MICHAKATO

Levis Rocky Ndekeno

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Pages

Thursday, February 4, 2016

Upimaji wa ubikira wakosolewa Afrika Kusini

Waziri mmoja wa Afrika Kusini ameshtumu kuwa kinyume cha sheria ufadhili wa elimu ya wasichana wanaopita kipimo cha ubikira.
Mwezi Uliopita,Manispaa ya uthukela katika jimbo la Kwazulu Natal nchini Afrika Kusini ilisema itawapa zawadi wanafunzi 16 wa kike kwa masharti kwamba wasalie mabikira.
''Mpango huo ulilenga kupunguza maambukizi ya virusi vya HIV na mimba za mapema miongoni mwa wasichana'',alisema Meya Dudu Mazibuko.
Katika taarifa ya gazeti la Daily Maverick,waziri wa maendeleo ya kijamii Bathabile Dlamini alielezea upimaji wa ubikira kama usiowezekana,mchafu na ukiukaji mkubwa na haki za kibiniaadamu.
''Kujamiana kwa mara ya kwanza hakutakikani,licha ya hilo kuna unyanyapaa miongoni mwa wasichana ambao hufeli kipimo hicho'',alisema,akiutaja mpango huo kama ''kosa la kingono''.
Bi. Dlamini ,ambaye ni kiongozi wa chama tawala cha ANC upande wa wanawake ndio kiongozi mwenye hadhi ya juu kupinga kipimo hicho.

Wanaotuhumiwa kumvua nguo Mtanzania mbaroni India

Wanaume wanne wanaotuhumiwa kuhusika katika kumshambulia na kumvua nguo mwanafunzi wa kike kutoka Tanzania wamekamatwa, shirika la habari la AP limeripoti.
Waziri wa mashauri ya kigeni wa India Sushma Swaraj, aliandika kwenye Twitter kwamba amezikitishwa sana na “kisa hicho cha aibu” kilichotokea Jumapili eneo la Bangalore.
Bi Swaraj amesema polisi wamewakamata washukiwa wanne ambao watafunguliwa mashtaka.
Wanafunzi Waafrika mjini Bangalore wamesema wanaishi na hofu ya kushambuliwa.
Bw Bosco Kaweesi, mshauri wa kisheria wa Chama cha Wanafunzi kutoka Afrika, anasema wanafunzi wengine watatu wa kike kutoka Tanzania waliokuwa pamoja na mwanafunzi huyo garini pia walipigwa.
Gari lao liliteketezwa.
Kaweesi amesema huenda kisa hicho kilitendeka kimakosa, akisema gari la wanafunzi hao lilikuwa limefuata gari la mwanafunzi kutoka Sudan ambalo lilimgonga na kumuua mwanamke aliyekuwa amelala pembezoni mwa barabara.
Wanafunzi hao hawakumfahamu mwanafunzi huyo wa kiume aliyetoka Sudan, ambaye pia alipigwa na gari lake kuteketezwa.

Trump ataka mchujo wa Iowa urudiwe


Donald Trump anataka uchaguzi wa mchujo wa kuteua atakayegombea urais kupitia chama cha Republican katika jimbo la Iowa urudiwe, akisema mshindi Ted Cruz alitumia ulaghai.
Bw Trump anasema wakati wa kikao cha Iowa, maafisa wa kampeni wa Cruz waliwaambia wapiga kura kwamba mgombea mwingine Ben Carson alikuwa amejitoa kwenye kinyang’anyiro hicho, habari ambazo hazikuwa za kweli.
Maafisa wa kampeni wa Cruz baadaye walimuomba radhi Carson, wakisema lilikuwa kosa lisilokusudiwa.
Bw Trump alimaliza wa pili katika mchujo huo wa kwanza kufanyika nchini humo kwa ajili ya uchaguzi mkuu baadaye mwaka huu.
Mchujo utakaofuata utafanyika New Hampshire Jumanne ijayo.
"Ted Cruz hakushinda Iowa, aliiba. Hii ndiyo maana kura zote za maoni zilionekana kukosea na ndiyo sababi alipata kura nyingi kuliko ilivyotarajiwa. Ni vibaya!,” Bw Trump amesema.
Awali, alikuwa ameandika kwenye Twitter kwamba Bw Cruz alishinda mchujo wa Iowa kwa njia haramu, lakini baadaye akafuta ujumbe huo.
Matamshi ya Bw Trump ni kinyume na hotuba yake ya kukubali kushindwa ambayo aliitoa Jumatatu usiku baada ya matokeo kujulikana, jambo ambalo lilishangaza wengi ikizingatiwa ukali wake.
Kambi ya Cruz haijafurahishwa na madai ya sasa ya Bw Trump.
“Ukweli umemfika nyota huyu wa runingani – alishindwa Iowa na sasa hakuna anayezungumza kuhusu ubabe wake, kwa hivyo anachomoza kwenye Twitter,” afisa wa mawasiliano wa Bw Cruz Rick Tyler aliandikia Politico kupitia barua pepe.
“Kuna makundi yanayosaidia watu kudhibiti uraibu wa kutumia Twitter, labda anafaa kuwasiliana na tawi moja.”
Katika historia, haijatokea uchaguzi wa mchujo ukarudiwa.
Bw Carson alikubali ombi la msamaha kutoka kwa Bw Cruz lakini maafisa wake wa kampeni wamesema kambi ya Cruz ilitumia “mbinu chafu”.
Jumatano, seneta wa Kentucky Rand Paul na seneta wa zamani wa Pennsylvania Rick Santorum walijitoa kwenye kinyang’anyiro cha kutafuta tiketi ya chama cha Republican baada ya kutofanya vyema Iowa.

Obama awakemea wanaoshtumu Waislamu


Rais Barrack Obama ameshtumu kile alichokitaja kuwa Matamshi machafu dhidi ya Uislamu,kufuatia tamko la hivi majuzi lililotolewa na mgombea wa urais kupitia tiketi ya Republican Donald Trump.
Katika ziara yake ya kwanza katika msikiti kama rais,Obama amesema kuwa matamshi machafu dhidi ya waislaumu hayakubaliki nchini Marekani.
Aliwapongeza Wamarekani Waislamu kama walio na heshima na uzalendo wa hali ya juu na taifa lao.Bwana Trump ametoa wito kwa waislamu kutoruhusiwa kuingia nchini Marekani.
Obama alikuwa akizungumza katika msikiti wa jamii ya waislamu mjini Baltimore Maryland.
Ametembelea misikiti katika maeneo mengine ya dunia katika ziara rasmi katika kipindi chake cha miaka saba akiwa rais.
Ikulu ya Whitehouse imesema kuwa ziara hiyo ni kutetea uhuru wa kidini na matamshi ya kutovumiliana dhidi ya jamii za walio wachache.
Obama amesema kuwa anajua kwamba Waislamu Wamarekani wanalengwa na kulaumiwa kwa vitendo vya wachache.
''Wamarekani wengi hawawajui Waislamu'',alisema.Wengi huwasikia Waislamu na Uislamu kutoka kwa vyombo vya habari baada ya tendo la ugaidi ama katika chombo cha habari kinachoouangazia Uislamu,TV ama hata katika filamu.
Rais Obama amekuwa na uhusiano wa kutatiza na Waislamu.Mapema katika uongozi wake aliapa kuimarisha uhusiano na waislamu katika mataifa ya kigeni baada ya vita vya Iraq.