MICHAKATO

Levis Rocky Ndekeno

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Pages

Thursday, January 23, 2014

Huyu ndiye mwandishi kutoka kenya aliyejitangaza kuwa anashiriki Mapenzi ya Jinsia moja.



Mwandishi maarufu wa vitabu nchini Kenya, Binyavanga Wainaina, amejitokeza hadharani kuwa yeye hushiriki mapenzi ya jinsia moja.

 Hii inamfanya Binyavanga kuwa mmoja wa wafrika mashuhuri kujitokeza hadharani.

 Alifichua hali hii katika taarifa yake kupitia kwa mtandano wa kijamii wa Twitter iliyowiana na siku ya kuzaliwa kwake.Ana umri wa miaka 43. (R.M).
Hii inakujia wakati ambapo kuna mjadala mkali nchini Kenya na katika baadhi ya mataifa ya Afrika kuhusiana na suala la haki za wapenzi wa jinsia moja.

 Hivi karibuni, Nigeria ilipitisha sheria ambayo inatoa adhabu kali kwa makundi ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, ilhali Rais wa Uganda alikataa kuhalalisha mswada kama huo uliopitishwa bungeni.

 Uamuzi wa Binyavanga kujitokeza hadharani umepokelewa kwa hisia mbali mbali nchini Kenya. Kunao waliompongeza ingawa baadhi wanahisi kuwa huenda jamii ikamnyanyapaa.

 Binyavanga aliwahi kushinda tuzo la mwanadishi bora zaidi Afrika la Caine mwaka 2002.


 Watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja nchini Kenya wanaweza kuadhibiwa kifungo cha miaka kumi jela ikiwa watapatikana na hatia.

Samsung Galaxy S5 inaweza kuzinduliwa February 23

Wale wanaoisubiria kwa hamu simu mpya ya Samsung wanaweza wasingoje kwa muda mrefu tena. Kuna tetesi kuwa kampuni hiyo inaweza kuitambulisja Galaxy S5, Feb. 23 kabla ya Mobile World Congress, ingawa simu hiyo itaingia sokoni April.

Kwa mujibu wa Eldar Murtazin, mhariri wa mtandao wa Mobile-Review.com , simu hiyo itatangazwa mjini Barcelona Feb. 23. Hakuna taarifa za kuaminika za namna simu hiyo itakavyokuwa lakini itapewa teknolojia ya mawasiliano kati yake na macho ya mtumiaji.

Watafiti: Kutumia smartphones usiku kunaharibu usingizi na utendaji kazi siku inayofuata

Tunafahamu usiku unaweza kuwa muda mzuri wa kupitia status za washkaji Facebook, kutazama picha mbalimbali Instagram ama kufuatilia mijadala kwenye Twitter lakini hicho kinaweza kuwa kikwazo kikubwa cha nia yako ya kutaka kupata usingizi wa kutosha ama kuwa na utendaji mzuri kazini.

 Kuzima smartphone saa 3 usiku kunaweza kukufanya ufanye kazi vizuri siku inayofuata, watafiti wamesema






Timu katika chuo kikuu cha Washington imesema matumizi ya simu usiku sana yanaweza kuharibu kabisa usingizi wako na namna utakavyofanya kazi siku inayofuata. Wameshauri wafanyakazi wawe na tabia ya kuzima simu ama lasivyo watajikuta wakishindwa kufurahia kazi kesho yake.
Watafiti hao wanasema kujiondoa kabisa na matumizi ya simu usiku ni njia ya kupata usingizi mzuri usiku. Wamewaomba waajiri kusubiri kutuma email hadi asubuhi
“Sababu ya hii kama tutakavyoelezea, ni kwamba smartphones ni mbaya kwa usingizi, na usingizi ni muhimu kwa uchapakazi wa mwajiriwa,” alisema Christopher Barnes, Profesa Msaidizi katika chuo kikuu cha Washington (Foster School of Business) aliyeongoza utafiti huo utakaochapishwa kwenye jarida la , Organizational Behavior and Human Decision Processes baadaye mwaka huu.
“Bahati mbaya smartphones zimetengenezwa mahsusi kuharibu usingizi. Sababu zinatufanya kiakili kuendelea na kazi hadi usiku, zinafanya kuwepo ugumu wa kujiondoa kisaikolojia kutoka kwenye masuala muhimu ya siku ili tupumzike na kulala. Pengine suala gumu kuliepuka kutoka kwenye smartphones ni kwamba zinatuweka kwenye mwanga, ukiwemo mwanga wa blue. Hata kiwango kidogo cha mwanga wa blue hupunguza uzalishaji wa kemikali ya usingizi, melatonin, ikimaanisha kuwa muonekano (display) unaweza kutengeneza madhara haya.”

Lil Wayne , Nick Minaj na Drake kuvunja ukimya wa Young Money, kuja na album ya kundi ‘Rise Of An Empire’ mwezi March

Kundi na label ya Young Money imetangaza ujio wa compilation album ya pili ya kundi hilo ‘Rise Of An Empire’ ambayo inafuatia ile ya kwanza iliyotoka 2009 iliyoitwa ‘We Are Young Money’.

  
 Mastaa wa familia ya Young Money wakiwemo Drake, Nick Minaj na Tyga wakiongozwa na boss wao Lil Wayne, watasikika kwa pamoja katika album hiyo inayotarajiwa kuingia sokoni March 11.
Wimbo wa kwanza kutoka katika album hiyo unaitwa ‘We Alright’, ambao umeshambuliwa na Bird Man n Lil Wayne, huku upande wa production akiwa amesimama member mpya wa Young Money, Euro.
Single ya Drake ya hivi karibuni ‘Trophies’ ambayo haikuingia katika album yake iliyopita ‘Nothing Was the Same’, itapatikana katika compilation album ya Young Money.

Bill Gates adai hadi kufikia mwaka 2035 hakutakuwa na nchi maskini duniani

Mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft, Bill Gates amesema hadi kufikia mwaka 2035 hakutakuwa na nchini maskini duniani.

Kwenye ripoti ya kurasa 25 iliyoandikwa na Gates na mke wake Melinda, ambao ni wenyekiti wa Bill & Melinda Gates Foundation, wamedai kuwa duniani imekuwa na afueni kuliko ilivyokuwa awali. Gates ametabiri kuwa hadi kufikia 2035, hakutakuwa na nchini itakayobaki kuwa maskini.
“Nchi maskini hazitakaa maskini daima. Baadhi ya nchini zinazoendelea tayari zimeshaendelea,” alisema Gates kwenye ripoti yake ya mwaka. “Nina imani kubwa kuhusu hili kiasi ambacho nipo tayari kufanya utabiri wangu. Hadi kufikia mwaka 2035, hakutakuwa na nchini maskini duniani.”
Gates amesema katika kipindi hicho karibu nchi zote zitakuwa na kipato cha kati ama zitakuwa tajiri.

Roma atoa sababu za kwanini hutoa wimbo mmoja kwa mwaka

Rapper Ibrahim Musa aka ‘Roma Mkatoliki’ amesema kile kinachoonekanan kama ukimya wake kinatokana na desturi aliyojiwekea tangu aanze muziki wa kutoa wimbo mmoja kwa mwaka.

Akizungumza  leo, Roma amesema ukiona yupo kimya katika muziki ujue anafanya shughuli za kiujasiriamali ambazo ni tofauti na muziki.
“Mwaka jana hakukuwa na kimya chochote kwa mtu anayemjua Roma kwa miaka yote,” amesema Roma. Roma kwa mwaka anatoaga wimbo moja. Kwahiyo mtu yoyote ambaye ana ‘judge’ kwanini Roma alikuwa kimya, ujue huyo kamjua Roma juzi.2007 ilitoka nyimbo ya kwanza, 2008 nyimbo ya pili, na nyimbo sita, kwahiyo kila mwaka natoaga nyimbo moja,sijawahi kutoa nyimbo mbili kwa mwaka. Kwa mwaka jana ni 2030. Nilikuwa kimya kwasababu ndio nyimbo iliyokuwa inachezwa.Na mwaka huu nitatoa nyimbo moja nanitakuwa kimya mpaka mwakani ndio kawaida ya Roma.”
“Nimeandaa nyimbo kama sita ndani ya ‘Tongwe records’ sema ni kuchagua nitoe nyimbo gani kwa mwaka huu. Sema nilikuwa kimya kidogo kutokana na majukumu ya maisha.Kama kawaida ya Roma ni nyimbo moja kwa mwaka, hata wimbo wangu 2030 ulitoka 28/12/2012. Lakini wimbo huu ni wa mwaka 2013 ndio maana ulipata air time nzuri 2013,” aliongeza.
Katika hatua nyingine, Roma amesema mwaka huu anatarajia kurudi shule baada ya kuhitimu na kushindwa kuendelea kutokana na muziki.
“Mimi ni mjasiriamali pia najarajia kurudi shule hivi karibuni,kwasababu nilihitimu nikashindwa kuendelea,ila mwaka huu nadhani suala la kurudi shule ni miongoni mwa mikakati yangu kwa mwaka huu.”