MICHAKATO

Levis Rocky Ndekeno

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Pages

Wednesday, June 25, 2014

June 25: Ni Miaka miaka mitano tangu kifo cha Michael Jackson






Michael Jackson alifariki June 25, 2009, katika muda aliokuwa akiutafuta sana usingizi huku akijiandaa kurejea kwa kufanya ziara yake ambayo aliamini ingemuondoa kwenye madeni mengi na kurudisha heshima yake kama mfalme wa pop. Katika siku zake za mwisho, Michael Jackson aliondoka nchini Marekani akiwa na wanae watatu muda mfupi baada ya kumalizika kwa kesi yake ya kulawiti watoto.

Alirejea Marekani kimyakimya mwaka 2006, baada ya kukaa huko Bahrain kwa mwaka mzima na miezi kadhaa nchini Ireland. Bill Whitfield na Jevon Beard walitumia miaka miwili kama walinzi wa MJ walisimulia mengi kwenye kitabu kipya kiitwacho s “Remember the Time: Protecting Michael Jackson in His Final Days.” Kipindi Jackson anashuka kutoka kwenye ndege binafsi jijini Las Vegas, watu aliokuwa nao walikuwa wanae na mlezi wa watoto wake tu. “Alikuwa peke yake,” Whitfield alisema kwenye mahojiano na CNN. Kikawa kitu kisicho cha kawaida. Kuna kitu hakipo sawa. Huu ni utani.”

Walinzi hao ambao wakati mwingine hawakuwa wakilipwa mshahara kwa miezi, walikuwa wakitumia fedha zao kusaidia masuala nyumbani kwa Jackson pale credit cards zake zilipokuwa zikiishiwa. Beard aliiambia CNN kuwa mameneja wake walikuwa wakimzunguka. “Jamaa alikuwa amechoka kiakili.” Whitfield na Beard walidai kuwa Jackson alikuwa na mambo yake ya siri yaliyokuwa yakijulikana labda kwa mashabiki wake waliokuwa wakimganda. Jackson alikuwa na mademu.

Mfalme huyo wa pop alikuwa akitumia muda wa faragha na mwanamke nyuma ya pazia kwenye siti ya nyuma ya gari wakati walinzi wakiendesha. Wanadai kuwa Jackson alikuwa akipenda wasichana na walimuona kwa macho yao akiwabusu. Wanawake hao, ambao walinzi waliamini walikuwa wakitokea Ulaya, hawakuwahi kwenda nyumbani kwake na hawakuwahi kukutana na wanae.

Alikuwa akirudi nyumbani kutoka kwenye mishe zake kabla ya wanae Prince, Paris na Blanket hawajaamika. Jackson aliwaagiza walinzi wake kuwazuia kaka zake, dada zake na baba yake kuingi kwake japo mama yake alikuwa akiruhusiwa kuingia nyumbani kwake.

Pamoja na kuwa hayupo tena, muziki wa Michael Jackson bado unaendelea kutoka ambapo sasa album yake Xscape ipo sokoni na iliuza kopi milioni 2.3 katika wiki tatu tangu itoke mwezi May. Ukurasa wake wa Facebook una likes milioni 75 ziadi hata Justin Bieber, Lady Gaga, Katy Perry, Taylor Swift na Bruno Mars.

Chanzo: CNN. Soma zaidi makala hiyo hapa.