MICHAKATO

Levis Rocky Ndekeno

Pages

Tuesday, February 2, 2016

Ted Cruz amshinda Trump mchujo wa Iowa

Seneta wa Texas Ted Cruz ameshinda mchujo wa uchaguzi wa mgombea wa uchaguzi wa Republican katika jimbo la Iowa, Marekani.
Huo ndio mchujo wa kwanza katika uchaguzi wa urais wa 2016 ambao utafanyika baadaye mwezi Novemba.
Cruz amepata asilimia 28 ya kura.
"Huu ni ushindi wa wahafidhina jasiri," mgombea huyo amesema baada ya kubainika kwa ushindi wake.
Mfanyabiashara Donald Trump alikuwa akiongoza kwenye kura za maoni kabla ya kura kupigwa lakini sasa amekuwa wa pili na asilimia 24.
Seneta wa Florida Marco Rubio amefanya vyema kuliko ilivyotarajiwa, na akamaliza nambari tatu na asilimia 23.
Kura za mchujo wa chama cha Democratic bado zinahesabiwa.
Asilimia 85 ya kura ambazo zimehesabiwa zinaonyesha pengo kati ya Hillary Clinton na mshoshialisti wa chama cha Democratic Bernie Sanders ni 1% pekee.
Akizungumza baada ya matokeo kujulikana, Marco Rubio amempongeza Bw Cruz na kusema ndiye mgombea ambaye anaweza kuunganisha chama cha Republican ambacho kimegawanyika.
Dakika chache baadaye, Bw Trump alipanda jukwaani katika ukumbi mwingine na kumpongeza seneta huyo wa Texas, na kusema anaridhika kumaliza katika nambari mbili.
Wagombea wawili wamejiondoa kinyang’anyironi

0 comments:

Post a Comment