MICHAKATO

Levis Rocky Ndekeno

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Pages

Tuesday, March 25, 2014

HABARI KWANZA: KAMATI YA UONGOZI YA BUNGE MAALUM YAFANYA KIKAO CH...

HABARI KWANZA: KAMATI YA UONGOZI YA BUNGE MAALUM YAFANYA KIKAO CH...:   Mwenyekiti wa Bunge Maalum Mhe. Samuel Sitta akiongoza kikao cha kwanza cha kamati ya Uongozi baada ya kuundwa leo. Kamati ...

Popo waeneza Ebola Guinea


Popo hutumiwa kutengeza kitoweo maarufu sana katika baadhi ya maeneo ya Guinea, lakini sasa inahofiwa kuwa popo wanachangia kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola kusini mwa nchi hiyo.

NI marufuku kula na kuuza popo Guinea

Maafisa nchini humo sasa wamepiga marufuku uuzaji na ulaji wa nyama ya popo katika juhudi za kudhibiti ugonjwa hatari wa Ebola, ambao kufikia sasa umesababisha vifo vya watu 62.
Habari zinazohusiana
Ebola ni kiini cha ugonjwa hatari Guinea
Wasi wasi kuhusu virusi vya Ebola
Uganda imethibitisha kuwepo kwa Ebola


Taarifa zinazohusiana
Afrika

Nchi za kanda hiyo zikiwemo Liberia na Sierra Leone, zimechukua hatua kabambe kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo zikiwemo kuwafanyia uchunguzi wa kiafya watu wanaongia mipakani.

Maafisa wa afya wanapata msaada kutoka shirika la afya duniani na ujumbe wa kuhamasisha watu unapeperushwa kupitia televisheni.

Watu watano kati ya sita walioingia nchini Liberia kutoka Guinea walikua na ishara za ugonjwa huo na wamethibitishwa kufa.

Hatahivyo maafisa wa utawala nchini Liberia bado hawajathibitisha kikamilifu kama kweli walikufa kutokana na ugonjwa wa Ebola.


Uhuru ahimiza ushirikiano Afrika Mashariki


Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amewataka wabunge wa bunge la jumuia ya Afrika Mashariki kuhimiza utekelezaji wa sheria zilizopitishwa na wabunge hao ili ziweze kuridhiwa na kutekelezwa na nchi washirika.

Miongoni mwa sheria zilizopitishwa na bunge hilo ni ushuru wa forodha, soko la pamoja na sarafu ya pamoja, mkataba ambao bado haujaanza kutekelezwa.
Taarifa zinazohusiana
Afrika Mashariki

Rais Uhuru Kenyatta ambaye ni mwenyekiti wa wakuu wa nchi za jumuiya hiyo yuko mjini Arusha makao makuu ya jumuiya hiyo kuzungumza na wafanyakazi na pia kuwafungulia kikao cha bunge kitakachodumu kwa wiki mbili zijazo.

Rais Kenyatta amezidi kusisitiza kuwa ushirikiano wa nchi hizo ndio ukombozi wao kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Rais Uhuru Kenyatta akiwa safarini kwenda Arusha

Rais Kenyatta kadhalika ameelezea nia ya mataifa yote ya jumuiya ya Afrika Mashariki kupambana vikali na tatizo la ujangili na kuutokomeza.

Rais Uhuru Kenyatta pia amesema jukumu la kukabiliana na vitendo vya ujangili ni la wananchi wote kwa sababu lina athari kwa kila mtu mkaazi wa Afrika Mashariki.

Ama kuhusu suala la uhuru wa uhamishaji wa mitaji na uhuru wa wananchi wa Afrika Mashariki kutembea kutoka nchi moja kwenda nyingine, amesema jambo hilo linaweza kumalizwa pindi kila nchi itapokamilisha taratibu za matumizi ya vitambulisho kwa raia wake:

Rais Uhuru Kenyatta na ujumbe wake wamerejea nyumbani kwa njia ya barabara kupitia mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Namanga. Ben Mwang'onda Dira ya Dunia BBC, Arusha.

Hewa chafu inaua mamilioni duniani


Watu milioni saba walifariki mwaka 2012 kutokana na hewa chafu. Hii ni kwa mujibu wa shirika la afya duniani .

Ripoti ya shirika hilo inasema kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya hewa chafu na maradhi ya moyo, tatizo la kupumua na ugonjwa wa Saratani.
Taarifa zinazohusiana
afya

Kifo kimoja kati ya vinane duniani kilitokana na hewa chafu , na kuifanya hali hiyo kuwa moja ya hatari ya mazingira chafu afya ya binadamu.

Tarkriban watu milioni sita waliofariki dunia walikuwa Asia ya Mashariki na katika eneo la Pacific.

Shirika hilo limesema kuwa takriban watu milioni 3.3 walifariki kutokana na hewa chafu katika nyumba zao kwa kutumia mkaa kukipikia na wengine milioni 2.6 walifariki kutokana na hewa chafu nje ya nyumba zao , hasa katika nchi zinazostawi.

Afisaa mmoja mkuu wa shirika hilo, Daktari Maria Neira, amesema kuwa, hewa chafu ina hatari kubwa kwa afya ya watu kuliko ilivyodhaniwa hasa kwa kusababisha maradhi ya Moyo na Kiharusi.

Ripoti hii inaonyesha umuhimu wa kushirikiana katika kuhakikisha kuwepo kwa hewa safi.

Shirika hilo limesema kuwa kupunguzwa kwa viwango vya hewa chafu kunaweza kuokoa maisha ya watu.

Kadhalika shirika hilo limesema: "usafi wa hewa tunayopumua unazuia maradhi ya kuambukizana na pia kuondoa hatari kwa watoto, wazee na wanawake.''
Taarifa zinazohusiana

Wanaowania Tuzo za KILI 2014 ndio hawa, zilizoachwa ziko hapa pia


 (BASATA) limetangaza rasmi matokeo ya mchakato wa kuwapata wateule rasmi yaani ‘nominees’ wa vipengele 34 vya tuzo za muziki Tanzania.
 Kabla ya kuanza kutajwa kwa wanaowania tuzo za KTMA 2014, BASATA ilitangaza nyimbo ambazo zimetolewa kwenye kuwania tuzo hizi kutokana na sababu za kimaudhui kama unavyoona hapa chini.











Nyingine ni
 WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI – Tubonge ya Jose Chameleone, Nakupenda pia ya Wyre na Alaine, Badilisha ya Jose Chameleone, Kipepeo ya Jaguar, Kiboko changu ya Amani, Weasal na Radio.
 WIMBO BORA WA TAARAB – Wasiwasi wako wa Mzee Yusufu, asie kujua hakuthamini Isha na Saida Ramadhani, Nipe stara Rahima Machupa, sitaki shari Leila Rashid, fahari ya mwanamke ya Khadija Kopa, mambo bado Khadija Yusufu, kila muomba Mungu ya Mwanahawa Ally.
 WIMBO BORA WA RAGGA/DANCEHALL – Nishai ya Chibwa ft Juru, Sexy Lady ya Dr. Jahson, My sweet ya Jettyman Dizano, feel alright ya Lucky Stone na wine ya Princess Delyla.
 WIMBO BORA WA KUSHIRIKISHWA/KUSHIRIKIANA – Muziki gani ya Ney wa Mitego ft Diamond, Joto hasira ya Lady Jaydee ft Prof J, kidela ya Ally Kiba na Abdu Kiba, bila kukunja goti ya MwanaFA, Ay ft J Martins na tupogo ya Ommy Dimpoz ft J Martins.
 RAPA BORA WA MWAKA WA BENDI – Kitokololo, Chokoraa, Ferguson, Canal Top na Totoo ze bingwa.
 MTUMBUIZAJI BORA WA KIKE WA MUZIKI – Khadija kopa, Vanessa Mdee, Isha Ramadhani, Luiza Mbutu, Catherine (Cindy)
 MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA TAARAB – Enrico, Ababuu mwana wa Zanzibar na Bakunde.
 MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA (BENDI) – Allan Mapigo, C9, Enrico, Amoroso na Ababuu mwana wa Zanzibar.
 WIMBO BORA WA REGGAE – Niwe nawe ya Dabo, hakuna matata ya Lonka, tell me ya Dj Aron ft Fidempha, bado nahitaji ya Chikaka ft Bless P & Lazzy B, Bongo reggae ya Warriors from the east.
 WIMBO BORA WENYE VIONJO VYA ASILI YA KITANZANIA – Kwejaga nyangisha ya Batarokota, Nalonji ya Kumpeneka, bora mchawi Dar bongo massive, tumbo lamsokota ya Ashimba, Aliponji ya Wanakijiji na Agwemwana ya Cocodo african music band.