MICHAKATO

Levis Rocky Ndekeno

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Pages

Thursday, June 12, 2014

Picha:Mabanda ya wafanyabiashara wa soko la Karume yateketea kwa moto


Moto mkubwa umetetekeza kabisa soko kubwa kabisa la mitumba la karume jijini Dar es Salaam usiku wa Jumatano, na kusababisha hasara kubwa kwa wafanyabiashara wote wa soko hilo.
Baadhi ya mabanda yakiteketea kwa moto

 Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, wamedai moto huo ulianza kuteketeza mabanda hayo majira ya saa 4 usiku, huku wakijaribu kutafuta msaada kuuzima bila mafanikio yeyote.

Wazima moto walifanikiwa kuudhibiti moto uloweza kufikia karibu na kiwanda cha Breweries, lakini haujasababisha hasara yeyote katika nyumba za jirani wa soko hilo kwa mujibu wa mwandishi habari wa Raia Mwema Mbaraka Islam alipozungumza na Sauti ya Amerika.

Anasema hakuna kibada cha biashara kilichosalimika na hakuna mtu aliyefanikiwa kuokowa mali yake. Mfanya biashara Wilson magembe anasema amepoteza kila kitu na ilikuwa vigumu kuweza kuchukua bidhaa zao kwa sababu moto uliwaka kwa haraka sana.







Picha: Jennifer Lopez na Pitbull wapamba sherehe za ufunguzi wa kombe la dunia 2014, Brazil





Maelfu ya mashabiki wamejitokeza jioni ya leo kwa saa za Brazil (June 12) katika sherehe za ufunguzi wa fainali za kombe la dunia 2014 kwenye uwanja wa ‘Arena de Sao Paulo’ nchini Brazil, ambapo Jennifer lopez, rapper Pitbull na mwimbaji wa Brazill Claudia Leitte wametumbuiza mbele ya mashabiki waliofurika kwa wingi na kuimba wimbo rasmi wa kombe la dunia kwa mwaka huu ‘We Are One (Ola Ola)’.Maandalizi ya sherehe hizo za ufunguzi yalifanywa kuanzia March mwaka huu, na jumla ya masaa 84 yalitumika kwaajili ya rehearsal za sherehe hizo.Mechi ya ufunguzi wa michuano hiyo inafanyika usiku huu kati ya wenyeji Brazil na Croatia.



Brazil waanza vyema kombe la dunia kwa kuichapa Croatia 3-1


Wenyeji wa michuano ya kombe la dunia, Brazil wameianza vyema baada ya kuichapa Croatia mabao 3-1.


 Croatia ndio walikuwa wa kwanza kupata bao baada ya mchezaji wa Brazil Marcelo kujifunga katika dakika 11. Brazil walijipatia goli lao la kuwasazisha kutoka kwa Neymar aliyezitikisa nyavu za Croatia katika dakika ya 29 kwa shuti la umbali wa yards 25. Mpaka timu hizo zinaenda mapumziko magoli yalikuwa 1-1.



Katika dakika ya 70 referee wa mchezo huo Yuichi Nishimura aliwapa penalty Brazil iliyotumiwa vyema na Neymar aliyeipa Brazil bao la pili.

Wakati zikiwa zimesalia dakika 2 kumalizika kwa mchezo huo, Brazil waliongeza bao la tatu lililofungwa kirahisi na Oscar aliyemwacha mlinda mlango wa Pletikosa akijitupab kujaribu kuuokoa bila mafanikio.

Ushindi wa Brazil umepokelewa kwa furaha kubwa na mashabiki wengi waliokuwa wamefurika kwenye uwanja uliopo mjini Sao Paulo.

Michuano hiyo inaendelea tena Ijumaa hii kwa mechi ya Mexico vs Cameron, Spain vs Netherlands na Chile vs Australia.

Agnes Masogange afunguka maisha yake ya jela yalivyokuwa