MICHAKATO

Levis Rocky Ndekeno

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Pages

Tuesday, January 5, 2016

Korea Kaskazini yafanya jaribio la bomu

Korea Kaskazini inasema kwa mara ya kwanza imefanikiwa kufanya majaribio ya bomu la nguvu ya maji{hydrogen}.
Tangazo hili limetolewa na runinga ya taifa baada ya kusikika mitetemeko ya kipimo cha tano nukta moja, karibu na eneo kuliko na kinu cha nyukilia. Wataalamu wa Marekani wanafanya uchunguzi ikiwa yalikua majaribio ya bomu hiyo au ilikua zana nyingine ya nyuklia isiyokuwa na nguvu.
Mwandishi wa BBC anasema bomu la nguvu ya maji lina uwezo mkubwa wa mulipuko ikilinganishwa na mabomu mengine yenye madini ya Plutonia ambayo Korea kaskazini imefanya majaribio katika miaka ya awali.
Mamkala za Pyongyang zimefanyia majaribio mengine matatu ya kinyukilia katika eneo kulikofanywa majaribio ya sasa kwa kipindi cha miaka kumi.

Mbunge ashtakiwa kumtusi mke wa Mugabe

Mbunge mmoja wa chama tawala nchini Zimbabwe anatarajiwa kufikishwa kortini kujibu mashtaka ya kumtusi mke wa Rais Robert Mugabe, Grace Mugabe.
Mbunge huyo Bw Justice Wadyajena anadaiwa kutumia “lugha ya matusi” dhidi ya mwanachama mwenzake wa chama tawala cha Zanu-PF aliyekuwa ameweka picha ya Bi Mugabe kwenye gari lake.
Kisa hicho kinatazamwa na wengi kama sehemu ya vizozo ya ndani ya chama kuhusu nani atamrithi Rais Robert Mugabe ambaye atatimiza umri wa miaka wa miaka 92 Februari.
Bw Wadyajena amenukuliwa kwenye nyaraka za mahakama kwamba alimwambia Jimayi Muduvuri: "Wewe ni mjinga sana, sawa na mama huyu wenu.” Atafikishwa kortini Victoria Falls.
Mke wa rais nchini Zimbabwe huitwa "amai", maana yake mama, na wafuasi wa chama cha Zanu-PF.
Mbunge huyo amekanusha madai hayo.

Wanawake 90 wabakwa Ujerumani mwaka mpya

Chansela wa Ujerumani, Angela Merkel, ameshtushwa na madai kwamba wanawake wapatao 90 walinyanyaswa kingono wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa 2016 mjini Cologne.
Polisi pamoja na mashuhuda wa matukio hayo wameelezea mashambulio hayo ya kingono kuwa yalitekelezwa karibu na eneo maarufu la Cathedral, ambalo lilikuwa limefurika idadi kubwa ya makundi ya wanaume wenye asili na muonekano wa Kiarabu ama Afrika Kaskazini.
Merkel ametoa agizo la kufanyika uchunguzi wa kubainiukweli kuhusiana na madai hayo na kisha kuwaadhibu wahusika, bila kujali asili yao ama historia za awali.
Meya wa mji wa Cologne, Henriette Reker, ameonya juu ya hatua zitakazochukuliwa akisa haki inafaa kutendeka bila ya kuwaelemea wakimbizi walioingia nchini Ujerumani.
Ameitisha mazungumzo ya dharura na maafisa wa polisi kuhusiana na mgogoro huo.
Polisi wameahidi kuimarisha ulinzi.

Obama aweka mikakati ya silaha Marekani

Katika hotuba yake iliyojaa kila aina ya hisia kali, Rais Obama amebainisha wazi mipango yake juu ya kuweka mikakati thabiti ya udhibiti silaha za moto, akisema kwamba Marekani haipaswi kukubali mauaji kama gharama ya uhuru.

Obama amesema kwamba hatua madhubuti zinapaswa kuchukuliwa ambazo zitajumuisha ufuatiliaji wa tangu awali wa upatikanaji silaha, pia uchunguzi wa afya ya akili utazingatiwa na hii ni pamoja na kumbukumbu za uhalifu wa mtuhumiwa zitahusishwa pia.

Pamoja na machozi yaliyokuwa yanashuka njia mbili juu ya mashavu ya Rais Barack Obama, amesema suala la upatikanaji wa silaha lilikuwa limeliteka nyara bunge la Congress, lakini suala hilo halitaiteka nyara Marekani yote wakati huu ambapo uhalifu wa silaha umeua wamarekani wengi mno ukilinganisha na ajali za barabarani.

Rais Obama anatarajiwa kuweka hadharani hatua zitakazochukuliwa dhidi ya matumizi mabaya ya silaha na hasa ikizingatiwa hii ni miaka ya upinzani mkali katika serikali yake.

Lakini chama cha wauza silaha nchini Marekani kilichoundwa mnamo mwaka 1871, chenye kufuatilia matumizi salama ya silaha na usalama wa silaha nchini Marekani na pia hutetea haki ya kuwa na silaha ama kuibeba wamekosoa hotuba ya Rais na kusema kwamba mapendekezo yake hayatazuia mauaji ya halaiki kutokana na aliyoyasema katika hotuba yake.

Kuwait yamuondoa balozi wake Iran

Kuwait imetangaza kwamba inamuondoa balozi wake kutoka Iran huku mvutano kuhusu kuuawa kwa mhubiri wa Saudi Arabia nchini Saudi Arabia ukizidi.
Ubalozi wa Saudi Arabia nchini Tehran ulivamiwa na kuchomwa moto na waandamanaji waliokuwa wakilalamikia kuuawa kwa mhubiri wa madhehebu ya Shia Sheikh Nimr al-Nimr na watu wengine 46 nchini Saudia Jumamosi.
Saudi Arabia ilivunja uhusiano na Iran baada ya tukio hilo, na washirika wake wa karibu Bahrain na Sudan wakafuata.
Marekani, UN na Uturuki ni miongoni mwa nchi zilizohimiza kuwepo kwa utulivu Mashariki ya Kati.
Saudi Arabia na Iran ndizo nchi kuu za Kisuni na Kishia mtawalia eneo la Mashariki ya Kati na zimekuwa wapinzani wakuu.
Nchi hizo huunga mkono pande pinzani katika mizozo Syria na Yemen

Obama kutangaza kudhibiti silaha Marekani

Rais Obama anatarajiwa kutangaza mpango wa kuhakiki silaha katika masoko ya sihala hii leo wakati atakapotangaza mpango huo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukutana na Mwanasheria Mkuu wa nchi hiyo amesema anataka kutumia mamlaka yake ya urais kwa sababu bunge la congress limeshindwa kushughulikia tatizo hilo.

" Habari njema ni kwamba sio tu ni mapendekezo yaliyo ndani ya mamlaka yangu ya kisheria kama rais lakini pia nina matumaini ni jambo llililopokelewa na wamerekani wengi wakiwemo wamiliki wa silaha, wanaounga mkono na wanaoamini. Kwa hiyo katika siku chache zijazo tutatekekeleza mpango huu, tutahakiksha watu wanaelewa tutakavyofanya mabadiliko haya na tutakavyotekeleza."

Rais Obama ametoa angalizo kuwa mpango usitarajiwe kuondoa silaha zote mikononi mwa wahalifu

" Japo ni lazima tuwe wazi kwamba hatua hii haitaondoa tatizo la makosa ya jinai katika nchi hii, wala haitaweza kuzuia mauaji ya watu wengi, wala hautaweza kuondoa kila silaha mikononi mwa wahalifu, kubwa utaokoa kwa kiasi kikubwa maisha ya watu katika nchi hii na kupungunza maumivu ya familia kuondokewa na wapendewa wao kulikosababishwa tna silaha zilizokuwa mikononi mwa watu wasio sahihi."

UN yashutumu kuvamiwa kwa ubalozi Iran

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshutumu vikali kushambuliwa kwa ubalozi wa Saudi Arabia nchini Iran na waandamanaji waliokasirishwa na kuuawa kwa mhubiri wa Kishia.

Taarifa ya baraza hilo haijazungumzia kutekelezwa kwa hukumu ya kifo dhidi ya mhubiri huyo maarufu, Sheikh Nimr al-Nimr.

Saudi Arabia ilivunja uhusiano wa kidiplomasia na Iran Jumapili baada ya ubalozi wake kuvamiwa na kuchomwa moto.

Jumatatu, naibu waziri mkuu wa Uturuki Numan Kurtulmus alihimiza nchi hizo mbili kutuliza mgogoro huo, ikisema eneo la Mashariki ya Kati tayari limo hatarini ya kulipuka.

Baraza la Usalama la UN, likijibu barua kutoka kwa Saudi Arabia, limeshutumu shambulio hilo la katika ubalozi Tehran pamoja na shambulio katika afisi ya ubalozi wa Saudia Arabia katika jiji jingine la Iran la Mashhad.

Baraza hilo limeitaka Iran kulinda mabalozi na mali ya ubalozi pamoja na wafanyakazi wake “kwa mujibu wa makubaliano ya kimataifa”.

Limetoa wito kwa pande zote mbili “kushauriana na kuchukua hatua za kupunguza wasiwasi katika kanda hiyo