, alipata elimu ya sekondari katika shule za sekondari za Kibaha (1966 – 1969) na Tanga (1970 – 1971).Alihitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1975 na kupata Shahada ya Uchumi,
Nyadhifa nyengine
Mwanyekiti wa Viongozi wa Afrika Kupambana na Malaria (ALMA) 2010-2011
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Januari 2010
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) Mwaka 2008
Mwenyekiti Mwenza wa Mchakato wa Helsinki kwenye Utandawazi na Demokrasia Mwaka 2004
Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Mwaka 2004
Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika (OAU) Mwaka 1997
Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Mwaka 1997
Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB) Mwaka 1995


0 comments:

Post a Comment