MICHAKATO

Levis Rocky Ndekeno

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Pages

Sunday, January 19, 2014

Rais JK asuka upya baraza la mawaziri awaacha mawaziri sita ateua wapya

NELSON MANDELA: HISTORIA YA KUSISIMUA YA MAISHA YAKE

Rolihlahla Mandela
A.K.A: Mandela
MAJINA YA UTANI: Madiba, Black Pimpernel
MAHALI ALIKOZALIWA: Mveso, Transkei, South Africa
KAZI: Mwanaharakati, Kiongozi wa dunia
TAREHE YA KUZALIWA: Julai 18, 1918
TAREHE YA KUFA: DESEMBA 05, 2013
MAHALI ALIKOFIA: Johannesburg, South Africa
ELIMU: Taasisi ya Clarkebury, Chuo cha Wesleyan, Chuo Kikuu Kishiriki cha Fort Hare, Chuo Kikuu cha London, Chuo Kikuu cha Witwatersrand, Johannesburg.
Nelson Mandela, Mwanasiasa maarufu nchini Afrika Kusini na duniani kwa ujumla ambaye alikuwa mtu muhimu katika kuutokomeza ubaguzi wa rangi nchini mwake, ni mtoto wa Chifu wa kabila la Tembu, Chifu Henry Mandela. Mandela alizaliwa katika mji mdogo wa Transkei.
CHAMA CHA ANC
Mandela alisoma katika Chuo Kikuu cha Fort Hare na Chuo Kikuu cha Witwatersrand. Akawa mwanasheria mwaka 1942. Mwaka 1944, alijiunga na Chama cha ANC, chama kilichodhamiria kuutokomeza utawala wa makaburu weupe pekee. Mwaka 1960, Chama tawala cha makaburu kilikipiga marufuku cha cha ANC na kuwashitaki viongozi wake kwa kosa la uhaini, lakini Mandela aliachiwa huru.
KUFUNGWA GEREZANI
Akiendeleza harakati zake za kupambana na makaburu, Mandela alikamatwa, akatiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani kuanzia mwaka 1964 hadi 1990, ambapo maisha yake kama kiongozi wa harakati za kupambana na ubaguzi wa rangi yakajulikana dunia nzima. Kama mfungwa wa dhamiri, Mandela mara kwa mara alikataa kuachiwa kwa masharti.
KUACHIWA HURU
Mwaka 1990, akiwa amekaa jela kwa miaka 26 na akiwa na umri wa miaka 71, iliachiwa huru bila masharti yoyote baada ya utawala wa kibaguzi kushinikizwa na jumuiya ya kimataifa. Mwaka 1993, Nelson Mandela alishinda Tuzo ya Nobel kwa harakati zake za kisiasa.

Namna ya kumsaidia mjamzito anayetapika

HALI ya kusikia kichefuchefu na hatimaye kutapika ni tatizo ambalo huwaathiri wanawake kati ya asilimia 50 hadi 80 wanaopata ujauzito duniani kote. Hali hii inaitwa morning sickness, yaani ugonjwa wa asubuhi. Unaitwa hivyo kwa sababu mara nyingi kichefuchefu husumbua zaidi asubuhi ingawa kinaweza kutokea mchana ama muda wowote.
Kichefuchefu kinatoka na nini? Wanawake wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo hili kwa karne nyingi, lakini chanzo chake hakifahamiki vyema ingawa kumekuwepo na nadharia nyingi ambazo bado zinafanyiwa kazi.
Inadhaniwa kwamba tatizo hili husababishwa na mabadiliko ya kifizikia na kikemikali tumboni; kuongezeka kwa homoni na kuongezeka kwa hali ya mjamzito kusikia harufu mbaya.
Nadharia moja kuhusu chanzo cha tatizo hili ni ile inayoonesha kwamba linatokana na kuongezeka kwa homoni aina ya estrogen na progesterone, humfanya mwanamke kusikia harufu mbaya huku tindikali pia ikiwa imeongezeka tumboni.
Inaaminika pia kwamba hali ya uchovu na hisia nzito ama mawazo mengi ambayo mara nyingi humpata mjamzito, vinachangia pia tatizo hili. Nadharia kuhusu homoni ambazo huwa nyingi zaidi wakati wa ujauzito, ndizo zinazozungumzwa zaidi kusababisha kichefuchefu.
Homoni za Progesterone zina tabia ya kulainisha misuli ya mwili na hii hufanyika ili kupunguza maumivu ya uzazi kwa kusaidia misuli ya tumbo la uzazi kulainika. Vile vile homoni hizi huathiri pia baadhi ya misuli kama vile tumbo na utumbo mwembamba.
Homoni za progesterone hupunguza kasi ya mfumo mzima wa uyeyushaji wa chakula mwilini, hali ambayo husababisha tumbo pia lisifanye kazi ya kutoa uchafu tumboni haraka na hivyo kuongezeka kwa tindikali nyingi.
Nadharia nyingine ambayo pia hukubalika na wasomi ni kwamba tatizo la kichefuchefu husababishwa na kujirundika kwa kitu kiitwacho kwa kitaalamu, human chorionic gonadotopin (hCG) kwenye tumbo. hCG huanza kuzalishwa baada ya mwanamke kunasa mimba na huendelea kuongezeka hadi mimba inapofikisha wiki 12 ambapo kasi ya hCG huanza kupungua.
Kwa wanawake wengi ni kipindi hiki pia ambacho tatizo la kichefuchefu huanza kupungua pia. Kuna nadharia nyingine ambayo pia hutajwa na wajuzi wakisema kuwa kichefu chefu chanzo chake ni kupungua kwa sukari mwilini, hasa katika wiki za awali za ujauzito.
Pia kuna nadharia inayoonesha kwamba wanawake wenye kawaida ya kula vyakula vyenye mafuta mengi huathirika zaidi kulinganisha na wale wanaokula vyakula visivyokuwa na mafuta.
Hata hivyo, tatizo hili la ‘ugonjwa wa asubuhi’ si kitu kibaya kwani tafiti nyingi zinaonesha kwamba wanawake wengi wanaokumbwa na tatizo hili ni mara chache kuwa na matatizo ya mimba kuharibika (miscarriages).
Pia madaktari wengi wanaamini tatizo hili na dalili nzuri kwamba baada ya mwanamke kuzaa, kuta za tumbo la uzazi hujengeka vyema.
Ingawa baada ya wiki 12 tatizo hili mara nyingi huanza kupungua, lakini baadhi ya akina mama huendelea kutapika hadi siku ya kujifungua. Hali hii ikitokea mara nyingi huathiri shughuli za mama za kila siku katika maisha yake pamoja na familia yake. Kutapika kunaweza kuathiri mtoto tumboni?
Si mtoto tu, hata mama yake kama atatapika sana na kuishiwa maji na chakula mwilini, vitu ambavyo ni muhimu kwake na kwa afya ya mtoto. Katika hali kama hiyo mjamzito anaweza kupungua uzito kwa kasi, jambo ambalo halishauriwi.
Tatizo la kutapika mjamzito huchukuliwa kama la kawaida lakini kuna wakati huwa baya zaidi na huitwa kwa kitaalamu hyperemesis gravidarium (HG). Wawanake ambao hukumbwa na tatizo hili mara nyingi ni wachache, yaani kati ya asilimia 0.5 hadi mbili ya wajawazito wote.
Kama HG haitatibiwa inaweza kuhatarisha maisha ya mama na mtoto tumboni. Tatizo hili la HG hutokea pale mjamzito anaposikia kichefu kuliko kawaida na kutapika kunakozidi mipaka. Inaweza kusababisha mjamzito kuishiwa maji, kupungua uzito na kupoteza virutubisho vingi vya mwili.
Mama anapofikia hali hii inabidi amuone daktari haraka kwa uangalizi wa karibu. Dalili za HG ni pamoja na kichefuchefu kinachokithiri, kutapika kunakoendelea (zaidi ya mara 3 au 4 kwa siku), kupungukiwa na maji mwilini na kupungua kwa virutubisho vya mwili kutokana na kupungua kwa maji.
Dalili zingine ni kupunguka uzito ama kushindwa kuongezeka uzito, mapigo ya moyo kuongezeka, ngozi kuonekana kavu na kichwa kuuma, na wakati mwingine mjamzito anaweza kupata hali kama ya kuchanganyikiwa. Ili kujua kama mjamzito kapungukiwa maji la kufanya ni pamoja na kuvuta ngozi yake ambapo hurudi taratibu.
Lingine ni ngozi inaonekana ikiwa kavu, kupungukiwa machozi ama mate, ulimi kukauka, kuchanganyikiwa ama, mawazo mengi ama hasira, kupungukiwa na mkojo (kukaa muda mrefu bila kukojoa ama kukojoa mkojo ‘kiduchu’) na mkojo kuwa wa rangi ya ugoro iliyokolea.
Kama mjamzito ana dalili hizo anatakiwa kumuona daktari haraka. Kuna hatua ambazo daktari atazichukua ili kusaidia tatizo lake na inasisitizwa kwamba hali ikifikia hivyo si tatizo la kupuuzia.
Namna ya kukabiliana na kichefuchefu Hatua za awali kwa mjamzito anayesumbuliwa na kichefu chefu ni pamoja na kwamba, kwa vile katika miezi mitatu ya mwanzo hadi minne, pua zake ni rahisi kusikia harufu, inashauriwa akae katika chumba chenye hewa ya kutosha ambacho hakisababishi hakikusanyi harufu kali kama vile mapishi ama sigara. Sambamba na hilo aepuke kukaa sehemu zenye harufu mbaya na inayokera pua.
Pili, aepuke kukaa eneo lenye joto kwa sababu joto linaaminika kuongeza kichefu chefu. Anashauriwa pia apendelee kula vitu vikavu, kama bisi, tambi, kaukau za chips na ikiwezekana afanye hivyo dakika 15 kabla ya kuamka kutoka kitandani asubuhi. Kwa hiyo ahakikishe vyakula vikavu haviko mbali na kitanda chake. Nne, ale chakula kidogo kidogo kila baada ya saa mbili ama tatu.
Tumbo linapobaki wazi kwa muda mrefu linaweza kuongeza hali ya kujisikia kichefuchefu. Ale chakula chenye protini ya kutosha na wanga (siyo mafuta) kwani hivyo vyote viwili husaidia kupigana na hali ya kichefuchefu. Pia chakula kisiwe na harufu kali ama kisiwe kimekaangwa sana. Vyakula chukuchuku vinafaa zaidi.
Tano, anyanyuke taratibu na asilale haraka haraka baada ya kula chakula na pia asiache kula bila sababu na hasa kula kile anachotamani. Katika hali ya kichefuchefu anashauriwa ajaribu kula hata kama si sehemu ya chakula ulichozea kila siku. Lingine ni kunywa maji nusu saa kabla chakula na nusu saa baada ya chakula.
Kwa lugha nyingine, asinywe maji pamoja na chakula. Ahakikishe unakunywa wastani wa glasi nane za maji kwa siku ili kuepuka hali ya kupungukiwa maji mwilini.
Kama harufu inamuudhi wakati wa kupika na yeye ndiye analazimika kupika, ajaribu kupikia sehemu yenye uwazi wa kutosha, madirisha makubwa ama hata nje ya nyumba. Kama inawezekana, atafute mtu mwingine amsaidie kutayarisha chakula.
Ajaribu pia kula chakula kilichopoa badala ya cha moto. Chakula kilichopoa kina harufu kidogo kulinganisha na cha moto. Pia inashauriwa kwamba chakula wakati huu kisiwe na chumvi nyingi. Harufu ya limao ama ndimu iliyokatwa inaweza kusaidia pia kupunguza kichefu chefu.
Anaweza pia kuweka limao kidogo kwenye chai yake au hata maji. Na mwisho mjamzito anayesumbuliwa na kichefuchefu apate muda mwingi wa kupumzika.
Kuongea mambo ya mimba na akina mama wengine wenye kujua tatizo lake kunaweza pia kusaidia hali ya kupunguza mgandamizo/ mawazo mazito kichwani, kwani kama ilivyoelezwa mwanzo, nadharia moja ambayo watu wanahisi kuwa inasababisha kichefuchefu ni hali hiyo ya mawazo mengi.
Vitu au dawa za kusaidia Tangawizi ni zao la asili ambalo mara nyingi linashauriwa katika kutibu kichefuchefu na kutapika kwa mwanamke mjamzito.
Baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa tangawizi inasaidia sana kupunguza kasi ya kichefu chefu kwa wanawake wajawazito. Mgonjwa pia anaweza kutumia kidonge cha Diclectin: Dawa hii muungano wa vitamin B6 na dawa zinazozuia mzio (antihistamine) aina ya doxylamine.
Dawa hizi zimetengenezwa viwandani kwa ajili ya kuzuia kichefu chefu na kutapika. Dawa hizi zimekuwa zikitumiwa zaidi nchini Canada na wanawake wengi wamesema kwamba zinawasaidia.
Hata hivyo, baadhi ya wanawake wamedai kusikia hali ya kizunguzungu wanapotumia aina hii ya dawa. Kadhalika kuna dawa mbalimbali ambazo madaktari wanaweza kumpa mgonjwa ili kusaidia katika tatizo hili.
Kumuona daktari Mbali na kumuona daktari kutokana na kutapika sana hadi kuonesha dalili ya kuishiwa maji ama kupungua uzito, inapaswa kumuona daktari endapo tatizo la kutapika halikomi baada ya kujaribu mambo ambayo tumeyaorodhesha hapo juu.
Pili mjamzito amuone daktari kama anatapika damu ama vitu ambavyo vinafanana na mbegu za kahawa. Mgonjwa akifika hospitali, daktari anaweza kutaka kujua historia ya ugonjwa wake, hususan kuhusu ni mara ngapi kwa siku kichefuchefu hutokea na kama kinakutokea kila siku ama la.

Anaweza kutaka kujua kama mgonjwa amekuwa akisafiri safiri, utaratibu wake wa kila siku kama umevurugwa, kama kuna hali inayomletea mawazo ama kumchanganya akili, aina gani ya chakula ambayo amekuwa akiitumia na kama yeye ama mumewe anavuta sigara. Makala haya yamepatikana kutokana na mtandao wa kompyuta.

Mke wa Lubuva afariki dunia India •

MKE wa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji mstaafu Damian Lubuva amefariki akiwa nchini India alikokuwa akitibiwa ugonjwa wa kisukari. Rais Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi, Lubuva kutokana na kifo hicho cha Martha Lubuva kilichotokea Januari 17 katika Hospitali ya Apollo iliyopo New Delhi, India.
“Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa za kifo cha mke wako,” alisema Rais Kikwete kupitia taarifa iliyotolewa juzi kwa vyombo vya habari. Alisema,
“Ninawahakikishia kuwa niko pamoja nanyi katika kuomboleza msiba huu mkubwa.”Mwili wa marehemu unatarajiwa kuletwa leo, Dar es Salaam.
Wakati huo huo, Rais Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Abdulrahaman Kinana kutokana na kifo cha Kada wa chama, Deusdedith Mtambalike.
Mtambalike aliyewahi kuwa Muu wa Wilaya katika Wilaya mbalimbali nchini, alifariki dunia Januari 16 mwaka huu nchini Afrika Kusini, alikokuwa akipatiwa matibabu.
Licha ya kuwa kada hodari wa CCM, Mtambalike aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya za Ngara na Muleba Mkoani Kagera, Igunga Mkoa wa Tabora, Ludewa Mkoa wa Iringa na Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma.
“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mheshimiwa Deusdedith Makandila Mtambalike, Kada makini wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na mmoja wa Viongozi makini katika Utumishi wa Umma aliyewahi kushika wadhifa wa Mkuu wa Wilaya katika Wilaya mbalimbali hapa nchini”, alisema.

Rais Kikwete alisema alimfahamu Mtambalike, kama mmoja wa Wakuu wa Wilaya aliyekuwa makini katika kazi zake, ambaye aliutumikia wadhifa huo kwa umakini na uaminifu mkubwa. Alisema kifo chake ni pigo kwa CCM, ambako alitoa mchango wa mawazo na ushauri.

Kikwete awatolea uvivu viongozi wa riadha

RAIS Jakaya Kikwete amewataka viongozi wa Riadha Tanzania (RT) kutotoa lawama kwa watu na badala yake waelekeze nguvu zao katika kuiandaa timu itakayoshiriki michezo ya 20 ya Jumuiya ya Madola. Michezo ya mwaka huu ya Jumuiya ya Madola itafanyika jijini Glascow, Scotland, kuanzia Julai 23 hadi Agosti 3 na Tanzania inatarajia kupeleka michezo mbalimbali ukiwemo wa riadha.
Kikwete akizungumza katika hafla ya kupokea kifimbo cha Malkia wa Uingereza Ikulu jijini Dar es Salaam jana, alisema kuwa, viongozi wa RT wamekuwa wakitupa lawama kwa watu mbalimbali badala ya kuiandaa timu kwa ajili ya michezo hiyo inayofanyika kila baada ya miaka minne.
Alisema kuwa viongozi wa RT wamekuwa wakitumia muda mrefu kutoa lawama kwa watu kuwa hawajaahidiwa kupata fedha za kuwaweka wachezaji kambini, wakati hilo ni moja ya majukumu yao.
“Mkianza kumtupia mtu lawama kamwe hamtafika popote na mlipoomba nafasi hizo kwani hamkujua majukumu yenu na badala yake mmekuwa mkitupa lawama badala ya kufanya maandalizi?" alihoji Kikwete huku akipigiwa makofi na wanamichezo waliofika katika hafla hiyo.
Alisema kuwa Watanzania wamekuwa na kiu kubwa ya kupata medali, hivyo ni matumaini yake katika michezo ya mwaka huu angalau timu ya Tanzania inaweza kurudi na medali moja.
Alisema kuwa tatizo kubwa la viongozi wa michezo wa Tanzania wamekuwa wakisubiri muda umemalizika ndio wanaanza maandalizi wakati wanatakiwa kuanza maandalizi mapema.
Alisema kuwa kupata medali katika michezo kama hiyo ni jambo linalowezekana, ambapo alitoa mfano wa Filbert Bayi aliyevunja rekodi ya dunia ya mbio za mita 1500 katika Michezo ya Jumuiya ya Madola Chrischurch, New Zealand mwaka 1974.
Aliongeza kuwa kupata medali kunawezekana, kwani mbali na Bayi pia kuna wachezaji kama bondia Titus Simba (sasa marehemu), Gidamis Shahanga na wengineo walipata medali katika michezo mbalimbali ya Jumuiya ya Madola.
Alisema ni kama viongozi wa RT wanataka kuongeza wasifu (CV) tu katika maisha yao na wala sio kutekeleza majukumu yanayowakabili katika kuendeleza mchezo huo.
“Inaelekea lengo lenu ni kuongeza CV tu kuwa huyo ni rais wa chama fulani lakini sio kuendeleza michezo," alisema Kikwete, maelezo yaliyofanya watu kuangua kicheko huku akishangiliwa kwa makofi.
Alisema RT wamekaa kuilaumu serikali badala ya kuandaa programu nzuri, ambapo aliwauliza kama wanataka yeye (Kikwete) ndiye akimbie ili alete medali.
“Badala ya kupanga programu nyinyi mnailaumu Serikali kwamba inapendelea soka, sasa mnataka mimi ndio nikimbie?” alisema Kikwete huku akishangiliwa.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fenella Mukangara, mabalozi wa nje waliopo nchini, wachezaji wa Tanzania waliopata medali katika Michezo ya Jumuiya ya Madola na rais na katibu mkuu wa RT Antony Mtaka na Suleiman Nyambui.

Aidha, kifimbo hicho leo kinakwenda Zanzibar ambako kitakimbizwa kabla ya kupokewa na Rais Dk Ali Mohamed Shein na baadae kurejea Dar es Salaam na kabla ya kwenda Sheli Sheli kuendelea na mbio zake.

Viongozi wa dini watembelea Songosongo

VIONGOZI wa dini wamemaliza ziara yao ya kutembelea shughuli mbalimbali katika sekta ya gesi na mafuta kwa kutembelea kisiwa cha Songosongo eneo la kwanza kuzalisha gesi asilia. Wakiwa kisiwani humo walikutana na uongozi wa kijiji cha Songosongo ambapo walipata taarifa mbalimbali za namna mradi wa gesi ulivyonufaisha kisiwa hicho ikiwemo pia mipango ya baadaye ya kuendeleza eneo hilo.
Akieleza kuhusu manufaa yaliyopatikana kisiwani humo kutokana na kuwepo uwekezaji wa gesi, mjumbe wa Kamati ya Ustawi wa Jamii Kijijini hapo, Chiku Abdalah alisema mbali ya kupata umeme na maji bure, kijiji kimefaidika na huduma nyingine za jamii, ikiwemo wanafunzi kupata msaada wa elimu pamoja na afya.
“ Tunawashukuru Pan Africa na Songas, wanatujali wanatusaidia elimu ya watoto wanatupatia maji, tunashirikiana nao vizuri,” alisema. Mjumbe wa Kamati ya Mipango, Uchumi na Fedha kijijini hapo, Yussufu Faraki alisema shule ya chekechekea imejengwa kijijini hapo na fursa za ajira kwa vijana zimepatikana.
“Tunakwenda vizuri na Songas na Pan African, wamekarabati shule, wametuwekea watu wa mahusiano, walituletea mkunga, wanalipa ada. Tunakubali changamoto zipo lakini kila mmoja anamhitaji mwenzake,” alisema Faraki.
Akielezea kuhusu ziara hiyo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Ngosi Mwihava alisema wamefika kijijini hapo kuona shughuli za maendeleo zinazotokana na uwekezaji katika sekta ya gesi asilia na kujenga welewa mpana kuhusu uwekezaji wa gesi na faida zake kwa maendeleo ya eneo la uwekezaji, ikiwemo pia maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Katibu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Kongamano la viongozi wa dini, John Mapesa alisema elimu ya Songosongo imejulikana kwa viongozi wa dini na namna wananchi wa eneo hilo wanavyoizungumzia sekta ya gesi na namna walivyonufaika nayo.
“Tumepata elimu ya kufaa, tunapoelekea katika kongamano letu, tutajua namna nzuri ya kuishauri serikali na Wizara katika sekta hizi kwa maendeleo ya faifa,” alisema. Ofisa Uhusiano wa Jamii wa Kampuni ya Songas, Nicodemus Chipakapaka alieleza kuwa, mbali na uchimbaji imejikita katika kutoa huduma za jamii kupitia elimu, afya ambapo shirika hilo limekuwa likigharimia wanafunzi wanaofaulu kuendelea na masomo ya sekondari kijijini hapo.
Mbali na hayo alieleza kuwa, Songas wamefanikiwa kuboresha zahanati ya kijiji, ikiwemo pia kuwezesha uwepo wa wahudumu wa afya wanaohudumia wananchi kijijini hapo.
Akieleza namna shirika la Pan Africa linavyosaidia katika shughuli za maendeleo kijijini hapo, Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Shirika hilo, Tura David alieleza kuwa, pamoja na mambo mengine, kwa kuzingatia umuhimu wa elimu na namna utakavyowanufaisha wana Songosongo, Shirika hilo limeanzisha mpango wa kusaidia wanafunzi 10 kila mwaka wanafaulu vizuri zaidi na kuwaendeleza katika shule zilizopo nje ya Songosongo na nje ya Wilaya hiyo.
Alisema shirika limejenga bweni la wasichana kijijini hapo lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 55. Kwa mujibu wa Mtaalamu wa Masuala ya gesi na Msimamizi Mkuu wa Mitambo ya Kusafisha Gesi kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Sultan Pwaga, mitambo mipya inayojengwa ya kuzalisha gesi kisiwani humo inatarajiwa kuzalisha futi za ujazo milioni 140 kwa siku, uzalishaji wa umeme wa zaidi ya megawati 10, ambapo pia kutakuwa na mtambo wa kukandamiza gesi, na mtambo wa kusafisha maji ya wastani wa lita 60,000 kwa siku ambapo wananchi wa Songosongo wanatarajiwa kufaidika na huduma za maji hayo.
Makamu Mkurugenzi Uzalishaji Songas, Elias Mnunduma alisema kwa sasa eneo hilo la Songosongo linazalisha gesi ya futi za ujazo milioni 105 kwa siku.
Asilimia 80 ya gesi inauzwa Tanesco kwa ajili ya kuzalisha umeme na asilimia 20 inapelekwa viwandani

Baraza jipya la mawaziri latajwa, Mulugo, Nangolo wapigwa chini, Migiro, Nkamia,Nyalandu wala shavu


Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sufue Jumapili hii amelitaja baraza jipya la mawaziri. Katika mabadiliko hayo mawaziri kadhaa wameondolewa kabisa kwenye baraza hilo, wengine wamehamishiwa wizara, wengine wakipandishwa cheo huku kukiwepo sura zingine mpya.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sufue
Hata hivyo hakuna mabadiliko kwenye Wizara za Uchukuzi, Ujenzi, Ofisi ya Rais, Ofisi ya waziri Mkuu, Mambo ya nje, Afrika Mashariki, Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na Kazi na Ajira.
Waziri wa Fedha sasa ni Saada Mkuya huku manaibu wake wakiwa ni Mwigulu Nchemba na Adam Malima. Nafasi hiyo iliachwa wazi kutokana na kifo cha Dr. Willliam Mgimwa nchini Afrika Kusini mwanzoni mwa mwezi huu.
Wizara ya Sheria na Katiba itakuwa chini ya Dr. Asha -Rose Migiro na naibu wake akibaki kuwa Angela Kairuki na Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi imeenda kwa Dr Titus Kamani huku naibu wake akiwa Kaika Telele.
Wizara ya Maendeleo ya jamii jinsia na watoto imekabidhiwa kwa Sophia Simba na naibu wake akiwa ni Pindi Chana.
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itaendelewa kuwa chini ya Shukuru Kawambwa na Naibu wake ni Jenister Mhagama. Aliyekuwa naibu waziri wa mwanzo Philip Mulugo ameondolewa.
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi itaendelewa kuwa chini ya Anna Tibaijuka na naibu wake akiwa George Simbachawene. Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika waziri anabaki kuwa Christopher Chiza na naibu wake akiwa ni Godfrey Zambi na Adam Malima akihamishiwa kwenye wizara ya fedha (Uchumi na Mapato).
Wizara ya Nishati na Madini anabaki kuwa Prof Sospeter Muhongo na manaibu wake wakiwa ni Steven Maselle na Charles Kitwanga. Wizara ya Maliasili na Utalii imekamatwa na aliyekuwa naibu wake, Lazaro Nyalandu huku unaibu ukienda kwa Mahmoud Mgimwa.
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeenda kwa aliyekuwa naibu Dr Seif Rashid na naibu wake akipewa mbunge wa Serengeti Kebwe Stephen Kebwe huku ni Dr Hussein Mwinyi aliyekuwa Waziri wa Afya akipewa wizara ya Ulinzi na JKT.
Wizara ya Mambo ya ndani sasa itakuwa chini ya Mathias Chikawe aliyekuwa wizara ya Sheria na Katiba, na naibu wake anaendelea kuwa Pereira Sillima. Nayo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Waziri anabaki kuwa yuleyule Dr Fenella Mukangara na shavu la unaibu likimwendea aliyekuwa mtangazaji wa TBC na mbunge wa Kondoa Kusini, Juma Nkamia.




Wasifu Wa Raisi Jakaya Mrisho Kikwete




Dr. Jakaya M Kikwete
 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania tangu 2011-12-30
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alizaliwa tarehe 7 Oktoba mwaka 1950 Msoga, mkoa wa Pwani, mtoto wa sita katika familia ya watoto tisa. Amemuoa mama Salma Kikwete na wamebarikiwa watoto nane.
Kazi
Mwaka 1976 alijiunga na Chuo Kikuu cha Maofisa wa Jeshi Monduli na kutunukiwa Cheo cha Luteni Kanali na baadaye kuwa Mkufunzi Mkuu na Kamisaa wa Siasa katika chuo hicho. Mheshimiwa Kikwete amefanya kazi katika Chama cha Mapinduzi kwa nyadhifa mbalimbali kwenye mikoa ya Singida na Tabora na  wilaya za Nachingwea na Masasi.

Mwaka 1988 aliteuliwa kuwa Mbunge na Naibu Waziri wa Nishati na Madini. Mwaka 1990 alichaguliwa kuwa mbunge wa  Jimbo la Bagamoyo na akateuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini. Nyadhifa nyingine alizoshika ni Waziri wa Fedha mwaka 1994 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuanzia mwaka 1995 hadi 2005.
Alishika rasmi wadhifa wa urais mwaka  2005 na kuchaguliwa tena 2010 kwa muhula mwingine wa  miaka mitano.
Elimu
Alipata elimu ya msingi na ya kati katika shule za Msoga na St. John Bosco Lugoba kati ya mwaka 1958 na 1965. Aidha, alipata elimu ya sekondari katika shule za sekondari za Kibaha (1966 – 1969) na Tanga (1970 – 1971).Alihitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1975 na kupata Shahada ya Uchumi,
Nyadhifa nyengine
Mwanyekiti wa Viongozi wa Afrika Kupambana na Malaria (ALMA) 2010-2011
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Januari 2010
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) Mwaka 2008
Mwenyekiti Mwenza wa Mchakato wa Helsinki kwenye Utandawazi na Demokrasia Mwaka 2004
Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Mwaka 2004
Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika (OAU) Mwaka 1997
Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Mwaka 1997
Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB) Mwaka 1995


Mtangazaji wa BBC, Komla Dumor afariki dunia

Mtangazaji wa BBC TV, Komla Dumor amefariki dunia ghafla jana akiwa nyumbani kwake mjini London, Uingereza.Alikuwa na umri wa miaka 41.



Dumor aliyezaliwa nchini Ghana alikuwa mtangazaji wa BBC World News na aliendesha kipindi cha Focus on Africa.
 Mtangazaji huyo alijiunga na BBC kama mtangazaji wa radio mwaka 2007 baada ya kufanya kazi ya uandishi wa habari kwa zaidi ya muongo mmoja nchini Ghana. Rais wa Ghana, John Dramani Mahama aliandika kwenye mtandao wa Twitter kuwa nchi yake imepoteza mmoja wa mabalozi wake muhimu.

Mwanaume wa Iran ambaye hajaoga kwa miaka 60 avunja rekodi, ‘World’s Smelliest & Dirtiest Man Alive’



Mr Amou Haji ni raia wa Iran mweye miaka 80, ambaye amevunja rekodi ya kutooga kwa miaka 60 na kuwa ndiye mwanaume mchafu kuliko wote duniani.

Kwa wale single ladies, Haji yuko single na anahitaji mpenzi, lakini mwanamke ambaye atapenda kuwa naye ni lazima akubaliane na lifestyle yake.
Mr Haji hupendelea kusmoke, na ili arelax hupenda kuvuta kiko chenye kinyesi cha wanyama. Upande wa chakula hupendelea kula nyama zilizooza za wanyama waliokufa, pamoja na maji lita tano kwa siku kwa kutumia kidumu cha mafuta chenye kutu. Chakula anachokipenda zaidi ni Nungu nungu aliyeoza. Mr. Haji pia anapohitaji kupunguza nywele zake huzichoma kwa moto.
  Baadhi ya wakazi wa kijiji anachoishi cha Dejgah huko Iran, waliwahi kutaka kumsaidia Haji aweze kuoga, lakini aliwatoroka. Usiku Mr Haqji hulala katika mashimo yanayofana na kaburi.
 Rekodi ya mwanaume aliyekaa muda mrefu bila kuoga iliyovunjwa na Mr Haji iliwekwa na mwanaume wa India Kailash Singh (66), aliyeishi bila kuoga kwa miaka 38.