MICHAKATO

Levis Rocky Ndekeno

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Pages

Sunday, May 21, 2017

Makala: Safari ya Nisher kwenye game

 Mwaka 2012 akiwa kama director mchanga anayechipukia kwenye game, Nisher alilazimisha macho yetu kutazama runinga ili kushuhudia video mpya ya Joh Makini ‘Sijutii’ ambayo aliifanya yeye. Maswali yakawa ni mengi juu ya ubora wa video ile, ila maswali mengi zaidi yalitaka kujua juu ya aliyetengeneza video huyo. Ndipo jina la Nisher lilipochomoza na watu kuelewa jamaa ni wa Arusha na kazi zake anazifanyika huko huko A Town.
Baada ya majibu hayo haikuwa ajabu kuona baadhi wasanii wakifunga safari kutoka Dar es Salaam hadi Arusha kufanya video na Nisher. Kama unabisha hilo kamuulize Ben Pol alipoifanyia video ya wimbo wake wa Jikubali.
Siku zilivyozidi kuenda jina lake likazidi kukua, yaani ilikuwa ni kazi juu ya kazi kama Darassa anavyoeleza katika wimbo wake wa Muziki. Hii ilikuwa ni zaidi ya ‘Bampa to Bampa’. Jamani twendeni taratibu.
Unakumbuka video kama Nje ya Box ya Weusi, Mama Yeyoo ya G Nako, Xo ya Joh Makini, Unanichora ya Ben Pol, Kijukuu ya Young Dee, 13 ya Young Killer, Bongo Hip Hop ya Fid Q, Press Play ya Dj Choka, Dole ya Mabeste na nyinginezo kiba? Zote zilitoka kwake.
                                        Nisher aliposhinda tuzo, ‘Tuzo za Watu’
Ukali wa video hizo bado hautoshi kuelezea uwezo wake kwenye game ulikuwa wa kiwango gani. Chukua na hii; Mwaka 2014 alishinda award ‘Tuzo za Watu’ akiwa kama Muongozaji wa video anayependwa. Hivyo ndivyo tunaweza kumzungumzia Nisher kwa ufupi
Kwa nini leo Nisher

Imenilazimu kumkumbuka Nisher kwa sasa. Narudia tena, imenilazimu kufanya hivyo kwa sababu kuu mbili. Mosi: Wiki hii makali wa Hip Hop, Joh Makini alikaririwa akisema kuwa ataendelea kushoot video za ngoma zake nje ya nchi kutokana na kufuata ubora huku akiwataka madirector wa ndani kubadilika.
                                                                           Nisher kazini
Kauli hii inaonyesha kuwa industry ya video Bongo bado ipo nchini na itachukua muda kukua kwa sababu wasanii wote walio mainstream wanakimbilia kushoot video nje.
Sababu ya pili kumkumbuka Nisher ni kwamba tangu mwaka huu kuanza ametoa video moja tu ambayo ni ya Edu Boy ‘Naiee’ aliyompa shavu Bill Nas. Uzuri ni kwamba bado ubora na ubunifu wa kazi zake uko pala pale, kama umefanikiwa kuitazama video hii ya Edu Boy utakubaliana na mimi kwa asilimia kubwa, pongezi za kutosha kwake Nisher.
Tuanzie hapa
Wakati Nisher anakaribia nusu mwaka akiwa na video moja mkononi, aliyekuwa mshindani wake mkubwa, Hanscana ameshatoa video 13 tangu kuanza mwaka huu.
Hanscana ameshatoa video kama Phone ya Ben Pol, Ollah ya Christiana Bella, Up In The Air ya Rose Ree, Sugar ya Mimi Mars, Kijuso ya Queen Darling, Kibabe ya Prof Jay, Shauri Yako ya Edu Kenzo, Down ya Quick Rocka, Ila ya Foby, Umenikamata ya Jux, Happy BithDay ya Harmonize, Hasara Roho ya Darassa, na Ukivaaje Utapendeza ya Dogo Janja.
Bila uoga naweza kusema Hancana kwa sasa amelishika soko la ndani, ni jambo zuri ambalo anastahili pongezi, tangu kuanza kwake hakuna alipopotea, ameendelea kushikilia mafanikio yake. Weka nukta hapo kwanza.
Nisher alifanikiwa sana kuleta ushindani mkubwa katika uongozaji wa video nchini. Kwa kipindi kifupi alichokuwepo katika game ilifika wakati watu walianza kumlinganisha na director mkongwe Adam Juma ambaye alileta mapinduzi makubwa katika utengenezaji wa video za muziki nchini.
Nisher alidumu kwenye game kwa kipindi kifupi sana lakini mchango wake mkubwa bado unaonekana. Alikuwa ni mwenye kujituma, mbunifu na mwenye vifaa vya kutosha, kiufupi si mtu wa mchezo mchezo. Leo hii yupo kimya, anajaribu kurudi kwenye game ambapo mapambano yamepamba moto.
Amekuwa akijaribu kurudi lakini amekuwa akikwamishwa na baadhi ya mambo. Huenda ‘ugonjwa’ unaomkwamisha Nisher kurejea ni kama ule unaokumbana nao Alikiba anapopamba kuirejesha nafasi yake katika Bongo Fleva (ufalme).
Nisher kuna kipindi alipumzika kufanya kazi kwa kuchukua mapumziko nje ya nchi, na pia alibainisha kuwa alifanya hivyo ili kupata muda wa kuwa karibu na mchumba wake. Unajua alipotaka kurudi nini alikumbana nacho?.
Chukua huu mfano, Alikiba alipoamua kupumzika kufanya muziki kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili, aliporejea alikuta Diamond Platnumz ameshasimamisha ufalme wake, hivyo kazi ikawa kubwa mara mbili. Mosi; kurejesha muziki wake ambao ulikuwa hujasikika kwa muda, pili; kupambana na utawala alioukuta.
Alikiba amefanikiwa kurejesha muziki wake ila itamchukua muda kuondoa utawala ambao ameukuta, utawala ambao kipindi anaamua kupumzika kufanya muziki, haukuwepo.
Hii ndio hali anayokumbana nayo Nisher anapotaka kurejea, wakina Hanscana, Khalfan na wengineo wameshasimika utawala wao, hivyo kazi ya kurejea ni kubwa si kitoto.
Twende mbele turudi nyuma, vyote vyote itakavyokuwa bado mchango wake unahitajika katika game, lakini kama ni hivyo mbona hapati nafasi?. Sababu ni hizi
Biashara na Weusi kuanguka
Katika wimbo ya Nako 2 Nako Soldiers ‘Hawatuwezi’ ambao wamefanya Lord Eyes, Ibra Da Hustler na Enika, kuna mstari Lord Eyes anaseme ‘Yule aliyetupandisha ndiye atakayetushusha’.
Kama nilivyotangulia kueleza kuwa tulianza kumfahamu Nisher kupitia Joh Makini, pia umaarufu wake kwa asilimia fulani ulichochewa na video alizokuwa anafanya na Weusi.
Weusi walipoanza kwenda kufanya video nje ya nchi, biashara na Nisher kwa kiasi fulani ilishuka, kitu kilichoanza kuondoa ushawishi wa kikazi aliokuwa nao kwenye game.
                                    Nisher alipokuwa akishoot video ya Joh Makini ‘XO’
Kilichoashiria anguko kubwa la kibiashara kati yao ni utata uliojitokeza katika video ya Arosto ambayo mwanzoni aliifanya Nisher lakini baadae G Nako akaja kutoa ya pili ambayo aliifanya kwa Hanscana.
Tunaweza kusema Weusi wamekinai huduma kutoka kwa Nisher, kama nitakuwa nimekosea nafasi ya kurekebisha ipo wazi. Kwa mujibu wa Nisher video ya Arosto pamoja na nyingine tatu ndizo zilikuwa katika mipango yake ya kumrejesha katika game.  Lakini hilo halikufanikiwa kitu ambacho naamini kimemnyima hata nguvu ya kuendelea kwa kasi aliyokuwa nayo mwanzo.
Kabla ya ujio huu wa sasa niliwahi kufikiri kuwa Nisher ameamua kuachana na utengenezaji wa video za Bongo Fleva baada ya kuona vipande vya movie yake aliyoipa jina la Alex katika mtandao, lakini sivyo bado jamaa anaiona nafasi yake katika game.
Maneno nje ya kazi
Hii huenda ikawa sababu ya pili kupotea kwa Nisher na itakayo kwamisha kufana kwa ujio wake. Sote tunafahamu tabia yake si mtu wa kuficha hisia zake, kama kitu anakijua atakuambia anakijua, kama kitu anacho atakuambia anacho wala hatokudanganya.
Falsafa zake ni kama za Rais John Magufuli, kama kitu ni cheupe atakueleza uhalisia wake, hawezi kukuambia ni rangi ya maziwa. Ndivyo alivyokuwa Nisher na watu wenye tabia hii mara nyingi ni watu wachache wanaoweza kuwaelewa. Kama unabisha, fuatilia changamoto anazokumbana nazo Rais wa Marekani kwa sasa, Donald Trump.
Nisher alikuwa haoni haya kukueleza kiasi cha fedha ulichonacho sitoweza kufanya kazi yako kwa sababu familia yake inajimudu kiuchumi. Jambo hili lilifanya watu wengi kuamini kuwa jamaa anaringa.  Kiufupi Nisher ni mtu wa kunyoosha maneno na ndio maana hakuogopa kutamka hadharani kuwa G Nako amemuingizia hasara ya sh. milioni tatu kwenye video ya Arosto.
Kuna kipindi prodyuza Samtimber wa Arusha alilalamika kuwa Nisher anamletea dharau katika kazi. Samtimber alienda mbali zaidi kwa kudai Nisher alikataa kufanya video ya wasanii waliorekodi studio kwake kwa madai audio ni mbuvu.
Unakumbuka kipindi walikuwa wanavutana na B.O.B micharazo kuhusu masuala ya kazi, stori za chini ya kapeti zikadai kuwa jamaa alikataa kufanya video ya kundi hilo la Hip Hop ili kulinda utawala wa Weusi katika game kwa kutoa video kali. Kiufupi hayo ndio yalikuwa maisha ya Nisher kwenye game.
Purukushani kama hizi na zile nilizotangulia kuzieleza huenda zilichangia kumpoteza Nisher kwenye game. Sasa sijaelewa hapa anayepaswa kulaumiwa ni Nisher mwenyewe au ni watu wa karibu aliokuwa anafanya nao kazi.
Endapo akifanikiwa kuruka vizingiti hivi viwili nina amini Nisher atarejeza vizuri zaidi na kulishika soko upya kama ilivyokuwa hapo awali
Anachopaswa kufanya Nisher
Binafsi bado nimaamini katika uwezo wa Nisher na nafasi yake katika game ipo pale pale, ni kitendo cha yeye kujipanga upya na kutafuta nafasi ya kufanya kazi na wasanii ambao wapo mainstream kwa sasa kama alivyoanza.
Licha ya kuwa wasanii wa aina kwa sasa wanakimbilia nje kufanya video lakini bado kuna uwezekano wa hata yeye kuongozana nao kwenda huku huku kufanya kazi. Bila hivyo ni vigumu kurejea kwa kasi ile.
Hanscana alisafiri hadi Kenya na Christian Bella kufanya video ya Ollah, hii ikiwa ni ishara kuwa jamaa anahitaji kukua zaidi. Unaweza kudharau hatua hiyo lakini kipindi cha nyuma wasanii wengi wa Bongo Fleva walikuwa wanakimbilia Kenya kufanya video na Ogopa DJs.
Ommy Dimpoz, Rich Mavoko, Madee, Chenge na Temba kwa nyakati tofauti walisafiri na Adam Juma hadi Afrika Kusini kufanya video, utamaduni huu ingeendelezwa ungesaidia madirector wetu kuwepo kwenye game kwa kipindi kirefu na kujulikana mbali zaidi.
Nisher akitaka kurejea atafute nafasi ya kuenda kufanya video nje ya nchi, kazi za ndani asizipe nafasi sana, endapo akifanikiwa nje ni rahisi kuliteka soko la ndani upya.