MICHAKATO

Levis Rocky Ndekeno

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Pages

Sunday, January 31, 2016

Marais wapinga kutuma jeshi la AU Burundi

Muungano wa Afrika AU hautatuma kikosi cha walinda amani hadi pale serikali ya rais Pierre Nkurunziza itakapotoa mwaliko.
Msemaji wa Muungano wa Afrika AU, amesema kuwa umoja huo hautatuma majeshi ya kulinda amani nchini humo hadi pale watakapopokea mwaliko kutoka kwa taifa hilo la kanda ya Afrika Mashariki.
Kauli hiyo ni kinyume na pendekezo la awali la umoja huo ambao uliibua taharuki kuhusu uhalali wake na wajibu wake wa kulinda maisha ya wananchi.
Mjumbe maalum wa umoja huo kanda ya maziwa makuu Ibrahima Fall, anasema kuwa haijawahi kuwa nia ya AU kutuma walinda amani, bila ya idhini ya taifa husika.

Mkutano wa viongozi na marais wa Afrika huko Ethiopia ulishindwa kupitisha mswada uliohitajika ilikuwatuma wanajeshi wapatao 5000 kulinda amani nchini Burundi kufuatia mauaji ya mamia ya wapinzani wa rais Nkurunziza.
Machafuko nchini humo yalitibuka baada ya Nkurunziza kutangaza nia ya kuwania uchaguzi katika muhula wake wa tatu.
Wapinzani wake walisema Nkurunziza alikuwa anakiuka katiba ya taifa na kisha maandamano yakaanza kukotokea hata jaribio la mapinduzi ambayo ilizimwa na kisha rais huyo akaibuka mshindi katika uchaguzi ambao ulisusiwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa wa upinzani.

Kulikuwa na pendekezo la kutuma kikosi cha wapiganaji 5,000 wa muungano wa Afrika ilikuokoa maisha ya wapinzani wa rais huyo.
Awali rais Nkurunziza alionya kuwa majeshi yake yangewakabili vikali jeshi hilo ''Vamizi'' akisema kuwa nchi hiyo iko salama na kuwa ni vitongoji vichache tu vya Bujumbura ambavyo ni ngome ya upinzanani.
Kauli ya mwaka jana wa Nkurunziza kuamua kuwania urais kwa muhula wa tatu ilisababisha vurugu nchini humo, ambapo mamia ya watu wameuwawa na wengine wengi wakitorokea mataifa jirani.

Magufuli alaani kuuawa kwa rubani porini

Rais wa Tanzania John Magufuli amesema amesikitishwa sana kitendo cha kuuawa kwa rubani Mwingereza aliyekuwa akisaidiana na maafisa wa Tanzania kupambana na ujangili.

Rubani wa helkopta Kapteni Roger Gower, alifariki baada ya majangili kuifyatulia risasi na kuidondosha helkopta aliyokuwa akiiendesha wakati alipoungana na askari wanyamapori waliokuwa wakikabiliana na majangili katika pori la akiba lililopo katika wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu.

Askari mmoja wa Tanzania alijeruhiwa wakati wa kisa hicho.

Tembo watatu pia walipatikana wakiwa wameuawa.

Dkt Magufuli ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha waliomuua rubani huyo wanakamatwa na wanafikishwa mikononi mwa vyombo vya sheria, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa kurugenzi ya mawasiliano ya ikulu.

Polisi tayari wamewakamata washukiwa watatu kuhusiana na mauaji hayo.

Kiongozi huyo amesema serikali yake itahakikisha inaendeleza mapambano dhidi ya ujangili kwa nguvu zake zote.

Amewataka wananchi na wadau mbalimbali wa hifadhi ya wanyamapori, kutokatishwa tamaa na tukio hilo na wasaidie kuwafichua watu wote wanaojihusisha na ujangili ama biashara ya bidhaa zitokanazo na ujangili.

Hivi karibuni, utawala nchini Tanzania umekuwa ukikosolewa kwa kushindwa kutoa maelezo ya kina kuhusiana na uwindaji haramu wa pembe za ndovu.

Uwindaji haramu umeenea sana katika pori ya Maswa na sio tukio la kwanza ambapo wanaharakati wanaolinda wanyama wa porini wanashambuliwa na wawindaji haramu.

Meli kubwa iliyoinama yazua wasiwasi Ufaransa

Meli ya kubwa iliyoegemea upande mmoja inakaribia kufika katika pwani ya Ufaransa, maafisa wa bahari wanasema, ingawa kuna matumaini ya kuiokoa kabla ya kuzama. Meli hiyo kwa jina Modern Express ambayo, imesajiliwa Panama, ilianza kulala upande mmoja Jumanne baada ya kutokea kwa hitilafu za kimitambo. Mabaharia wote 22 wameondolewa kutoka kwenye meli hiyo.

Juhudi za kuisimamisha zimefeli, lakini maafisa wanasema jaribio jingine litafanywa leo Jumatatu.
Juhudi za leo zikishindikana, basi meli hiyo itagonga pwani ya Ufaransa kati ya Jumatatu usiku na Jumanne asubuhi. Hali mbaya ya hewa ilitatiza juhudi za uokoaji Jumapili. Meli hiyo imebeba tani 3,600 za mbao na mashine kadha za uchimbaji, na imeinama kwa pembe ya kati ya nyuzi 40 na 50. Ina tani 33 za mafuta.

Nigeria yaomba mkopo wa dharura

 Nigeria inaomba mkopo wa dharura wa jumla ya dola bilioni tatu unusu kutoka kwa Benki ya Dunia kujaribu kuziba pengo kwenye bajeti yake.

Uchumi wa Nigeria umeathiriwa sana na kushuka kwa bei ya mafuta duniani.

Waziri wa fedha nchini humo Levis Rocky amesema amekuwa akifanya mazungumzo na maafisa wa Benki ya Dunia.Serikali mpya ya Rais Muhammadu Buhari ilikuwa imeacha pengo katika ufadhili wa bajeti yake katika juhudi za kujaribu kusisimua uchumi wa taifa.

Lakini tofauti kati ya mapato na matumizi imeendelea kuongezeka na kuilazimu Nigeria kuomba usaidizi kutoka nje.

Nigeria silo taifa la pekee kuathiriwa na kushuka kwa bei ya mafuta duniani.
Azerbaijan, nchi nyingine inayozalisha mafuta kwa wingi, pia imeanza mazungumzo na Benki ya Dunia.
Uchumi wa Venezuela nao umekuwa katika hali ya tahadhari.
Kushuka kwa bei ya mafuta kulichangia sana katika kushuka kwa jumla ya mapato ya taifa Urusi mwaka jana.

Tuesday, January 12, 2016

Museveni: Siwezi kuaachia madaraka kirahisi

Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda amesema hawezi
kuachia madaraka kwa sababu mazao yake yote aliyoyapanda ndiyo
yanaanza kutoa matunda.
Akizungumza kwenye mkutano wake wa kampeni za kuelekea Uchaguzi
Mkuu nchini humo, Museveni alisema akiachia madaraka kwa sasa
atakuwa hajawatendea haki raia wa Uganda.
“Wale wanaosema, ‘muache aende, muache aende’ wanapaswa
kufahamu kwamba huu siyo wakati wa kufanya hivyo,” alisema
Museveni wakati akihutubia mkutano wa kampeni katika wilaya ya
Ntungamo
“Huyu mzee aliokoa nchi hii, mnaweza kumtaka aondoke? Ninawezaje
kuacha shamba la migomba ambayo nimeipanda mwenyewe na
limeshaanza kutoa matunda?” alihoji Museveni na kuongeza:
“Lazima tuzingatie maendeleo, wakati wangu utafika na nitaondoka.”
Wagombea saba watashiriki kwenye kinyang’anyiro cha urais nchini
humo Februari 18 mwaka huu ili kumuondoa Museveni madarakani.
Kiongozi huyo aliyekaa madarakani tangu mwaka 1986, anachuana
vikali na wapinzani wake, Dk Kizza Besigye na Amama Mbabazi,
aliyekuwa waziri mkuu.Mbabazi alisema akishinda urais atapitisha
kipengele cha muda wa rais kukaa madarakani wa vipindi viwili.
“Wakati yeye (Museveni) aliponiambia kwamba hangestaafu na
kuniomba nimuunge aendelee kuwania urais , nilisema hapana na sasa
niko hapa,” alisema Mbabazi kwenye mkutano wa kampeni nchini humo
“Katika siku100 za kwanza nikiwa rais, tutarejesha vipindi vya rais
kukaa madarakani katika katiba na tutafanya tuwezalo kuhakikisha
kuwa katika miaka mitano ya kwanza tutafanya juu chini kuandaa kizazi
chenye umri mdogo ili kitwae madaraka Uganda,” alisema Mbabazi.
Museveni: Siwezi kuaachia madaraka kirahisi -

Mahakama yalipinga Bunge:Venezuela

Mahakama kuu ya Venezuela imeamuru masuala yote ambayo yatatekelezwa na bunge la nchi hiyo ambalo linadhibitiwa na upinzani hayatatambuliwa rasmi hadi pale wabunge watatu wanaoshtumiwa kutochagua kihalali watakapoondolewa.
Uamuzi huo bila shaka utaongeza sintofahamu iliyopo baina chama tawala cha Nicolas Maduro,na kile cha muungano wa upinzani kilichoshinda viti vingi bungeni katika uchaguzi wa December.
Bunge jipya la nchi hiyo linadaiwa kupuuza amri ya mahakama kuu iliyotoa zuio kuapishwa wa upinzani,ambao walikuwa wakihofia kuikosatheluthi mbili ya kura zote za bunge.

Picha za Salah Abdeslam zaibuka


Picha za kwanza za mshukiwa wa shambulizi la mji wa Paris Salah Abdeslam zimeripotiwa kuibuka, kwa mujibu wa kituo cha runinga cha urafansa BFM.
Picha hizo zilinaswa asubuhi ya tarehe 14 mwezi Novemba na camera za CCTV katika kituo kimoja cha mafuta nchini Ufarasa siku moja baada ya mashambulizi yaliyosababisha vifo vya watu 130.
Katika picha hizo Salah Abdeslam anaonekana mtulivu akitembea huku akiwa ameweka mikono yake mfukoni.
Salah Abdeslam anaripotiwa kuwaita marafiki zake wawili Mohammed Amri na Salah Hamza Attou akiwa mjini Paris mapema tarehe 14 mwezi Novemda waje kumpeleka nchini Ubelgiji.
Wakiwa njiani kutoka Paris kwenda Brussels, wanaume hao watatu walisimama katika kituo cha mafuta karibu na mpaka wa Ubelgiji kwa takriban dakika 15 ambapo Camera ya CCTV iliwanasa.
Wakati huo wanaume hao tayari walikuwa wamepita katika vizuizi vitatu vya polisi, lakini hawakusimamishwa kwa sababu Salah Abdeslam hakuwa amehusishwa na mashambulizi ya Paris.
Mohammed Amri na Salah Hamza Attou baadaye waliamuacha Salah Abdeslam katika wilaya ya Laeken mjini Brussels, na wawili hao walikamatwa katika eneo la Molenbeek siku moja baadaye na sasa wanakabiliwa na mashtaka ya ugaidi huku Salah Abdeslam akiwa bado hajapatikana.

Afisa mkuu wa polisi afungwa jela Uchina

Naibu mkuu wa polisi wa zamani nchini Uchina amefungwa jela miaka 15 kwa makosa ya ufisadi, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.
Li Dongsheng alikuwa na uhusiano na Zhou Yongkang, aliyefungwa jela maisha mwezi Juni mwaka jana kwa makosa ya ufisadi.
Habari za kuhukumiwa kwake zimeripotiwa katika mitandao ya kijamii ya runinga ya taifa nchini humo CCTV.
Afisa huyo anadaiwa kupokea hongo ya takriban yuan 22m ($3.3m; £2.3m).

Karibu 400 wanahitaji matibabu Madaya


Mkuu wa huduma za kibinadamu katika umoja wa mataifa anasema kuwa karibu watu 400 waliozingirwa katika mji wa Madaya nchini Syria wanahitajika kuondolewa mjini humo kwa dharuara ili kupata matibabu .
Stephen O'Brien alitayasema hayo baada ya mkutano wa baraza kuu la umoja wa mataifa uliofanyika kujadili hali katika mji huo unaodhibitiwa na waasi karibu na mji wa Damascus.
Mapema msafara wa malori ya misaada ulipeleka tani 40,000 kwa wenyeji ambao wamezigirwa na serikali kwa miezi kadha.
Umoja wa mataifa unasema kuwa umapata ripoti kuwa watu wanakufa kutokana na njaa.
Msaada wa siku ya Jumapili ndio wa kwanza kuruhusiwa kuingia katika mji wa Madaya tangu mwezi Oktoba wakati shirika la mpango wa chakula la umoja wa mataifa lilipeleka msaada wa mwezi mzima kwa watu 20,000.
Pia magari yaliyobeba misaada yaliingia miji miwili inayozingirwa na waasi katika mkoa wa kaskazini wa Idlib chini ya makubaliano kati ya pande zinazopigana.

Watu 10 wauawa katika mlipuko Uturuki


Mlipuko mkubwa umetokea katika mji mkuu wa Uturuki, Istanbul.
Mlipuko huo umetokea katikati mwa mji wa kale wa Istanbul.
Eneo hilo huwa kivutio kikuu cha watalii.
Maafisa wa polisi kwa sasa wamedhiiti eneo hilo.
Afisi ya gavana wa Istanbul inasema kuwa watu kumi wameuwawa na 15 kujeruhiwa.
Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa zasema kuwa ni shambulizi la kujitoa muhanga.

Kesi ya naibu rais wa Kenya yaendelea

Kesi ya uhalifu inayomkabili naibu rais wa Kenya William Ruto katika mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ya The Hague hatimaye imeanza.

Ruto yuko katika mahakama hiyo na mwandishi Joshua Arap Sang ambaye pia anajaribu kutoa ushahidi utakaosababisha kufutiliwa mbali kwa kesi hiyo inayohusishwa na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 nchini Kenya.

Mnamo mwezi Disemba mwaka jana mahakama hiyo ilifutilia mbali mashtaka dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kwa ukosefu wa ushahidi,lakini mwendesha mashtaka anahoji kwamba bwana Ruto na mwandishi Joshua Sang wana kesi ya kujibu.

Washtakiwa wanasema kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kutoa ushahidi wa kutosha kwa kesi hiyo kuendelea huku wakikana mashtaka hayo.

Monday, January 11, 2016

Myanmar yatafuta muafaka

Serikali ya Myanmar inafanya majadiliano na makundi kadhaa ya kikabila nchi humo ili kupata mwafaka.

Kikao hicho cha siku 5 kinafuatia kutiwa saini hapo October kwa makubaliano ya kusitisha mapigano baina ya serikali na makundi 8 ya wapiganaji.

Waandamana kupinga wahamiaji

Maelfu ya waandamanaji wamefanya mkutano katika mji wa Leipzig Kupinga wahamiaji.

Waandamanaji hao wanaopinga waislamu wanalaumu kuingia kwa wingi kwa wahamiaji kunasababisha ongezeko la udhalilishaji wa kijinsia na ujambazi unaolenga wanawake.

Wamemtolea hasira zao Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ambaye wanamlaumu kwa kile walichoita kuiteketeza nchi yao kwa kuruhusu wahamiaji zaidi ya milioni mwaka uliopita.

Maafisa nchini humo wanasema wengi waliohusika na matukio ya unyanyasaji wa kijinsia wakati wa mkesha wa mwaka mpya asili yao ni wahamiaji

UN wakuta hali mbaya Madaya,Syria


Image caption Magari ya Umoja wa mataifa UN,yakipeleka misaada

Mratibu wa msafara wa kutoa misaada katika mji wa Madaya nchini Syria, Yacoub El Hillo amesema wameowaona watoto wakiwa katika hali mbaya kutokana na kukosa chakula.

El Hillo ameongeza kuwa picha zilizopigwa awali zikionyesha wakazi wa maeneo hayo wakiwa katika hali mbaya kwa kukosa chakula ni za kweli kabisa na ni sawa na kile walichokishuhudia baada ya kufika eneo hilo.

Misaada ya chakula na dawa imepelekwa pia kwenye vijiji viwili kaskazini mwa Syria ambavyo vinaunga mkono Serikali na ambavyo vimeathirika kutokana na mashambulizi dhidi ya waasi.

Naye balozi wa umoja wa mataifa wa Syria Bashar Al Jaafari, amekaririwa akidai kuwa shida katika mji wa madaya imesababishwa na upande wa waasi.

Taarifa kuhusiana na hali ya kibinadamu Madaya ni matokeo ya taarifa za uongo na upuuziaji wa vitendo vibaya vinavyotokea katika maeneo mengine ambayo yanashambuliwa na makundi ya waasi.

Ukweli wa mambo kwa kile kinachoitwa mapigano ni kwamba katika baadhi ya maeneo waasi wanawatumia raia kama kinga yao”

Hata hivyo baadhi ya wanadai pia kuwa waasi wamehifadhi chakula kwaajili ya familia zao na wamekuwa wakiuza ziada ya chakula hicho kwa kiwango kikubwa ambacho ni Zaidi ya dola 400 kwa kilo moja ya mchele.

Serikali ya Syria imekanusha madai ya kwamba inatumia uhaba wa chakula kama moja ya mbinu za kivita

Thursday, January 7, 2016

Watu 14 wauawa shambulio la waasi DR Congo

Watu 14 wameuawa baada ya waasi wa kundi FDLR kushambulia kijiji kimoja mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Ripoti kutoka shirika la habari la AFP na jeshi zinasema shambulizi hilo lilifanyika eneo la Miriki, Kilomita 110 (maili 65) kaskazini mwa mji wa Goma.

Viongozi kadhaa wa waasi wa FDLR wamehusishwa na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 katika nchi jirani ya Rwanda.

Kundi hilo la waasi wa Kihutu limedaiwa kuchochea vita vilivyodumu miongo miwili mashariki mwa DR Congo

Mshukiwa wa ugaidi afungwa miaka 20 Kenya

Mshukiwa wa ugaidi aliyeshtakiwa kuwaingiza watoto katika kundi la al-Shabab amehukumiwa kufungwa jela miaka 20 na mahakama Mombasa.

Samuel Wanjala Wabwire almaarufu Salim Mohammed alishtakiwa kuwapa watoto mafundisho ya itikadi kali.

Alikuwa ameshtakiwa pia kuwa mwanachama wa kundi hilo kutoka Somalia.

Watoto waliotoa ushuhuda kwenye kesi yake wanasema aliwafunza kwamba Wakristo ni makafiri ambao wanafaa kuuawa.

Baadhi ya watoto hao walisilimu.

Bw Wabwire alikuwa mwalimu wa shule ya msingi na pia imam katika Masjid Jihad.

Alikabiliwa pia na shtaka la tatu la kueneza itikadi kali na vita vya kidini. Anadaiwa kutoa mafunzo ya karate msikitini.

Alikamatwa mwezi Juni mwaka 2015 eneo la Kaloleni, jimbo la Kilifi.

‘Watu wengi’ wauawa kituo cha mafunzo Libya

Watu wengi wameuawa baada ya lori lililokuwa limetegwa bomu kulipuka katika kituo cha kuwapa mafunzo maafisa wa polisi katika mji wa Zliten, magharibi mwa Libya.

Mkazi wa Zliten ameambia BBC kwamba kulikuwa na makurutu 400 waliokuwa wakipokea mafunzo katika kituo hicho mlipuko ulipotokea.

Lori hilo lilikuwa la kubeba maji.

Haijabainika iwapo lililipuka langoni ama lililipuka ndani ya kituo hicho.

Meya wa Zliten Miftah Lahmadi anasema watu 40 wamefariki.

Majeruhi kwa sasa wanapelekwa hospitali zilizoko mji mkuu Tripoli kwa sababu hospitali ya Zliten imelemewa na majeruhi.

Shirika la habari la AFP linasema shirika la habari linalotii serikali iliyoko Tripoli linasema idadi ya waliofariki ni zaidi ya 50 na kwamba watu 127 wamejeruhiwa.

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, Martin Kobler, amesema shambulio hilo lilikuwa la kujitoa mhanga

Tanzania kutimua wageni wasio na vibali

Tanzania imeanza rasmi operesheni ya kuwasaka na kuwafurusha raia wa kigeni wanaoishi na kufanya kazi nchini humo kinyume cha sheria.
Naibu waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania Hamad Masauni ameambia wanahabari kwamba operesheni hiyo imeanzishwa baada ya kubainika kwamba kuna raia wengi wa kigeni wanaofanya kazi Tanzania kinyume cha sheria.
Operesheni hiyo hiyo inafanyika siku chache baada ya wizara inayohusika na ajira kumuagiza kamishna wa kazi nchini humo kufuta vibali vya kazi vya muda kwa wageni.
"Serikali haiwezi kukaa kimya wakati vijana wanakosa ajira huku kazi zile walizotakiwa kufanya zikifanywa na raia wa kigeni,” Bw Masauni amenukuliwa na gazeti la Mwananchi.
Afisa wa uhamiaji wa mkoa wa Dar es Salaam John Msumile amesema wanatarajia kuwakamata wageni zaidi ya 350.
Kuhusu vibali va kazi vya muda, Bw Masauni amesema serikali itaandaa utaratibu mwingine wa kushughulikia watu wanaotaka kufanya kazi Tanzania kwa muda.
Hii ni baada ya serikali kupokea malalamiko mengi kuhusu suala hilo.
Mwishoni mwa mwaka waziri katika afisi ya waziri mkuu anayehusika na ajira Jenista Mhagama pamoja na naibu waziri Anthony Mavunde walifanya ziara za kushtukiza katika kampuni mbalimbali.
Waligundua raia kadha wa kigeni waliokuwa wakifanya kazi bila vibali halali.

Irain yasema Saudi Arabia imeshambulia ubalozi

Kituo cha utangazaji cha Iran cha Irinn kimesema makombora yalianguka katika majengo ya ubalozi huo na kusababisha uharibifu.
Wakazi wa Sanaa wanasema kulitokea mashambulio kadha kutoka angani asubuhi, yakitekelezwa na majeshi ya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya waasi wa Houthi.
Uhusiano kati ya nchi hizo mbili umedorora tangu kuuawa kwa mhubiri wa Kishia Sheikh Nimr al-Nimr aliyeshtakiwa makosa yanayohusiana na ugaidi nchini Saudi Arabia.

Iran imesema Saudi Arabia imeshambulia ubalozi wake nchini Yemen kwa makombora.
Kituo cha utangazaji cha Iran cha Irinn kimesema makombora yalianguka katika majengo ya ubalozi huo na kusababisha uharibifu.
Wakazi wa Sanaa wanasema kulitokea mashambulio kadha kutoka angani asubuhi, yakitekelezwa na majeshi ya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya waasi wa Houthi.
Uhusiano kati ya nchi hizo mbili umedorora tangu kuuawa kwa mhubiri wa Kishia Sheikh Nimr al-Nimr aliyeshtakiwa makosa yanayohusiana na ugaidi nchini Saudi Arabia.
Ubalozi wa Saudi Arabia mjini Tehran ulishambuliwa na kuchomwa moto na waandamanaji wakati wa maandamano yaliyotokea maeneo ya Washia kulalamikia mauaji hayo.
Saudi Arabia nayo ilijibu kwa kukatiza uhusiano wa kidiplomasia na Iran, hatua ambayo washirika wake kama vile Bahrain, UAE, Kuwati, Sudan, Somalia na Djibouti walifuata.
Iran na Saudi Arabia zimekuwa zikiunga mkono makundi pinzani katika mizozo inayoendelea nchini Syria na Yemen.

Tazama picha ya kwanza ya filamu mpya ya Lupita Nyong'o "The Queen of Katwe"


picha ya kwanza ya filamu mpya ya muigizaji wa Kenya,Lupita Nyong'o The Queen of Katwe imesambaa mtandaoni. Filamu hiyo imefanywa na kampuni ya Disney. Muigizaji huyo anacheza kama mama wa Madina Nalwanga. Atacheza uhusika mkuu kwenye filamu nyingine iitwayo Americanah

Wafungwa wawili wa Guantanamo wapelekwa Ghana


Wafungwa wawili waliokuwa wakizuiliwa katika gereza la Guantanamo Bay, Cuba, wamehamishiwa Ghana.
Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema idhini ilitolewa kwa Khalid al-Dhuby kuachiliwa huru 2006 na kwa Mahmoud Omar Bin Atef mwaka 2009.
Wawili hao, wanaotoka Yemen, wamezuiliwa kwa zaidi ya mwongo mmoja na hawajawahi kufunguliwa mashtaka.
Ghana imetoa idhini kwa wawili hao kukaa nchini huko kwa miaka miwili, waziri wa mashauri ya kigeni wa Ghana Hanna Tetteh amesema.
Kwa mujibu wa stakabadhi za jeshi la Marekani, Mahmoud Omar Bin Atef ni raia wa Yemen aliyezaliwa Saudi Arabia mwaka 1979 .
Alikamatwa nchini Afghanistan 2001.
Khalid al-Dhuby naye ni mzaliwa wa Saudi Arabia, aliyezaliwa in 1981 na kwenda Afghanistan kupigana.
Taifa hilo la Afrika Magharibi hawalijawahi kuwapokea wafungwa kutoka Guantanamo awali.

Nchi kadha zimewapokea wafungwa wa zamani wa Guantanamo, zikiwemo Uganda na Cape Verde.
Watu 780 walizuiliwa Guantano tangu 2002, lakini kwa sasa ni 105 pekee waliosalia gerezani. Hamsini kati ya hao wameidhinishwa kuachiliwa huru.
Jela hilo ilijengwa na Marekani baada ya amshambulio ya tarehe 11 Septemba mwaka 2001 na hutumiwa na Washington kuwazuilia „wapiganaji maadui”.
Rais Barack Obama amesema anataka kufunga gereza hilo kabla ya kuondoka madarakani mapema 2017.

TRA yaweka rekodi ya Sh1.4trilioni Desemba

          Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana. Kulia  ni Kaimu Kamishna wa Kodi za Ndani, Yussuf Salum.
Serikali ya Awamu ya Tano imekusanya ziada ya Sh900
bilioni kupitia kodi katika kipindi cha miezi miwili tangu aingie
madarakani.

Wakati Novemba makusanyo hayo yalikuwa Sh1.3 trilioni, ikiwa ni ongezeko
la Sh400 bilioni, Desemba makusanyo hayo yanayosimamiwa na Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA), yalifikia Sh1.4 trilioni sawa na ongezeko la
Sh500 bilioni kutoka wastani wa makusanyo ya Sh900 bilioni zilizokuwa
zinakusanywa kila mwezi na Serikali ya Awamu ya Nne.

Iwapo makusanyo hayo ya ziada ya Sh900 bilioni yangeelekezwa kwenye
ununuzi wa magari ya wagonjwa, yangenunuliwa magari 3,000 kwa gharama ya
Sh300 milioni kila moja na kuwezesha kila mkoa kupata magari 120.

Takwimu za ongezeko la Desemba zilitolewa Dar es Salaam jana na Kaimu
Kamishna wa TRA, Alphayo Kidata ambaye alisema kuanzia Julai hadi
Desemba mwaka jana, mamlaka yake ilikuwa imekusanya wastani wa Sh6.4
trilioni ambayo ilikuwa ni sawa na asilimia 95.5 ya lengo la kukusanya
Sh6.5 trilioni.

Kidata alisema sababu za ongezeko la makusanyo hayo ni kuziba mianya ya
upotevu wa mapato na kuweka mifumo mizuri ya ufuatiliaji.

Katika hatua nyingine, Kidata alisema jumla ya Sh11.8 bilioni
zimekusanywa kutoka kwa wafanyabiashara walioondosha makontena katika
Bandari Kavu kinyume na taratibu za forodha.

Alisema kuwa makusanyo hayo yanajumuisha Sh5.3 bilioni kutoka kwa
kampuni na wafanyabiashara 19 ambao wamemaliza kulipa kodi za makonteza
yao na wengine 19 ambao wamelipa sehemu ya kodi wanayodaiwa.

*Yafafanua madai ya Bakwata*

Wakati huohuo; TRA imefafanua madai ya kuwapo upendeleo katika kutoa
masharti ya ufuatiliaji wa misamaha ya kodi kwa taasisi zisizo za
kiserikali na mashirika ya dini, ikisema unafanywa kwa kufuata taratibu
na sheria.

Tamko la Kidata kwa vyombo vya habari limekuja kufuatia kauli
iliyotolewa hivi karibuni na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata),
kuwa kumekuwapo na sintofahamu katika agizo la TRA lililowataka kupeleka
taarifa kuhusu magari yaliyosamehewa kodi na matumizi yake ndani ya siku
saba, likihoji iwapo agizo hilo lilitolewa pia kwa taasisi nyingine.

Kidata alisema Sheria ya Mamlaka ya Mapato Tanzania inaipa mamlaka hiyo
kusimamia, kukagua na kuhakiki mapato ya Serikali na kuzuia aina yoyote
ya ukwepaji wa kodi kwa maendeleo ya Taifa.

“Mamlaka inayo dhamana ya kusimamia kusiwepo na matumizi mabaya ya
misamaha ya kodi ambayo hutolewa kwa mujibu wa sheria kifungu cha 5 (3)
cha TRA,” alisema Kidata. Alisema TRA haina upendeleo na haibagui wala
kulenga taasisi moja ya kidini.

Katika taarifa hiyo Kidata alisema kwa kipindi cha Oktoba hadi Desemba
2015, TRA iliwaandikia barua walipakodi 65 na katika wahusika hao kuna
taasisi na mashirika ya dini ni 39.

Kidata alisema ukaguzi huo husaidia TRA kupata taarifa muhimu ili
kuishauri Serikali namna bora ya kutoa misamaha kwa manufaa ya Taifa.

Serikali yawasaka wanaoishi nchini kinyume cha sheria

                     Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Yussuf Masauni akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam jana.

Wizara ya Mambo ya Ndani imeanza operesheni ya kuwasaka
raia wa kigeni wanaoishi na kufanya kazi nchini kinyume cha sheria ili
warudishwe makwao.

Operesheni hiyo imeanza ikiwa zimepita siku chache tangu Naibu Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu
wenye Ulemavu, Anthony Mavunde kumuagiza kamishna wa kazi nchini kufuta
vibali vya kazi vya muda kwa wageni.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani,
Hamad Masauni alisema wameanza operesheni hiyo baada ya kubaini kuwapo
kwa raia wengi wa kigeni wanaoishi na kufanya kazi nchini kinyume cha
sheria.

“Serikali haiwezi kukaa kimya wakati vijana wanakosa ajira huku kazi
zile walizotakiwa kufanya zikifanywa na raia wa kigeni. Kibaya zaidi
kuna baadhi ya kampuni, viwanda na taasisi zilizoajiri wageni
zinawadhalilisha na kuwanyanyasa wafanyakazi wa Kitanzania, tumeanza
kuwabaini na wataondolewa,” alisema.

Masauni aliwataka maofisa Uhamiaji kuwachukulia hatua za kinidhamu wote
watakaobainika kuhusika kutoa vibali kinyume cha sheria. Aliiagiza
Uhamiaji kutoa ripoti ya kila kinachoendelea kwenye operesheni hiyo.

Aidha, alitaka operesheni hiyo isitafsiriwe kuwa Tanzania haitaki raia
wa kigeni, isipokuwa lazima sheria na kanuni zilizopo zifuatwe.

Ofisa Uhamiaji wa Mkoa wa Dar es Salaam, John Msumile aliwataka wananchi
kutoa ushirikiano wakati wa operesheni hiyo na kwamba, wanatarajia
kuwakamata wageni zaidi ya 350.

“Tumeanzia Kariakoo na tutasambaa kwenye manispaa zote za Mkoa wa Dar es
Salaam, naomba kila mmoja ashiriki kwenye operesheni hii ya kuwaondoa
raia hawa wa kigeni wanaoingia nchini kinyume cha sheria,” alisema.

Kuhusu vibali vya muda, Masauni alisema Serikali inaandaa utaratibu
mwingine wa kushughulikia wageni waliotakiwa kupewa vibali vya muda
baada ya kupata malalamiko juu ya suala hilo.

“Tumepata malalamiko kupitia balozi zetu juu ya kufutwa vibali hivi kwa
sababu vilianza kutolewa kwa kukiuka sheria, kwa kuwa vina umuhimu wake,
Serikali inaangalia namna ya kushughulikia jambo hili,” alisema.

Alisema ushughulikiaji wa suala hilo utakwenda sambamba na kuwabaini
waliokuwa wakikiuka sheria kwa kutoa vibali hivyo kiholela na
kuisababishia Serikali hasara.

Pia, alisema Serikali ipo kwenye mchakato wa kuanzisha mahakama ya
kijeshi ya Uhamiaji ili kukomesha vitendo vya rushwa na ukiukwaji
mwingine wa sheria unaofanywa na baadhi ya watumishi wa idara hiyo.

200,000 kukosa pa kuishi Dar sababu ya bomoabomoa

Operesheni ya bomoabomoa inayoendelea kwa waliojenga
nyumba mabondeni jijini Dar es Salaam itawaacha zaidi ya watu 200,000
wakiwa hawana makazi.

Ubomoaji huo ulioanza katikati ya Desemba mwaka jana, umezikumba nyumba
takriban 600 katika mitaa ya Hananasif na Suna, Manispaa ya Kinondoni.

Wakazi hao ni wale ambao Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira
(NEMC) limeziwekea alama ya X nyumba zao ambazo ni zaidi ya 10,000 hadi
kufikia juzi, kwa mujibu wa Ofisa Mazingira Mwandamizi wake, Arnold
Kisiraga.

Hadi jana mchana, Kisaraga alisema walikuwa wakiweka alama ya X katika
nyumba za mabondeni zilizopo eneo la Stakishari, Segerea na kwamba
wataendelea hadi Pugu, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Idadi hiyo imefikiwa kwa kuzingatia takwimu za Sensa ya Watu na Makazi
ya mwaka 2012 ambayo inabainisha kuwa kila kaya jijini hapa inakadiriwa
kuwa na wastani wa watu wanne chini kidogo ya wastani wa Tanzania Bara
wa watu watano (4.7) kwa kaya.

Mkurugenzi wa Sensa za Watu na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo
alisema kwa sasa wana takwimu za kaya pekee ambazo sehemu kubwa ya watu
wake wamepanga.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Suna, Salim Hamis alisema katika mtaa
wake kuna nyumba zaidi ya 900 ambazo kila moja inaweza kuwa na kaya kati
ya tano hadi saba.

“Wapangaji ni wengi katika nyumba hizi usione nyingi ni ndogo. Wengi
wana hali ya chini ndiyo maana tumebanana hapahapa kwa kuwa hakuna namna
tena,” alisema Hamis.

Kisiraga alisema makadirio ya awali ya nyumba 8,000 yalijikita kwa
kuangalia zinazotambuliwa na Wizara ya Ardhi na manispaa lakini
wamebaini “vijumba vidogo” vinavyoonekana kama vimeungana na nyumba
kubwa za jirani kumbe vinajitegemea. Sehemu kubwa ya nyumba hizo zipo
Kinondoni. Alisema kadri wanavyozidi kupita mabondeni kuweka alama ya X
ndivyo idadi ya nyumba zilizojengwa maeneo hatarishi zinavyoongezeka.

“Hii inatokana na mito kuendelea kupanuka kutokana kingo zake kuharibiwa
na wachimba mchanga na kufanya nyumba za jirani kuingia kwenye mita 60
zinazokatazwa kisheria. Kuna baadhi ya nyumba zilikuwa maeneo salama
miaka 10 iliyopita lakini kwa sababu mto umesogea kwao basi watabomolewa
kwa kuwa wapo maeneo hatarishi,” alisema Kisiraga.

Kuhusu hatua hiyo, mmoja wa wakazi walioathirika, George Mkondoa
alisema: “Bado tupotupo tu hapa hatuna pa kwenda. Baadhi ya vitu
nimejaribu kuvipeleka nyumbani Bagamoyo lakini vimebaki nusu. Hivyo
ilinibidi nijenge kibanda kidogo kwa muda tuishi na familia yangu.”

Chiku Salim aliyekuwa na nyumba ya vyumba viwili aliyoibomoa mwenyewe,
alisema  hana pa kwenda kujenga licha ya kuokoa mabati na vifaa vingine
katika nyumba yake.

Mmoja wa wapangaji, Steven Herman alisema: “Ubomoaji ulikuja ghafla na
wengi unakuta walikuwa wamebakiza miezi mitatu au minne kodi zao ziishe
hivyo kuhamishwa ghafla kumeleta mtihani wa kupata nyumba haraka ndiyo
maana unakuta tunahaha hapa.” Alisema shida hizo zingeepukika iwapo
wangekuwa na elimu ya kutosha kuhusu matumizi ya ardhi na mipango miji.

Mkurugenzi wa kampuni ya maendeleo ya ardhi na makazi ya Space &
Development, Renny Chiwa alisema:

“Ili kuwaokoa wananchi hao, ni lazima kuweka mazingira rafiki ya ukuaji
wa sekta binafsi katika maendeleo na makazi. Kampuni zikipata mikopo ya
nyumba kwa riba na masharti nafuu ushindani utakua na zitajenga
maghorofa ambayo vyumba vyake vinaweza kupangishwa kati ya Sh30,000 hadi
100,000 kwa mwezi.”

Mtafiti wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Patience Mlowe alisema
wananchi walifanya makosa kuvamia maeneo hayo kinyume na sheria na
Serikali ilikosea kwa kuwaacha waendeleze makazi kwa kuwasogezea huduma
za Serikali za Mitaa, maji na umeme hivyo kuwapa uhakika wa maisha ya
kudumu na kushauri utengenezwe mpango maalumu wa kuwasaidia.

“Hakuna Mtanzania anayeunga mkono wananchi hawa waendelee kukaa maeneo
hatarishi ya mabondeni. Ila kinachoendelea sasa kinawaathiri
kisaikolojia, kinawaumiza. Wale ni Watanzania, Serikali lazima iwasaidie
tu. Watafutiwe makazi mbadala kwa muda wanapojipanga kusimama tena,”
alisema Mlowe.

Alisema ubomoaji huo, unaowaacha wananchi hao kama wakimbizi katika nchi
yao, unavunja haki za binadamu na unalitia doa Taifa kimataifa.

“Hatujui mpaka sasa mpango wa Serikali juu ya watoto wadogo waliobaki
bila makazi na ambao wanasubiri kwenda shule baada kuanza kufunguliwa,”
alisema.


Fatma Karume amshauri Dk Shein akae pembeni

Mwanasheria wa kujitegemea nchini, Fatma Karume
amemshauri Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein kuachia madaraka.

“Dk Shein lazima aondoke kwa sababu kuendelea kubaki madarakani ni
kuwanyang’anya Wazanzibari haki yao ya msingi,” alisema Fatma ambaye ni
mtoto wa aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na mwandishi wa habari hizi ofisini
kwake jijini Dar es Salaam jana, Fatma alisema kuwa mzozo wa Zanzibar
umesababishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha
Salum Jecha kutangaza kufutwa matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu visiwani
humo wakati hana mamlaka kisheria kufanya hivyo.

Fatma alisema Jecha hana mamlaka kikatiba na kisheria kufuta matokeo
hayo kwa kuwa maamuzi kama hayo yanatakiwa kufanywa na ZEC yenye
mwenyekiti, makamu mwenyekiti na wajumbe watano; watatu kutoka CCM na
wengine wawili kutoka CUF.

“Akidi ya vikao vya ZEC ni mwenyekiti na wajumbe wanne. Kama kikao
kilifanyika, akidi ilitimia na jambo hilo likakubaliwa na tume hiyo,
basi waonyeshe ni wapi walipokubali wajumbe wengine. Hata makamu
mwenyekiti hajashiriki kwenye maamuzi hayo kwa sababu kisheria uchaguzi
hauwezi kufutwa bila kupata akidi hiyo,” alifafanua Fatma.

Mwanasheria huyo alisema kuwa amekuwa akiwasikia baadhi ya wana CCM
Zanzibar wakisema kuwa Jecha ndiyo tume na tume ndiyo Jecha, hivyo ana
haki ya kufuta uchaguzi. Lakini Fatma alisema Jecha hana mamlaka kusema
jambo ambalo halijakubaliwa na tume.

Alipoulizwa ikiwa hatua ya aliyekuwa mgombea urais kupitia CUF, Seif
Sharrif Hamad ya kutangaza matokeo aliyodai yalimpa ushindi si kosa,
Fatma alisema, “Sikumuona Maalim Seif alipokuwa anatangaza matokeo hayo
hivyo sijui kama alijitangaza kuwa mshindi au alitangaza matokeo kama
yalivyobandikwa kwenye vituo.

“Katika nchi zilizokomaa kidemokrasia mgombea anaweza kuona mwelekeo wa
matokeo na akampigia mwenzake kumpongeza. Nadhani Maalim Seif alisoma
jumla ya matokeo ya uchaguzi kama yalivyobandikwa kwenye vituo, hivyo
hilo si kosa ati,” alisema na kuongeza: “Ninasikitishwa na tabia hii.
Sikutegemea kama CCM watatumia nguvu kutaka kubaki madarakani kwa njia
hii. Sikutegemea kama watavuruga katiba…ndiyo maana nina huzuni.”

Jambo jingine alilosema litazua mgogoro Zanzibar ni mamlaka yenye haki
ya kuidhinisha fedha za uchaguzi wa marudio ikiwa watalazimisha ufanyike.

“Kisheria fedha hizo ni lazima zikubaliwe na Baraza la Wawakilishi.
Baraza lipo wapi? Ili mtu awe waziri lazima awe mjumbe wa Baraza la
Wawakilishi. Rais alivunja Baraza Agosti na kwa hiyo hadi ilipofika siku
ya kuapishwa rais mpya, Zanzibar hakuna Baraza wala Waziri. Ina maana
fedha za wananchi zinatumiwa bila idhini ya Baraza, ” alisema.

Alisema kinachofanyika Zanzibar ni ‘ukoloni’ wa watu weusi dhidi ya watu
weusi ambao unawakosesha Wazanzibari haki yao msingi ya kumchagua
kiongozi wanayemtaka.

“Hali si shwari Zanzibar. Watu wamekata tamaa kwa sababu unapokuwa na
Serikali ambayo inanyang’anya haki ya wananchi ya kupiga kura,
kuandamana, watu wanakosa imani na Serikali hiyo,” alisema.

Kurudia uchaguzi

Kuhusu kurudiwa uchaguzi nchi nzima, Fatma alisema ulipofanyika uchaguzi
mwaka 2000 ambao Amani Karume aligombea kwa mara ya kwanza, zilitokea
dosari katika majimbo 10 ya Unguja. CUF walipotaka uchaguzi urudiwe nchi
nzima, CCM chini ya Benjamin Mkapa waligoma wakasema ni katika majimbo
yenye dosari tu.

“Nini kimetokea mwaka huu? Kama dosari zilijitokeza Pemba kama
wanavyodai kwa nini urudiwe Unguja? Kwa nini hawataki kutumia uamuzi wa
mwaka 2000 wa kurudia maeneo yenye dosari tu?” alihoji.

“Mkapa alisema wazi kwenye kipindi cha Hard Talk cha BBC akihojiwa na
mtangazaji Tim Sebastian uchaguzi hauwezi kufutwa ila utarudiwa tu
katika baadhi ya majimbo. Kwa nini leo mambo yamebadilika na CCM inataka
uchaguzi mpya?” alihoji.

Fatma ambaye alikataa kueleza msimamo wake kisiasa, alisema iwapo
uchaguzi huru na wa haki utafanyika leo Zanzibar, CCM haiwezi kushinda
kwa sababu Wazanzibari wanajionea yale ambayo wanafanyiwa na chama hicho.

“CCM imeshindwa Zanzibar kwa sababu ilishindwa kuwashawishi watu wake na
badala inawakemea, ikawanyima haki zao. Kisaikolojia wapiga kura
wanataka haki zao na wasibaguliwe lakini ukiwapelekea jeshi na vifaru,
unazidi kuwapoteza,” alisema.

Sherehe za Mapinduzi

Wakati zikiwa zimesalia siku nne kufikia kilele cha maadhimisho ya miaka
52 ya Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar, Fatma alisema kwa hali ilivyo
haina maana kutokana na CCM kung’ang’ania kukaa madarakani kwa nguvu.

“Ninajisikia kusalitiwa. Madhumuni ya Mapinduzi haikuwa kuiweka CCM
madarakani milele bali kurejesha madaraka kwa wananchi,” alisema.

Alisema aliambiwa kuwa waliofanya mapinduzi (wakiongozwa na Abeid Amani
Karume) walitabiri kuwa ipo siku Zanzibar itakuwa na uchaguzi au
Serikali ya Umoja wa Kitaifa lakini CCM hawataki.

“Wakati hao waliofanya mapinduzi wakisema hivyo, CCM haikuwepo,
ilikuwepo ASP. Hao ASP hawakuwa wakijiaminisha kuwa watakaa madarakani
milele,” alisema.

“Wakati tunaadhimisha mapinduzi ya Zanzibar, ni vyema Watanzania
wakafahamu kuwa malengo ya mapinduzi hayo yalikuwa ni kuondoa ubaguzi wa
aina yoyote na kuweka misingi ya kidemokrasia lakini CCM wamevuruga,”
alisema Fatma.   



UN kuichukulia hatua Korea Kaskazini

Siku moja baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio la bomu la haidrojeni, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekubaliana kuanza mikakati ya kuiwekea vikwazo.

Hata hivyo baadhi ya Wataalamu wameonyesha kuwa na wasi wasi kuhusu jaribio la sasa la nyuklia la Korea Kaskazini ambalo ni la nne katika mwongo mmoja, wakisema huenda lisiwe la haidrojeni kutokana na mlipuko uliotokea.

Bomu la hydrojeni ni moja ya mabomu hatari ya jamii atomiki au nyuklia yenye nguvu zaidi. Wataalam wanasema bomu hili la hydrojeni lina uwezo mkubwa kiasi kwamba linaweza kulipua mji mmoja wote kwa mlipuko mmoja.

Kufuatia jaribio hilo jamii ya kimataifa imendelea kulaani tukio hilo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Waziri wa zamani wa Mambo ya nje ya Korea Kusini Ban Ki moon akisema jaribio hilo la bomu la nyuklia ni hatua ya kuogopesha.

"Hili jaribio kwa mara nyingine limekiuka maazimio kadhaa ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na wito wa pamoja wa jamii ya kimataifa kukomesha vitendo hivyo. Pia linakwenda kinyume kabisa na utamaduni wa kimataifa wa majaribio ya mabomu ya nyuklia. Tendo hilo linaonekana ni la kuogopesha kwa usalama wa kanda na kupuuza juhudi za kimataifa za kuacha kutengeneza silaha za nyuklia. Ninalaani kwa nguvu jambo hilo."

Huko Marekani nayo Ikulu ya White house imesema utafiti wake wa awali kuhusu jaribio hilo la bomu nyuklia la Korea ya Kaskazini hauthibitishi madai kwamba nchi hiyo imefanikiwa kulipua bomu la haidrojeni.

Msemaji wa White house Josh Earnest amesema Korea ya Kaskazini inafaa kutengwa zaidi kama itaendelea na matendo yake ya ukiukaji wa makubaliano ya kimataifa kuhusu silaha za nyuklia ikiwa ni pamoja na kufanya majaribio makombora ya angani.

"Tumesikitishwa sana na matokeo ya uharibifu wa amani na utulivu baada ya matendo ya ukiukaji wa Korea Kaskazini kuzidi kuongezeka. China na Urusi nao pia wamesikitishwa. Ndio maana tunafanya bidii kuiweka pamoja jamii ya kimataifa na kuweka wazi kwa Korea Kaskazini kwamba njia ni moja tu iliyobaki ambayo ni nzuri kwa raia wa Korea Kaskazini, ambayo itakuwa nzuri kwa uchumi wa Korea kaskazini, nzuri kw

a nchi Korea Kaskazini kwa maana ya uwezo wao wa kujihusisha na jamii ya kimataifa."
 

Tuesday, January 5, 2016

Korea Kaskazini yafanya jaribio la bomu

Korea Kaskazini inasema kwa mara ya kwanza imefanikiwa kufanya majaribio ya bomu la nguvu ya maji{hydrogen}.
Tangazo hili limetolewa na runinga ya taifa baada ya kusikika mitetemeko ya kipimo cha tano nukta moja, karibu na eneo kuliko na kinu cha nyukilia. Wataalamu wa Marekani wanafanya uchunguzi ikiwa yalikua majaribio ya bomu hiyo au ilikua zana nyingine ya nyuklia isiyokuwa na nguvu.
Mwandishi wa BBC anasema bomu la nguvu ya maji lina uwezo mkubwa wa mulipuko ikilinganishwa na mabomu mengine yenye madini ya Plutonia ambayo Korea kaskazini imefanya majaribio katika miaka ya awali.
Mamkala za Pyongyang zimefanyia majaribio mengine matatu ya kinyukilia katika eneo kulikofanywa majaribio ya sasa kwa kipindi cha miaka kumi.

Mbunge ashtakiwa kumtusi mke wa Mugabe

Mbunge mmoja wa chama tawala nchini Zimbabwe anatarajiwa kufikishwa kortini kujibu mashtaka ya kumtusi mke wa Rais Robert Mugabe, Grace Mugabe.
Mbunge huyo Bw Justice Wadyajena anadaiwa kutumia “lugha ya matusi” dhidi ya mwanachama mwenzake wa chama tawala cha Zanu-PF aliyekuwa ameweka picha ya Bi Mugabe kwenye gari lake.
Kisa hicho kinatazamwa na wengi kama sehemu ya vizozo ya ndani ya chama kuhusu nani atamrithi Rais Robert Mugabe ambaye atatimiza umri wa miaka wa miaka 92 Februari.
Bw Wadyajena amenukuliwa kwenye nyaraka za mahakama kwamba alimwambia Jimayi Muduvuri: "Wewe ni mjinga sana, sawa na mama huyu wenu.” Atafikishwa kortini Victoria Falls.
Mke wa rais nchini Zimbabwe huitwa "amai", maana yake mama, na wafuasi wa chama cha Zanu-PF.
Mbunge huyo amekanusha madai hayo.

Wanawake 90 wabakwa Ujerumani mwaka mpya

Chansela wa Ujerumani, Angela Merkel, ameshtushwa na madai kwamba wanawake wapatao 90 walinyanyaswa kingono wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa 2016 mjini Cologne.
Polisi pamoja na mashuhuda wa matukio hayo wameelezea mashambulio hayo ya kingono kuwa yalitekelezwa karibu na eneo maarufu la Cathedral, ambalo lilikuwa limefurika idadi kubwa ya makundi ya wanaume wenye asili na muonekano wa Kiarabu ama Afrika Kaskazini.
Merkel ametoa agizo la kufanyika uchunguzi wa kubainiukweli kuhusiana na madai hayo na kisha kuwaadhibu wahusika, bila kujali asili yao ama historia za awali.
Meya wa mji wa Cologne, Henriette Reker, ameonya juu ya hatua zitakazochukuliwa akisa haki inafaa kutendeka bila ya kuwaelemea wakimbizi walioingia nchini Ujerumani.
Ameitisha mazungumzo ya dharura na maafisa wa polisi kuhusiana na mgogoro huo.
Polisi wameahidi kuimarisha ulinzi.

Obama aweka mikakati ya silaha Marekani

Katika hotuba yake iliyojaa kila aina ya hisia kali, Rais Obama amebainisha wazi mipango yake juu ya kuweka mikakati thabiti ya udhibiti silaha za moto, akisema kwamba Marekani haipaswi kukubali mauaji kama gharama ya uhuru.

Obama amesema kwamba hatua madhubuti zinapaswa kuchukuliwa ambazo zitajumuisha ufuatiliaji wa tangu awali wa upatikanaji silaha, pia uchunguzi wa afya ya akili utazingatiwa na hii ni pamoja na kumbukumbu za uhalifu wa mtuhumiwa zitahusishwa pia.

Pamoja na machozi yaliyokuwa yanashuka njia mbili juu ya mashavu ya Rais Barack Obama, amesema suala la upatikanaji wa silaha lilikuwa limeliteka nyara bunge la Congress, lakini suala hilo halitaiteka nyara Marekani yote wakati huu ambapo uhalifu wa silaha umeua wamarekani wengi mno ukilinganisha na ajali za barabarani.

Rais Obama anatarajiwa kuweka hadharani hatua zitakazochukuliwa dhidi ya matumizi mabaya ya silaha na hasa ikizingatiwa hii ni miaka ya upinzani mkali katika serikali yake.

Lakini chama cha wauza silaha nchini Marekani kilichoundwa mnamo mwaka 1871, chenye kufuatilia matumizi salama ya silaha na usalama wa silaha nchini Marekani na pia hutetea haki ya kuwa na silaha ama kuibeba wamekosoa hotuba ya Rais na kusema kwamba mapendekezo yake hayatazuia mauaji ya halaiki kutokana na aliyoyasema katika hotuba yake.

Kuwait yamuondoa balozi wake Iran

Kuwait imetangaza kwamba inamuondoa balozi wake kutoka Iran huku mvutano kuhusu kuuawa kwa mhubiri wa Saudi Arabia nchini Saudi Arabia ukizidi.
Ubalozi wa Saudi Arabia nchini Tehran ulivamiwa na kuchomwa moto na waandamanaji waliokuwa wakilalamikia kuuawa kwa mhubiri wa madhehebu ya Shia Sheikh Nimr al-Nimr na watu wengine 46 nchini Saudia Jumamosi.
Saudi Arabia ilivunja uhusiano na Iran baada ya tukio hilo, na washirika wake wa karibu Bahrain na Sudan wakafuata.
Marekani, UN na Uturuki ni miongoni mwa nchi zilizohimiza kuwepo kwa utulivu Mashariki ya Kati.
Saudi Arabia na Iran ndizo nchi kuu za Kisuni na Kishia mtawalia eneo la Mashariki ya Kati na zimekuwa wapinzani wakuu.
Nchi hizo huunga mkono pande pinzani katika mizozo Syria na Yemen

Obama kutangaza kudhibiti silaha Marekani

Rais Obama anatarajiwa kutangaza mpango wa kuhakiki silaha katika masoko ya sihala hii leo wakati atakapotangaza mpango huo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukutana na Mwanasheria Mkuu wa nchi hiyo amesema anataka kutumia mamlaka yake ya urais kwa sababu bunge la congress limeshindwa kushughulikia tatizo hilo.

" Habari njema ni kwamba sio tu ni mapendekezo yaliyo ndani ya mamlaka yangu ya kisheria kama rais lakini pia nina matumaini ni jambo llililopokelewa na wamerekani wengi wakiwemo wamiliki wa silaha, wanaounga mkono na wanaoamini. Kwa hiyo katika siku chache zijazo tutatekekeleza mpango huu, tutahakiksha watu wanaelewa tutakavyofanya mabadiliko haya na tutakavyotekeleza."

Rais Obama ametoa angalizo kuwa mpango usitarajiwe kuondoa silaha zote mikononi mwa wahalifu

" Japo ni lazima tuwe wazi kwamba hatua hii haitaondoa tatizo la makosa ya jinai katika nchi hii, wala haitaweza kuzuia mauaji ya watu wengi, wala hautaweza kuondoa kila silaha mikononi mwa wahalifu, kubwa utaokoa kwa kiasi kikubwa maisha ya watu katika nchi hii na kupungunza maumivu ya familia kuondokewa na wapendewa wao kulikosababishwa tna silaha zilizokuwa mikononi mwa watu wasio sahihi."

UN yashutumu kuvamiwa kwa ubalozi Iran

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshutumu vikali kushambuliwa kwa ubalozi wa Saudi Arabia nchini Iran na waandamanaji waliokasirishwa na kuuawa kwa mhubiri wa Kishia.

Taarifa ya baraza hilo haijazungumzia kutekelezwa kwa hukumu ya kifo dhidi ya mhubiri huyo maarufu, Sheikh Nimr al-Nimr.

Saudi Arabia ilivunja uhusiano wa kidiplomasia na Iran Jumapili baada ya ubalozi wake kuvamiwa na kuchomwa moto.

Jumatatu, naibu waziri mkuu wa Uturuki Numan Kurtulmus alihimiza nchi hizo mbili kutuliza mgogoro huo, ikisema eneo la Mashariki ya Kati tayari limo hatarini ya kulipuka.

Baraza la Usalama la UN, likijibu barua kutoka kwa Saudi Arabia, limeshutumu shambulio hilo la katika ubalozi Tehran pamoja na shambulio katika afisi ya ubalozi wa Saudia Arabia katika jiji jingine la Iran la Mashhad.

Baraza hilo limeitaka Iran kulinda mabalozi na mali ya ubalozi pamoja na wafanyakazi wake “kwa mujibu wa makubaliano ya kimataifa”.

Limetoa wito kwa pande zote mbili “kushauriana na kuchukua hatua za kupunguza wasiwasi katika kanda hiyo

Monday, January 4, 2016

Japan yataka mazungumzo ya amani na Urusi

Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe ameitisha mazungumzo ya amani kati yake na Rais wa Urusi Vladimir Putin kujadili mkataba wa Amani kati ya nchi hizo mbili.
Mataifa hayo mawili hayakutia saini mkataba wa amani baada ya kumalizika kwa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia kutokana na mzozo kuhusu umiliki wa visiwa vinne.
Bw Abe ameambia wanahabari kwamba viongozi wote wawili wanakubaliana kwamba ni jambo la kushangaza kuwa mkataba huo haujatiwa saini kwa miaka 70.
Tangu achukue uongozi 2012 Bw Abe amekuwa akijaribu kuimarisha uhusiano kati ya Tokyo na Moscow.
Muungano wa Usovieti uliteka visiwa kadha ambavyo Japan huviita Northern Territories mwaka 1945. Urusi huviita Southern Kurils.
Viongozi hao wawili walijadili suala hilo mara ya mwisho 2013.
Nchi hizo mbili zilirejesha uhusiano wa kidiplomasia mwaka 1956.
"Bila mkutano mkuu, tatizo la visiwa vya Northern Territories haliwezi likatatuliwa,'' alisema, alipokuwa akihutubia wanahabari kikao cha Mwaka Mpya.
Aliongeza kwamba ataendelea kuzungumza na Bw Putin “kila fursa inapotokea”